Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Kalamu,

Mapambano yoyote ni kutumia mbinu mbalimbali na ukitumia Akili zaidi unawini kama kumsukuma mlevi vile, kule kutumia makele kama yakina Mrema,

Mfano kama tungepigana vita ya Uganda tukifikiri tuko fit kwa maguruneti tungezidiwa lakini tulitumia mbinu tofauti,,, eventually tulishinda vita...

Lakini hatukushinda kumimina B52 kama za Bush kule Afghkanistan, that was my message

"Mapambano yoyote ni kutumia mbinu mbalimbali"-kilitime.
Ninakubaliana na wewe moja kwa moja, including 'communication skills' Sawa.
 
Ninarudia hoja yangu, hadi CCM ione haja ya kuwepo Katiba mpya. Kwa maoni ya CCM ni rahisi na ina mantiki kuifanyia marekebisho Katiba iliyopo kwa kuzingatia ripoti ya tume kuliko kuandika Katiba mpya. Swali jingine ni lipi lifanyike kati ya kuandika Katiba mpya au kufanya mabadiliko makubwa ya Katiba bila kuandika upya Katiba?
 
Mkjj,

Katiba iliyopo imepitwa na wakati, haijaonyesha mafanikio na wala haimnufaishi mlengwa (mwananchi). Viongozi wa sasa ambao ni sababu ya matatizo yetu wamekwa na hii Katiba mbovu. Ili kukata uhusiano na uozo uliopo ni afadhali kuandika Katiba mpya.
 
Haki haotolewi kama sadaka, hupiganiwa.
Hata wakoloni hawakupenda kutupa Uhuru wetu, ni pressure dio iliowafanya wakubali.
so ni kazi kwetu kutoa hiyo pressure in different forms

Mazingira ya kisiasa ya Tanzania bado yanaruhusu kufanyika kwa zaoezi hili kwa njia salama. Tunapozidi kuchelewa na wakati utawala/dola ama serikali inazidi kupoteza legitimacy ni kukaribisha "all means necessary" strategy ambayo gharama yake ni kubwa kwa mtanzania na hata mtawala wa sasa.

Sioni mantiki ya serikali yenye "uhalali" wa asilimia Themanini (80%) kuogopa kuchukua hatua ya kubadilisha hii katiba kwa wakati huu ambao bado kuna mazingira yanayowahakikishia nafasi ya kuendeleza ushawishi wao hata katika kuundwa kwa hiyo katiba mpya.

katiba mpya ni kete nyingine ya kurejuvinate uhalali wa CCM kwa miaka 20 ijayo. Kete ya kubadili sura ya rais (new president same governemnt/regime) tu imeshaishiwa nguvu na sio ya kuendelea kutegemewa.

Unless rais wa nne (JK) alimaananisha yale maneno yake ya "naamini katika continuity" na haikuwa strategy ya kuhakikisha smooth transition from his predecesor Mzee Ben. Kwangu mimi naona hii ni kete ya ulaji kwa JK mwenyewe kama binafsi na rais wa Tanzania na vilevile tabaka tawala kwa jina la CCM.

Wanapozidi kuchelewa ni kujipiga bao la kisigino "wengine" wajichukulie ujiko na kulazimika kubadili katiba kwa nguvu ya wananchi. Meaning change of status Quo in totality something opposite to their interests.

Watambue kuwa JK (kasi mpya) generation ni kizazi cha mpito tu na ushawishi wa kizazi hiki ambacho bado ni mwendelezo wa "CCM as a way of life mentality" ni ushawishi wa kupita wa miaka michache tu.

The new generation of "CCM is not THA Tanzania" kiko njiani kinapiga hodi na hiki hakitakuwa na msalimie mtume katika kuondoa UCCM na hata Unyerere wa Tanzania yetu (something sad).

Sasa ni wao kutumia akili kwa faida yao na faida ya watanzania zaidi ya jeuri ya power iliyopo sasa.

Tanzanianjema
 
Mkjj,

Bila shaka jibu lao litakuwa HAPANA, ndiyo maana hakuna sababu ya kusuburi baraka za CCM ili kufanikisha hili zoezi. Muathirika ni mwananchi na wala siyo mtawala (CCM); kwahiyo, upinzani unabidi uanze kampeni za mabadiliko ya katiba kama unavyofanya kampeni za ucahguzi mkuu.

Upinzani unabidi uende kwa wananchi, uwa elimishe wananchi udhaifu wa katiba ya sasa halafu uwaambie kwanini tunataka mabadiliko ya katiba.

Ninadhani mtu yeyote anayeomba mabadiliko ya katiba Tanzania atakuwa na kesi nzuri tu kwa wananchi na hata katika jumuiya ya kimataifa.
 
Huyu Mkjj sometimes haeleweki, sasa kwa nini lile suala la wanafunzi wa Kitanzania walioko Ukraine mbona alilivalia njuga na wakati CCM na Serikali yake walilikataa? si angeliwacha tu mpaka CCM/Serikali watakapo kuwa tayari kulishughulikia? kwa sababu kama Wanafunzi walikuwa katika hali mbaya hata wananchi vile vile wapo katika halil mbaya kwa matokeo ya Katiba hii mbovu.

Au ndio kaingia woga baada ya kupewa mkwala?

Suala sio kusubiri mpaka CCM wakubali ni kuwalazimisha wakubali coz kama Katiba iliyopo ina maslahi nayo sio rahisi wao kukubali mabadili.
 
Upinzani unabidi uende kwa wananchi, uwa elimishe wananchi udhaifu wa katiba ya sasa halafu uwaambie kwanini tunataka mabadiliko ya katiba.

Ninadhani mtu yeyote anayeomba mabadiliko ya katiba Tanzania atakuwa na kesi nzuri tu kwa wananchi na hata katika jumuiya ya kimataifa.

tz_devel,

Kama nilivyosema kabla ya hapo, wakuelimishwa ni wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wawakilishi wa Zanzibar wenye mamlaka ya kubadilisha katiba ki-sheria na kamati kuu (CC), halimashauri kuu(NEC) ya CCM, wenye uwezo wa kuanzisha mchakato wa kuomba kubadili katiba. Bila vyombo hivi, viwili/vitatu kuamua ... tunatwanga maji kwenye kinu....

By the way, I also struggled to understand why we needed a new constitutions until I found my own reasons which is not tallying with Opposition party's one;
kwa sababu wao wanaiomba katiba mpya wanazungumzia madhumuni ambayo kwangu mimi sioni pia yana umuhimu/msingi mkubwa kwa kuwa mengi yanalenga mambo machache na ya ubinafsi kama kawaida ya Wabongo,,, kila mmoja anatetea masilahi yake... mengi wanayoongelea ni yamejikita kwenye uchanguzi which is non-sense....haya ya upinzani yote yanahitaji marekebisho ya katiba and not katiba mpya!!! again they have failed to communicate, my fried told me they need to go to school for communication skills:


Ungeniuliza mimi kwanini unataka katiba mpya: Nina nia moja kubwa tu na haihusiani na mambo ya uchaguzi direct nayo ni! well kuna zingine ndogo ndogo lakini nataka ifuatayo:


Nahitaji chombo kingine ambacho kiko juu ya Rais wa nchi ambacho (kama vile board ya shule vile ambapo mwalimu mkuu yuko answerable kwa board ya shule) sio bunge hapana, bunge linakuwa linaangalia day-2-day activities za serikali no problem liendelee hivyo hivyo.

Rais wa nchi anatekeleza sera za chama chake za miaka mitano tu. tangu aingie madarakani; hili linasababoshwa wakati mwingine changes za marais zisiguarantee kama rais mchaguliwa wa chama husika anfuatilia vision ya nchi, kwa kuwa ataangalia sera ya chama chacke ambayo haiiendi mbali zaidi ya miaka mitano na hii ni hatari sana, maana taifa hili hakuna mtu wa kumshikilia responsible kwa kutotekeleza vision kwa mfano 2025; pia hakuna namna ya kusema Tanzania bwana we need this, whether president is from CCM, CUF or MAKINI...

Hiki chombo ambacho kitakuwa juu ya rais kitakuwa responsible kuhakikisha rais yeyote anaelekea kutekeleza vision ya nchi; na composition ya chombo hiki haitafuata siasa, bali representation ya vyombo muhimu kabisa vya jamii; kwa mfano
  1. viongozi wakuu wa dini
  2. majaji wakuu wastaafu, au mtu atakaye chaguliwa na majaji wa rufani
  3. wataalamu wasiozidi wawili kutoka kila fani muhimu ya uchumi/taaluma; e.g. uhasibu (NBAA), NBMM, ERB, ICT,
  4. wawakilishi wa vijana, waliochaguliwa na baraza la vijana
  5. wawakilishi wa wanawake waliochaguliwa na baraza lawanawake wote bila kujali siasa
  6. Wawakilishi wa pande za Muungano
  7. Marais wastaafu, wa Zanzibar na Tanzania
  8. Maspika wastaafu wa Zanzibar na Tanzania
  9. wawakilishi wa wabunge
  10. wawakilishi wa baraza la wawakilishi Zanzibar
  11. Wawakilishi kutoka vyuo vikuu vya umma
  12. etc, etc
Kwa maana kuwe na full representation lakini hata hivyo kuwe na sifa ambazo tunaamini wakuwa responsible kumuongoza rais kuhakikisha kila atakayechaguliwa anatekeleza pamoja na sera zake yakini vision ya taifa, in other words, hawa tutahitaji waformulate sisi kujua miaka 15, 25, 50 Tanzania itakuwa vipi na nini kifanyike... wawe na shule au kuwe na namna wawe wanashauri au kupigwa shule vizuri sana kuhakikisha maslahi yataifa yanatiliwa manani

Well huenda nikashindwa kuelezea nia halisi ambayo ni nzuri tu lakini kwa kifupi nataka kumshika chombo, mtu mwingine responsible kwa kuangalia nchi inaenda wapi; raisi is a political figure ambaye ni mwajiriwa tu wakutekeleza sera zake na what country needs tena kwa kipindi kifupi 5 years: Kwa hiyo maraisi wetu wanakimbilia kufanya quick fix ambazo haziipeleki nchi popote kama billion 21 za JK.

Pia Board hiyo itakayokuwa juu ya rais, sijui marekani ndio senate whatsoever;;; ndio itakuwa inaamua maamuzi makali ya mstakabali wa nchi afuta bunge kupitisha, kama vita pia etc. etc...

Sababu nyingine ya pili kwangu kuhitaji katiba mpaya ambayo sio kubwa sana ni kupunguza madaraka ya rais; kwenye uteuzi wa viongozi du kila mahali;

Sababu ya Tatu:-
Viongozi wa Board, vyombo vikubwa wanapoteuliwa wapitishwe na bunge kwanza kwa maana viongozi kama kamshina wa PCB, lazima awekwe kiti moto kwanza na baada ya hapo apigiwe kura kukubalika ama la... sasa hii yawezekana ile board ya kumuongoza rais au Bunge,,, mtaangalia wataalamu, lakini hata IGP au questioned bungeni na akishindwa pia waombe aondolewe kwa hoja binafsi wakishindwa kati...


Duhhh nasikia usingizi; nisameheni kwa kutowezapangilia hoja zangu...Mwisho yanayopigiwa kelele na Upinzani ni cha mtoto kwangu... kwa mfano; tume huru ya uchaguzi; tume huru ya uchaguzi zanzibar wametafsiri kama tume ambayo ina CCM na CUF which is non-sense; tume huru ni watu wanaochaguliwa kwa taaluma yao na sio vyama vyao.... lakini again katiba yenu ingekuwa na senate whatsoever president au watu watapendekeza hiyo senate/board hiyo ya kumuongoza rais, juu ya rais itayapitisha majina na ikibidi ipite bungeni pia.

Naomba kutoa hoja
 
Yaani nchi iwe inaendeshwa na "board" kwani imekuwa NGO? Tayari mna Bunge, mnataka board tena? It is your fault kama mnachagua Wabunge wa hovyo wanaoshindwa kuisimamia Serikali. Hata hii system board ikiwa na mapungufu mtataka kubadilisha katiba tena, sio?
 
MugongoMugongo, well mimi sio mtaalamu wa maneno mazuri; probably nimechagua neno baya; lakini ukisoma kwa undani ukiacha uhafidhina utaelewa tu!!! Call it senate; maana nadhani umetawaliwa sana kwa hiyo hutakubali neno lolote zaidi ya yale uliokaririshwa na mwalimu wako!!!

Anyway, wenye kutumia akili na sio mioyo yao wataelewa namaanisha nini?
 
Kilitime,
Ni kitu kama Senate- or House of Lords! Ila ningependa kiwe na nguvu zaidi kikatiba! Ni wazo zuri- tunahitaji kuwa na something to question the president- zaidi ya Bunge. Hii pia itasaidia Balance of Power kwa Serikali. Tatizo lililopo raisi/CCM wanweza kuamua chochote- na hakuna wa kuwauliza- wana majority ktk kila kitu! This is not healthy to our nation!
 
Yes Mzalendohalisi,

Nashukuru kunisaidia ili vijana wa JF wakorofi wanielewe.

Nataka kitu kisichofungwa na vyama vya siasa,,, bunge la sasa limefungwa na vyama vya siasa be it CCM, CHADEMA etc, na linacheck daily, activities; I want something responsible for strategic vision ya kitaifa, kwa masilahi ya taifa... for long term.

Mfano tukiingia mikataba ya miaka 25, etc... akina John Komba, na Marehemu (mungu amuweke mahali pema) hawawezi/wasingeweza ku-anticipate kwamba ni mambo gani ya kuangalia katika vipindi vijavyo..So tunahitaji chombo kingine pale juu zaidi... hapa ndio maadili ya viongozi yatafuatiliwa kwa mfano inabidi ile tume iwe responsible kwa hii senate... etc. etc. PCB, should report to this senate, mipango mizito ya wizara ya mipango inatakiwa pia iwe iko challenged na senate ikitumia wataalamu itakawaweka etc..

Hii kwangu ni No. ya kuhitaji katiba mpya: yaani changes from pale juu kabisa kwenye mzizi wa katiba
 
Mzee Mwanakijiji,

Nashindwa kidogo kuelewa unalenga wapi hasa ktk swala la Katiba kurekebishwa ama kuundwa Upya. Katiba yetu is beyond repair!...pancha zimeisha zibwa sana na kama ni viraka vimeshonana juu kiasi kwamba Tanzania leo hii haina tena dira isipokuwa ile tunayotungiwa na nchi za Ulaya - Millenium Development Goal (MDG) ambayo ni baada ya miaka 40 ya Uhuru wetu ati tumekumbushwa tena upya yale alokuwa akiyasema Nyerere. Adui wetu ni walewale toka Uhuru, yet leo hii imekuwa somo kwetu kiasi kwamba wataalam wamekuja tukumbusha sisi upya kuwa adui wetu wakubwa ni Umaskini, Maradhi na Ujinga.

Na tunajivuna mbele ya hawa mabwana kwa kuitangaza hiyo MDG wakati ni somo tuliklojifunza toka miaka ya 70 kisha wengine wanasema bila aibu kuwa agenda hii haijabadilika. Ndugu yangu watu wanakufa leo hii kwa maradhi hayo kuliko wakati wowote ule!..somewhere, something is very wrong!..Umaskini umezidi, maradhi yamezidi na hata Ujinga ndio kama hivyo unaona!.. Katiba inaonekana Poa tu!

Tuwe na aibu kiidogo tutazame nyuma na kungalia wapi tulikosea na kama ni Katiba basi iundwe upya kwa maslahi ya nchi yetu laa sivyo basi hakuna mtu wala chama kinachoitakia kheri Tanzania.
na kwa nini kila siku hatuishi kujiuliza NJIA kuhusu mambo yanayohusu mustakabari wa nchi yetu...seems we've lost faith!
 
Kilitime,

Kwanza, Tunahitaji mabadiliko ya kidemokrasia ili tuwe na demokrasia ya kweli. Mimi binafsi si waamini wapinzani na kama ni kuwatumia ni kwasababu ndiyo chombo halali ambacho kinaweza kuongoza hayo mabadiliko.

Pili, sioni sababu ya kuwaelimisha Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, kwani hawa waheshimiwa wako pale kwa manufaa yao wenyewe.

Swala ninaloongelea ni mapinduzi ya kidemokrasia ambayo yatakuwa na acts of civil disobedience, sits-ins, na general strikes. Kwani ni mapambano kati ya wananchi na watawala (CCM)/aliyenacho na asiyekuwa nacho. Maelfu ya wananchi wataandamana kila siku mpaka watawala wakubali mabadiliko ya katiba.

Mwisho, checks and balance ndiyo njia pekee itampunguzia madaraka Rais na Waziri Mkuu na italipa Bunge na Mahaka uwezo wa kukosoa Executive Branch.

By the way, Congress = Senate (upper house) + House of Representatives (lower house). Nadhani ulikuwa na maana ya Congress.
 
Kwanza, Tunahitaji mabadiliko ya kidemokrasia ili tuwe na demokrasia ya kweli. Mimi binafsi si waamini wapinzani na kama ni kuwatumia ni kwasababu ndiyo chombo halali ambacho kinaweza kuongoza hayo mabadiliko.

By the way, Congress = Senate (upper house) + House of Representatives (lower house). Nadhani ulikuwa na maana ya Congress.

tz_devil
Nakubaliana na wewe lakini wenye kufanya mabadiliko haswa kisheria sio vyama vya upinzani ni 2/3 ya Bunge na Baraza la wawakilishi, ndio maana naona umuhimu wao zaidi kuliko kwa sasa wapinzani ambao ni promota tu na wakishindwa kuwasiliana vizuri ndio wanatuletea usiku zaidi

I think kwenye hoja yangu... nilitaka hiyo (upper house) kwa maana nisaidia natambaa kwenye hili nataka kulinganisha

1. house of representatives = kama bunge la jamhuri/baraza la wawakilishi (comtemporary issues, routing business, in 5 years terms)

2.Senate = Tanzania hatuna ? au? (hii ndio mimi naihitaji... lakini kwa tafsiri kwamba wawe wanazungumzia mambo mazito zaidi ya muda mrefu)

kwa hiyo kwa mambo mazito kabisa kabisa = we need both and hence congress, lakini haya ya kila siku tunahitaji representatives ... dones

Ahsante kwa kuendelea kunielimisha
 
tz devil,

Katika hilo mimi naweza kuwaamini zaidi wananchi wa Zanzibar kuliko Bara, unaweza jikuta ukumbini peke yako ukisubiriwa na mbwa wa FFU... Bara bado kabisa tumedumazwa na Ujamaa wa kisocialist kuogopa serikali na vyombo vya serikali kama vile ni Miungu watu.

Hii ndio mirathi alotuachia Mwl. na kwa ujinga wetu tunajisifia kuwa ni ujanja wa kunguru.
 
Kilitime,

Sauti ya uma ni sauti ya Mungu...shinikizo la wananchi ndiyo silaha yetu kubwa katika haya mabadiliko. In fact, ni njia mojawapo ya kuwawezesha wananchi kisiasa.

Back to your question

Congress has two chambers, House of Representatives (simply the House) currently 435 representatives, 2 yrs term – may be re-elected an unlimited number of times. The Senate (upper house). Each state is represented by two members. Currently 100 members, six – year term. Tanzania hatuna Senate.

Kwahiyo, Bunge letu ni sawa na Congress, ispokuwa tuna chemba moja na wenzetu wanazo mbili. Na tumaini hii itakuwa imekupa mwanga kidogo. Just google it, you will get all the enchilada.

Mkandara,

Umenivunja mbavu na hao mbwa wa FFU. Ni kweli tumedumazwa na nidhamu ya uoga na ndiyo maana hawa watawala wana take advantage ya udhaifu wetu
 
Sijui kwa nini Watanzania tu Waoga kusema Ukweli.Hii Katiba yetu haihitaji marekebisho ya namna yoyote."Huwezi kuweka viraka kwenye chupi iliyochakaa",Dawa ni kutafuta chupi mpya!!,Katiba yetu imepitwa na wakati,ni vyema tuanze sasa kutafuta Utaratibu wa kuundwa katiba Mpya itakayokithi matakwa ya Watanzania bila kujali Itikadi zao kichama.Tuna wanazuoni mahili kama Prof.Shivji,Prof.Haroub Othman na Jaji Warioba (na wengine wasiotajwa hapa) wanaoweza kwa dhati kusimamia hili,wakipewa Ushirikiano mzuri.


Bunge linapoteza Muda kujadili Upuuzi wa Ahadi za Uongo za kuwepo Mahakama ya Kadhi Mkuu, badala ya kujadili KATIBA!.Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye anafagilia suala la Mahakama ya Kadhi(Hizi zilikuwa Ahadi za kipuuzi za kutafuta kura kwa waislamu),Leo hii tutapitisha sheria ya kuruhusu Mahakama hiyo, tunawaambia nini wenzetu wa madhehebu mengine!Ndugu wa Tanzania tujipe muda zaidi wa kufuatilia nini kinafanywa na Viongozi wetu,inaonekana sasa tunawapa uongozi watu wasio na sifa.Watu wanapewa madaraka kwa sababu tu "mwela tabiha" (Uzuri wa sura),nafikiri Uwezo wa Uongozi(rekodi yake ya nyuma) na hekima ndio viwe vigezo vya dhati kwa kumpata kiongozi wa NCHI.

Tuna miaka 46 sasa toka tupate Uhuru,lakini mpaka leo mtanzania wa kawaida hajapata ahueni ya maisha,imekuwa ni hadithi za mafanikio kila siku bila kuona mambo hayo kwa vitendo!


Mama Nagu abanwe kuhusu suala zima la KATIBA MPYA,kama hawezi kutoa maelezo mwafaka ni vyema awapishe wenye uwezo huo.Sio wakati wa kulindana sasa,kila mtu anapaswa awajibike ipasavyo kwenye Wizara yake!.

Wanahadaa wananchi kwa kuwafukuza Uongozi akina Kataraiya kwa Matumizi mabaya ya pesa kidogo za Umma,lakini wale wezi wa kweli wa Mamillioni ya pesa ndio wanaongezewa madaraka na kutetewa kwa nguvu zote! Tuwe Fair CC (Central Commitee) anza kwanza na akina Lowassa,Balali na huyu Mzindakaya Ili tuone kwamba kweli mmeamua kujisafisha!Sio uonevu wa hawa wanaoiba/wanaofuja Tsh 2m.Naona naanza kupanda Munkari!Naomba kutoa Hoja.
 
Back
Top Bottom