Upinzani unabidi uende kwa wananchi, uwa elimishe wananchi udhaifu wa katiba ya sasa halafu uwaambie kwanini tunataka mabadiliko ya katiba.
Ninadhani mtu yeyote anayeomba mabadiliko ya katiba Tanzania atakuwa na kesi nzuri tu kwa wananchi na hata katika jumuiya ya kimataifa.
tz_devel,
Kama nilivyosema kabla ya hapo, wakuelimishwa ni wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wawakilishi wa Zanzibar wenye mamlaka ya kubadilisha katiba ki-sheria na kamati kuu (CC), halimashauri kuu(NEC) ya CCM, wenye uwezo wa kuanzisha mchakato wa kuomba kubadili katiba. Bila vyombo hivi, viwili/vitatu kuamua ... tunatwanga maji kwenye kinu....
By the way, I also struggled to understand why we needed a new constitutions until I found my own reasons which is not tallying with Opposition party's one;
kwa sababu wao wanaiomba katiba mpya wanazungumzia madhumuni ambayo kwangu mimi sioni pia yana umuhimu/msingi mkubwa kwa kuwa mengi yanalenga mambo machache na ya ubinafsi kama kawaida ya Wabongo,,, kila mmoja anatetea masilahi yake... mengi wanayoongelea ni yamejikita kwenye uchanguzi which is non-sense....haya ya upinzani yote yanahitaji marekebisho ya katiba and not katiba mpya!!! again they have failed to communicate, my fried told me they need to go to school for communication skills:
Ungeniuliza mimi kwanini unataka katiba mpya: Nina nia moja kubwa tu na haihusiani na mambo ya uchaguzi direct nayo ni! well kuna zingine ndogo ndogo lakini nataka ifuatayo:
Nahitaji chombo kingine ambacho kiko juu ya Rais wa nchi ambacho (kama vile board ya shule vile ambapo mwalimu mkuu yuko answerable kwa board ya shule) sio bunge hapana, bunge linakuwa linaangalia day-2-day activities za serikali no problem liendelee hivyo hivyo.
Rais wa nchi anatekeleza sera za chama chake za miaka mitano tu. tangu aingie madarakani; hili linasababoshwa wakati mwingine changes za marais zisiguarantee kama rais mchaguliwa wa chama husika anfuatilia vision ya nchi, kwa kuwa ataangalia sera ya chama chacke ambayo haiiendi mbali zaidi ya miaka mitano na hii ni hatari sana, maana taifa hili hakuna mtu wa kumshikilia responsible kwa kutotekeleza vision kwa mfano 2025; pia hakuna namna ya kusema Tanzania bwana we need this, whether president is from CCM, CUF or MAKINI...
Hiki chombo ambacho kitakuwa juu ya rais kitakuwa responsible kuhakikisha rais yeyote anaelekea kutekeleza vision ya nchi; na composition ya chombo hiki haitafuata siasa, bali representation ya vyombo muhimu kabisa vya jamii; kwa mfano
- viongozi wakuu wa dini
- majaji wakuu wastaafu, au mtu atakaye chaguliwa na majaji wa rufani
- wataalamu wasiozidi wawili kutoka kila fani muhimu ya uchumi/taaluma; e.g. uhasibu (NBAA), NBMM, ERB, ICT,
- wawakilishi wa vijana, waliochaguliwa na baraza la vijana
- wawakilishi wa wanawake waliochaguliwa na baraza lawanawake wote bila kujali siasa
- Wawakilishi wa pande za Muungano
- Marais wastaafu, wa Zanzibar na Tanzania
- Maspika wastaafu wa Zanzibar na Tanzania
- wawakilishi wa wabunge
- wawakilishi wa baraza la wawakilishi Zanzibar
- Wawakilishi kutoka vyuo vikuu vya umma
- etc, etc
Kwa maana kuwe na full representation lakini hata hivyo kuwe na sifa ambazo tunaamini wakuwa responsible kumuongoza rais kuhakikisha kila atakayechaguliwa anatekeleza pamoja na sera zake yakini vision ya taifa, in other words, hawa tutahitaji waformulate sisi kujua miaka 15, 25, 50 Tanzania itakuwa vipi na nini kifanyike... wawe na shule au kuwe na namna wawe wanashauri au kupigwa shule vizuri sana kuhakikisha maslahi yataifa yanatiliwa manani
Well huenda nikashindwa kuelezea nia halisi ambayo ni nzuri tu lakini kwa kifupi nataka kumshika chombo, mtu mwingine responsible kwa kuangalia nchi inaenda wapi; raisi is a political figure ambaye ni mwajiriwa tu wakutekeleza sera zake na what country needs tena kwa kipindi kifupi 5 years: Kwa hiyo maraisi wetu wanakimbilia kufanya quick fix ambazo haziipeleki nchi popote kama billion 21 za JK.
Pia Board hiyo itakayokuwa juu ya rais, sijui marekani ndio senate whatsoever;;; ndio itakuwa inaamua maamuzi makali ya mstakabali wa nchi afuta bunge kupitisha, kama vita pia etc. etc...
Sababu nyingine ya pili kwangu kuhitaji katiba mpaya ambayo sio kubwa sana ni kupunguza madaraka ya rais; kwenye uteuzi wa viongozi du kila mahali;
Sababu ya Tatu:-
Viongozi wa Board, vyombo vikubwa wanapoteuliwa wapitishwe na bunge kwanza kwa maana viongozi kama kamshina wa PCB, lazima awekwe kiti moto kwanza na baada ya hapo apigiwe kura kukubalika ama la... sasa hii yawezekana ile board ya kumuongoza rais au Bunge,,, mtaangalia wataalamu, lakini hata IGP au questioned bungeni na akishindwa pia waombe aondolewe kwa hoja binafsi wakishindwa kati...
Duhhh nasikia usingizi; nisameheni kwa kutowezapangilia hoja zangu...Mwisho yanayopigiwa kelele na Upinzani ni cha mtoto kwangu... kwa mfano; tume huru ya uchaguzi; tume huru ya uchaguzi zanzibar wametafsiri kama tume ambayo ina CCM na CUF which is non-sense; tume huru ni watu wanaochaguliwa kwa taaluma yao na sio vyama vyao.... lakini again katiba yenu ingekuwa na senate whatsoever president au watu watapendekeza hiyo senate/board hiyo ya kumuongoza rais, juu ya rais itayapitisha majina na ikibidi ipite bungeni pia.
Naomba kutoa hoja