Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Mama Nagu kasema wazi hakuna cha Katiba mpya! ila CC wakisema wanataka Katiba mpya guess what...
 
UNAJUA UKITAMKA KAMATI KUU, AU CC WENGINE WANADHANI NI DUDE KUBWAAA!!! LA HASHA NI HAWA WAHESHIMIWA HAPA

HATIMA YA TAIFA HILI LIKO CHINI YA HAWA HAPA CHINI!!! WAKIAMUA JAMBO LAFANYIKA WAKISEMA NO, LIA MPAKA UGAREGARE....

WAJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (2002-2007)

1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti
2. Ndugu John Samwel Malecela - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu

5. Ndugu Jaka Mwambi - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe


8. Ndugu Edward Ngoyai Lowassa - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe

11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
13. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
14. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
15. Ndugu Aggrey Mwanri - Mjumbe

16. Dr. Asha - Rose Migiro - Mjumbe
16. Ndugu Samwel Sitta - Mjumbe
17. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
18. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
19. Ndugu Amina Salum Ali - Mjumbe
20. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
21. Ndugu Pindi Chana - Mjumbe
22. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
23. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
24. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
25. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
26. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
27. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
28. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
29. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
30. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
31. Ndugu Kingunge Ngombale-Mwiru - Mjumbe
32. Ndugu Juma Suleiman N'hunga - Mjumbe
33. Ndugu Salim Ahmed Salim - Mjumbe
34. Ndugu Abiud Mugini Maregesi - Mjumbe
35. Ndugu Yussuf Moh'd Yussuf - Mjumbe
 
Shukran Bwana Kilitime,kwa kuweka hapa wajumbe wa CC ambao naona ndio Chombo chenye nguvu kwenye Utawala wa nchi.Katika Orodha yako naona kuna baadhi ya WAJUMBE ushiriki wao sio active kutokana na shughuli zao, ama kustaafu kwa hiari siasa na masuala yahusuyo Uongozi:
1; Dr.Asha Migiro - Yupo New York na masuala ya UN.
2; Dr.Salim A. Salim - Ametangaza kupumzika shughuli za Uongozi.
3; Amina s. Ali - Yupo New York muakilishi wa AU huko US/UN
4; Abihud Maregesi - kuna taarifa isiyothibishwa kuwa kafukuzwa
ndani ya CCM.
 
Shukran Bwana Kilitime,kwa kuweka hapa wajumbe wa CC ambao naona ndio Chombo chenye nguvu kwenye Utawala wa nchi.Katika Orodha yako naona kuna baadhi ya WAJUMBE ushiriki wao sio active kutokana na shughuli zao, ama kustaafu kwa hiari siasa na masuala yahusuyo Uongozi:
1; Dr.Asha Migiro - Yupo New York na masuala ya UN.
2; Dr.Salim A. Salim - Ametangaza kupumzika shughuli za Uongozi.
3; Amina s. Ali - Yupo New York muakilishi wa AU huko US/UN
4; Abihud Maregesi - kuna taarifa isiyothibishwa kuwa kafukuzwa
ndani ya CCM.


Mwawado,

Hawa wapo hadi baada ya uchaguzi huu wa mwaka huu (2007)... Dr. SAS kwa mfano amesema hatagombea hamaanishi kwa sasa hayupo...

By the way, kujua nchi kweli yaweza kurudishwa kwenye mstari ni kwa kuangali kama hawa waheshimiwa ni wasafi wote, kama ndio then at least naweza pata usingizi leo.
 
Kilitime,

Mheshimiwa umenipa somo, amini usiamini siku zote mimi nildhani kuna Kamati kuu ya Taifa mbali kabisa na hiyo ya CCM.
Hata niliposoma hoja yako iliyotangulia nilianza kujiuliza kwani kamati kuu kazi yake nini? kumbe ni haohao tunaowapigia kelele ndio wameshika!...
Je, kuna wajumbe ndani ya hiyo kamati kuu ambao sio Member wa CCM?
 
Mkandara, jibu ni hapana. Tunapozungumzia Kamati Kuu.. tunazungumzia Kamati Kuu ya CCM. Ila nadhani wazo la Kamati Kuu ya Taifa lingekuwepo kama ile ya chama cha Kikomunisti cha China... lakini ingekuwa non partisan na ingekuwa juu ya vyama vyote..
 
Mabadiliko Tanzania yatakuja tu watake wasitake,kwa spidi ya hawa viongozi wetu wanavyo kwenda,siku sio mbali kama alivyosema Mkjj hiyo siku yaja,wengi watazinduka kutoka usingizini na kuona nuru ya kweli japo tutapita katika kipindi kigumu ktk historia ya nchi lakini tutapata pumziko la milele.

Hapo tanzania mpya itajengwa upya.
Ccm wanachofanya sasa ni kuvuna rasili mali ya nchi na kujilimbikizia kana kwamba hakuna kesho na kuwafungia walalahoi katika kachumba kadogo (rejea kule mbeya wale mahabusu yalivyo kufa chini ya kamanda mwema)siku wananchi watakapochoshwa na umasikini,shida walizonazo ndio kuanguka kwa ccm na vibaraka wake.
 
Mwawado,

Hawa wapo hadi baada ya uchaguzi huu wa mwaka huu (2007)... Dr. SAS kwa mfano amesema hatagombea hamaanishi kwa sasa hayupo...

By the way, kujua nchi kweli yaweza kurudishwa kwenye mstari ni kwa kuangali kama hawa waheshimiwa ni wasafi wote, kama ndio then at least naweza pata usingizi leo.

Wengi hatukujua hiyo CC ni ya watu gani. Ahsante sana kwa kutujulisha.
 
Kilitime,

Hivi huyu Rostum na Lowassa wameingiaje humo? Just curious.

Ahsante!
 
Kwa hiyo jibu rahisi sana kuwa nchi yetu inaendeshwa na KATIBA ya chama CCM, hiyo ya Taifa ipo for display ONLY!.
 
Waungwana,

Wikiend yangu ilikuwa ndefu sana kiasi kuwa sasa hivi "maboksi" yanayoningoja ni mengi sana. Kwa hali hiyo nimeshindwa kupitia mada zote zilizotolewa nyuma kwenye thread hii ambayo nadhani ni ya muhimu kwangu kuliko thread yoyote tangu nijiunge. Kama maoni yangu yatakuwa ni marudio ya yaliyokwisha zungumzwa, basi naombeni samahani. Katiba yetu hii inatoa madaraka makubwa sana kwa viongozi na haitoi mwanya wa kudhibiti madaraka hayo, jambo hili linachangia sana kurudisha nyuma maendeleo ya nchi hii.

  1. Viongozi wa serikali wanaweza kuwapiga makofi wananchi hadharani kama vile ni watoto wao bila hata kujali umri wao au hesima zao katika familia zao. Hii inasabababisha wanachi wetu wengi washindwe kujiamani na kudhani kuwa kila kitu wataamuliwa na kufanyiwa na viongozi na serikali. Yote hii ni kwa sababu viongozi hao wana madaraka makubwa dhidi ya raia wambao hawana fursa ya kuwadhibiti viongozi wao: wanawaogopa.
  2. Viongozi wetu wanatumia nafasi zao kujitajirisha kwa kuliingiza taifa hili ama katika hasara kubwa sana au katika madeni makubwa kuwa faida yao binafsi. Ukiwauliza wanatoa majibu ya kejeli yasiyokuwa na manufaa kwa nchi kama vile:
    • "wananchi ni wavivu wanaotumia muda wao vijiweni badala ya kutumia 'fursa' walizowekewa na serikali,"
    • "Wanaohoji mambo hayo wana wivu wa kike."
    Nafasi hizi wanazopata kujitajirisha na hasara inayopatika nchini vyote vinatokana na mianya mingi katiba yetu ambayo inawapa viongozi madaraka makubwa.
  3. Kuna mambo mengi sana yanayoonyesha kuwa serikali haijali; na yote hayo ni kwa sababu ya katiba kuwa na mianya ya kuwafanya viongozi wa serikali wasijali.

Tatizo kubwa katika katiba yetu ni ukosefu wa "checks and balances," na kuwepo kwa "absolute power" mikononi mwa watu wachache, na kuwaacha wanachi kama ni "objects of pity" mbele ya serikali. Hii absolute power inasababisha viongozi wawe "above the law" na "untouchables." Wakati inawanyanyua viongozi juu vile, katiba hii hii inawatelemsha wananchi chini sana kama vile hawana haki katika nchi hii. Ninaona kama vile katiba inawafanya wananchi wawe kama wabeba machela lilokaliwa na viongozi, huku wao wenyewe wakiwa hawajui machela hilo linakwenda wapi.

Katiba hii inatakiwa kuandikwa upya, siyo kufanyiwa marekebisho ya hapa na pale. Inawezekana kabisa kuwa katiba hii ilitufaa sana mwaka 1977 ilipoandikwa kwa mara ya kwanza, lakini leo hii bada ya mabadiliko makubwa duniani na nchini hapa, haitoshelezi kabisa. Mabadiliko ya katiba hii sijo jambo la kujadili kama yananatikwa ila tujadili tu namna ya kuyafanya.

Kutokana na CCM kuhodhi madaraka ya mwelekeo wa nchi hii, ninadhani kabisa kuwa kama tunataka marekebisho halisi katika katiba yetu lazima tuwatumie wana CCM au watu neutral wanaoweza kusikilizwa na CCM; tusitegemee kuwa opposition itasukuma jambo hili hadi likakubaliwa na serikali ya CCM.

Maoni yangu kuwa kuwa, tutafute nafasi ya kuwa-court wana CCM maarufu wanaoweza kusupport ukweli huu; ninadhani (in my naivity) kuwa Rais Mwinyi, Jaji Warioba, Dr. Salim Ahmed Salim ni kati ya wana CCM wachache wanaoweza kusupport jambo hili. Sina uhakika na msimamo wa Mzee Kawawa katika swala la kubadilisha katiba ambayo iliandikwa chini ya uangalizi wake. Vile vile tuwacourt majaji- wasitaafu wote. Swala la kujadili hapa labda liwe ni namna gani tuwacourt watu hawa na kuwaweka katika ngalawa moja ya kudai mabadiliko haya ya katiba.
 
Kama maoni yangu yatakuwa ni marudio ya yaliyokwisha zungumzwa, basi naombeni samahani. Katiba yetu hii inatoa madaraka makubwa sana kwa viongozi na haitoi mwanya wa kudhibiti madaraka hayo, jambo hili linachangia sana kurudisha nyuma maendeleo ya nchi hii.

Kichuguu
Naungana na wewe katika hili!



Maoni yangu kuwa kuwa, tutafute nafasi ya kuwa-court wana CCM maarufu wanaoweza kusupport ukweli huu; ninadhani (in my naivity) kuwa Rais Mwinyi, Jaji Warioba, Dr. Salim Ahmed Salim ni kati ya wana CCM wachache wanaoweza kusupport jambo hili. Sina uhakika na msimamo wa Mzee Kawawa katika swala la kubadilisha katiba ambayo iliandikwa chini ya uangalizi wake. Vile vile tuwacourt majaji- wasitaafu wote. Swala la kujadili hapa labda liwe ni namna gani tuwacourt watu hawa na kuwaweka katika ngalawa moja ya kudai mabadiliko haya ya katiba.

Niwahisema hili nakapingwa sana na wanaJF.
 
Kilitime,

Je, kuna wajumbe ndani ya hiyo kamati kuu ambao sio Member wa CCM?

Mkandara;

Duh! mkuu hao ndio sisiem damu, sasa tena uweke wasiokuwa sisiemu, wote CCM, tena lazima uwe umetoka NEC, au ujumbe wa Heshima, well kwenye hoja yangu ya Senate nilikuwa namaanisha watu wachaguliwe kwa elimu zao, hekima zao, heshima zao, katika jamii, wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jamii, watoto (14-18yrs)walemavu, vijana, wasomi, wanadini etc.

Sinahakika kama ulikuwa ukiunganisha na hoja hiyo iliyokuwa imepita.
 
Kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kusikiliza hotuba ya Bi. Nagu kuhusu suala la Katiba mpya basi mtapata nafasi hiyo siku ya Jumatano. Leo (Jumanne) unaweza kusikiliza majibu ya serikali kuhusu suala la kadhi.
 
Kilitime,

Yeah ndugu yangu nilikuwa nje kabisa ktk hili. lazima nikubali maanake nilidhani kamati kuu ya serikali ni kitu kingine kabisa nje ya kamati kuu ya CCM.

Kwa maana hiyo nina imani ndio maana swala la katiba mpya limekuwa gumu sana, pia swala la Zanzibar limetazamwa kwa Upande mmoja tu.. Upande wa CCM. Na ukitoa wazo nje ya fikra za wengi utaonekana wewe muasi kama alivyokuwa Mzee wetu Malecela... lile lilikuwa somo kwa viongozi wengi hasa hawa ambao wapo ktk makati kuu ya CCM.

Basi bora turudi ktk mpango wa chama kimoja akam nilivyokuwa nikisema hapo zamani.
Chama CCM ndio kiwe na tabaka mbili - moja Progresive na nyingine Conservative, kisha mgawanyo ufanyike kwa imani za watu ktk mirengo hiyo miwili. Akina Freeman, Lipumba, Seif, Mrema, Mtikila na wengine wote wa join upande wanao amini kuwa ndio mrengo unaofaa kuongoza nchi.

Hiyo hoja ya senate ndugu yangu, siwezi kukubaliana nayo kama tutafuata utaratibu wa US kwa sababu CCM wataongeza hesabu ya viongozi wao yaani kwa sasa hivi tunataka kuwapa hata wazee wao wastaafu kazi mpya. Unafikiri nani ataweza shindana na Malecela akitaka kuwa senate wa Dodoma! basi hao kina Malecela ni wengi mno Tanzania nzima na hakuna wa kuwashinda toka CCM. Labda ufanyike uteuzi badala ya kuchaguliwa!

Problem kubwa ya nchi yetu ni kwamba watu wote waliopata umaarufu mikoani wamepitia SIASA za chama kimoja ama matajiri maarufu, utajiri wao pia umetokana na mkono wa CCM.

Hizi politics za kina Mrema, Mbowe bado kabisa hazijaweza kuvunja imani za watu ambao jina CCM limewakuza wao. Na yapo majina ambayo hayawezi kufutika kirahisi hasa unapotoa nafasi za bwelele!
 
Wananchi kuulizwa kuhusu kunyongwa

Na Ramadhan Semtawa
SERIKALI inaandaa utaratibu wa kuwauliza wananchi iwapo sheria ya adhabu ya kifo iendelee kutumika au ifutwe.

Hatua ya ya serikali imekuja wakati tayari wanaharakati wa Haki za Binadamu nchini, wameonyesha kupinga adhabu hiyo na kutaka ifutwe.

Hoja ya msingi ya watetezi wa haki za binadamu nchini haitofautiani na wa kimataifa, ambao wanaona adhabu ya kifo kama inayoondoa haki ya kuishi kwa wanaokutwa na makosa na pia haitoa nafasi ya mtu kujirekebisha.

Hata hivyo, mchakato huo ambao haujaelezwa utaanza lini, utakwenda pamoja na elimu kwa wananchi kuhusu kuwepo kwa adhabu hiyo katika sheria za nchi kwa sasa.

Akizungumzia hatma ya adhabu hiyo juzi katika kipindi maalumu cha Bungeni Wiki Hii, kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TvT), Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Mary Nagu, alisema yeye binafsi anapinga adhabu ya kifo.

Hata hivyo, Dk Nagu alifafanua kwamba, kwa kuwa nchi inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria, hivyo kila mabadiliko yanapaswa kufuata vyombo hivyo.

"Binafsi, napinga adhabu ya kifo, lakini kama tunavyojua nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na katiba," alisema Dk Nagu na kuongeza:,

"Kwa hiyo serikali itaanda mchakato ili wananchi waamue kuhusu adhabu ya kifo, lakini kabla ya hapo watapaswa kupata elimu kuhusu adhabu hiyo," alisisitiza.

Alisema wananchi lazima waelimishwe kuhusu sheria iliyounda adhabu hiyo ili hata wakitoa maoni, wawe na ufahamu wa jambo wanalochangia.

Katika hatua nyingine, Dk Nagu, alitetea uamuzi wa serikali ya CCM kuingiza katika ilani yake ya uchaguzi, suala la kutaka kupatia ufumbuzi wa Mahakama ya Kadhi nchini, akisema chama hicho hakikurupuka.

"Naomba niseme CCM haikukurupuka kuweka suala la kupatia ufumbuzi wa mahakama ya Kadhi katika ilani yake," alisema Dk Nagu baada ya mbunge wa Karatu, Dk Wilbrod Slaa, kusema uamuzi huo wa chama hicho hicho tawala ni wa kukurupuka.
 
Back
Top Bottom