Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Hili la mjadala wa Katiba halitatokea kama CCM hawataki period. What CCM wants CCM gets, it doesn't want this so we won't get it. Ndio maana mimi naona kujaribu kubadilisha Katiba wakati hauna nguvu ya kufanya hivyo ni kutwanga maji kinuni. Hadi pale wapinzani wananguvu ya kulazimisha siyo kuomba kama wanavyofanya sasa.
Damn! I guess it won't be in our lifetime...
Alisema, mabadiliko ya katiba ya nchi ni ya lazima na kwamba hivi sasa vyama vya upinzani vipo katika mchakato wa kuandaa katiba mpya.
Petition: Tumwombe Rais Mwinyi Atuongoze Mjadala wa Kuboresha Katiba.
Ninashauri kuwa tumwombe mzee wetu Rais Ali Hassan Mwinyi atungoze katika kuendesha mjadala wa kuboresha katiba yetu. Alitungoza kwenye mabadiliko makubwa ya kutoka kwenye uchumi wa kijamaa na kutuingiza kwenye uchumi wa soko huria, halafu akatungoza kutoka mfumo wa chama kimoja kutuweka kwenye mfumo wa vyama vingi, mnaonaje akitusaidia hili dogo la kutuongoza kufanya mjadala wa kuboresha katiba yetu hasa kwa vile viongozi waliopo sasa hawataki kusikia neno katiba?
I support this wholeheartdeadly; this mzee is far more credible than many other CCM politicians. Hiyo kusema kuwa Mwinyi hakusaidi katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa ni kukataa ukweli ulio uwazi. Tukumbuke huyu alikuwa Rais mwenye mamlaka kamili na angeweza kufanya kama alivyofanya Mugabe leo, tena kwa sisi wadanganyika ingekuwa balaa zaidi!
Hili la mjadala wa Katiba halitatokea kama CCM hawataki period. What CCM wants CCM gets, it doesn't want this so we won't get it. Ndio maana mimi naona kujaribu kubadilisha Katiba wakati hauna nguvu ya kufanya hivyo ni kutwanga maji kinuni. Hadi pale wapinzani wananguvu ya kulazimisha siyo kuomba kama wanavyofanya sasa.
Wakati Waziri anasema nilete maoni ya mabadiliko ya katiba kuhusu mfumo wa uchaguzi, tayari mnamo 31/5/2006 nilikuwa nimeandika barua kwa Rais kuhusu suala hili. Maoni gani tena yanatakiwa? nahisi serikali hii haina uratibu wa mambo yake. Barua hii ilichapishwa kama ilivyo na gazeti la Mtanzania. Wizara ya sheria na Katiba ilijibu barua yangu kuonesha wamepokea maoni yangu. Leo Waziri anasema nilete maoni tena.
Hata kama serikali haitaki, vuguvugu la wanannchi kuhusu katiba litachukua kasi. Serikali iachague tu, kufanya mabadiliko/kunadika katiba kwa hiari au kwa shinikizo.
Serikali ya CCM inafaidika na katiba iliyopo sasa, haioni umuhimu wowote wa kuibadilisha. Kwa nini iibadilishe katiba kama inafaidika nayo?
Hapa ndipo uongozi makini wa vyama vya ushindani unapotakiwa, kusimamia mageuzi haya ya katiba. Bila kuibadili hii katiba, demokrasi yetu itakuwa haijakamilika. Viongozi wa ushindani, acheni kuomba ruhusa. Ongozeni wananchi wachukue haki yao ya kuwa na katiba mpya. Mmekwishawaeleza wananchi kuwa hamtashiriki uchaguzi ujao bila ya kuwa na katiba mpya. Hiyo haitoshi, waambieni hapatakuwepo na uchaguzi 2010 bila ya katiba mpya. Wakati ni huu sasa hivi, kufanya mipango ya kuzuia uchaguzi huo.
Mabadiliko ya katiba ni lazima - Mbowe
source:
http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/07/28/95288.html
"Mabadiliko ya katiba ni lazima - Mbowe"
Alisema, "mabadiliko ya katiba ya nchi ni ya lazima na kwamba hivi sasa vyama vya upinzani vipo katika mchakato wa kuandaa katiba mpya."
Vyama vya upinzani visituandalie katiba mpya. Vishughulikie kuishinikiza serikali ya CCM ikubali kubadili katiba. Utaratibu wa kuandaa katiba mpya ni wa wananchi kupitia katika wawakilishi na wataalamu mbalimbali watakaoteuliwa katika kamati mbalimbali zitakazohusika na uandaaji huo wa katiba.