Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Mkuu Zitto, naona umekuja na gia kubwa sana, tuliza boli mkuu mimi sina jazba na wewe, punguza munhari,

Nilishiriki kikako cha kamati, Peacock, ambako washiriki wote tulitoa mawazo yetu na kufanyiwa ukarabati wa pamoja, ni forum ambayo haikuwa ya upinzani peke yao na ulifanyika chini ya mwenyekiti wake Mwana sheria wa kujitegemea Bwana Michael, na kila msihiriki alipewa nafasi ya kuihakiki kabla ya kuisha kwa forum, au seminar mkuu na kila mshiriki akaongeza au kupunguza anayoyataka,

Anyway karibu tena mkuu, hapa giladi tukate ishus ila tu punguza munhari na jazba, maana hizi topic ni muhumu sana kwa taifa letu, na tunataka ziendelee kukatwa kiroho mbaya, sasa ukianza munhari utaharibu mkuu topics mkuu, jaribu kuuheshimu ule ujumbe wa Mwalimu Kichuguu kuwa cool down mkuu!

Ahsante, ila tutaendelea tu kutoa maoni yetu kuhusu katiba kama tulivyoanza, na wewe kama kiongozi unayeheshimika ni vyema ukachangia zaidi kuliko kujaribu kuharibu topic mchango wako ni muhimu sana kwenye hili la katiba! Tumekupokea kwa hesima kubwa sana mkuu na tunaheshimu sana kurudi kwako ndani ya forum, ila usianze kuharibu mapema mkuu, punguza jazba!

Ahsante Mkuu!
 
Hii thread sijaifuatilia sana, ila ilivyoanza nilijua kuwa itakuwa inatoa dukuduku zangu kuhusu katiba yetu. Miezi kadhaa iliyopita niliwahi kuandika hapa aina ya katiba tunayotaka kwa vile hii ya sasa haitufai. Nina imani kabisa maoni yanayotolewa na FMES na wachangiaji wengi hayapingani na maoni yangu ya awali.

Hongera sana FM ES kuliweka hili swala tena hapa. Ninashauri kuwa kama una nafasi ya kuandika kwenye magazeti ya nyumbani kwa kiswahili, ufanye hivyo kusudi wananchi wengi wafahamishwe mapungufu ya katiba yetu. Kama huna channels za magazeti yetu, nakushauri ushirikiane na Mwanakijiji kuiweka hadharani, as unbiased as possible. Msiifanye kama agenda ya vyama vya upinzani bali iwe ni ajenda kwa future ya watanzania wote.
 
Walikuwa wapi siku zote hizi na je wataruhusiwa kuiona mikataba mipya au itaendela kuwa siri?

Wabunge sasa wataka marekebisho ya mikataba
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi
Posted Date::10/18/2007
SIKU moja baada ya Ripoti ya Dunia ya Uwekezaji kuonyesha sekta ya madini kutoinufaisha zaidi Tanzania kiuchumi, baadhi ya wabunge wametaka kuwepo mabadiliko ya mara kwa mara ya sheria za madini ili ziweze kukidhi maslahi ya taifa na kwenda na wakati.

Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara, imeeleza kuwa jana pamoja na mambo mengine walijadili suala la ripoti hiyo ya Uwekezaji Duniani, hasa kipengele kinachohusu madini.

Mwananchi ilifanikiwa kuzungumza na baaadhi ya wabunge mara baada ya mkutano huo, ambao kwa sharti la kutotajwa majina, walisema lazima sheria za madini zifanyiwe mabadiliko mara kwa mara kadri sekta inavyokua.

Kwa nyakati tofuati baadhi ya wabunge wa kamati hiyo, walisema udhaifu wa sheria ya madini ya mwaka 1998, ndiyo unafanya makampuni ya kigeni kuchota madini na kwenda nayo nje huku nchi ikibakiwa na faida ndogo.

Mmoja wa wabunge hao alisema, kinachoonekana sasa ni kama makampuni hayo yanalipa kodi lakini ukweli ni kwamba hayalipi kodi zaidi ya mrahaba.

"Tatizo kubwa ni sheria, jambo la muhimu ni kuhakikisha sheria zinafanyiwa mabadiliko mara kwa mara si kuacha sheria ikae, sasa hivi tatizo hilo linafanya makampuni ya madini kuchimba madini na kuondoka na sehemu kubwa ya faida," alisema.

Mbunge mwingine alisema, udhaifu huo wa kisheria ndiyo unafanya wawekezaji katika sekta ya madini kuingiza hata wafanyakazi na vyakula kutoka nje badala ya kununua nchini.

Alisema kama wawekezaji katika makampuni ya madini yangetumia malighafi, nguvu kazi na hata kununua mahitaji mengine muhimu kama chakula kutoka nchini, nchi na wananchi wangeweza kunufaika.

"Utakuta kwa mfano, Kahama wawekezaji badala ya kununua kuku kwa wananchi wa vijiji vya pale, wao wanaagiza kutoka nje, hili nalo ni tatizo," alisema.

"Lakini kitu kingine ni kwamba, wananchi wenyewe wanapaswa kuandaliwa kuweza kupata fursa hizi, maana swali linaweza kuja wananchi wenyewe wamejiandaa kuzitumia fursa hizo?"

Alisema makampuni makubwa ya madini karibu yote ni ya kigeni na kuongeza kwamba ni vema kukawepo utaratibu ambao utahusisha Watanzania kuwa wanahisa katika migodi mikubwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara, William Shelukindo, alipoulizwa jijijini Dar es Salaam jana katika ofisi za Bunge, alisema kamati itatoa taarifa yake rasmi kwenye kikao kijacho cha Bunge.

Shelukindo alisema ndani ya ripoti hiyo, itaeleza kwa kina nini cha kufanya ili kufanya madini yanufaishe zaidi nchi na kwamba wabunge wa kamati hiyo na wengine wataweza kuchangia kwa uwazi bungeni.

Ripoti hiyo ya uwekezaji ya mwaka 2007, Tanzania inaonekana licha ya kuwa na utajiri wa madini bado haijaweza kunufaika kutokana na mipango iliyo wazi.
 
Nadhani huu ni mwanzo mzuri ingawa sijui kama JK,EL, na Rostam Aziz watakubali kitumbua chao kuingia mchanga! yangu macho
 
Walisubiri mpaka ripoti ya Dunia kuhusu uwekezaji ktk sekta ya madini ndipo waamke usingizini? Hii bado danganya Toto Juzi tu EL amekaririwa akisema mkataba wa madini wa Buzwagi hauna hitilafu hata kama ungesainiwa hapa Bongo.

Hata kama sheria itabadilishwa bado kina Karamagi watajirekebishi vifungu vya mikataba abayo tayari imeandaliwa na wataalamu wa sekta hiyo kwa maslahi yao Binafsi.
Suala muhimu hapa ni watu kama karamagi kuachia madaraka kwanza na kuwaachia watu waadilifu kushika nyadhifa nyeti.

Mabadiliko hayo ya uongozi ndio sasa yaendane na mabadiliko ya sheria za madini.
Vinginevyo sheria zitabadilishwa halafu bado viongozi wasio waadilifu watazipindisha kwa maslahi yao
 
..kwani walikuwa wapi kuona haya leo?

..wao si ndo wako na wananchi kwa karibu zaidi?

..kwahiyo walikuwa wamepumbazwa mazingaombwe au?

..hawa wanataka chapwa bakora!
 
Nadhani huu ni mwanzo mzuri ingawa sijui kama JK,EL, na Rostam Aziz watakubali kitumbua chao kuingia mchanga! yangu macho

Mwafrika wa kike,

Kadiri muda unavyoenda utagundua issue kwenye mikataba ya madini ni sheria iliyotungwa na bunge na wala sio Karamagi kama watu wanavyolazimisha!!!

"Tatizo kubwa ni sheria, jambo la muhimu ni kuhakikisha sheria zinafanyiwa mabadiliko mara kwa mara si kuacha sheria ikae, sasa hivi tatizo hilo linafanya makampuni ya madini kuchimba madini na kuondoka na sehemu kubwa ya faida," alisema.

Mbunge mwingine alisema, udhaifu huo wa kisheria ndiyo unafanya wawekezaji katika sekta ya madini kuingiza hata wafanyakazi na vyakula kutoka nje badala ya kununua nchini.

Alisema kama wawekezaji katika makampuni ya madini yangetumia malighafi, nguvu kazi na hata kununua mahitaji mengine muhimu kama chakula kutoka nchini, nchi na wananchi wangeweza kunufaika.

"Utakuta kwa mfano, Kahama wawekezaji badala ya kununua kuku kwa wananchi wa vijiji vya pale, wao wanaagiza kutoka nje, hili nalo ni tatizo," alisema.

"Lakini kitu kingine ni kwamba, wananchi wenyewe wanapaswa kuandaliwa kuweza kupata fursa hizi, maana swali linaweza kuja wananchi wenyewe wamejiandaa kuzitumia fursa hizo?"

Alisema makampuni makubwa ya madini karibu yote ni ya kigeni na kuongeza kwamba ni vema kukawepo utaratibu ambao utahusisha Watanzania kuwa wanahisa katika migodi mikubwa.

Sasa waambieni wawakilishi wenu kwanini walitunga hiyo sheria ambayo wameiona obsolete ndani ya miaka 9 tu!

Usually try to think outside the box!
 
Mwafrika wa kike,

Kadiri muda unavyoenda utagundua issue kwenye mikataba ya madini ni sheria iliyotungwa na bunge na wala sio Karamagi kama watu wanavyolazimisha!!!

Sasa waambieni wawakilishi wenu kwanini walitunga hiyo sheria ambayo wameiona obsolete ndani ya miaka 9 tu!

Mkataba wa Buzwagi uliandikwa na kusainiwa na bunge au unataka kusema nini hapa? Jaribu kuwa clear kidogo
 
Hawana jipya,ngoja warudi kwenye nyumba kisha wakae kama kamati ya wabunge wa chama,wote watafyata na hawataongea tena.
 
Janja ya Nyani wanatuzuga tu wakishakaa kama kamati watapiga soga mwisho wasiku hakuna kitakachofanyika.

"It ain't over till its over"
 
Walisubiri mpaka ripoti ya Dunia kuhusu uwekezaji ktk sekta ya madini ndipo waamke usingizini?

Naam Wabunge wa CCM walisubiri hiyo ripoti, maana kelele za Watanzania ambao hawakuhitaji kuiona ripoti yoyote kufahamu kwamba mikataba ya uchimbaji wa madini haina maslahi yoyote. Kama kawaida yao walitumia kejeli, dharau na kiburi cha hali ya juu ili kuonyesha mikataba hiyo haina matatizo yoyote!
 
Kadiri muda unavyoenda utagundua issue kwenye mikataba ya madini ni sheria iliyotungwa na bunge na wala sio Karamagi kama watu wanavyolazimisha!!!

Sasa waambieni wawakilishi wenu kwanini walitunga hiyo sheria ambayo wameiona obsolete ndani ya miaka 9 tu!

Usually try to think outside the box!

Hivi Mzee Kilitime unataka kuniambia kwamba Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huwa linatunga sheria au huwa linatumika kama rubber stamp kupitisha hizo sheria? How many times baada ya serikali kugundua kwamba kuna upinzani mkubwa sana kuhusu baadhi ya miswaada ya sheria wamekuwa wakiwaita wabunge wa CCM na kuwaweka sawa ili wasipinge kupitishwa kwa hizo sheria ambazo mara nyingi zimekuwa zikitungwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya serikali na siyo kwa ajili ya maslahi ya umma/Taifa!

Kwa mtazamo wangu ni kwamba sheria zinazotungwa na serikali na then kupitishwa na Bunge siku zote hazipo kwa maslahi ya umma bali kwa maslahi ya walio serikalini. Kwa hiyo watu wa kulaumiwa ni wabunge wa CCM ambao wamekuwa wakiburuzwa na utii kwa chama chao kwa kufuata kile kilichoamuliwa na serikali. Siku zote ukiwasikiliza wabunge wa CCM kwenye debate za budget au miswaada ya sheria, utasikia anaanza kwa kutoa kasoro kibao ikiwa ni pamoja na kuonyesha wazi kwamba hakubaliani na bajeti au mswaada huo, halafu mwisho wa kuchangia utamsikia anasema anaunga mkono kwa 100%, huo kama siyo unafiki wa nidhamu ya chama ni nini? Mhe Seleli alimuwakia Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini na Waziri wa Miundombinu wakati wa kujadili bajeti ya 2007/08. Baada ya hiyo session wabunge wa CCM waliitwa kuwekwa sawa, baada ya hapo hatukumsikia tena Seleli akiongea kwenye kikao hicho mpaka Bunge lilipoahirishwa.

Kwa kifupi ni kwamba Bunge la sasa kuwa na wabunge wengi wa CCM kunalifanya likose nguvu, heri hata ya kurudi kipindi kile cha Bunge la chama kimoja maana enzi hizo hakukuwa na swala la kuwekana sawa au kujadili hoja kwa kuangalia itikadi za chama. Angalia jinsi ambavyo hoja ya Zitto ilivyojadiliwa kiitikadi kiasi kwamba hata ukisoma hansard unaweza kupata kichefuchefu maana hata huwezi kuelewa wawakilishi wetu walikuwa wanatetea nini. Matokeo yake ndiyo haya ambayo sasa yamelepekea kuvuja kwa mkataba wenyewe na baada ya moto kuwaka kila mtu akawa anajisemea la kwake. No wonder mpaka leo hii Zitto hajapewa barua ya kusimamishwa maana inawezekana Spika na Katibu wa Bunge hawajui watoe sababu zipi za kumsimamisha. Mpaka leo hii Spika Sitta hajasema wazi wazi sababu za kumsimamisha Zitto. Mama Makinda alijikanyaga akasema hoja ni safi, tatizo lilikuwa ni lugha, LUGHA GANI???? Ina maana kumwambia mtu muongo au kadanganya kuna neno jingine zaidi ya hilo? Ukifuatilia sana maswala ya Bunge letu unaweza kupata kichefuchefu na hasa wachangiaji wa hoja wanapokuwa wanachangia huku wakiwa wametanguliza msimamo wa kichama/kiitikadi!!!

Katika Bunge lolote duniani, serikali huwa iko comfortable pale inapokuwa na numbers za kutosha kudominate votig decision. Lakini kwa baadhi ya nchi, wabunge wako more independent kiasi kwamba hawaingiliwi na serikali. Tofauti na Bunge letu ambapo mbunge akicheza kinyume na matakwa/itikadi ya chama chake basi asubiri kushukiwa na rungu la kutopitishwa kwenye mchakato wa kuteuliwa kugombea ubunge. Hata kama utashinda kwenye kura za maoni bado unaweza kupigwa panga vile vile na huna mahali pa kwenda kushitaki.
 
Mimi naamini mikataba yote itabadilishwa katika kipindi kisichozidi miaka mitatu kinyume cha hivyo ni CCM kuanguka na kufa kifo cha mende au yatatokea yale yanayotokea Nigeria.
 
Mimi naamini mikataba yote itabadilishwa katika kipindi kisichozidi miaka mitatu kinyume cha hivyo ni CCM kuanguka na kufa kifo cha mende au yatatokea yale yanayotokea Nigeria.

Umemsikia lakini Lowassa anavyosema kwamba Buzwagi ni SAFI! Lowassa huyo huyo ukimuuliza Richmonduli atakuambia nayo ni SAFI! Huyo ni Waziri Mkuu ndiyo anasema hayo, je, unategemea atabadilisha hiyo mikataba?

Migodi inayozalisha sasa imekuwa kwenye production kwa zaidi ya miaka 5, na si ajabu life span ya hiyo migodi inaelekea ukingoni. By the time wanakubali kubadilisha mikataba, madini yote yalishaisha na hakuna lolote la maana ambalo Tanzania itafaidi baada ya kubadilisha hiyo mikataba!
 
Hawa wabunge wamesubiri watu hao hao wanaofaidi maliasili zetu kutuambia kuwa hazitunifaishi ndio wafanye changes...? Hiki nacho kiini macho tuu.
 
Umemsikia lakini Lowassa anavyosema kwamba Buzwagi ni SAFI! Lowassa huyo huyo ukimuuliza Richmonduli atakuambia nayo ni SAFI! Huyo ni Waziri Mkuu ndiyo anasema hayo, je, unategemea atabadilisha hiyo mikataba?

Hivyo ndivyo vitumbua vinavyotajwa na wana JF, akiambiwa yeye ni FISADI anakataa anaomba ushaidi anatishia kwenda mahakamani bila kujua ukitetea hata mkataba wenye UFISADI ndani yake nawe ni FISADI.

Kwani yeye hana macho, hawezi kusoma na kuelewa? Nini kinamfunga macho? Jibu-Kitumbua
 
Kinachonochanganya ni majibu ya serikali bungeni na viongozi wa ngazi zote kinachosemwa leo na kesho yake ni vitu viwili tofauti,sijui tatizo lao hasa nini? kwani wakibanwa vizuri wanakubali kuwa kuna tatizo na wanatoa kauli tofauti na walizo toa mwanzo,hapa ndio naliona tatizo kubwa.
 
...hawa wapuuzi kweli kweli kazi yao ngono tuu kule dodoma na mavitambi ya bia,wapumbavu sana hawa!
 
Mwafrika wa kike,

Kadiri muda unavyoenda utagundua issue kwenye mikataba ya madini ni sheria iliyotungwa na bunge na wala sio Karamagi kama watu wanavyolazimisha!!!

Sasa waambieni wawakilishi wenu kwanini walitunga hiyo sheria ambayo wameiona obsolete ndani ya miaka 9 tu!

Usually try to think outside the box!

Kilitime, Mbona unataka kutuchanganya hapa!! Toka lini sheria na mkataba vikawa kitu kimoja?

Serikali imesema mikataba ni siri. Wewe unasema tuwaulize wabunge wetu kwa nini walitunga sheria za madini. Kama hilo unalosema ni sahihi, kulikuwa na haja gani ya wabunge wa upinzani kuhoji uhalali wa mikataba ya madini wakati wenyewe ndio wahusika wakuu katika hilo sakata??? (i.e., waliotunga sheria=mikataba)
 
Kilitime, hivi bunge ndio lilipitisha sheria zinazofanana na yale tulioyaona kwenye mktaba wa buzwagi. Bunge ndio liliweka kiwango cha pesa kinachopaswa kwenda kwenye halmashauri za wilaya (i.e., kisizidi let say $200,000 kwa mwaka. Bunge ndio liliweka sheria inayosema mrahaba usizidi asilimia 5%

Naomba unijibu tafadhali.
 
Back
Top Bottom