Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hiyo. Wale wanaotaka kwa lugha ya Kiingereza pia ipo, nitawawekea kama itahitajika.
 
Ushukuriwe Mkuu. Ya kiingereza itasaidia. Ombi lingine. Wale walioisha ipitia watuelezee ni vifungu vipi vina matatizo ili tuanzie hapo.
 
Mama Nagu lazima aitetee katiba maana ndiyo inampa kibri na ulaji; siku akijikuta yuko nje ya mfumo ndo atajua kuwa katiba ina matatizo.
 
Viongozi wanapaswa kujua kuwa katiba sio mali yao ila ni mali ya wananchi na kama wenye mali wanataka ibadilishwe hawana budi kutii maamuzi ya mwenye mali tatizo hapa ni kuwa wananchi wanajisahau kuwa wao ndio wamiliki halali wa nchi hii na sasa wanawaachia viongozi mafisadi waimiliki kwa niaba yaoa kitu ambacho mimi nakiona kama nia igizo la ze comedy....

Katiba yetu haikidhi mahitaji ya sasa kama tunayo katiba inasema kuwa nchi hii ni ya ujamaa na kujitegemea halafu waziri wa sheria anadhubutu kujitopkeza na kusema kuwa katiba inakidhi mahitaji ya sasa huu ni unafiki mkubwa sana .

Wasingoje hadi walazimishwe na nguvu ya umma kuibadilisha katiba wafanye sasa wangali na nguvu wasiongoje hadi watakapojikuta hawana nguvu ndipo waanze kusema mara ohoo sikusema kuwa katiba sio mbaya....
 
Ushukuriwe Mkuu. Ya kiingereza itasaidia. Ombi lingine. Wale walioisha ipitia watuelezee ni vifungu vipi vina matatizo ili tuanzie hapo.

Haya Fundi,
Katiba kwa lugha ya Kiingereza hii hapa.
Ibara ya 74 (1) inasema kwamba raisi wa nchi ndiye anayeteua tume ya uchaguzi. Sasa wapinzani ndio wanalalamikia kipengele hiki, kwa mantiki kwamba,

1. Kama mwenyekiti wa tume anateuliwa na raisi, ikitokea raisi (ambaye aghalabu huwa mwenyekiti wa sisiemu) akashindwa uchaguzi, je mwenyekiti wa tume ambaye ndiye hutangaza matokeo atakata tawi alilokalia? Kwa maana nyingine atatangaza kushindwa kwa mwajiri wake?

2. Kwa nini bunge lisiachiwe kazi hii ya uteuzi wa tume ya uchaguzi?
Uchambuzi utaendeleaa.......
 
Attachments

Ndio yale yale ya Kenya!
 
Ndio yale yale ya Kenya!

Kabisa mkuu, akina Kivuitu wanatokana na makosa haya ya kikatiba. Tusiporekebisha hili basi tusitarajie kuing'oa sisiemu madarakani kirahisi!
 
Bada ya hiyo quote msemaji wa serikali ndugu mtoto wa Fisadi ana mawazo gani ?
 
Ibara ya (67)1 inasema..
Bila kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yoyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa ama kuteuliwa kuwa mbunge endapo:-
a)ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

b)ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
c)katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Swali:
Kwa sisi ambao hatuna vyama ama hatutaki kujiunga na vyama, ina maana hatuna haki ya kuwa wabunge? Ndipo hapa Mtikila alipoishinda serikali katika kesi yake ya kudai wagombea huru! Kwa nini bunge ambalo ndilo lenye mamlaka ya kurekebisha katiba halitaki kuondoa kipengele hiki onevu?
Katiba bado ina mushkeli!
Irekebishwe!
Itaendelea....>
 
37.-(1)
Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote.

My Take
Sasa, mnapotoa ushauri kwamba raisi amchunguze Mkapa, mnatarajia nini kama katiba yenyewe inamlinda? Ina maana raisi ana mamlaka ya kukataa jambo hata kama lina manufaa kwa jamii, ili mradi tu yeye halimpendezi!
Bado katiba ina mawaa!
Inaendelea....
 
37(3)
Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana na masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi.
(b) Spika wa Bunge au, kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi
(c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.

My Take
Kuna mgongano wa kimaslahi kati ya mihimili ya dola hapo katika vipengele b, na c. Kwamba, spika ni kiongozi wa bunge (Legislature), na Jaji mkuu anahusika na tafsiri za sheria kupitia mahakama (Judiciary) ambao ni mhimili wa pili wa dola (state).

Sasa basi, ikiwa mmojawapo wa hao makaimu akakaimu nafasi ya raisi ambaye ni kiongozi mkuu wa serikali (Executive) pale raisi na makamu wake wanapokuwa hawapo ofisini, anakuwa anavaa kofia mbili, kitu ambacho ni kinyume na utawala bora. Na hii ilishatokea sana enzi za utawala wa Mkapa, ambapo spika Msekwa alikuwa anakaimu nafasi ya uraisi.
Katiba ina mawaa.
Itaendelea.....
 
Serikali yadai katiba ya Tanzania haina kasoro
Na James Magai

Asante Lunyungu, wakuu jukwaani. Idimi utanisamehe kwa bump
Hoja fupi, tuendelee chini ya quotes...

�Kwa mfano tulipotoka serikali ya kikoloni na kwenda serikali ya uhuru tulitunga katiba mpya. Pia tulipoachana na Malkia wa Uingereza tulitunga katiba mpya na baada ya kuwa na Muungano tukawa na katiba mpya tuliyonayo sasa,� alibainisha Dk Nagu.

Kwa hiyo ina maana tumetunga katiba mpya mara tatu-basi inawezekana mara ya nne. Kwa kweli kuna mengi katika hili,my take: Pesa zinawasumbua vichwa, incha za mapanga zitangolewa-Sioni kwa sababu gani lisijadiliwe bila visingizio,kwani njia mbadala za kufanya hivyo vikifuatwa, ki-katiba, baya lipo wapi? Mabadiliko kama haya mara nyingi yanahusishwa na vurugu-na hiyo ni propaganda ya waliobeba mapanga. Ambacho hakieleweki ni waziri kuingiza itikadi hapo"lakini akaonya kuwa ni sheria kuu ambayo ikitikiswatikiswa inaweza kusababisha nchi kuondokana na amani" -my take-na kuwa kama chombo hicho cha propaganda. Ana balance Vipi kama Waziri wa Sheria? Anyways sio kuwaondoa kwenye mada bali kutoa maoni na hoja fupi.

Hivi karibuni vyama vya upinzani nchini vilifanya mkutano na vyombo vya habari na kutoa tamko kuwa mwaka 2008 ni mwaka wa mapambano ya kukamilisha agenda ya kutungwa kwa katiba mpya na kwamba tayari wamekwisha kamilisha rasimu ya katiba mpya ambayo wataanza kuipeleka kwa wananchi ili kupata maoni kabla ya kluishinikiza serikali kuipitisha.

Nimeona docs nyingi za Katiba ya Tanzania humu Jukwaani, Je kuna ambaye anayo hiyo mpya-(inayotarajiwa)-kama vielelezo nilivyovikuza hapo juu? Kuna ambaye ataweza kutuletea hapa?

Kwa muda mrefu wapinzani wamekuwa wakidai kuwa Katiba ya Tanzania ina mapungufu hivyo inatakiwa kuandikwa upya lakini serikali imkuwa kikipinga hadi bungeni.

Hayo mapungufu hayawezi kurakabishwa bila ya kuandika Katiba mpya?

I submit
Asante
 
Jamani, Katiba mnayoangalia imefanyiwa marekebisho baadhi ya vipengele hapo juu havipo tena. Nadhani mabadiliko ya mwisho ni yamwaka 2005 au 2000.
 
Wakuu,

Mimi nitasema tu haki yangu kama haingiliwi tutaendelea(na Katiba tuliyonayo). Katiba Mpya wanayodai wapinzani iko wapi? Sasa mbona na wao wanaanza mazingaombwe?

Hivi karibuni vyama vya upinzani nchini vilifanya mkutano na vyombo vya habari na kutoa tamko kuwa mwaka 2008 ni mwaka wa mapambano ya kukamilisha agenda ya kutungwa kwa katiba mpya na kwamba tayari wamekwisha kamilisha rasimu ya katiba mpya ambayo wataanza kuipeleka kwa wananchi ili kupata maoni kabla ya kluishinikiza serikali kuipitisha.
Au ndio kishinikizo kwanza halafu Katiba?
?????
 
Jamani, Katiba mnayoangalia imefanyiwa marekebisho baadhi ya vipengele hapo juu havipo tena. Nadhani mabadiliko ya mwisho ni yamwaka 2005 au 2000.

Hiyo iliyofanyiwa marekebisho inapatikana wapi? Hasa tukizingatia kuwa inatakiwa kuwa accessible kwa wananchi wote!
 
Asante Lunyungu, wakuu jukwaani. Idimi utanisamehe kwa bump
Hoja fupi, tuendelee chini ya quotes...

Kwa hiyo ina maana tumetunga katiba mpya mara tatu-basi inawezekana mara ya nne. Kwa kweli kuna mengi katika hili,my take: Pesa zinawasumbua vichwa, incha za mapanga zitangolewa-Sioni kwa sababu gani lisijadiliwe bila visingizio,kwani njia mbadala za kufanya hivyo vikifuatwa, ki-katiba, baya lipo wapi? Mabadiliko kama haya mara nyingi yanahusishwa na vurugu-na hiyo ni propaganda ya waliobeba mapanga. Ambacho hakieleweki ni waziri kuingiza itikadi hapo"lakini akaonya kuwa ni sheria kuu ambayo ikitikiswatikiswa inaweza kusababisha nchi kuondokana na amani" -my take-na kuwa kama chombo hicho cha propaganda. Ana balance Vipi kama Waziri wa Sheria? Anyways sio kuwaondoa kwenye mada bali kutoa maoni na hoja fupi.

Nimeona docs nyingi za Katiba ya Tanzania humu Jukwaani, Je kuna ambaye anayo hiyo mpya-(inayotarajiwa)-kama vielelezo nilivyovikuza hapo juu? Kuna ambaye ataweza kutuletea hapa?

Hayo mapungufu hayawezi kurakabishwa bila ya kuandika Katiba mpya?
I submit
Asante

Asante kwa ku-submit mkuu, tunapokea!
Katiba niliyo nayo (hard copy) imechapwa mwaka 2003 na mpiga chapa mkuu wa sirikali, Dar Es Salaam na niliinunua pale UDSM duka la vitabu. Haina marekebisho muhimu ambayo tunayalilia!Sirikali inakataa hata kufanya marekebisho muhimu ambayo wapinzani wanadai, ndio maana wapinzani wanataka katiba yetu iandikwe upya. Mfano, mwaka juzi, Mtikila (Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha DP) aliishinda sirikali katika kesi ya kudai mgombea huru. Hata mwaka jana, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi (Bw R R Kiravu, kama nitakosea jina mnisamehe) alikataa kutumia hukumu ya mahakama kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi mdogo wa ubunge kule Tunduru na kuwakashfu wapinzani, akidai kwamba utaratibu huo utatekelezwa mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu!
Huu mie naita ni wendawazimu uliopita kiwango. Pia wapinzani wanadai raisi apunguziwe madaraka, sirikali haitaki kukubali hili. Tuieleweje? Bado watu watataka katiba mpya iandikwe, kama sirikali haitaki kufanya haya marekebisho madogo madogo lakini muhimu.
Napingana na Nagu kwa kila hali.
Tuendelee na mjadala!
 
Back
Top Bottom