Hivi kweli mnataka mabadiliko ya Katiba na mko tayari kulipia gharama yake?
There is nothing to fear but fear itself! Katiba ina viraka vingi, nadhani ni muda muafaka ikafanyiwa comprehensive review.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi kweli mnataka mabadiliko ya Katiba na mko tayari kulipia gharama yake?
Ushukuriwe Mkuu. Ya kiingereza itasaidia. Ombi lingine. Wale walioisha ipitia watuelezee ni vifungu vipi vina matatizo ili tuanzie hapo.
Ibara ya 74 (1) inasema kwamba raisi wa nchi ndiye anayeteua tume ya uchaguzi. Sasa wapinzani ndio wanalalamikia kipengele hiki, kwa mantiki kwamba,
1. Kama mwenyekiti wa tume anateuliwa na raisi, ikitokea raisi (ambaye aghalabu huwa mwenyekiti wa sisiemu) akashindwa uchaguzi, je mwenyekiti wa tume ambaye ndiye hutangaza matokeo atakata tawi alilokalia? Kwa maana nyingine atatangaza kushindwa kwa mwajiri wake?
2. Kwa nini bunge lisiachiwe kazi hii ya uteuzi wa tume ya uchaguzi?
Uchambuzi utaendeleaa.......
Ndio yale yale ya Kenya!
Serikali yadai katiba ya Tanzania haina kasoro
Na James Magai
�Kwa mfano tulipotoka serikali ya kikoloni na kwenda serikali ya uhuru tulitunga katiba mpya. Pia tulipoachana na Malkia wa Uingereza tulitunga katiba mpya na baada ya kuwa na Muungano tukawa na katiba mpya tuliyonayo sasa,� alibainisha Dk Nagu.
Hivi karibuni vyama vya upinzani nchini vilifanya mkutano na vyombo vya habari na kutoa tamko kuwa mwaka 2008 ni mwaka wa mapambano ya kukamilisha agenda ya kutungwa kwa katiba mpya na kwamba tayari wamekwisha kamilisha rasimu ya katiba mpya ambayo wataanza kuipeleka kwa wananchi ili kupata maoni kabla ya kluishinikiza serikali kuipitisha.
Kwa muda mrefu wapinzani wamekuwa wakidai kuwa Katiba ya Tanzania ina mapungufu hivyo inatakiwa kuandikwa upya lakini serikali imkuwa kikipinga hadi bungeni.
Au ndio kishinikizo kwanza halafu Katiba?Hivi karibuni vyama vya upinzani nchini vilifanya mkutano na vyombo vya habari na kutoa tamko kuwa mwaka 2008 ni mwaka wa mapambano ya kukamilisha agenda ya kutungwa kwa katiba mpya na kwamba tayari wamekwisha kamilisha rasimu ya katiba mpya ambayo wataanza kuipeleka kwa wananchi ili kupata maoni kabla ya kluishinikiza serikali kuipitisha.
Jamani, Katiba mnayoangalia imefanyiwa marekebisho baadhi ya vipengele hapo juu havipo tena. Nadhani mabadiliko ya mwisho ni yamwaka 2005 au 2000.
Asante Lunyungu, wakuu jukwaani. Idimi utanisamehe kwa bump
Hoja fupi, tuendelee chini ya quotes...
Kwa hiyo ina maana tumetunga katiba mpya mara tatu-basi inawezekana mara ya nne. Kwa kweli kuna mengi katika hili,my take: Pesa zinawasumbua vichwa, incha za mapanga zitangolewa-Sioni kwa sababu gani lisijadiliwe bila visingizio,kwani njia mbadala za kufanya hivyo vikifuatwa, ki-katiba, baya lipo wapi? Mabadiliko kama haya mara nyingi yanahusishwa na vurugu-na hiyo ni propaganda ya waliobeba mapanga. Ambacho hakieleweki ni waziri kuingiza itikadi hapo"lakini akaonya kuwa ni sheria kuu ambayo ikitikiswatikiswa inaweza kusababisha nchi kuondokana na amani" -my take-na kuwa kama chombo hicho cha propaganda. Ana balance Vipi kama Waziri wa Sheria? Anyways sio kuwaondoa kwenye mada bali kutoa maoni na hoja fupi.
Nimeona docs nyingi za Katiba ya Tanzania humu Jukwaani, Je kuna ambaye anayo hiyo mpya-(inayotarajiwa)-kama vielelezo nilivyovikuza hapo juu? Kuna ambaye ataweza kutuletea hapa?
Hayo mapungufu hayawezi kurakabishwa bila ya kuandika Katiba mpya?
I submit
Asante