Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Mkuu
Wananchi ndo wakulaumiwa, wananchi wakiipa kura upinzani 90% na ccm 10% nafikiri wataiba wee mpaka watashindwa kuiba kura na hatimaye upinzani kushika hatamu. Sijasoma katiba hasa kwenye hiyo kipengele sijui inasema je?

kwa vile unaweza kuandika ina maana unaweza kusoma; so usome utujulishe kinasemaje.
 
Ninataka kuanzisha thread ya kujadili Katiba ya Tanzania. Nina kopi mbili za katiba hiyo, moja ni ya kiswahili, na moja ni ya kiingereza. Kwa bahati mbaya, kama tulivyoona kwenye hotuba ya bajeti, katiba hizo mbili zinatoa tafsiri zinazotofautiana katika baadhi ya vifungu vyake. Je ni lugha ipi itumike katika kujadili katiba hiyo kwa ufanisi?
 
Mkuu kama tusipoweza jivunia lugha yetu bungeni basi ndio tumedoda Utumwani..
 
Katiba yenyewe ipo katika lugha gani ?
 
Mkuu kama tusipoweza jivunia lugha yetu bungeni basi ndio tumedoda Utumwani..
Unajua kaka, katiba yetu inahitaji kuchambuliwa kwa kina kwa sababu ina mapungufu mengi sana. Nadhani kijamvi hiki kinaweza kusaidia kuibua mawazo mazuri ya kuiboresha katiba yetu. Sasa nilipokuwa najiandaa kuanzisha thread ya namna hiyo nikagundua kuwa tukichambua ile version ya kiswahili inawezekana tukawa tunakosea kwa sababu inaweza ikawa ina tofauti na version ya kiingereza.

Kwa bahati mabaya baada ya kweka poll, nimeshindwa kuifanyia mabadiliko, nadhani ningeongeza option ya lugha zote. baada ya kufikiri, nimeona ni afadhali niwe nakopi vifungu vya katiba kutoka kila version ya (kiswahili na kiingereza) na kuviweka hapa ili tuwe tunaviangalia kwa pande zote mbili.
 
Kuna nakala iliyoandikwa kiswahili, na vile vile ipo nakala iliyoandikwa kwa kiingereza!!!

Kama kulikuwa na umuhimu wa kuwa na nakala za Kiswahili na Kiingereza, lugha rasmi Tanzania, then kuna umuhimu mjadala uwe katika lugha hizo hizo.
 
Unajua mkuu wangu wenzetu huku hata mtu hana elimu kubwa, mtegemea zaka anayeishi ktk project anazijua haki zake kwa sababu katiba yao ipo ktk lugha yao ya asili. Ni majuzi tu mshikaji wangu alikuwa akinambia kwamba asilimia 50 ya viongozi wa nchi duniani huzungumza lugha zao wakiwa UN na wale tunazungumza lugha za watu wengine ndio hao nchi maskini duniani.

Hivyo, umaskini unakuja na mengi mkuu wangu kwanza inatakiwa wananchi wako wawe Huru na moja ya Uhuru wao ni kufahamu tamaduni na haki zao..
 
nimefurahi kuona kiswahili kimepewa kipaumbele kwenye poll hapo juu. Watanzania wengi hawana kiingereza cha kutosha kuweza kuifahamu katiba pia si muhimu kwa vile tuna lugha yetu..hata hivyo makala nyingi ninazosoma kwenye thread tofauti humu hushindwa hata kuelewa kiswahili kinachozungumzwa na inasikitisha kuona kuwa tunakubali standard ya lugha yetu kuporomoka, au pengine ni mimi tu nnahisi hivyo
 
Kuna haja ya kufunza katiba kwa watanzania wengi zaidi.

Nnacho amini ni kuwa watanzania wengi hasa wa rika la chini hawaijui katiba hata kijuujuu tu.

Kichunguu ukituwekea vipengele kwa lugha zote mbili utasaidia kuelimisha wengi tu

I am ready for katiba 101
 

Uko sawa mkuu,

Tutasingizia Kiingereza sana, lakini hata kiswahili hatukijui. Kibaya zaidi tunajidai kukumbatia Kiswahili wakati bado hata hakijapata msamiati mkubwa. Kibaya zaidi ya yote hayo, tunakumbatia vyetu nusu nusu, kama kweli tunataka kukumbatia vyetu tuachane na mambo ya katiba zilizoandikwa, katiba ambazo mpaka leo misingi yake ni sheria za Waingereza na Warumi.

Sikatai kuzungumza Kiswahili katika mashauri haya kutasaidi wengi kufuatilia, lakini tunapotaka kushirikisha wengi tusisahau wengine watakaotafuta misamiati katika kiswahili na kuikosa na hawa tusiwalazimishe kujadili Kiswahili.

Kwa kuelewa hili, ndiyo maana katiba ipo katika lugha mbili, na ndiyo maana mjadala unapaswa kuendeshwa katika lugha zote, kila mtu awe na uhuru wa kuchagua.
 
Athari za kutawaliwa ni mbaya.

Tuliandika Sheria na Kila kitu chetu kwa Lugha ya Kigeni na baadae tukasema tukuze vya kwetu. Katiba ya Kiswahili ni Tafiri ya ile ya Kiingereza ambayo msingi wake ni yale tuliyoyaiga kwa mkoloni. Hata wahauri wa mwanzo kabisa wa Serikali ya Mwalimu walikuwa vijana wa Malkia na ndio walioandaa katiba ya mpito ya Tanganayika (Interim Constitution) na pia makubaliano ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar yaliyokuja kuwa Sheria ya Muungano na baadae kuingizwa katika katiba ya sasa.

Kimsingi, yaliyomo katika Katiba ni haki na wajibu wa raia, yanapaswa kueleweka kwa lugha ambayo raia anaifahamu yaani Kiswahili.Yamkini ilipaswa hata sheria zote za nchi ziwe kwa kiswahili.

Hata hivyo, japo kuwa lugha ya Mahakama ambayo ndicho chombo kinachosimamia haki za raia ni Kiswahili na Kiingereza, hukumu zote katika mahakama za juu zinapaswa kuandaliwa kwa lugha ya Kiingereza na hapo ndipo hata mantiki ya kutumia lugha ya kiswahili inapotea kabisa.

View attachment KATIBA 00A(SWAHILI)[1].pdf


View attachment 11644
 
Tunaanza na DIBAJI - Preamble




KISWAHILI




-------------------------------------------------------------------------------------------------- KIINGEREZA[/SIZE][/U]




Maoni Yangu

  1. Ni lazima Katiba hii ibadidlishwe kuondoa neno ujamaa katika dibaji hiyo na sehemu nyingineyo yoyote ya katiba; nitakuwa nalionyesha kwa rangi nyekundu kila tutakapolifikia. Siyo kweli kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa kwa vile imeshamiri ubepari. Tunaikosesha heshima katiba yetu kwa kuweka vifungu vya uongo, yaani ambavyo siyo vya kweli.
  2. Dibaji ya kiingereza inasema kuwa Tanzania ni "secular state" yaani haufungamani na dini yoyote, lakini tafsiri ya kiswahili haikonyesha hivyo. Sijui wenzangu mnaonaje hilo, je lilifanyika makusudi.
  3. Dibaji ya katiba hii inaonyesha kuwa Tanzania tunafuata utawala wa kidemokrasia uliojengwa kwa mihimili mitatu isiyoingiliana: Serikali, Bunge, na Mahakama. Halafu bunge linawakilisha wananchi likiwa na wajumbe waliochaguliwa na wananchi hao:

    Je ni Kweli kuwa
    • Bunge letu linawakilisha wananchi kama katiba inavyotaka iwapo kuna wajumbe ambao hawakuchaguliwa na wananchi? Kwa sasa bunge la Tanzania lenye wajumbe 325, waliochaguliwa na wananchi ni 231 tu, sawa na asilimia 71. Je bunge hilo kweli linafanaya kazi kwa niaba ya wananchi?
    • Serikali haiingiliani na bunge huku ikiteua wabunge kuwa mawaziri, na veile vile rais kuteua wabunge wengine?
    • Je ni kweli kuwa serikali inawajibika kwa bunge huku waziri mkuu akiwa na sauti ya mwisho bungeni na wakati mwingine hufikia hatua ya kuwakemea wabunge?
 
 
Ndugu Mzizi Mkavu

Siyo kwamba nachukia ujamaa, lengo langu wakati naannzisha tthread hii ni kuangalia upungufu wa katiba yetu ili tupate mawazo ya kuinyoosha. Kuweka ndani ya Katiba kuwa tunajenga taifa la kijamaa ilhali tunajua kuwa hatufanyi hivyo, ni ama tudharau na kukiuka katiba yetu makusudi, au katiba hiyo siyo ni kitu serious.

Ningependa kila kilichoko ndani ya katiba kiwe ni kitu sahihi; kwa hiyo neno ujamaa liondoplewe tu. Katiba imeshasema tunajenga taifa lenye misingi ya haki kwa watu wote; hilo ni lengo linalotosha kabisa kuliko kuongeza ujamaa ambao siyo kweli.
 

Wazo lako ni zuri Kichuguu, lakini ingependeza zaidi kama ungeweka attachment ya katiba hiyo kwa hizo lugha mbili ili wale ambao hawajawahi kuziona wapate fulsa hiyo kupitia hapa. Au mtu yeyote aliye na versions hizo angetuletea jamvini kutujuvya. Sio kila mtu anajua Katiba. Ama kusema kweli, hata mimi binafsi nasikia tu lakini sijapata kuzitia machoni au hata kuzigusa. Kwa Tanzania ni rahisi zaidi kuiona katina ya CCM kuliko kuliko ya Nchi. Katiba ya TANU niliwahi kuwa nayo japo sijui iliko sasa hivi baada ya mtu mmoja kuiazima nikasahau kumwandika jina, naye aka-take advantage kuingia nayo mitini.

Ni kweli wakati mwingine tunaswagwa kwa sababu ya ujinga wetu wa kutojua haki zetu kiasi kwamba tunadhani mwanasheria ndio wajibu wake zaidi. Kama mtu akijua kwamba ulinzi wake umo katika katiba pengine hata watu wa serikali za mitaa wasingewaonea sana wananchi. Hata tunaambiwa na Misahafu kwamba Neno na likae kwa wingi mioyoni mwenu, asije Shetani akawadanganya kwa kutokujua kwenu nini Mungu wenu anayataka kutoka kwenu.
 
Mahakama iliwahi kusema katika kesi ya Director of Public Prosecutions v. Daudi Pete [1993] TLR 22 (CA) katika ukurasa wa 23 kama ifuatavyo: "As the Constitution of the United Republic of Tanzania is established in the Kiswahili language, the controlling version in interpreting the Constitution is the Kiswahili and not the English version."

Kwa hiyo kama mnatafsiri Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, msitumie version ya Kiingereza, tumieni ya Kiswahili!
 
Kichunguu, nimependa wazo lako na kitu kizuri sana kujadili katiba ambayo ndiyo siyo tu sheria mama bali mwongozo wetu sote. Ila kwenye upande wa poll, maelezo yake yana utata kwani mtu anayeingia mara moja hawezi kujua kama unalenga huu mjadala wa humu jamvini bali mijadala ya kawaidia mitaani.

Kuhusu mapungufu uliyoonesha kwenye utangulizi, nakubaliana na wewe kabisa.
1. Tz siyo nchi ya kijamaa ki-uhalisia. Kilichoandikwa kwenye katiba siyo kinachoendelea. Kwa hiyo tunahitaji kubadili hiyo dhani ili tusionekane tunafanya mzaha na katiba.
2. Bunge letu lina wabunge wasiochaguliwa na wananchi. Hivyo ama katiba ibadilishwe ili tuwape nafasi au tuwaondoe.
3. Hiyo omission ya neno circular state ni hatari sana. Kwa hiyo ni muhimu ama katiba mpya itungwe kwa kiswahili ili baadaye itafsiriwe ka lugha nyingine au watu wa kutafsiri wawe makini sana. Hii dhana muhimu na kwa hiyo haikutakiwa kuachwa kwenye toleo la kiswahili!
 

Sawa mkuu lakini kipi kilitangulia? Hili ni muhimu ili tuweze kujua original intention ya waandishi. Vinginevyo tunaweza kuparamia treni kwa mbele. Ingawa katika misingi ya kisheria hakuna tatizo ila katika kujadili nadhani tuanze na kile kilichotangulia.
 

Asante sana ndugu Bucha na nanihii kwa ufafafunuzi nzuri kuhusu lugha ya katiba.

hata hivyo baadaye niliamua kuwa kuwa itakuwa ni vizuri tukaziangalia zote mvbili hasa ukizingatia kuwa lugha zote ni official languages hapa kwetu. Nitakuwa naleta version zote mbili kwa kila kifungu nitakachokuwa naongelea; itasaidia pia kuona hata mapungufu katika tranalation baina ya lugha hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…