Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Kwa tafsiri hii ya ujamaa katika katiba yetu, sioni kama ina tatizo kwa neno ujamaa kuendelea kuwapo kwenye katiba:

ndugu yangu,

Unachoona kwenye definition hiyo ya "Ujamaa" ni kiraka. Nimeangalia tena kwenye definitions za maneno yaliyotumika katika katiba ya kiingereza, hakuna maana ya "Socialism" ila wamerudia tena "Ujamaa" and "Ujamaa na kujitegemea" kwa kiswahili vile vilem wakati maneno yale hayakutumika katika hiyo katiba ya kiingereza.

Neno Ujamaa au Socialism linajulikana na kuna vitabu vingine vinavyoongelea mfumo wa kijamaa, kwa hiyo kuwa na neno hilo katika katiba halafu tukalipaka rangi nyingine liwe na maana tofautio na linavyojulikana ni makosa, ; hiyo ni kutaka kuchanganya wananchi wasiielewe vizuri katiba yao.
 
Kwa tafsiri hii ya ujamaa katika katiba yetu, sioni kama ina tatizo kwa neno ujamaa kuendelea kuwapo kwenye katiba:

Mhh, hapa kwa kweli nimeachwa solemba. Hii definition ndiyo ya ule ujamaa tuliokuwa tunajenga miaka ya 70? Unaweza kuongelea ujamaa bila kutaja umiliki wa njia kuu za uchumi kuwa chini ya umma? Hapa nahitaji kuelimishwa, nimekwama kabisa!
 
Ule wa miaka ya 70 kwa kiasi fulani ulichanganyika na ukomunisti. Kwa ujumla ukiangalia ibara ya 9 ya katiba (ukiacha kifungu J) tafsiri ya ujamaa bado ni relevant.
 
kama tunatakiwa kunukuu au kutumia katiba iliyoandikwa kwa kiswahili tunapata mashaka kidogo na kutokuwepo kwa maelezo ya kuwa tanzania haifuati dini yoyote! au hapo ndipo 'wadini' wanapopata loopholes?

Suala la wabunge nadhani hakuna tatizo................hata hao wabunge waliochaguliwa na Raisi wako pale kutetea au kwa aajili ya wananchi. So aim ya wabunge wale pia ni sawa na wabunge wengine wenye majimbo.
 
kama tunatakiwa kunukuu au kutumia katiba iliyoandikwa kwa kiswahili tunapata mashaka kidogo na kutokuwepo kwa maelezo ya kuwa tanzania haifuati dini yoyote! au hapo ndipo 'wadini' wanapopata loopholes?

Gaijin, ni kweli katiba haisemi kwamba Tanzania ni nchi isiyofuata dini yoyote. Hata hivyo bado mimi naona hakuna 'loophole' kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya katiba.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
 
kama tunatakiwa kunukuu au kutumia katiba iliyoandikwa kwa kiswahili tunapata mashaka kidogo na kutokuwepo kwa maelezo ya kuwa tanzania haifuati dini yoyote! au hapo ndipo 'wadini' wanapopata loopholes?

suala la wabunge nadhani hakuna tatizo................hata hao wabunge waliochaguliwa na Raisi wako pale kutetea au kwa aajili ya wananchi. So aim ya wabunge wale pia ni sawa na wabunge wengine wenye majimbo.

Kwa maoni yangu hiyo si kweli. Wale wanaweza kutumikia wananchi ila wakiamua kutumikia matakwa ya yule aliyewapeleka bungeni (iwe ni chama au Rais) hawana wa kuwauliza ukilinganisha na wabunge wa majimbo!
 
Gaijin, ni kweli katiba haisemi kwamba Tanzania ni nchi isiyofuata dini yoyote. Hata hivyo bado mimi naona hakuna 'loophole' kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya katiba.

Soma sehemu ya UTANGULIZI (Preamble) ambayo iasema kwamba: KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia, ujamaa na isiyokuwa na dini.

Sasa ukichanganya hiyo sehemu ya UTANGULIZI (Preamble) na Ibara ya 19 (2) huoni kwamba Tanzania ni nchi isiyo na dini?
 
Nadhani swali la kujiuliza ni je dibaji/preamble ya katiba ina nguvu ya kisheria kama ibara za katiba? Ingawa dibaji inatoa mtizamo wa kijumla wa madhumuni ya watunzi wa katiba, sidhani kama ina nguvu ya kisheria kuzidi ile ya ibara za katiba!

Sijui unapotumia maneno "nguvu ya kisheria kuzidi ile ya Ibara za Katiba" unamaanisha nini hapa! Mimi nijuavyo, Katiba inatakiwa isomwe yote kwa ujumla wake na si kushindanisha Ibara au sehemu za Katiba hiyo hiyo!
 
Soma sehemu ya UTANGULIZI (Preamble) ambayo iasema kwamba: KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia, ujamaa na isiyokuwa na dini.

Sasa ukichanganya hiyo sehemu ya UTANGULIZI (Preamble) na Ibara ya 19 (2) huoni kwamba Tanzania ni nchi isiyo na dini?

Hiyo Preamble ya kiswahili ni hii hapa
attachment.php
Sehemu uliyopigia msitari inayosema na isiyokuwa na dini. siioni. Tutafika ibara ya 19 baadaye nayo tutaiona.

Hata hivyo mkanganyiko huo ndio unaonifanya nisema kuwa Katiba yetu inahitaji kuandikwa upya. Ukisoma katiba za nchi nyingine, information zinaflow smoothly, siyo zinaruka ruka hapa na pale. Inaudhi eti unasoma ibara ya kwanza kumbe eti unatakiwa ujue kuwa tasfiri ziko kwenye ibara ya 155 ukurasa wa mwisho kabisa, mambo gani hayo?
 
Hayo maneno na isiyokuwa na dini yaliongezwa mara baada ya Mabadiliko ya Kumi na Nne ya Katiba ya Nchi ya mwaka 2005. (Rejea Sheria Namba 1 ya 2005). Gonga hapa kwa reference zaidi.

Uwe unatumia the most current versions za Sheria ili kukwepa ku-mislead watu!
 
Gaijin, ni kweli katiba haisemi kwamba Tanzania ni nchi isiyofuata dini yoyote. Hata hivyo bado mimi naona hakuna 'loophole' kwa mujibu wa ibara ya 19(2) ya katiba.

Wakuu zangu nimekuwa pembeni nikiwasoma lakini hapa naona loopholes ipo kwani katiba inaposema shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

Bila shaka hapa inazungumzia UENDESHAJI WA JUMUIYA za kidini ambazo ni kama taasisi za kidini zinazoanzishwa na waumini wake jambo ambalo kidogo lina walakini kwani zipo dini ambazo hazina jumuiya isipokuwa dhebebu la imani..Bakwata chombo cha waislaam ni Jumuiya ilichoanzishwa na serikali na kukabidhiwa Waislam, na ndicho chombo kinachotambuliwa na serikali kama Jumuiya ya Waislaam.

Pili, katiba inaposema swala la kutangaza dini na Ibada linajipinga lenyewe, je ikiwa kiongozi mmoja atachukua hatua ya kutangaza dini yake - Huo Ubinafsi wake utaeleweka kwa wananchi?

Tatu, Kiongozi anaposhiriki kuchanga na ufunguzi wa msikiti au kanisa huwa ni mtu binafsi au mgeni rasmi kutoka serikalini ambaye anawakilisha mamlaka aliyopewa. Yapo mengi yanayochanganya kusema kweli!
 
Huwezi kujadili katiba kikamilifu kama huna civil society ya kusema.

Huwezi kuwa na civil society ya kusema kama huna middle class ya kusema

Huwezi kuwa na middle class ya kusema kama huna economic development ya kusema

Huwezi kuwa na economic development ya kusema kama huna dedication ya kutosha kutoka leadership na status quo

Huwezi kuwa na dedication to economic development ya kutosha kutoka status quo bila ya pressure from further down (for fear of rocking their boat)

Huwezi kuwa na pressure from further down kama huna grassroot organizations na elimu ya uraia.

Huwezi kuwa na elimu ya uraia ya kutosha bila msaada wa status quo.

So basically, what you have here is a situation in which you must have a status quo that is altruistic and generous enough to leave the door open to a potential way to have itself unseated.You need to have an extremely enlightened leadership to allow that for the sake of the nation, and CCM is simply not that noble.

I know some of these assertions are oversimplified for the sake of clarity, but dep down this is the gist of it. And this is why we cannot develop economically or politically.

This is the vicious cycle of poverty we are revolving in.
 
Wakuu nauliza wapi ninaweza kupata nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Natanguliza shukrani.
 
Nenda bookshop, mbalimbali utapata, nenda pale UDSM BOOKSHOP Utapa bei ni elfu 5, au kama tanga nenda bookshop iliyo karibu na eckenford chuo cha ualimu utapata napo pia bei elfu 5
 
Kwenye bookshop za serikali au tembelea tuvuti ya Bunge letu
Asante sana Mkuu. Nimekwenda kwenye tovuti ya Bunge na sikuona link inayoonyesha katiba. Kwa sasa hivi niko nje ya nchi na siwezi kuipata madukani.
 
Leo huko Kenya (uhuru Park jijini Nairobi) Rais Kibaki anatia saini yake katika Katiba mpya ya nchi hiyo iliypitishwa na kukubaliwa na wananchi. Kuna baadhi ya vipengele -- kama vile haki za raia -- vinaanza kutumika mara moja.

Katiba hii imekuja baada ya miaka mingi ya ukandamizaji wa demokrasia ulioshia katika mauaji ya mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1500 walikufa katika vurugu.

Swali langu hapa ni: Kwa nini Wakenya wanatupita katika nyanja ya demokrasia wakati sisi ndio tulanza kupata uhuru kabla ya wao?

Jee nasi labda tunatakiwe tufe kwanza ndiyo tupate Katiba mpya -- maana kuna methali inayosema kwamba iUkiitaka pepo lazime ufe kwanza.

Au CCM inaona kwa vile inaendelea kutawala makundi ya makondoo ndiyo maana haitaki hata kusikia habari hiyo ya Katiba? Maana suala hilo hata halimo ktk Ilani yao ya uchaguzi!

Wanaendelea kuinjoi tu na kuzoa mamia ya viti kwa kupitia ushindi wa meza kwani Katiba iliyopo inawa-favour sana. Lakini watambue kwamba wakiendelea kuibana hii mlipuko wake unaweza ukawa mkubwa kuliko hata wa Kenya.
 
Dr Slaa kaahidi kushughulikia katiba mpya hivyo tumpe kura itafanyika
 
Hiyo ni kweli tumpe Dr,Slaa ili tufanye mabadiliko ya katib. jana hata Tendwa mwenyewe kasema kuwa ina mapungufu makubwa.

Is high time tumpe Urais mtu mwenye uelekeo wa mabadiliko ya kweli nchini. Hawa wanaagalia maslahi yao maana kuna vitu vitanyang'anya tonge mdomoni. Ila uatsikia kama upepo ukigeuka kama hilki la salaries za wafanyakazi wakiona linmakwenda kombo watafanya nao.

Lakini kwa sasa Dr. Slaa tumpeni ili tufanye maendeleo nchini
 
Back
Top Bottom