Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Eti kuna mtu anasema kuwa CCM na JK ni watu wanaofanya maamuzi magumu, Hivi hata neno lenyewe maamuzi magumu si la Dr. Slaa alipokuwa akiomba watu wawajibishwe kwa Ufisadi!

Sasa suala dogo tu kama hili bado wanasubiri mamboyawe vinginevyo (Japo hautuombi na ni mbali sana kwetu) Ndo waanze kufikiria.
Ni chama cha Makondoo kwelikweli,
 
Haya mambo ya katiba kubadilishwa na kuangushwa kwa sisiem kutatokea muda si mrefu, lets just play our part and the change will take place soon.
 
Nafuatilia kwa ukaribu vitu kama viwili nimeviona! Moja first lady wa kenya ni mjeuri alipoingia kwanza kaja na mtoto nakadiria miaka kati ya saba na kumi. Akapelekwa kwenye kukakaa akawa bado kasimama anaangalia angalia mpaka nikaona odinga nadhani na musyoka wakateta jambo!

Raila anashangiliwa sana akicheza karata yake vizuri he may be the next president of kenya.

Kipindi cha ukaguzi wa gwaride walio askari(maofisa wa jeshi)walio msindikiza kibaki walikuwa wanapishana urushaji mikono sijui kama ilikuwa sahihi?
 
Uwezekanao wa Tanzania kupata katiba mpya upo mikononi mwa watanzania wenyewe. SIKU YA JUMAPILI TAREHE 31/10/2010 KUANZIA SAA MOJA ASUBUHI MPAKA SAA KUMI NAMBILI JIONI WATANZANIA WAKIAMUA KWA DHATI WANAWEZA KABISA KUPATA KATIBA MPYA KWA KUPIGA KWA WINGI KURA ZA NDIO KWA WAPINZANI. HIYO NDIO NJIA PEKEE NA SAHIHI YA KUPATA KATIBA MPYA
 
Rais yeyote atakayeshinda, suala la Katiba mpya ni muhimu sana.:eyeroll2:
 
Hawawezi badili katiba once wanajua kabisa ya sasa inawafavour.
 
Hivi hawa CCM huwa hawana akili ya kufanya mambo kuepusha yale yalotokea Kenya? Ningependa (Mungu apishe mbali) yatokee chini ya ya JK tuone atafanya nini. Hii kuchecheka kwake haitamwia vigumu kufanya kama alivyofanya Zenawi kule Ethiopia baada ya uchaguzi wa mwaka 2005. Aiamrisha polisi wafyatulie risasi wapinzani waliojuwa wakiandamana (kupinga wizi wa kura) hasa baada watazamaji wa kimataifa kutamka uchaguzi haukuwa huru na haki.

Lakini hata hapa glimpse tuliipata huko Visiwani mapema mwaka 2001 pale makumi ya watu walikufa kwa risasi za polizi huku wakiandamana kwa amani kudai tume huru. sasa hivi twaona mabadiliko makubwa ya Katiba kule Visiwani.

Sasa swali ni kama alivyouliza Marksman ktk topic yake -- huku Bara Watz wangapi watatakiwa kwanza kufa ili demokrasia ya haki ipatikane?
 
Dr Slaa kaahidi kushughulikia katiba mpya hivyo tumpe kura itafanyika

We unawazimu wa mchana hivi kwa fikra zako Slaa atakuwa Rais? nipe sababu zenye mshiko za Slaa na CHADEMA au chama chochote cha upinzani kushika nchi.....acheni ndoto za mchana nyie imeshindikana Zanzibar itawezekana Bara?
 
We unawazimu wa mchana hivi kwa fikra zako Slaa atakuwa Rais? nipe sababu zenye mshiko za Slaa na CHADEMA au chama chochote cha upinzani kushika nchi.....acheni ndoto za mchana nyie imeshindikana Zanzibar itawezekana Bara?
Mkuu hata huku bara inawezekana lakini wamekosea njia. Kitendo cha wao kuwa nyuma ya dini fulani zaidi ndo imekuwa kikwazo kwani hata mimi sitowapigia kura. Lakini kama wangekuja kiTanzania basi bila shaka kura yangu wangeipata.
 
We unawazimu wa mchana hivi kwa fikra zako Slaa atakuwa Rais? nipe sababu zenye mshiko za Slaa na CHADEMA au chama chochote cha upinzani kushika nchi.....acheni ndoto za mchana nyie imeshindikana Zanzibar itawezekana Bara?

Tatizo lingine huku bara watu wajamii fulani fulani ni rahisi kurubunika, ni tofauti kabisa na kule zanji ambapo watu wakiamua hakuna anayerudi nyuma. Is fully tofauti na wengi wabara ambao ni wanafiki, na ni haohao waliokuwa wakiishabikia CCM miaka 5 iliyopita na sasa hivi wamebadilikia chama fulani na siajabu miaka 5 ijayo watahamia chama fulani

Huo ni unafiki ulioje! huku bara ni aibu tu na ubabaishaji uliovuka mipaka.
 
kwanza katiba yenyewe hawajui ndio nini? CCM wanatawala maiti lakini NARC wanatawala wagonjwa ndo maana katiba mpya imepatikana. Safari bado ndefu sana Tanzania.
 
Tatizo lingine huku bara watu wajamii fulani fulani ni rahisi kurubunika, ni tofauti kabisa na kule zanji ambapo watu wakiamua hakuna anayerudi nyuma. Is fully tofauti na wengi wabara ambao ni wanafiki, na ni haohao waliokuwa wakiishabikia CCM miaka 5 iliyopita na sasa hivi wamebadilikia chama fulani na siajabu miaka 5 ijayo watahamia chama fulani
Huo ni unafiki ulioje! huku bara ni aibu tu na ubabaishaji uliovuka mipaka.

Watanzabara tuna matatizo ya akili, amani na uvumilivu+ujinga mtupu
 
Leo huko Kenya (uhuru Park jijini Nairobi) Rais Kibaki anatia saini yake katika Katiba mpya ya nchi hiyo iliypitishwa na kukubaliwa na wananchi. Kuna baadhi ya vipengele -- kama vile haki za raia -- vinaanza kutumika mara moja.
Katiba hii imekuja baada ya miaka mingi ya ukandamizaji wa demokrasia ulioshia katika mauaji ya mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1500 walikufa katika vurugu.
Swali langu hapa ni: Kwa nini Wakenya wanatupita katika nyanja ya demokrasia wakati sisi ndio tulanza kupata uhuru kabla ya wao?
Jee nasi labda tunatakiwe tufe kwanza ndiyo tupate Katiba mpya -- maana kuna methali inayosema kwamba iUkiitaka pepo lazime ufe kwanza.
Au CCM inaona kwa vile inaendelea kutawala makundi ya makondoo ndiyo maana haitaki hata kusikia habari hiyo ya Katiba? Maana suala hilo hata halimo ktk Ilani yao ya uchaguzi! Wanaendelea kuinjoi tu na kuzoa mamia ya viti kwa kupitia ushindi wa meza kwani Katiba iliyopo inawa-favour sana. Lakini watambue kwamba wakiendelea kuibana hii mlipuko wake unaweza ukawa mkubwa kuliko hata wa Kenya.

Mabadiliko ya katiba ya Kenya hayatokani na machafuko au mauaji ya wakati wa uchaguzi uliopita bali yanatokana na ahadi ya Rais Kibaki alivyoingia madarakani kwa mara ya kwanza - aliahidi kubadilisha katiba ndani ya siku 100 lakini kulikuwa na malumbano kwa muda mrefu sana hasa kati ya wabunge walioteuliwa kushughulikia suala hilo!
 
Juzi juzi mtangazaji wa BBC alimbana Abdulrahman Kinana kuhusu kwanini Tanzania haifanyi mikakati kubadili katiba yake yenye alama za kimaskini yaani viraka vingi.

Kinana katika kujibu alinifanya nishangae sana alijibu akasema, namnukuu:

".....kwanza Kenya walifanya mabadiliko ya katiba kufuatia mauaji yaliyotokana na matoke ya uchaguzi 2007...." Mtangazaji akamtupia sawali jingine akasema, namnukuu.. "Kwahiyo mnasubiri mauaji kama Kenya ndipo mfanye mabadilio ya katiba?"

Hakika hii ni taabu kweli tukiwa na jamii iliyochakachuliwa tunapata majibu bandia mengi kama bidhaa za China.
 
Utafiti nilioufanya NIMEGUNDUA watanzania takribani 70% hawajui KATIBA ya nchi inasema nini! 50% hawajawahi hata kuishika KATIBA hii tuliyonayo!.

Je, nini sababu za watanzania kutokuisoma KATIBA? Wakati inauzwa kwa Tsh 5000/=tu? Je, kuna haja ya kuwauliza kama wanataka KATIBA MPYA wakati iliyopo hawaisomii? Nini kifanyike ili kujenga UTAMADUNI wa kusoma KATIBA?
 
Kwani kila sheria unapotungwa na katiba huandikwa upya tena? Maana naweza tafuta na kukuta sheria zote za mwaka 1968 wakati nasikia zipo mpya za karibuni .Vilevile tuelimishwe umuhimu wa kujua au kuelewa au kusoma katiba.Sisi si mahodari wa kusoma vitabu
 
Back
Top Bottom