Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Utafiti nilioufanya NIMEGUNDUA watanzania takribani 70% hawajui KATIBA ya nchi inasema nini! 50% hawajawahi hata kuishika KATIBA hii tuliyonayo!.

Je, nini sababu za watanzania kutokuisoma KATIBA? Wakati inauzwa kwa Tsh 5000/=tu? Je, kuna haja ya kuwauliza kama wanataka KATIBA MPYA wakati iliyopo hawaisomii? Nini kifanyike ili kujenga UTAMADUNI wa kusoma KATIBA?

Ni kweli kabisa watanzania wengi hawajui katiba yao. Ila, kwa mtazamo wangu, kujua nini kifanyike ili kuondosha hio hali, kuna umuhimu wa kufanya Uchunguzi mwengine. Kama umeweza kufanya uchunguzi ukajua idadi, sasa ni wakati wakajua ni sababu zipi zinazopelekea hii hali, 'Qualitative research'.

Kutoka hapo sasa tunaweza tukatambua njia au nini cha kufanya kuondosha hii hali.
 
Pamoja na mahakama kupigwa "stop" na katiba kupokea, kusikiliza na kuamua migogoro ya kura ya Urais lakini uzoefu wa huko nyuma waonyesha mahakama kuu yaweza kuyapokea malalamiko ila ushahidi ndiyo huwa tatizo la kuendelea na utatuzi wa migogoro ya kura ya Uraisi.

Na ushahidi unaotakiwa ni wa kupinga utaratibu tu na wala siyo mambo mengineyo

Tuombe Mwenyezi Mungu atuone huruma na haki itendeke.
 



Pamoja na mahakama kupigwa "stop" na katiba kupokea, kusikiliza na kuamua migogoro ya kura ya Uraisi lakini uzoefu wa huko nyuma waonyesha mahakama kuu yaweza kuyapokea malalamiko ila ushahidi ndiyo huwa tatizo la kuendelea na utatuzi wa migogoro ya kura ya Uraisi.

Na ushahidi unaotakiwa ni wa kupinga utaratibu tu na wala siyo mambo mengineyo………………Ipo kazi…………………..

Tuombe Mwenyezi Mungu atuone huruma na haki itendeke
Mwaka huu tutayaona ya Kenya. Tume ya Uchaguzi itamtangaza JK mshindi usiku wa manane na hapo hapo ataapishwa hata kama atakuwa hospitali? Akishatangazwa na kuapishwa kazi imeisha, tunaye Rais. Hapo sasa!!! Tunanyamaza???
 
Ibara ya 41 (7) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kitakaposomeka kinyume, basi watanzania wote tutakuwa huru; kwa sasa uhuru bado. Ibara hii inaruhusu chakachua ya matokeo ya Urais. Na lazima kifungu hiki kilichomekwa na Andy Chenge, kwani alikuwa bingwa wa kuchomeka vifungu mpaka alipowahi kustukiwa na kutetewa na Fred Sumaye kule bungeni!

Namna ya kukibadilisha ni kumpa kura ya ndio Dr. Slaa. Hata hakikosa Urais mwaka huu, basi tuwe na wabunge wengi wa upinzani ili wawe na nguvu ya kuanzisha suala ili na kulipitisha bila shida. Sasa je, tuko tayari kupata wabunge wa upinzani zaidi ya theluthi mbili? Je, tunataka matokeo ya Urais yawe yanachunguzwa ili kuepuka chakachua, kauli za vitisho vya akina Shimbo? Basi kama ndio, chagua Dr. Slaa, chagua mbunge wa upinzani hasa Chadema, wewe wakala fanya kazi yako vizuri, nyie UNDP database yenu iwe imara - source code isiwe accessible kabisa!

Mungu Ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
Asanteni kwa kusoma thread hii!
 
Ibara ya 41(7) yasomeka hivi:-

"When a candidate is declared by the Electoral Commission to have been duly elected in accordance with this Article, then no court of law shall have any power to inquire into the election of that candidate."

Hii Ibara haizuii Mahakama kuu kuchunguza kama taratibu za kisheria za kumtangaza mgombea kuwa Rais zilifuatwa. Huu ndio uamuzi wa Mahakama Kuu iliyoutoa mwaka 1995 wakati upinzani ulipokimbilia mahakamani.

Mfano kama NEC haikuheshimu matokeo yaliyopo machoni pao na kumtangaza mgombea ambaye alishindwa mahakama inao uwezo wa kutengua uonevu uliofanywa na NEC na kumtangaza yule ambaye ndiyo chaguo la watanzania walio wengi.

Hivi vifungu, usivisome haraka haraka ukafikiri NEC waweza kufanya watakavyo bali wanapaswa kutenda haki kulingana na sheria ya uchaguzi.

Sheria ya uchaguzi inaikataza NEC kumtangaza mgombea ambaye hakupata kura nyingi kuwashinda wenzie kuwa ndiye mshindi.
 
So it is only Judge Lewis who is above the law that whoever he wants to pronounce as a president he can just do regardless of the peoples' choice!
 
Wadau nisaidieni kujua hili, katiba inasemaje ktk uundaji serikali iwapo chama fulani kitashinda urais na kikapata wabunge wachache bungeni? au kama hoja hii imeisha jadiliwa humu jf naomba link
 
Ibara ya 41(7) yasomeka hivi:-



Hii Ibara haizuii Mahakama kuu kuchunguza kama taratibu za kisheria za kumtangaza mgombea kuwa Rais zilifuatwa. Huu ndio uamuzi wa Mahakama Kuu iliyoutoa mwaka 1995 wakati upinzani ulipokimbilia mahakamani.

Mfano kama NEC haikuheshimu matokeo yaliyopo machoni pao na kumtangaza mgombea ambaye alishindwa mahakama inao uwezo wa kutengua uonevu uliofanywa na NEC na kumtangaza yule ambaye ndiyo chaguo la watanzania walio wengi.

Hivi vifungu, usivisome haraka haraka ukafikiri NEC waweza kufanya watakavyo bali wanapaswa kutenda haki kulingana na sheria ya uchaguzi.

Sheria ya uchaguzi inaikataza NEC kumtangaza mgombea ambaye hakupata kura nyingi kuwashinda wenzie kuwa ndiye mshindi.

Ibara hii inahusu Urais tu na si wagombea wa ngazi ya Ubunge na Udiwani, soma vizuri kifungu hiki!
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema.....

41. -(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.

42.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla ya kupita siku saba.

Hii ndiyo fimbo ya CCM - wanajivunia "tume yao ya uchaguzi". Mpaka hapo tutakapokuwa na tume huru ya uchaguzi tuendelee kuhesabu maumivu!
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema.....

41. -(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya
kuchunguza kuchaguliwa kwake
.


42.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla
ya kupita siku saba.


Hii ndiyo fimbo ya CCM - wanajivunia "tume yao ya uchaguzi". Mpaka hapo tutakapokuwa na tume huru ya uchaguzi tuendelee kuhesabu maumivu!

Nafikiri huo ni woga ambao hauna sababu kwa maana katiba ni nini? si ilitungwa na kuandikwa na watu ili kulinda jamii ya watu wa Tanzania!! sasa kama mtu atawavunjia utu na heshima watanzania kwa kuwanyima matakwa yao halali hata akiapishwa saa nane usiku bado ajue tu moto huko pale pale, haki ya watu haiwezi kufa au kunyamazishwa inaweza tu kucheleweshwa, so to say ''THE RIGHT IS NEVER ASKED FOR IT IS ALWYS DEMANDED''

Sasa wakati watu wakidai haki yao ya msingi hapo ndo pagumu hawatajari katiba inasema nini, kwa manufaa ya nani!!! watataka tu haki yao ipatikane!! kwa ufupi NEC ihakikishe inalinda haki za watu kwa maana watangaze mtu aliyeshinda kwa haki maana ndo itakuwa haki ya watu na kulinda na kuieshimu katiba yenyewe inayowapa mamlaka ya kumtangaza mtu kuwa mshindi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA TUPE MTU WA UKWELI SIO MSANII
 
Ninawashukuru wote kwa michango yenu katika ujenzi wa taifa hili changa..............................
 
Heshima mbele wana Jamvi.

Mimi naomba kufahamu katiba inasemaje kama mtu anataka kumchagua Rais mbali na kituo alichojiandikisha, Maana logically, Rais na wa Watanzania wote na anaruhusiwa kuchaguliwa na kila aliye na kadi halali ya kupigia kura.

Je kwa maana hiyo wanachuo hawawezi kutumia fursa hiyo kufanya uchaguzi wa Rais huko waliko?
Nijuavyo kuna watu wengi wanaweza kukosa kupiga kura kwa sababu mbalimbali, ikiwepo kusafiri kikazi, emergency, kwa wafanyabiashara na wanachuo ambao wanaelekea kunyimwa haki yao ya msingi.

Tafadhali naomba ufafanuzi kwa hili..sijui katiba inasemaje kwa hili.
 
Heshima mbele wana Jamvi.

Mimi naomba kufahamu katiba inasemaje kama mtu anataka kumchagua Rais mbali na kituo alichojiandikisha, Maana logically, Rais na wa Watanzania wote na anaruhusiwa kuchaguliwa na kila aliye na kadi halali ya kupigia kura.

Je kwa maana hiyo wanachuo hawawezi kutumia fursa hiyo kufanya uchaguzi wa Rais huko waliko?
Nijuavyo kuna watu wengi wanaweza kukosa kupiga kura kwa sababu mbalimbali, ikiwepo kusafiri kikazi, emergency, kwa wafanyabiashara na wanachuo ambao wanaelekea kunyimwa haki yao ya msingi.

Tafadhali naomba ufafanuzi kwa hili..sijui katiba inasemaje kwa hili.

Unajua Katiba kama Sheria Mama huwa haiweki details ya Mambo inayoyazungumzia, mfano katiba inatamka kwamba Mtu yeyote aliyefikisha Umri wa miaka 18 ana haki ya kupiga kura kuchagua kiongozi anayemfaa, ila katiba hailezei ni wapi na vipi hizo kura zipigwe. Chini ya Katiba kuna Sheria na Kanuni, zipo sheria za Uchaguzi na Kanuni zinazoelekeza ni vipi ucahguzi ufanywe.

Sasa labda hapa tuzungumzie Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake zinasemaje naaamini hapa kuna wataalamu wa Sheria watasaidia
 
Ninavyofahamu mimi kura ya Rais inaweza kupigwa toka popote nchini kwa vile kimsingi hilo ndilo jimbo lake la uchaguzi ila za madiwani na wabunge ni lazima zipigwe eneo mahalia yaani mpigaji alipojiandikisha. Mimi si mwanasheria lakini nazungumzia uzoefu wa kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika uchaguzi uliopita yaani 2005, ukipenda jimbo la Mikumi ambalo safari hii nimeshindwa kwenda kuli-contest kutokana na kuwepo nje ya nchi ingawa nasikia tunae mwakilishi pale.

Tunaomba magwiji wa sheria mtueleze ili watu wasibabaike au kukatishwa tamaa siku ya upigaji kura.
 
Jamani naomba watu tutoe mawazo yetu kwenye hili, yawezekana likawaweka watu wengi huru zaidi na wakatimiza haki yao ya kupiga kura angalao kwa kumchagua Rais..

Mnaoijua sheria mko wapi????????????? Msaada please...
 
Ni ruksa ilimradi mpiga kura ajitambulishe kwa msimamizi wa kituo kwa kuonyesha kitambulisho au kwa kupata maelekezo kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (sura ya 343) 30 Juni 2010 inatuelekeza nini?
35C (3) Tume inawezakutoa maelekezo na kuweka masharti ambayo mtu anaweza, katika siku ya uchaguzi wa Rais, kuruhusiwa kupiga kura katika kituo cha kupiga kura mbali ya kile alichopangiwa[/FOwanafunzi wa vyuo ambao hawajafungua vyuo wanaruhusiwa kisheria kuchagua Rais nje ya vituo walivyopangiwa]


https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/78962-pata-elimu-bomba-ya-upigaji-kura-31-okt-2010-a.html
 
Nashukuru kwa maelezo yako Mkuu, kwa hiyo tutakao kua mbali na vituo vya kupigia kura pamoja na wale wanafunzi wa vyuo tuna haki ya kumchagua raisi sio..
 
Hii niliipata kwenye barua za wasomaji gazeti la mwananchi

KUWA MWANACHAMA WA CHAMA FULANI, HAKUNA MAANA YOYOTE, KWANI UNAPATA FAIDA GANI ZAIDI YA KUTUMIWA NA WANASIASA KAMA KONDOM……..KISHA UCHAGUZI UKIISHA UNATUPWA WAO WANABAKI NA FAMILIA ZAO WAKIISHI KWA RAHA.

Bernald kalinga
Mahenge-Morogoro.

My take;
Nafikiri katiba mpya itasaidia sana watu kutokuwa na mashaka, na pia kujua haki zao za kimsingi, kwa kauli ya huyo bwana hapo juu kuna ukweli kabisa kwa mazingira ya sasa.
 
ukifikiri sana unaweza ukahisi hata wewe ni km hicho kifaa kinachotumika kwa uroda hapo juu,
Tusilifikirie hilo, sote tujitokeze j2 kuung'oa uyoga na kuusimika m'buyu wa ukweli Dr. Slaa.
 
Back
Top Bottom