Mahakama iliwahi kusema katika kesi ya Director of Public Prosecutions v. Daudi Pete [1993] TLR 22 (CA) katika ukurasa wa 23 kama ifuatavyo: "As the Constitution of the United Republic of Tanzania is established in the Kiswahili language, the controlling version in interpreting the Constitution is the Kiswahili and not the English version."
Kwa hiyo kama mnatafsiri Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, msitumie version ya Kiingereza, tumieni ya Kiswahili!
Asante sana ndugu Bucha na nanihii kwa ufafafunuzi nzuri kuhusu lugha ya katiba.
hata hivyo baadaye niliamua kuwa kuwa itakuwa ni vizuri tukaziangalia zote mvbili hasa ukizingatia kuwa lugha zote ni official languages hapa kwetu. Nitakuwa naleta version zote mbili kwa kila kifungu nitakachokuwa naongelea; itasaidia pia kuona hata mapungufu katika tranalation baina ya lugha hizo.
Kichunguu, nimependa wazo lako na kitu kizuri sana kujadili katiba ambayo ndiyo siyo tu sheria mama bali mwongozo wetu sote. Ila kwenye upande wa poll, maelezo yake yana utata kwani mtu anayeingia mara moja hawezi kujua kama unalenga huu mjadala wa humu jamvini bali mijadala ya kawaidia mitaani.
Kuhusu mapungufu uliyoonesha kwenye utangulizi, nakubaliana na wewe kabisa.
1. Tz siyo nchi ya kijamaa ki-uhalisia. Kilichoandikwa kwenye katiba siyo kinachoendelea. Kwa hiyo tunahitaji kubadili hiyo dhani ili tusionekane tunafanya mzaha na katiba.
2. Bunge letu lina wabunge wasiochaguliwa na wananchi. Hivyo ama katiba ibadilishwe ili tuwape nafasi au tuwaondoe.
3. Hiyo omission ya neno circular state ni hatari sana. Kwa hiyo ni muhimu ama katiba mpya itungwe kwa kiswahili ili baadaye itafsiriwe ka lugha nyingine au watu wa kutafsiri wawe makini sana. Hii dhana muhimu na kwa hiyo haikutakiwa kuachwa kwenye toleo la kiswahili!
Kwa vile dibaji hii inetangaza msingi wa Katiba yote, je itakuwa ni sahihi kuwa vifungu vyote huko mbele ambavyo vitapingana na dibaji hii viondolewe? Nitavionyesha kila tutakapovifikia. Utashangaa kuona kuwa kuna vifungu vilikuwa viantumbukizwa kwenye katiba bila mpangilio wowote.
Buchanan Lakini mbona wasomi wetu majaji(Learned judges)wa mahakama zetu wanatoa hukumu zao kwa kiingereza? bila shaka watatumia version za kiingereza kama reference!Mahakama iliwahi kusema katika kesi ya Director of Public Prosecutions v. Daudi Pete [1993] TLR 22 (CA) katika ukurasa wa 23 kama ifuatavyo: "As the Constitution of the United Republic of Tanzania is established in the Kiswahili language, the controlling version in interpreting the Constitution is the Kiswahili and not the English version."
Kwa hiyo kama mnatafsiri Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, msitumie version ya Kiingereza, tumieni ya Kiswahili!
Kwa vile dibaji hii inetangaza msingi wa Katiba yote, je itakuwa ni sahihi kuwa vifungu vyote huko mbele ambavyo vitapingana na dibaji hii viondolewe? Nitavionyesha kila tutakapovifikia. Utashangaa kuona kuwa kuna vifungu vilikuwa viantumbukizwa kwenye katiba bila mpangilio wowote.
Asante sana ndugu Bucha na nanihii kwa ufafafunuzi nzuri kuhusu lugha ya katiba.
hata hivyo baadaye niliamua kuwa kuwa itakuwa ni vizuri tukaziangalia zote mvbili hasa ukizingatia kuwa lugha zote ni official languages hapa kwetu. Nitakuwa naleta version zote mbili kwa kila kifungu nitakachokuwa naongelea; itasaidia pia kuona hata mapungufu katika tranalation baina ya lugha hizo.
Naomba ututajie hiyo Kesi ambapo Mahakama ya Rufani ilikuja kusema tena tutumie lugha zote mbili.
Buchanan Lakini mbona wasomi wetu majaji(Learned judges)wa mahakama zetu wanatoa hukumu zao kwa kiingereza? bila shaka watatumia version za kiingereza kama reference!
Wanasheria bwana, ... wana mambo yao!! Mimi nilidhani mleta hoja alikuwa analenga kutumia lugha mbili hapa kwenye mjadala na siyo kwenye sheria katika utaratibu wa kutafsi katiba. Mimi nadhani tutumie lugha zote mbili hapa ili tueleweshane vizuri. Halafu pale panapohitaji msisitizo wa kisheria mnaweza kuingia kwenye 18 zenu! Pia ningeomba mpunguze nukuu za hukumu ili sisi wengine tusianze kupata allergy!
Nadhani swali la kujiuliza ni je dibaji/preamble ya katiba ina nguvu ya kisheria kama ibara za katiba? Ingawa dibaji inatoa mtizamo wa kijumla wa madhumuni ya watunzi wa katiba, sidhani kama ina nguvu ya kisheria kuzidi ile ya ibara za katiba!
Naomba ututajie hiyo Kesi ambapo Mahakama ya Rufani ilikuja kusema tena tutumie lugha zote mbili.Asante sana ndugu Bucha na nanihii kwa ufafafunuzi nzuri kuhusu lugha ya katiba.
hata hivyo baadaye niliamua kuwa kuwa itakuwa ni vizuri tukaziangalia zote mvbili hasa ukizingatia kuwa lugha zote ni official languages hapa kwetu. Nitakuwa naleta version zote mbili kwa kila kifungu nitakachokuwa naongelea; itasaidia pia kuona hata mapungufu katika tranalation baina ya lugha hizo.
Kichuguu, kwani katibu huwa haianzi na tafsiri ya maneno muhimu tunayotegemea kukutana nayo kwenye document yenyewe? Kama hiyo tafsi basi haya mapungufu mengine (aya ya 2) yesingejitokeza!
Katiba nyingi nilizowahi kusoma huwa hazitoi definition ye terminologies kama inavyofanyika kwenye sheria na mikataba; katiba ya Tanzania pia haina definition yoyote.
Ibara ya 151 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ina tafsiri (definitions) mbalimbali kama ifuatavyo:
151. Ufafanuzi Sheria Na. 14 ya 1979 ib. 13; 1 ya 1980 ib. 17; 15 ya 1984 ib. 52 na 53; 4 ya 1992 ib. 38; 3 ya 2000 ib. 19; T.S. Na. 133 la 2001
(1) Katika Katiba hii, ila iwapo maelezo yahitaji vinginevyo–
"amri ya jeshi" maana yake ni sheria au amri iliyotolewa kwa mujibu wa sheria, ya kusimamia nidhamu katika jeshi;
"askari" likitumika kuhusiana na jeshi lolote maana yake ni pamoja na askari yeyote ambaye kwa mujibu wa amri ya jeshi hilo ni mtu anayewajibika kinidhamu;
"Baraza la Wawakilishi" maana yake ni Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lililotajwa katika ibara ya 106 ya Katiba hii na linalotekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Zanzibar, 1984;
"Bunge" maana yake ni Bunge la Jamhuri ya Muungano lililotajwa katika ibara ya 62 ya Katiba hii;
"Chama cha Siasa" maana yake ni chama cha siasa kilichoandikishwa kikamilifu kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992; *
"Idara ya Mahakama" maana yake ni kama ilivyofafanuliwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara ya 116 ya Katiba hii;
"Idara ya Mahakama ya Zanzibar" maana yake ni Idara ya Mahakama inayojumlisha mahakama zote ambazo ziko katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
"Jaji Mkuu" maana yake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani aliyetajwa katika ibara ndogo ya (1) ya ibara ya 118 ya Katiba hii ambaye ameteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (2) ya ibara hiyo ya 118 au iwapo Jaji Mkuu hayupo au anashindwa kutekeleza kazi zake kwa sababu yoyote, Kaimu Jaji Mkuu aliyeteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hiyo ya 118 ya Katiba hii, na kama Kaimu Jaji Mkuu naye hayupo au anashindwa kutekeleza kazi za Jaji Mkuu, Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyepo kazini kwa wakati huo na ambaye yuko kwenye daraja la juu zaidi la madaraka kupita Majaji wote wa Rufani waliopo;
"Jaji Mkuu wa Zanzibar" maana yake ni Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar ambaye, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar 1984, ndiye Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Zanzibar;
"Jeshi" maana yake ni jeshi lolote kati ya majeshi ya ulinzi na ni pamoja na jeshi lolote jingine lilioundwa na Katiba hii au kwa mujibu wa sheria na linalotawaliwa kwa amri ya jeshi;
"Jumuiya ya Madola" maana yake ni jumuiya ambayo wanachama wake ni Jamhuri ya Muungano, Uingereza na kila nchi ambayo iliwahi kutawaliwa na Uingereza;
"kiapo" maana yake itabidi ifahamike kwa maana ya kawaida ya neno hilo na ni pamoja na tamko rasmi la namna yoyote linaloruhusiwa kisheria kutumiwa badala ya kiapo;
"kiapo cha uaminifu" maana yake ni kiapo cha kuwa mwaminifu kwa Nchi na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
"Maadili ya Kazi ya Jaji" maana yake ni masharti ya kimaadili yanayoongoza mwenendo wa watu wafanyao kazi ya Jaji au ya Hakimu;
"madaraka ya kazi katika utumishi wa Umma Jamhuri ya Muungano" maana yake itabidi ifahamike kwa mujibu wa maana ya kawaida na maneno hayo na ni pamoja na utumishi katika Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano na katika Jeshi la Polisi au jeshi linginelo lilioundwa kwa mujibu wa Sheria;
"mahakama" maana yake ni mahakama yoyote yenye mamlaka katika Jamhuri ya Muungano isipokuwa mahakama iliyoundwa kwa amri ya jeshi; lakini kwa ajili ya ibara ya 13, ya 14 na ya 15 za Katiba hii, itakuwa ni pamoja na mahakama iliyoundwa kwa amri ya jeshi;
"Mahakama Kuu" maana yake ni Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar;
"Mambo ya Muungano" maana yake ni mambo yote ya umma ambayo yametajwa na ibara ya 4 ya Katiba hii kuwa ni Mambo ya Muungano;
"Mamlaka ya Nchi" ni pamoja na Serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano, pamoja na Serikali na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;
"Mwanasheria Mkuu" maana yake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano aliyetajwa katika ibara ya 59;
"Serikali" maana yake ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au Halmashauri ya Wilaya au ya Mji, na pia mtu yeyote anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali au Halmashauri;
"Serikali za Mitaa" maana yake ni vyombo vya kiserikali vilivyoundwa kwa mujibu wa ibara ya 145 ya Katiba hii kwa madhumuni ya kutekeleza madaraka ya umma;
"Tanzania Bara" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungnao ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Tanganyika;
"Tanzania Zanzibar" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na ambalo kabla ya Sheria hii kutungwa liliitwa Tanzania Visiwani;
"Uchaguzi Mkuu" au "uchaguzi unaofanywa na wananchi" maana yake ni uchaguzi wa Rais na uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha wilaya za uchaguzi unaofanywa baada ya Bunge kuvunjwa;
"Ujamaa" au "Ujamaa na Kujitegemea" maana yake ni misingi ya maisha ya jamii ya kujenga Taifa linalozingatia demokrasia, kujitegemea, uhuru, haki, usawa, udugu na umoja wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano;
"Waziri" maana yake ni Mbunge aliyekabidhiwa madaraka ya kazi ya Waziri, isipokuwa Naibu Waziri, na maana hiyo itatumika pia kwa Makamu wote wa Rais;
"Zanzibar" maana yake ni sawa na maana ya Tanzania Zanzibar.
Sijui mwenzetu ulitaka kuwe na definition zipi!
Ndugu Mzizi Mkavu
Siyo kwamba nachukia ujamaa, lengo langu wakati naannzisha tthread hii ni kuangalia upungufu wa katiba yetu ili tupate mawazo ya kuinyoosha. Kuweka ndani ya Katiba kuwa tunajenga taifa la kijamaa ilhali tunajua kuwa hatufanyi hivyo, ni ama tudharau na kukiuka katiba yetu makusudi, au katiba hiyo siyo ni kitu serious. Ningependa kila kilichoko ndani ya katiba kiwe ni kitu sahihi; kwa hiyo neno ujamaa liondoplewe tu. Katiba imeshasema tunajenga taifa lenye misingi ya haki kwa watu wote; hilo ni lengo linalotosha kabisa kuliko kuongeza ujamaa ambao siyo kweli.
"Ujamaa" au "Ujamaa na Kujitegemea" maana yake ni misingi ya maisha ya jamii ya kujenga Taifa linalozingatia demokrasia, kujitegemea, uhuru, haki, usawa, udugu na
umoja wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano;