Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Wana jf nawapeni pole sana kwa misiba inayolikunba taifa letu. Kwanza nikwa mh. Regia Jembe la CHADEMA, umati tulioshuhudi ulidhihirisha ndie alikuwa chaguo la watu(kazi ya Mungu haina makosa). Pili nihli la mh. Sumari polen wanajf nawana arumeru.

Mada yangu nijuu ya upungufu wakatiba ye2 wanajf nimepata nafasi yakuisoma katiba japo siokwaundan ila vpenge vinavyohusu bunge na wabunge, katiba haijasema lolote juu ya mbunge mteule anapofariki bilakuapishwa inakuwaje au ndg zangu mmeona mnijulishe. Ingekuwa nikatiba iliyojitosheleza ingezungumza muda wambunge kukaa nje ya kiapo naninichakufanya. Tunataarifa sumari kwamwaka mzima hajaapishwa kutokana nakuumwa wala wananchi wa arumeru hawajapata uwakilish kwa muda wote huo.

Wana jf na wananchi kwa ujumla natoa wito tushiriki ktk mchakato wakatiba mpya wale wenye elimu ya sheria wachukue muda wao kuwa elimisha wananchi mapungufu yaliyopo kwenye katiba na wala tusikubaliane nahawa wabunge wa ccm ambao badala yakutoa elimu kwa wananch wanajitetea tu kuwa alichofanya rais ni sahihi kusain sheria yamchakato nakuisifia serikali yao hatunahaja namasifa yao tunataka ELIMU Jinsi yakuanda katiba itakayogusa mambo yote ya msingi na sio masifa yasionafaida kwetu NAWASILISHA!
 
Kwa haya tunayojionea sasa juu ya hali za ugonjwa kwa viongozi wetu waandamizi wa serikali, ni wakati muafaka kwa kufikiria namna mpya ya kudeal na viongozi wa namna hii.

Kuumwa ni jambo ambalo kila binadamu linaweza kumpata, lakini kama kiongozi wa umma anaumwa kwa muda mrefu, huku akiendelea kutumia mali za umma [kwa maana ya gharama za matibabu, usafiri (wa kwenda na kurudi kwenye matibabu)], nafikiri kiongozi kama huyo anapaswa ajiuzulu ili aweze kupata fursa ya kuweza kutibiwa vyema huku akiacha watu wengine waweze kufanya kazi ambazo kiongozi huyo alishindwa kuzifanya kutokana na ugonjwa wake.

Mfano, waziri wa maji Mark Mwandyosa, hadi leo hii anaumwa, bado anaendelea kugharamikiwa na serikali; hivi kuna ubaya gani kama akipumzishwa (kwa maana ya kujiuzulu au kuombwa ajiuzulu) ili kumfanya atulie zaidi kiakili huku akiendelea kutibiwa? Kwa maana nina uhakika ugonjwa wake una madhara katika utendaji wa wizara ya maji!

Kwa hiyo napendekeza kwa kuwepo kwa muda maalamu ambao kiongozi wa umma anayeumwa akiuzidi, basi iwe ni automatically ameachia ngazi. Hii itasaidia sana katika kupunguza gharama ambazo serikali inazitumia na pia itasaidia maamuzi na utendaji katika sehemu zao za kazi kutoathirika kutokana na kiongozi huyo kuwa mgonjwa.
 
kama siku nikipata nafasi ya kutoa mchango wangu kitu kikubwa ninachota IBARA inayosema mgombea lazima awe na miaka 40 na zaidi nadhani kutokana na kupungua kwa viwango vya kuishi pia kawa sasa vijana wanapanulka akiri mapema na tunawahi kumaliza shure na tumeshazama katika siasa kwa kishindo na tumeonyesha ubora waetu nadhani yapaswa ipunguzwe. Lakini pia kipengere kinachosema mgombea ni lazima atoke kwenye chama nayo naona haina mshiko.

Na mwisho kipengere kisemacho RAIS ana mamlaka ya kumtoa mfungwa naona inanyima nguvu mahakama na kukifanya kisiwe chombo huru na kinachochoe illiberal democracy
 
Sheria inayoongoza bunge ipo kama ambavyo sheria za utumishi zilivyo kwa mtu ambaye ni mgonjwa ila kubwa ni utetezi wa maslahi ya chama ndani ya bunge ndo maana halijawahi kuzungumziwa
 
Ubadilishwaji wa Katibu, umehidhinishwa na Raisi, kwahiyo tusubiri tuone ni nini kitafanyika; sidhani kama Tanzania kuna system ya 'White Paper' kwahiyo wananchi hawana 'say' kwenye mchakato huu.
 
kwa maoni yangu naomba katiba ijayo ibara ya 7 na 11 zisiwepo kabisa au 2saidianekuzibadilisha kwa sababu hazitoi msingi wa kinacho maaninishwa , kwa kifupi katiba ya sasa haioneshi namna ya kuenforce elimu , hivo 2we makini vinginevo wadogo na watoto we2 wataendelea kujaza mistari ya hiphoip kwenye mitihan yao.
 
Katiba mpya ni lazima iwe na kipengele cha kupitia(review) mikataba ya serikali upya kila baada ya miaka mitano. kama mkataba haumnufaishi mtanzania uvunjwe na kuangaliwa upya.
 
Hapo ndio kutakua na uwekezaji wa tija na lazma watanzania wapate manufaa na uwekezaji
 
labda kwa mimi ningependa katiba mpya iwe kama ifatavyo;

Kiongozi yeyote atakaye hujumu mali ya serekali wamchukulie hatuwa kali na ikiwezekana mali zake zitaifishwe hiyo ingesaidia kila mtu kuwa makini na kile alichoshikilia
 
mimi ninapendekeza azimio la arusha liwekwe kwenye katiba liwe kisheria kero ya fisadi itaisha.azimio la zanzibari life kabisa
 
Kuna mambo mawili tofauti, swala la katiba na swala la mikataba. Mimi sioni sababu ya kuandika katiba mpya wakati mapungufu ya katiba ya sasa yanaweza kufanyiwa marekebisho. Hakuna hati yoyote ile duniani inayotayarishwa na binadamu ambayo haina mapungufu, na kama ile katiba ya 1977 ilivyokuwa na mapungufu na hii inayotayarishwa itakuwa na mapungufu.

mwanzoni serekali haikutaka kubadilisha katiba, walipoona itakuwa ni kaulimbiu ya wapinzani na wanaosimama pembeni wakakubali, lakini sana sana katiba tutakayoipata ni ile ile ya 1977 ikiwa na madadiliko. Kwa kiasi kikubwa wengi hawaelewi kuwa katiba ni hati inayoelezea mfuma wa utawala na haki, siyo hati ya kisiasa ya kuelezea sera na maamuzi ya kimaendeleo, kwa mfano wengi wanataka katiba mpya izungumzie maswala ya maji, umeme, barabara nk.

Hii ni kutokuelewa maana ya katiba, ninaamini 99% wa watanzania hawajaisoma katiba ya sasa lakini wanashabikia katiba mpya. Kikwete alitoa mfano wakati anazindua Tume ya Maoni, kuwa wananchi wahamue ni mfumo gani wa utawala wanataka, proportional representation, presidential democracy, parliamentary democracy nk. Ni wangapi wanaelewa haya? Sababu ya Tanzania kuwa na mixed Presidential - Parliamentry System ni kuwa uongozi ukiwa hauna nguvu serekali inapinduliwa, dola zetu ni changa na je, kuna mtu anafikiri Tanzania itaweza kuitisha uchaguzi mkuu mara tatu kwa mwaka mmoja kama ikikosekana majority bila ya serekali kupinduliwa? Wengi wetu tuko"naive" tunachanganya katiba na sera, vitu viwili tufauti.

Swali zuri linahusu Sheria ya Uzururaji, ambayo inapingana na katiba ya sasa, sijasikia hata siku moja watu wakilalamika kuhusu sheria hiyo inayotumika na mgambo/polisi kunyanyasa wanyonge, haki ya kuwa mahali popote, wakati wowote bila ya kuvunja sheria haipo. Kimsingi haki zilizopo kwenye katiba ya 1977 hazitekelezwi, je hizo za katiba mpya zitatekelezwa? Sifikiri.
 
Katiba mpya ni lazima iwe na kipengele cha kupitia(review) mikataba ya serikali upya kila baada ya miaka mitano. kama mkataba haumnufaishi mtanzania uvunjwe na kuangaliwa upya.

tena mi naona bora iwe miaka 2 na nust tu. Endapo mkataba mbovu uvunje na aliyehusika anawajibishwa vikali
 
MZEE WABUSARA hiinikweli selikali hii ya awamya4 nimadudu mtup hivyo jambo ambalo spika na naibu wanafanya bunge la CCM.
 
Katiba mpya ni lazima iwe na kipengele cha kupitia(review) mikataba ya serikali upya kila baada ya miaka mitano. kama mkataba haumnufaishi mtanzania uvunjwe na kuangaliwa upya.

Miaka mitano ni mingi sana katika kufanya tathmini. Miaka miwili mpaka mitatu inatosha kujua iwapo mkataba huo unamanufaa au la. Kuwe na chombo cha kuhakiki mikataba hiyo na ku-review mbali na shughuli nyingine.
 
Katiba mpya ni lazima izingatie jinsi ya kuondoa vurugu zinazochochewa na watu wanaopinga muungano huko z'bar. Kiundwe chombo kitakachosimamia muungano.
 
Hawana ishu hao katiba mali ya ccm hiyo.yawananchi bado
 

Maneno mazur sana mkuu ila ukiyaleta mbele ya wabunge wetu utaitwa mchochezi na usiyetaka nchi itawaliwe. Tufanyeje kuondokana na hali hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…