Joshua Bukuru
Member
- Apr 16, 2011
- 76
- 95
Serikali ni watu na nahofia neno wananchi labda ungetumia neno umma. Ipo tofauti kati ya maneno umma na wananchi. Neno wananchi linaingia moja kwa moja kama mmiliki wa nchi na rasilimali zake. Umma unajumuisha asasi zote za kiraia, watawala na watawaliwa, walemavu na wasio walemavu, mashirika binafsi na yale ya serikali, dini zote na vyama vyote vya siasa vyenye usajili na visivyo na usajili. Unaposema serikali ni wananchi kupitia bunge, mimi nadhani si sahihi kwa kuwa huu ni mgawanyo wa madaraka uliopo katika mihimili yetu mitatu ya uongozi nchini. Katika mchakato huu wa katiba mpya, bunge lina nafasi yake katika kufanya maamuzi, watawala wana sehemu yao, vile vile mahakama nayo ina nafasi yake.
Lengo la mchakato tunataka kuwa na katiba inayotaja mambo yote,toa uhuru kati ya mihimili yetu 3 na umma uachiewe uwe na maamuzi ya mwisho juu ya muundo wa katiba. Tatizo lililopo ni pale serikali inapotaka kuhodhi madaraka yote kikatiba au katiba ile kuwa muundo wa kutetea chama au kikundi Fulani cha watu au kumpa mtu Fulani madaraka na mamlaka zaidi. Hapa tutakuwa tunaingia kwenye utawala wa kifalme au tunamfanya mtu Fulani kuwa dikteta.
Tatizo linacholewesha maendeleo Tanzania ni kuwa hatuna committed leaders ambao wanaingia madarakani kwa ajili ya kutumikia umma wa mtanzania. Tulionao kwa kipindi cha miaka taklibani 50 ni wale wenye kujali matumbo yao binafsi, mtanzania baadaye. Japo wengi huthibitika bado tuna mfumo ule wa kuleana au kikingiana kifua, na hii ndiyo inayofanya maendeleo yaonekane kama agenda isiyowezekana.
Viongozi wetu wanasafiri kwa dhana ya kutanua na kuficha mali nje tu na si kujifunza toka kwa mataifa yaliyoendelea. Ipo haja ya madaraka ya rais kupunguzwa katika katiba yetu ijayo na ipo haja pia ya kuwa na serikali tatu ambazo lazima zilindwe kwa mujibu wa katiba.