Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

hii sio katiba iliyo in force sasa hivi, ni ya zamani.

katiba ya mwisho ni version yenye amendments za 2005

tukijadili Katiba tuanze na kuwa na Katiba



Sasa mkuu watu watajadili vipi katiba mpya wakati hii ya sasa hawaijuwi? hii ndio njia sahihi ya kuelimishana na kuhamasisha Watanzania wajenge utamaduni wa kujisomea, sio tusubili kila kitu tusemewe na wanasiasa.
 
Wana JF hivi kuna mwenye Katiba ambayo ni toleo la mwisho. Maana hii katiba imechakachuliwa kiasi kwamba hatujui ni ipi tunapaswa kama wadau tuisome nasi tujiandae kutoa mapendekezo yetu kwa wahusika. Maana wakati mwingine sisi tulioko,mbali either tunajisahau au tunasahauliwa kuwa ni raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tunapaswa kushiriki kikamili kwa maswala muhimu ya nchi yetu. Nitashukuru kama nitapata Katiba ya toleo la mwisho.

Ansanteni.
 
hiyo ndiyo latest mkuu. hata werema haielewi kaishia kuchanganyikiwa tu na kuiita ni kitu kidogo sana. in reality TZ hatuna katiba, hata ukifundishwa miaka kumi huwezi kuielewa. ni sawa na nguo yenye viraka vya kila sampuli, vingine ni viraka vipya lakini vimeshatoboka toboka.
 
Daa asnte muacici hata mimi nilikuwa sina hii CURT 1977
 
Nakuambieni huyu werema hata haifahamu vizuri katiba ndio maana ana kurupuka tu kwenye kauli zake.
Wadau tudai katiba mpya na ishirikishe wananchi kwenye uandaaji wake. Katiba ya nchi si mali ya mtu wala chama. Na ikiisha kukubalika serikali ihakikishe kila mwananchi ana copy yake na ifundishwe mashule walau vipengele vyake!
 
Wana JF hivi kuna mwenye Katiba ambayo ni toleo la mwisho. Maana hii katiba imechakachuliwa kiasi kwamba hatujui ni ipi tunapaswa kama wadau tuisome nasi tujiandae kutoa mapendekezo yetu kwa wahusika. Maana wakati mwingine sisi tulioko,mbali either tunajisahau au tunasahauliwa kuwa ni raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tunapaswa kushiriki kikamili kwa maswala muhimu ya nchi yetu. Nitashukuru kama nitapata Katiba ya toleo la mwisho. Ansanteni.

Mkuu hiyo version ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar siyo the latest. katiba hiyo ilifanyiwa marekebisho kwa mara ya mwisho mwaka 2005. Ni vizuri rejea zote kuhusu katiba ya Jamhuri ya Muungano zikafanyika kwa kuzingatia version ya mwaka 2005 ili kutopotosha mambo.
 
Mkuu hiyo version ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar siyo the latest. katiba hiyo ilifanyiwa marekebisho kwa mara ya mwisho mwaka 2005. Ni vizuri rejea zote kuhusu katiba ya Jamhuri ya Muungano zikafanyika kwa kuzingatia version ya mwaka 2005 ili kutopotosha mambo.

Naiomba mkuu hiyo ya 2005
 
Mkuu hiyo version ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar siyo the latest. katiba hiyo ilifanyiwa marekebisho kwa mara ya mwisho mwaka 2005. Ni vizuri rejea zote kuhusu katiba ya Jamhuri ya Muungano zikafanyika kwa kuzingatia version ya mwaka 2005 ili kutopotosha mambo.

what is so special kwenye hiyo ya 2005 ambacho si kiraka cha hicho kiraka cha 1977??
 
Mimi nadhani suala la katiba ni suala mtambuka na si suala la wanasheria tu. Katiba ni zaidi ya sheria. Umhimu wa wanasheria ni katika kuchora kanuni zitakazokuwemo katika katiba katika lugha inayokubalika kisheria ambayo haitaleta utata wa kuifasiri
 
Jamani mbona mi nina hardcopy revised 2008. Nahisi lattest ni 2008 sio ya 2005 au?
 
Katiba hii inatakiwa wanajamii wananchi washirikishwe siyo wanaitengeneza vigoo tuuuu tuuuuuuu!! itakuwa haina mabadililko jamani
 
  1. Muhimu kwangu mimi ni kupunguza nguvu alizonazo Rais.Tukumbuke kuwa si marais wote wana calibre ya Mwalimu.Bhati mabaya sana mazingira ya nguvu za Rais yakitumika vibaya nchi inayumba.Yeye ni binadamu hivyo ni lazima aweze kukosolewa na kuwajibishwa pia,ikibidi kisheria.Kwa sasa hili halipo.
  2. Pia ningependa Rais asiteue wasaidizi wake toka kwa wabunge bali wawe huru na mihimili mingine na ikiwezekana atangaze timu yake wakati wa uchaguzi ili kura zipigwe kwa serikali na sio mtu.
  3. Rais pia apunguziwe mamlaka ya kuteua ili kupunguza uwezekano wa watu kupewa nyadhifa kama zawadi kwa ukaribu walionao kwa Rais.Ikiwezekana nyadhifa ambazo ni technical zijazwe kwa competitive means.
  4. Tulete majimbo na mfumo wake uwe wa kuchaguliwa
 
Waanabodi ninakerwa na jambo hili naomba tujadili. Hivi serikali ni nani? Nilidhani ni wananchi ambao wanawakilishwa na bunge?

Kutokana na majadiliano yanayoendelea bungeni kuhusu mikataba ambayo serikali haitaki ijadiliwe sisi kama wananchi ambao tumewachagua wabunge hawa tunapenda kuonyesha msimamo wetu kwa kufanya maandamano ya amani na mkutano mkubwa kutoa msimamo wetu. Mikataba yote ipelekwe bungeni. Sisi wananchi ndio tunasema.

Tanzania kweli ni nchi ajabu sana duniani. Ni kama nchi isio na watu wenye uchungu nchi yao. Jamani mawaziri mnasafiri sana nchi za watu na kuona maendeleo yao. Hivi kweli mna vision kuwa kuna siku Tanzania itaendelea? Ni lazima mfike mahali pa kuona wivu wa maendelo ya nchi siyo yenu binafsi tu. Tafadhali mheshimiwa Mbowe tunaomba uandae mkutano huo na kutoa tamko. Aliye karibu na mheshimiwa tafadhali mpelekee salamu. Msisubiri mpaka wakati wa uchaguzi tu.

" KWA MTAJI HUU NDOTO YA KUWALETEA WATANZANIA WOTE MAISHA BORA NA MEMA HAIWEZEKANI KABISA - IT IS NOT POSSIBLE FULLSTOP"

Sauti za wabunge hawa zisipuuzwe

KAMA kweli wabunge ndio wawakilishi wa wananchi, serikali sasa itaondoa pamba masikioni, itawasikiliza na kutekeleza wanachopendekeza.

Kwa siku nyingi sasa, kilio cha wabunge kuhusu mikataba ya madini na mikataba mingine mikubwa, kimezidi kiwango.

Kilio chao kimevuka mipaka ya kawaida. Kimewagusa hata wale ambao hawakuwa na shauku ya kukisikia.

Wabunge wanataka mikataba ipitiwe. Wanataka kujua kilichomo kwenye mikataba hiyo. Serikali haiwakilishi wananchi. Bunge ndicho chombo cha wananchi.

Wabunge wanapojadili jambo lenye manufaa kwa nchi, wanafanya hivyo kwa niaba ya wananchi wao.

Haiwezekani wabunge wapige kelele za kutaka kupitiwa mikataba, lakini serikali iendelee kuwa jeuri.

Awamu ya Tatu ya uongozi wa taifa hili ilitamba kwa kaulimbiu hewa ya uwazi na ukweli. Hapakuwa na uwazi wala ukweli.

Mikataba ilisainiwa. Wageni wakamilikishwa mali za taifa. Mikataba mingi ya kipuuzi kabisa ikasainiwa. Mzigo wa mikataba hiyo sasa unabebwa na walipa kodi wa nchi hii.

Serikali haikuwa wazi. Ilipuuza maoni ya wananchi, na hata ikafikia hatua ya kuwatisha wabunge waliosimama kidete kuhoji uoza fulani fulani.

Inasikitisha, na kwa kweli inakasirisha, kumsikia leo Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, akiunga mkono kupitiwa upya kwa mikataba ya madini!

Yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kuponda wote waliohoji mikataba hiyo, hata akafikia hatua ya kuwaita waliohoji kuwa ni wavivu wa kufikiri.

Waandishi wa habari walioandika au kuhoji mikataba hiyo, walionekana si wazalendo, na ni watu wasiokuwa na maarifa yoyote.

Serikali ya Awamu ya Tatu ilijaa ujuaji na ubabe. Net Group Solution walipingwa mno. Watanzania wengi walisimama kuipinga kampuni hiyo na hata wakurugenzi wake ambao wengi walikuwa ‘vihiyo’.

Lakini kilichofanywa na serikali ni kuwaita FFU wenye bunduki na gesi za kutoa machozi, kuwasindikiza Wazungu hao hadi ofisini.

Kimsingi yamefanyika mambo mengi ya ajabu katika nchi hii. Ndiyo maana tunasema kilio hiki cha wabunge sasa, lazima serikali ikifanyie kazi.

Miktaba ya kipuuzi, kwa mfano ya kuukodisha Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwa dola 1,000 kwa mwaka, ni laana isiyosameheka mbele ya Mola.

Hivi kweli Tanzania kwa utajiri wake ina sababu ya kuomba misaada mingi kama ilivyo sasa? Je, kwa ukwasi uliopo, kuna sababu ya watu kufa kwa magonjwa kama malaria?

Laana ya Tanzania ni nini? Je, si kweli kwamba laana ya Tanzania ni viongozi jeuri na wasioambilika? Kama kweli sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, basi sauti hii ya wabunge lazima iheshimiwe. Serikali ipeleke mikataba bungeni.

Katiba yenyewe hii hapa:


Download your copy

Sikiliza bwana Mheshimiwa, Bunge letu ni bunge la vyama, maana dhana ya chama kwanza ndo inadunda. Sasa huyu mbunge akinyang'anya kadi ya chama amakwisha. Suala hapa ni wananchi kuja na mapendekezo ya kamati itakayokusanya maoni, kuandaa katiba, ipigiwe kura, ikikubalika ikabarikiwe na hawa wabunge chama fulani. lakini wao ambomo kwayo kuna akina nanihii, richmotors, hata.
 
Sasa, kwanza hebu nieleze katiba ni nini?, Pili serikali ni nini, Tatu wale ambao hawana chama wanawakilishwa na nani? Hivi kila siku nasikia neno mtumishi wa umma, umma ni nini na utumishi ni nini. Aloo ninasikia kuna rungu la dola, na wenye kubeba rungu hilo ni watumishi wa umma, halafu wanaweza kuushulikia umma kirahisi tu. Kwanza katiba ni ya nini? Si Mahakama inatosha, basi hat ile ya kadhi.

Mzee mmoja aliniambi, katiba ni sheria za mahakama sisi tunataka haki na amani hatuhitaji katiba. Nilijaribu kumuuliza Mkukuta ni nini, aliniambia ni gari la kubebea manamba.

Sasa hapa nilipo nimeona kati, ndoo naanza kuisoma. yule mzee hatanidanganya tena, anaitwa Siasa Bin Uongo.
 
"Sheria ya 1992 katiba ya Jamhuri ya Tanzania.
Na.4 ib.3


2.
-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo."

Naanza kuchambua: Kama neno Tanzania Bara linatumika basi Tanzania Visiwani lingetunika, au Tanzania Tanganyika na Tanzania Zanzibar. Sasa nimenza kugundua hii Katiba ina hila, haitaki kabisa nena Tanganyika. Naendelea kusoma ....

 
Katiba yetu tuliyo nayo, samahani labda sio yetu, kwasababu haina mwingizo wa mapendekezo ya wananchi (umma). Sasa Tuanze na kuangalia serikali.

Nafikiri serikali ni chombo kinachoundwa na umma kwa ajili ya kushuhulikia maswala ambayo mwana wa nchi mmoja mmoja hataweza kuyamudu, "these are gray areas". Sasa kuna mambo kadha wa kadha yanafuata.
1 Kuajiri watumishi mbalimbali wa umma
2 Kuchagua wasimamizi wa mambo mbalimbali
3 Kuunda vyombo mbalimbali kwa utumishi wa umma, na kadhalika na kadhalika.

Serikali iko chini ya wananchi

Umma unakutana na kuunda mkataba kati yake na watumishi wake yaani serikali ambao huitwa katiba. Katiba inarudisha nguvu kwa umma, na hivyo umma unakuwa na malaka ya kuiamuru serikali kufanya yale iliyowatuma serikali. Umahiri wa uendelezaji wa katiba ndio utakaohakikisha kwamba serikali iliyopo madarakani inawajibika kwa umma.

Kwa bahati mbaya Serikali za Afrika zinafikiri kwamba zipo juu ya wananchi, na viongozi wa Afrika huhisi kuwa wafalme. Na Katiba za kikoloni zimetoa sana mwanya wa utawala wenye mithili ya kifalme.

Natoa tu angalizo kwamba, zoezi la kuandika katiba mpya ni kazi yamuda mrefu, kuna mambo yanayoweza kungoja katiba mpya na yale ambayo yanahitaji mabadiliko ya haraka.

Kabla madini yetu hayajaisha tunahitaji kuangalia suala la hii mikataba ya mirahaba ya asilimia 3

Suala la wabunge kubanwa sana na vyama vyao, wanakua waoga, wanatakiwa waweze kuhama vyama na viti vyao, nguvu irudi kwa mbunge juu ya chama chake.

Nguvu za bunge ziwe juu kidogo zaidi ya Raisi

Vyombo muhimu kama, usalama wa taifa, tume ya uchaguzi, PCCB, NK viwajibike kwa bunge

Tunaendelea kuchangia, Nafikiri Forum mbali mbali zibuniwe kujadili hii katiba mpya. na kwa sababu hii ni katiba mpya, bunge kiwechombo cha kuratibu mchakato mzima, na si watakaoandika katiba.
 
Back
Top Bottom