Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya Bunge kuhusiana na mradi na mkataba wa Umeme kati ya Tanesco na RDC, umebainisha kuwakulikuwa na mapungufu makubwa ya kiutendaji ambayo yalitoa mwanya kwa kuvunjwa kwa sheria, miiko na kanuni na kuishia kuruhusu Uhujumu wa Taifa kwa kutumia ofisi za Serikali.
Hivyo basi, tuwasilishe ombi kwa wabunge wetukutaka Mikataba yote iliyopita ya Uwekezaji, Ubia, au Ununuzi yaliyofanywa na Serikali au Mashirika yake,yawasilishwe kwa Bunge kwa uchunguzi na uhakiki.
Mikataba bomu kama IPTL, RDC, ATCL, NBC, Kiwira, Rada, ATC-Airbus, Kopta za Jeshi, Bomba la Mafuta, Buzwagi, na mingine ambayo imefanyika katika miaka 13iliyopita, irudiwe, ihakikiwe na ikiwezekana isitishwe au iandikwe upya kwa Manufaa ya Taifa.
Majibu ya Kishenzi kutoka Serikali kuwa Mikataba ni siri ya mwekezaji na mtumishi wa serikali aliyetia sahihi yasikubaliwe.
Tumeona Richmond ilivyotaka kufanywa siri na tunabaini kuwa Waziri Mkuu alihusika na kuliaibisha Taifa kwa kushinikiza na kuliingiza Taifa hasara kwa kuleta mkataba wa kibiashara kwa kutumia Kampuni ya kitapeli.
Tusikubali kulaghaiwa na kwa kutumiwa kwa utashi wa Siasa, bali manufaa na maslahi ya Taifa yapewe kipaumbele!