Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Ombi

Mh Zitto wahamasishe waheshimiwa wabunge wenzio wawe wanapitia humu wajifunze. Badala ya kung'ang'ania kusoma Ijumaa, Sani, Kasheshe and the like.

Cha kufanya ni kurefer something cha JF katika moja ya hotuba zangu bungeni na kuifanyia introduction. Hii itasaidia wabunge kujua na hivyo naamini wengi wataanza kupta humu
 
Zitto tunaomba uwe Balozi wa JF bungeni naamini wengi wakisoma humu watajifunza mengi na wengi naamini hata nafsi zao zita wasuta na watajifunza mengi. JF forum naamini wanaweza kujifunza hata kuliko semina wanazozifanya. WITO Kwa Zitto. jitahidi kwa njia yeyote il waheshimiwa wenzio wawe wanapitia humu na kusoma watajifunza mengi. Hilo ni wazo!
 
Shukrani Mheshimiwa Zitto Kwa Hoja yako ya kuitambulisha JF kwa Waheshimiwa Wabunge! Kwa mtazamo wangu wabunge wengi wana Ukata wa Habari,na wanadanganywa Ukweli na wakuu wao wa Kazi.Kwa kuingia humu watachambua upi ni Ukweli na upi ni Uongo!,na wanaweza kupata Hoja nzito za kujadiliana huko Bungeni.

Kwa mara nyingine Tunaomba uwakilishi wako Mahiri uendelee huko kwenye Jumba la kutunga Sheria.Tunakusikiliza na tunafuatilia kwa ukaribu kila unachozungumza!Good Job!
 
Cha kufanya ni kurefer something cha JF katika moja ya hotuba zangu bungeni na kuifanyia introduction. Hii itasaidia wabunge kujua na hivyo naamini wengi wataanza kupta humu
Mh. Zitto!
Ni wazo zuri Itambulishe tu huko Lakini Waheshimiwa wengi sidhani kama wanataka kujifunza kwani yaliyopo mitaani na yanayowakabili wapiga kura wao ni somo tosha Lakini wapi Kimya kimya!
 
Waraka namba Moja kwa Spika wa Bunge Mhe. Msekwa
Na Zitto Zuberi Kabwe
Mapendekezo Yako ya Mfumo wa Bunge Hayajengi Demokrasia ni Gharama kwa Wapiga Kura!
Mheshimiwa Pius Msekwa
Spika wa Bunge
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dodoma.

Moja ya suala kubwa linalikutofautisha wewe na viongozi wenzako wa serikali ya Tanzania na pia wa vyama vya siasa ni maandishi. Wewe mheshimiwa huna uvivu wa kuandika na katika kipindi cha miaka kumi sasa tangu uwe Spika wetu wa Bunge hapo mwaka 1994 umeandika vitabu zaidi ya vitano na pia umetoa makala kadhaa katika magazeti nchini. Ni lazima kama muungwana na mdau katika siasa za nchi yetu nikupongeze katika hili.

Nimesoma katika somo la historia pale shule za sekondari Kigoma na Kibohehe kuwa moja ya sifa kubwa za viongozi wa awali wa Afrika ilikuwa ni uwezo wa kuweka mawazo yao maandishi na hivyo kusababisha majadiliano ya kitaaluma. Viongozi wetu wa awali waliotuongoza katika kuleta uhuru hawakuwa wavivu wa kuandika na hawakusema kuwa wanasubiri kustaafu ili waanze kuandika. Mwalimu Nyerere aliandika, Nkrumah, Kaunda na wengineo wengi.

Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima napenda kukujulisha kuwa mimi naona mengi ya maandishi yako yanapotosha na yanaonesha ubabe wa hali ya juu na kukosa utamu wa uandishi wa kitaalamu. Hususan maandishi yako ya hivi karibuni yamekuwa ni kama kuleta ubishani usio na maana kwa kujenga hoja ambazo kama hazitetei chama chako basi kinadanganya na kupindisha ukweli kukidhi haja zako binafsi za kutaka kuonekana wewe ndio mjuzi pekee wa masuala ya katiba nchini petu.

Mimi kitaaluma ni mchumi. Hata mimi ni msomi mzuri tu wa masuala ya siasa na hivyo ninatumia uelewa wangu wa masuala ya kusoma katika kujibu hoja zako zilizoko katika kijitabu chako ulichotoa juzi kwa lugha ya kimombo 10 years after the transition to Multi-Partysm:The current Multi-Party Democracy landscape in Tanzania. Katika waraka huu wa kwanza kwako naomba uniruhusu nikupe changamoto la kisomi katika sehemu ya tatu ya kijitabu chako ambacho ni sehemu ya mpango wa Bunge wa Elimu ya uraia.

Katika sehemu hii ambayo katika nakala ya kijitabu chako nilichonacho mimi ipo ukarasa wa 19, umejenga hoja kuwa ili chama cha siasa kiwe chama tawala ni lazima kiwe na viti vingi zaidi bungeni kuliko vyama vingine ndani ya bunge. Na umesema kabisa kuwa hii ni kanuni ya msingi (basic principle). Hivyo basi kwa Tanzania ili chama kiwe chama tawala, basi ni lazima kiwe na viti visivyopungua 116 (viti vya majimbo). Umeendelea kujenga hoja yako kuwa sababu pekee iliyopelekea CCM kuwa chama tawala ni kushinda viti vingi katika Bunge. Hatimae umetoa changamoto kwa vyama vya siasa kama CHADEMA kupata wingi wa viti bungeni ili viwe vyama tawala.

Mheshimiwa Spika, sijui kama ulikuwa umepitiwa katika kuandika kijitabu hiki au ni kulewa tu mamlaka kulikokufanya kwa makusudi uache uchambuzi muhimu wa masuala tata katika katiba yetu. Maelezo yako yatakuwa sahihi kama yalivyo iwapo tu kama mfumo wa serikali yetu ni wa kibunge. Lakini kwa mfumo mchanyato tulio nao sisi Tanzania maelezo yako sio sahihi kiufundi na kitaalamu kwa sababu Rais ndie anaeunda serikali kwa kuteua Waziri Mkuu na pia Mawaziri wote. Wakati Katiba yetu inasema kuwa Waziri Mkuu atatokana na chama chenye wabunge wengi, lakini bado waziri mkuu huyu ni lazima ateuliwe na Rais ambae kwa mfumo wa serikali anaweza kutoka chama tofauti kabisa cha siasa. Sasa hapo Mheshimiwa Spika ni chama kipi kitakuwa chama tawala? Cha Rais (mfano kutoka CCM) au cha Waziri Mkuu (mfano anatoka CHADEMA)?

Mheshimiwa Spika dhana ya chama tawala kwa mujibu wa katiba ya Tanzania bado ni dhana tata na kwa makusudi hukutaka kufafanua suala hili maana ni moja ya suala ambalo wapinzani wanalijengea hoja ya kujadili upya katiba yetu.

Katika hili nakupa mfano ambao umetokea juzi tu katika nchi jirani ya Malawi. Hivi majuzi baada ya uchaguzi wa Malawi chama Tawala cha UDF kimeshinda kiti cha Urais lakini kimehindwa vibaya viti vya ubunge na kufanikiwa kupata viti 48 tu sawa na asilimia 26 ya viti vyote. Mfumo wa utawala wa Malawi hauna tofauti sana na mfumo wetu maana nao wanafuata mchanyato wa mfumo wa kibunge na mfumo wa kiurais. Sasa mheshimiwa Spika katika hali kama hiyo chama tawala ni kipi? Ni UDF au ni MCP ? Mheshimiwa nakukumbusha kuwa Malawi ni nchi ya Jumuiya ya Madola maana wewe unapenda sana kutumia mifano kutoka Jumiya ya Madola.

Ni katika suala hili hili Mheshimiwa Spika umeshindwa kuweka wazi kuwa ndani ya Tanzania kuna mgogoro mkubwa kati ya CHADEMA na CCM juu ya kwamba ni sera zipi zitekelezwe katika Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Ugomvi huu licha kuwa na tatizo la kikatiba lakini linakuzwa na viongozi kama wewe kwa kushindwa kuweka ukweli wa mambo katika mambo haya. Kijitabu chako kizima hujaonesha kamwe kuwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna Halmashauri za Wilaya zinazoongozwa na vyama tofauti na CCM na hivyo kuifanya CCM kuwa chama cha upinzani katika Halmashauri hizo za Hai, Kigoma na Karatu. Huku nako kwa maoni yako mheshimiwa CCM ni chama tawala?

Katika kijitabu chako unasema kuwa CHADEMA ambayo sasa ina viti vinne katika bunge, kama inataka kuwa chama tawala ni lazima ipate mafanikio ya ajabu ya kupata viti 116 kutoka katika majimbo. Licha ya kukubali kuwa siasa ni sanaa ya uwezekano politics is an art of possible lakini unabeza kuwa hali hii haiwezekani.

Hivi Mheshimiwa Spika unaweza kuniambia kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2002 huko Zimbabwe, chama cha MDC kilikuwa na wabunge wangapi? Licha ya kuwa hali ya kisiasa yaweza kuwa tofauti (ambapo pia yafaa kutoa tafsiri ya ideal political situation), chama cha MDC kiliweza kutoka viti 0 vya Bunge la Zimbabwe mpaka kuinyima ZANU-PF theluthi mbili ya viti. Lakini pia matukio ya juzi yanatuonesha kuwa chama cha UDF kimeporomoka kutoka viti zaidi ya nusu katika Bunge mpaka viti asilimia 26 tu. Mheshimiwa kila kitu kinawezekana kwa muda mwafaka na CCM yaweza kuondolewa madarakani kama jinsi ambavyo chama cha Institutional Revolutionary Party cha Mexico kilivyoweza kungolewa licha ya kukaa madarakani kwa miaka 70 (samahani kwamba Mexico sio nchi ya Jumuiya ya Madola).

Mheshimiwa katika kijitabu chako unajenga hoja wazi wazi kuwa yaliyotokea katika Jamhuri ya Kenya hayawezi kutokea nchini Tanzania. Ni kwa nini mheshimiwa unaamua kabisa kutumia pesa za umma kuchapisha kijitabu kinachokosa uchamubuzi yakinifu? unajenga hoja zako hivi:

Kwamba hali ya Kenya kisiasa ilikuwa ni tofauti na hali ya sasa ya Tanzania kwa sabau kuu mbili, kwanza nguvu ya chama cha KANU katika bunge la Kenya haikuwa ni kubwa sana maana haikuwa na viti vingi bungeni na hivyo Kenya kuwa na bunge linaloelea (hung parliament) na kwa wapinzani ilikuwa ni kiruko kidogo tu (a small jump).

Pili, na sababu hii wewe una sema ndio muhimu zaidi, upinzani wa Kenya chini ya Mseto wa Upinde wa Mvua (NARC) haukuundwa na wapinzani peke yao bali kulikuwa na viongozi wa KANU waliohamia upinzani.

Mheshimiwa kwanza kabla ya kukubalia hoja yako moja napenda niseme kuwa suala hapa sio sababu ulizo toa kwani haya ni maelezo ya hali na sio sababu (explanation of the situation without giving factors that led to changes in Kenya). Suala la kuwa na kiruko kidogo (small jump) licha ya kukataa dhana yako hii lakini nakubali inaelezea hali ya Kenya ya wakati huo.

Lakini sababu yako ya pili Mheshimiwa haina uzito wa kisomi kwani umeshindwa kueleza ni nini kilitokea kabla ya hapo. Nakukumbusha kuwa Mheshimiwa Raila Odinga tingatinga alikuwa ametoka upinzani na kujiunga na KANU mwaka mmoja kabla ya uchaguzi na huyu huyu alisomba viongozi wote wa chama chake cha NDP na baadhi ya viongozi wa KANU na kuunda Rainbow Coalition kabla ya kujiunga na akina Mwai Kibaki wa NAK kuunda NARC. Hivyo basi kimsingi ni muhimu sana kuangalia nyuma kidogo kabla ya kuweka hitimisho.

Sasa mheshimiwa unasema kuwa suala la viongozi wa CCM kutoka kujiunga na upinzania haliwezekani, wakati huo huo hapo juu unasema siasa ni sanaa. Mimi ninachokwambia ni kuwa huwezi kamwe kuondoa uwezekano huu wa hali hii kutokea na kwa hali ya sasa ya CCM kuna uwezekano mkubwa sana hali hii kutokea.

Sababu ambayo ninaweza kukubali kama ungeitoa ni kwamba hali ya siasa ya Kenya ni ya kikabila, vyama ni vya kikabila na hivyo ni suala la viongozi wa makabila kusema tunapiga kura wapi na watu wote wa kabila hilo kufuata. Hii Tanzania haiwezekani. Tanzania wananchi watapiga kura kufuatia sera za vyama na mvuto wa viongozi. Hii ni sifa kubwa tuliyonayo Watanzania na ni lazima tuidumishe.

Nimalizie waraka wangu wa leo kwa hoja ya kamati yako ya kuongeza idadi ya Wabunge kufikia 350 ili kuwezesha nchi kuwa na mfumo wa uwakilishi wa uwiano.

Kuwa na mchanyato wa uwakilishi wa uwiano na mfumo wa sasa ni suala zuri sana. Hata hivyo sio lazima kuongeza idadi ya wabunge ili tuweze kuwa na mageuzi haya. Tunaongeza idadi ya wabunge bila ya kujali gharama ambazo taifa litabeba kwa mishara ya wabunge, upanuzi wa jengo la Bunge, marupurupu ya Wabunge na maposho makubwa makubwa.

Mheshimiwa mimi nakupa ushauri na ninaomba uuweke katika kamati yako ndogo ili mabadiliko ya katiba yatakapofanyika basi hili ndio lipelekwe bungeni.

Tanzania ina Halmashauri za Wilaya 130, kwa kuwa Mbunge ni diwani basi kila Halmashauri ya Wilaya iwe na Mbunge mmoja tu badala ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji kuwa na Wabunge mpaka watatu. Sioni sababu ya Manispaa moja kuwa na Wabunge watatu wakati majimbo kimsingi sio maeneo ya utawala na hakuna ngazi ya uongozi katika Jimbo kiasi kwamba inakuwa ngumu hata kwa Mbunge kufikisha maoni ya Wananchi Bungeni. Ngazi ya Utawala ipo katika Vijiji, Mitaa na hata Kata (maana katika kata kuna kamati ya maendeleo ya Kata). Jimbo hakuna kitu na inasumbua Wananchi tu.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali aendelee kuwa katika Bunge kwa Mujibu wa nafasi yake. Nafasi zote zinazobaki zigawiwe kwa vyama kwa mujibu wa kura ambazo chama kimepata. Kwa kuwa Mikoa inapishana idadi ya watu basi kuwe na orodha ya mikoa na orodha ya Taifa. Orodha ya Taifa kwa vyama isiwe na zaidi ya viti 30 na orodha ya Mikoa iwe ni viti 134. Mikoa igaiwe orodha kutokana na idadi ya sasa ya Wabunge ambayo Mkoa unayo. Hivyo basi chama kitapata uwiano wa wabunge kutokana na asilimia ya kura kilichopata katika Mkoa husika, na hapa kura za ubunge ndio zihesabiwe.

Katika Orodha ya Taifa, kura za mgobea Urais ndio zitoe asilimia ya viti chama kitapata. Hii itasaidia sana kuhakikisha kuwa vyama vinaingia katika kampeni kwa mujibu wa sera ili kupata asilimia ya kutosha na hivyo viti vya kutosha.

Ili kutimiza lengo la idadi ya kutosha ya Wabunge wanawake, basi hapa tuige wenzetu wa nchi za Skandinavia. Kwamba katika orodha ya kila chama, basi katika kila baada ya mgombea wa jinsia moja pawe na mgombea wa jinsia nyingine. Yaani kama mgombea namba moja ni Mwanamke basi namba mbili awe mwanaume. Hii italeta ushindani ndani ya vyama na hivyo kukuza demokrasia ndani vyama hivyo na pia kufikisha lengo la kuwa na Wabunge wa kutosha wa wanawake.

Mheshimiwa Spika naomba kwa leo niishie hapa ili uweze kupata muda wa kutafakari. Mungu akipenda nitakuandikia waraka mwingine siku za usoni ili uweze kupata mawazo tofauti na mawazo yako na tufanikiwe kujenga nchi yetu.

Nakutakia kazi njema bunge lijalo

Zitto Kabwe,
Köln/Bonn, Germany
 
Suala la mikataba kuletwa Bungeni, alianza Maua Daftari
Parl Questions - Principal Question(s)


Honourable Kabwe Zuberi Zitto [ CHADEMA ]
Kigoma Kaskazini Constituency
Session Number Principal Question Number To the Ministry of Sector Date Asked 22 June 2006

Kwa kuwa, Serikali imekodisha Uwanja wa Ndege wa K.I.A kwa muda wa miaka thelathini (30) kwa gharama ya dola za Kimarekani 1000 kwa mwaka:-

(a) Je, Serikali ipo tayari kuuleta Mkataba wa makubaliano ya kukodisha uwanja huo hapa Bungeni ili Wabunge waweze kuufahamu?

(b) Je, Serikali ipo tayari kuupitia upya Mkataba huo ili nchi ifaidike na mapato ya uwanja huo ambao ulijengwa kwa gharama kubwa?


ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION # 61 SESSION # 4
Answer From Hon. Dr. Maua Abeid Daftari INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT

NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Miundombinu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) umekodishwa kwa Kampuni ya Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO) kwa Mkataba wa miaka 25 na sio 30. Katika ukodishaji huo Serikali ni mmoja wa wabia na ina hisa asilimia 24. Katika Mkataba huo kipo kipengele 30.4 ambacho kinatufunga pande zote mbili zinazoingia Mkataba huo kutoa habari kwa mtu yeyote ambaye si mhusika wa moja kwa moja na utekelezaji wa Mkataba huo.

Mheshimiwa Spika, mkodishaji ameweza kufanya mambo mbalimbali ya kuboresha kiwanja hicho ikiwa ni
-kulipia mkopo uliochukuliwa na Serikali,
-kufanyia matengenezo magari ya zimamoto na ukarabati wa Kituo cha Zimamoto,
-ukarabati wa paa ambalo lilikuwa linavuja, upakaji rangi majengo ya abiria, ukarabati a vyumba vya kufikia abiria na chumba maarufu,
-ujenzi wa barabara ya kutoka BP Fuel Farm hadi DAHACO,
-ununuzi na kujenga mitambo mbalimbali ya kuongozea ndege, misaada kwa taasisi za kidini, shule na afya na elimu kwa wafanyakazi na uboreshaji wa shughuli za mazingira.
Jumla ya Shs.8,772,896,600/= zilitolewa na KADCO kwa kazi hizo.

Wizara yangu imeona umuhimu wa kuupitia upya mkataba huo kipengele kwa kipengele kazi ambayo ilianza na bado inaendelea, shughuli hii inafanywa na jopo la wataalamu kutoka Wizara zifuatazo:- Wizara ya Fedha, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Miundombinu, Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro. Tunategemea baada ya pande mbili kufikia muafaka, marekebisho hayo yatafikishwa katika ngazi za juu Serikalini kwa maelekezo zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Katika Mkataba huo kipo kipengele 30.4 ambacho kinatufunga pande zote mbili zinazoingia Mkataba huo kutoa habari kwa mtu yeyote ambaye si mhusika wa moja kwa moja na utekelezaji wa Mkataba huo.


Katika suala la nyongeza hukumuuliza kwamba, kwa mawazo yake wabunge sio wahusika na mikataba hiyo?
 
watanzania hawana uchungu na nchi yao,ccm imetufikisha mahali kila mtu amechanganyikiwa na maisha hata kuwaza juu ya nchi yetu kila mtu anafikiria watoto wake watakula nini.
Mungu atupe roho ya matumaini hadi siku ya kuingia kaburini.
 
watanzania hawana uchungu na nchi yao,ccm imetufikisha mahali kila mtu amechanganyikiwa na maisha hata kuwaza juu ya nchi yetu kila mtu anafikiria watoto wake watakula nini.
Mungu atupe roho ya matumaini hadi siku ya kuingia kaburini.


Hiyo sentensi iko bold sana katibu tarafa. Watu wanauchungu sema hawajui waanzie wapi.
 
yebo yebo,
humeshawahi kupatwa na kuzunguzungu.hiyo ndio hali ya watanzania wa leo, bado tupo tunatafakari kipi kinazunguka kati ya jua na dunia maana kila kunapo kucha na afadhali ya jana.
 
Hey! nimesoma sawasawa au Mh Zitto umekosea ku type? KIA imekodishwa kwa dola 1000 kwa mwaka! sawa na takriban dola 83 kwa mwezi au less than dola 3 kwa siku!

Now I know why we r where we r!
 
Masatu,
Hukukosea. Na hawa viongozi waliopitisha deal eti nao wamesoma, tena sana tu.
 
Hey! nimesoma sawasawa au Mh Zitto umekosea ku type? KIA imekodishwa kwa dola 1000 kwa mwaka! sawa na takriban dola 83 kwa mwezi au less than dola 3 kwa siku!

Now I know why we r where we r!

Huo ndio ukweli, KIA imekodishwa kwa dola 1000 kwa mwezi. KLM peke yake ikishuka pale inalipa dola 5000 kila siku
 
Wakati wa kubadili katiba bado - Nagu

na Mobin Sarya na Analis Mwandu
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mary Nagu, amesema hakuna umuhimu wa mabadiliko ya katiba, badala yake wanawake waingie zaidi kwenye nafasi mbalimbali za uongozi ili kuleta usawa.

Kauli hiyo, inaashiria kuzima ndoto za viongozi wa vyama vya upinzani za kuwepo kwa mabadiliko ya katiba ili kurekebisha baadhi ya mambo muhimu kwa maslahi ya nchi.

Nagu, alisema hayo alipotoa hotuba ya kufungua semina ya kuwawezesha wanawake katika siasa, iliyoandaliwa na umoja wa vyama vyenye wawakilishi bungeni (TDC) na kufadhiliwa na umoja kama huo kutoka Finland (DEMO).

Katika hotuba yake, Nagu aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele kugombea nafasi mbalimbali za uongozi serikalini na kuacha fikra za kudai mabadiliko ya katiba kwa kuwa muda wa kufanya hivyo haujafika.

Wanawake tujitahidi huu moto tuliouwasha tuendelee nao ili kuhakikisha hata kule bungeni tunapata nusu kwa nusu ya uwakilishi, msijiingize katika kudai mabadiliko ya katiba kwani si ya lazima, alisema Nagu.

Naye Mwenyekiti wa umoja huo, John Cheyo, Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), alimweleza waziri huyo kuwa, upo umuhimu wa mabadiliko ya katiba ili kuziba mapungufu yanayojitokeza wakati wa uchaguzi.

Source: Wakati wa kubadili katiba bado - Nagu
 
Ndio tatizo la mawaziri ambao kwao CCM mbele, Tanzania nyuma.
 
Katika hotuba yake, Nagu aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele kugombea nafasi mbalimbali za uongozi serikalini na kuacha fikra za kudai mabadiliko ya katiba kwa kuwa muda wa kufanya hivyo haujafika."Wanawake tujitahidi… huu moto tuliouwasha tuendelee nao ili kuhakikisha hata kule bungeni tunapata nusu kwa nusu ya uwakilishi, msijiingize katika kudai mabadiliko ya katiba kwani si ya lazima," alisema Nagu.[/QUOTE
Huyu kweli waziri wa sheria...Kazi kwelikweli!
basi atuambie muda huo muafaka wa kuwa na fikra za kubadili katiba utafika lini
 
Hahaaa

Sometimes nikisoma mawazo ya viongozi wetu nacheka mwenyewe....pengine kichwani ana idea ya kubadili katiba in 2050...!!
 
Back
Top Bottom