Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Anaandika Gerald John Komba, mtoto wa kwanza wa marehemu Kepteni John Komba.
________________________________
Wakati namuuguza Marehemu Baba, siku moja nilimshuhudia akilia Machozi. Nilimuuliza, kuna tatizo gani Baba?
Akaniambia "Gerald, ndugu zako wananiua"... sikumjibu kitu, lakini lile neno lilijirudia mara mbili mbili katika akili yangu, baadae nikaona ni kauli ya kuipuuzia kwa sababu niliiona kama ilitoka kutoka kwa mtu imara sana ninayemjua muda wote, Baba asingeweza kukiri kitu kama kile, kwanza hakuwa mwepesi kuongea mambo mazito namna ile.
Baadae akaendelea "Gerald, leo Benki inanifilisi na mali zangu zinashikiliwa. Ndugu zangu wanafanya Sherehe, wanakula na kulewa kwa kuipongeza Benki kunifilisi. Hawa hawa niliowahifadhi, watoto wao walikuja kwangu uchi nikawavisha na wengine nikawasomesha. Kuna ambao leo wangekuwa magerezani au wangekuwa wamekufa lakini ni mimi nilietumia jina langu kuwatoa vifungoni na kuokoa uhai wao, leo narudi kwenye umasikini niliopambana nao hadi hapa nilipo lakini hao hao wanafanya Sherehe kuwapongeza Benki kunifilisi, kweli?"
Aliniambia Baba, na wiki iliyofuata akafariki dunia kwa msongo wa mawazo uliomshambulia sambamba na kisukari, ukawa mwisho wa kuonana na baba yangu na kuongea nae hapa Duniani... naumia sana.
Sijaandika ili nikuumize rafiki yangu hapana, natamani tu nikuambie mawili matatu, huenda ukaelewa sura halisi ya hilo tabasamu unaloliona la huyo kiumbe aliye mbele yako.
FAHAMU KWAMBA, Sio kila unayemsaidia atapenda mafanikio yako, unaweza kutoa kwa moyo kumbe unajipalilia miiba ndugu. Kepten Komba aliwasaidia watu ambao wakati mauti inamvuta katika shimo wao walikuwa wanasherehekea na kuipongeza benki kumfilisi.
Kwa akili za kawaida haiingii akilini lakini mwanadamu hana hofu ya Mungu japo anamtaja mara kwa mara "Bikira Maria Mama wa huruma tuombee"
Leo wale wale waliokuwa wakifurahi mwenzao akiaga dunia na kuanza maisha mapya ya kaburi ndio hao hao wanaita "Press conference" na kupitisha bakuli kwa viongozi wakubwa tu wa nchi, kwamba wanatafuta mtu mwenye sauti ya uimbaji kama ya Kepten John Komba, wakati Komba huyo huyo ana mtoto wake anayeimba sauti ile ile kama ya baba yake, na wanakula njama ili waue kipaji chake ili asisikike, na hawataki kabisa kusikia Komba ana mtoto mwimbaji. Eee Mungu Umezidi upole!!Fanya hima Baba kuisimamisha dunia ili nishuke maana dunia ina Mambo Magumu sana.
Rafiki nimeandika ili usije ukadhani watu wakubwa wanapokuja kwenu wakitabasamu, eti hawana majeraha katika mioyo yao, hapana, wako wanaolia na wanaowaumiza ni watu wa karibu yao sana lakini hawasemi.
Nakuandikia ili usije ukafikiria kwamba, unapomsaidia atakusaidia baadae, we toa tu, usikumbuke Shukrani, maana wanasema fadhila ya punda ni mateke.