IamBrianLeeSnr
JF-Expert Member
- Nov 10, 2022
- 2,010
- 4,179
Habari wanajamii, nielekee kwenye hoja husika moja kwa moja.
Nilikuwa na matarajio mengi sana juu yake lakini imekuwa ndivyo sivyo. Nilifikiria sana baada ya kumfungulia thread/Uzi kwakuwa nilimhada na kumpenda sana ila haikuwa bahati yangu kama wasemavyo wahenga, ng’ombe wa maskini hazai, hili ni kweli kabisa.
Hivyo kwa hali hii baada ya kutambua ukweli nimeazimia kusonga mbele na kuweka akili yangu kwenye majukumu yangu zaidi. Nafahamu ipo siku nitapata mwingine mwenye upendo wa kweli zaidi ya huyu aliyeuponda na kuumiza mtima wangu, nina hakika Mungu atanipa mwongozo mzuri sana juu ya hili na kunisimamia vizuri katika hili.
NB: Wanawake wazuri na wenye hekima bado wapo wengi, sitakata tamaa ya kupenda kabisa, nitampata mzuri zaidi yake naamini.