Halafu wewe mfuasi wa lucifer, usidhani mimi ninacheza ama kutaniana na shetani.
1). Kwanza naagiza malakika Coalieli akuonyeshe nafasi yako halisi unayostahili, kwa sababu unajifanya na wewe ni binadamu wakati umejaa mashetani,
2). Laana zote unazozikusudia, si kwangu na uzao wangu tu, bali kwa binadamu yeyote, kwa kuwa unatumiwa na shetani, zikurudie wewe mwenyewe na sio watoto wako.
(chukua hii).
Zaburi 109:17, Yeye alipenda kulaani watu, laana na impate yeye (yaani wewe) mwenyewe. Hukuwatakia wengine baraka, basi asipate (usipate ) baraka wewe mwenyewe.
3). Usijidanganye kwamba una ubavu wa kuni laani na watu wangu. Mungu wangu ni Mkuu sana na sikia asemavyo kwa habari ya ulozi na laana za kichawi uzitumainizo:-
Hesabu 23: 23 Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu.
4) Laana zako hazina sababu ya kunigusa mimi na watu wangu wote, kwa kuwa nimehesabiwa haki na Mungu kwa njia ya Agano la Damu ya Yesu Kristo.
Mithali 26:2 Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi, ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu.
Lakini kwa kuwa umekusudia maovu juu ya nyumba ya Mungu, bila shaka baya litakupata wewe ghafla iwapo hautatubu uovu wako na kuuacha "Kwa Jina La Yesu Kristo".,