Mpaka leo kuna watu wanaishi nyumba za kupanga?

Kijana! Usiwasimange vijana wenzio.Hujui mapito wanayopitia ni ya namna gani. Wewe unatakiwa tu umshukuru Mungu aliyekujalia wazazi na hatimaye ukaishi kama ulivyotutajia.
Kwamba wazazi wao alichemka hilo acha kabisa ndg. zingatia na kumbuka vijana wengine labda hawawajui wazazi wao, wengine wazazi wao walishatangulia mbele za haki wakati wao wakiwa ni wadogo au wengine wazazi hawakuwa na uwezo hata kama walitamani sana kuwafanyia watoto wao kama wewe wazazi wako walivyokufanyia.
Ili kurudisha fadhila kwa Mungu, hebu jiwekee ka-tabia ka kuwahurumia na kuwasaidia vijana wenzio japo kidogo kulegeza vyuma vilivyokaza.
 
Haya wahi wali maharage kabla haujaisha hapo kwa mama ntilie
 
Mkuu umeamua kuja kuchekesha watu siyo.. uzuri wa JF wote matajiri.
 
Japo hukutumia njia au lugha nzuri kufikisha ujumbe, ujumbe wako bado una mantiki. Ni vyema wazazi kupambana kuwajengea future nzuri watoto kwa kuwatafutia rasilimali kama viwanja au hata kama mfuko unaruhusu, kuwajengea ili watoto wanapoanza maisha, wasianzie kwenye sifuri.
 
Tunakusamehe bure. Kuna vichaa vya aina nyingi hicho ulicho nacho ni kichaa pia!! Huwapata watu ambao hawakuwa na ndoto ya mafanikio halafu wakajikuta wamepata kitu kidogo!! Pole!!
 
Wote tukijenga nani ataitwa mpangaji??
Wenye nyumba wanaotegemea nyumba zao kama njia ya kipato wataishije??Acha tusidiane maisha.
 
Duniani tunapita, sie makao yetu ni mbinguni.

Sasa wewe unajiona mjanja kujenga njiani, hapa tutapanga tu. Tutajenga kwa dhahabu huko tuendako, we jenga kwa tofali saivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…