Enyi watu badilikeni basi inakuaje mpaka leo kuna watu wanatumia tecno? Kuna jamaa mmoja nimepishana nae njiani eti linatumia tecno aisee nilishikwa na kichefuchefu nusura nitapike yaani jinsi nilivyokerekwa na kuchukia baada kumuona linatumia tecno hebu badilikeni.
Yaani mimi nikimuona mtu anatumia tecno na infinix hata akiniomba msaada simsaidii jinsi ninavyokerekwa hivyo yaani mtu akitumia tecno na infinix mimi naona kama ni wagonjwa akili.
Serikalu fanyeni muanze kutoa mikopo ya hizo za Samsung na iPhone watu waache kutumia mabomu.
This thread posted by using Samsung note 10 plus 5G
Kwa tunaojua kompyuta tunawacheka mnaopigwa pesa kifala kununua bidhaa za Apple na wadogo zao katika sekta ya simu, yaani Samsung.
Hizo shobo unazojaribu kuleta zilianziaga kwenye kompyuta ambako kulikuwa na vita kati ya Microsoft na Apple.
Kiufupi Apple wamejikita zaidi kwa wateja wanaopenda sifa. Wanawapiga bei kubwa kwa teknolojia ileile inayopatikana kwa bei ndogo kwa kampuni zingine.
Wanajua watu wanaopenda sifa wanapenda kujivunia kwamba wanamiliki vitu vya bei kubwa.
Ila kama unajua kitu inayoitwa "value for money" katika manunuzi na kama unajua kuchambua teknolojia ya kompyuta huwezi hata siku kujisifia kwa kununua bidhaa za Apple.
Watu wanaotumia bidhaa za Apple ni watu shallow, wapenda misifa na hawajui mambo ya teknolojia kivile ndo maana inakuwa rahisi kwa wao kupigwa.
Na vilevile mmedandia bidhaa ambazo zimelenga soko la Marekani. Marekani kuna pesa za burebure kwa sababu ndo nchi pekee ambayo pesa zake zinaongoza kwa kutumiwa na nchi zingine duniani.
Kwa hiyo uhitaji wa nchi zingine wa dola ya Marekani unaisaidia sana Marekani kuchapisha dola nyingi bila ya kushusha thamani ya dola, na hivyo kupelekea uwepo wa pesa nyingi za bure Marekani, na kufanya bei za vitu vya Marekani kuwa kubwa.
Sasa wewe Mtanzania unapojiingiza katika kununua bidhaa zilizolenga soko la Marekani kwa pesa zako za madafu unakuwa unapoteza hela bila kujijua.
Kwa simu za mkononi sasa hivi hakuna brand inayotoa "value for money" nzuri zaidi ya TECNO na Infinix.
Falsafa ya TECNO na Infinix imeigwa kwenye TV za kisasa na kampuni ya Hisense. Sasa wewe na ufala wako nenda kanunue flat screen za Samsung uingie kwenye vyoo vya sokoni kudandia bidhaa ambazo zimelenga nchi zenye ukwasi kuliko Tanzania.
Hakuna kitu ambacho utakipata kwenye iPhone au Samsung ambacho TECNO na Infinix hawana.
Utakachopata iPhone ambacho TECNO na Infinix hawana ni bei kubwa tu. Lakini katika ubora hakuna tofauti kati ya high-end TECNO/Infinix na iPhone toleo lolote jipya.