Mpaka Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani, uchumi wa Tanzania ulikuwa ni mkubwa kuliko wa Kenya. Marais waliomfuatia walikwama wapi?

Mpaka Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani, uchumi wa Tanzania ulikuwa ni mkubwa kuliko wa Kenya. Marais waliomfuatia walikwama wapi?

Weka hapa hizo takwimu, hata logic ya kawaida tu inakwambia, labda nikuulize kwa nini Jumuiya ya AM ilivunjika kama ni kweli Tanzania ilikuwa ni tajiri zaidi ya Kenya? Unaijua sababu hasa?
takwimu zipo kwenye video clip ya uzi. rudia kuusoma uzi, comrade!
 
Mwalimu hakuacha uchumi wowote sema Mwalimu kaondoka wakati Moi na mwenyewe keshavuruga uchumi wa Kenya!

Kilichowasaidia Wakenya na ndio maana wakatupiga gap ni kwa sababu tayari uchumi wao ulikuwa kuwa kwenye private sectors!

Sasa wakati sisi tuna-struggle kuondokana na uchumi hodhi ambao ulikuwa umeshavurugika kuanzia mwishoni mwa miaka ya 70, na hatimae kuuingiza kwenye private sector, Kenya tayari walishakuwa na misingi imara ya ya private sector.

Na ndio maana, hata wakati TZ inaingia kwenye soko huria, moja ya kampuni ambazo zilikuja kuwekeza sana TZ ni kutoka Kenya kwa sababu tayari walishakuwa na strong private sector!
Upo vizuri
 
takwimu zipo kwenye video clip ya uzi. rudia kuusoma uzi, comrade!

Weka chanzo cha takwimu zako, isitoshe nimekuuliza kwa nini Tanzania yetu ilijitoa Jumuiya ya AM kama ilikuwa tajiri kuliko Kenya? Tanzania miaka yote tulikuwa tunategema bidhaa kutoka Kenya, sasa kwa nini kama tulikuwa na uchumi mkubwa? Ni baada ya kuanzia miaka ya 90' ndiyo tukaanza kuwa na Makampuni yetu ambaye yaliweza kuuza bidhaa Kenya kabla ya hapo kila kitu kilitoka Kenya, kwa nini?
 
Hizi porojo kweli Tanga wezi wengi, nyerere aliyekuwa kibaraka wa wazungu unajaribu kumsafisha kwa jiki, kadanganye watoto wenzio huko madrasa
Ana kashfa gani ambayo mtu mdogo kama mimi nianze kumsafisha? Mtazamo wako sio lazima iwe wangu sababu wewe si biblia wala Quran.
Ili hoja iwe ina mashiko, toa evidence za namna gani Nyerere alikuwa kibaraka wa wazungu.
Vinginevyo nikukumbushe tu, Hakuna watu walioiletea shida nchi yetu kwa ubabaishaji wao huku wakijidai ni wazalendo, kama Baadhi ya nyinyi mnaojiita wazee
 
Siyo kweli, haijawahi kutokea, mpaka Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani Tanzania yetu ilikuwa nchi ya 3 kwa umaskini Duniani baada ya Baglandeshi na Msumbiji, Kenya haijawahi kuwa nchini hivyo kwa maana ni capitalistic economy tangia ukoloni, miaka ya 70 Tanzania ilikuwa inategema misaada ktk nje kwa > 85%, Kenya haijawahi kutegemea misaada kwa kiwango hicho, siku zote imekuwa ikifadhili bajeti zake kwa kodi kama tufanyavyo sisi leo hii.

Tanzania yetu haijawahi kuipita Kenya Kiuchumi tangia kuchukuliwa na Mkoloni Muingereza labda wakati wa Mjerumani hapo sijui hali ilikuwaje, ...
Kenya walianza kunitegemea kwa budget baada ya ile kashfa kubwa ya 1992. Hata hivyo, Kenya was and has always been a preferred investment destination in the region
 
Kenya walianza kunitegemea kwa budget baada ya ile kashfa kubwa ya 1992. Hata hivyo, Kenya was and has always been a preferred investment destination in the region

Tanzania hatujawahi kuwa na Uchumi mkubwa kuliko Kenya, na hii inaanzia kwenye Ukoloni, Kenya ndiyo iliyokuwa Makao makuu ya British East Afrika, na makao makuu ya British East Afrika yalikuwa Nairobi na siyo Dar, hata Umoja wa Afrika Mashariki ulianzishwa na Uingereza na waliweka makao makuu Nairobi ya karibia kila kitu na Dar na Kampala zilikuwa ni matawi tu, na ndiyo moja ya sababu ya huo umoja kufa, ...
 
Mtaongea Sana, lakini ukweli ni kwamba Tanzania na kenya zinazidiana kwenye bahadhi ya vitu, yahani kuna bahadhi ya sectors kenya wapo vizuri zaidi ya Tanzania na kuna bahadhi ya sectors Tanzania wapo vizuri kuliko Kenya.

Lakini mwisho wa siku hizi nchi mbili zote ni utopolo, kenya ubepari wao unafanya viongozi wa kishirikiana na mabeberu kuifilisi nchi yao kwa masilai yao binafsi na kuacha raia wengi wakihishi kwenye lindi la Umasikini, wakati Tanzania ujamaa umetengeneza jamii ya watu wavivu na wajinga ambao umekua mtaji wa viongozi wetu kuipeleka nchi wanavyotaka wao.

Mwisho wa siku kenya na Tanzania zote ni nchi maskini
 
Kuna shida mahali.

Pamoja na watu kumnanga (very incorrectly and unfairly) Mwalimu Nyerere (RIP mzee wetu) kuhusu sera zake za uchumi, inaonekana dhahiri kuwa alikuwa akifanya vizuri zaidi kiuchumi kwa kuchukulia nchi ya Kenya kama benchmark. Nimeichukulia Kenya kama benchmark kwa vile ndiye mshindani wetu mkubwa kiuchumi kwenye EAC na mara zote Tanzania tumekuwa tukifanya kila jitihada kutaka kuwa juu yake.

Mnyonge mnyongeni lakini...

Sasa ukiangalia graphic trend kwenye video clip hii hapa chini utagundua kuwa wakati mwalimu alipokuwa anaondoka madarakani, Tanzania ilikuwa always juu ya Kenya kiuchumi (GDP) miaka ya 80s hadi anaondoka ofisini 1985. I mean pamoja na changamoto nyingi sana zilizopelekea mdororo wa kiuchumi kwenye late 70s (kuvunjika kwa EAC, vita vya Kagera, nk), bado Tanzania ilibaki kuwa ni "economy giant" kwenye EAC.

Sasa embu angalia performance ya marais waliofuata (ukimuondoa mzee Ruksa) vs Kenya kuanzia 1996:

Mkapa:
1996 aliingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $6B
2005 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $2B
Alijitahidi kupunguza GDP gap, so tunaweza kumpongeza kwa hilo lakini alishindwa kufanya alichokifanya Mwalimu (yaani kuifanya TZ iwe economically superior to KE)!

JK:
2006 aiingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $8B
2015 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $17B
JK aliruhusu gap lipanuke zaidi, pamoja na kwamba alijitahidi ku boost per capita kwa kiwango kikubwa kuliko Mkapa ($480B vs Mkapa's $330B).

JPM:
by 2016 Kenya walikuwa wametuzidi GDP kwa $20B
by 2020 Kenya tayari wameshatuzidi GDP kwa $44B
JPM is the worst performer vs Kenya. Sijui itakuwaje tukimpa tena nchi October - tunaweza kujikuta Kenya wametuzidi kwa $100B!

Kazi kwenu Watanzania. October hiyo yaja!

GDP na GNP ni kamfumo ka ubepari na huko ndio kana mashiko haswa. Kwa nchi kama TZ kuzungumzia hayo mambo ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa kwa enzi zile, japo kwa sasa si haba sababu kiasi fulani yanatiliwa maanani ila sii kipimo halisi cha ukuaji wa uchumi bali kuangalia affordability ya watu kuwa na uwezo wa kupata mahitaji yao muhimu.

Yapo mataifa ambayo yana per capita kubwa sana (kama vile EQUATORIAL GUINEA) ila wanaishi maisha duni sana, the same goes to Kenya
 
wacha matusi nyang'au wewe 😅😅😅...!! una maana Watz bado ni wavivu hata sasa chini ya #hapakazitu??!!
Hapa kazi tu) anayo bidii na bidii yake ni ya kuwaamsha wa vivu ambao ni wengi sasa. Eh bwana eh fanyeni kazi kwa bidii uvivu huu una wagharimu sana...amkeni saa kumi asubuhi
 
Kuna shida mahali.

Pamoja na watu kumnanga (very incorrectly and unfairly) Mwalimu Nyerere (RIP mzee wetu) kuhusu sera zake za uchumi, inaonekana dhahiri kuwa alikuwa akifanya vizuri zaidi kiuchumi kwa kuchukulia nchi ya Kenya kama benchmark. Nimeichukulia Kenya kama benchmark kwa vile ndiye mshindani wetu mkubwa kiuchumi kwenye EAC na mara zote Tanzania tumekuwa tukifanya kila jitihada kutaka kuwa juu yake.

Mnyonge mnyongeni lakini...

Sasa ukiangalia graphic trend kwenye video clip hii hapa chini utagundua kuwa wakati mwalimu alipokuwa anaondoka madarakani, Tanzania ilikuwa always juu ya Kenya kiuchumi (GDP) miaka ya 80s hadi anaondoka ofisini 1985. I mean pamoja na changamoto nyingi sana zilizopelekea mdororo wa kiuchumi kwenye late 70s (kuvunjika kwa EAC, vita vya Kagera, nk), bado Tanzania ilibaki kuwa ni "economy giant" kwenye EAC.

Sasa embu angalia performance ya marais waliofuata (ukimuondoa mzee Ruksa) vs Kenya kuanzia 1996:

Mkapa:
1996 aliingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $6B
2005 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $2B
Alijitahidi kupunguza GDP gap, so tunaweza kumpongeza kwa hilo lakini alishindwa kufanya alichokifanya Mwalimu (yaani kuifanya TZ iwe economically superior to KE)!

JK:
2006 aiingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $8B
2015 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $17B
JK aliruhusu gap lipanuke zaidi, pamoja na kwamba alijitahidi ku boost per capita kwa kiwango kikubwa kuliko Mkapa ($480B vs Mkapa's $330B).

JPM:
by 2016 Kenya walikuwa wametuzidi GDP kwa $20B
by 2020 Kenya tayari wameshatuzidi GDP kwa $44B
JPM is the worst performer vs Kenya. Sijui itakuwaje tukimpa tena nchi October - tunaweza kujikuta Kenya wametuzidi kwa $100B!

Kazi kwenu Watanzania. October hiyo yaja!

Na Lissu ndiyo aliyemtukana sana Mwalimu Nyerere. Kumbukumbu zipo
 
Umesema Mkapa aliondoka 2005 wakiwa wametuzidi kwa $2B halafu tena JK ameingia wakiwa wametuzidi kwa $8B
Sijaelewa hapo boss.!
 
Ethiopia is massive and rich. Their problem was a prolonged wars.
Kenya assimilated most of the investors coming in this region because of their political approach to the economy.
Time is up now for others to catch up. Kenya is marred by corruption. The country is stinking corruption almost in every walk of life. Before we know , if they dont work to rectify the problems now, they will be operating in the world of shit
No country on this continent that can boast of being corruption free.

In Tanzania the government is spending money without the approval of the parliament but only the president is the one who approves in direct violation of the provisions of the government procurement act of 2004.

There are some state corporations and institutions whose finances cannot be audited by the CAG Office under order from the Head Of State..!! All this shows nothing but hallmarks of surreptitious acts of corruption.
 
nyerere ndio aliyeharibu ustawi was taifa kwa kutuachia katiba ya kifalme,uchumi wetu unaharibiwa na watawala wenye mamlaka makubwa
kupiliza,embu imagine MTU anachukua hela za umma na kwenda kununua korosho,lengo awakomeshe wafanya biashara,Tanzania ni chi ya wajinga
 
No country on this continent that can boast of being corruption free.

In Tanzania the government is spending money without the approval of the parliament but only the president is the one who approves in direct violation of the provisions of the government procurement act of 2004.

There are some state corporations and institutions whose finances cannot be audited by the CAG Office under order from the Head Of State..!! All this shows nothing but hallmarks of surreptitious acts of corruption.

Kuamua kutumia hela bila bunge kuamua ndio corruption? Which state corporations which the AG is not allowed to audit?
 
Kuamua kutumia hela bila bunge kuamua ndio corruption? Which state corporations which the AG is not allowed to audit?
Matumizi ya pesa za umma lazima yaidhinishwe na bunge sasa hii ya mtu mmoja kunyakua mamlaka ya bunge inatoka wapi na sisi walipa kodi tunajua kazitumiaje? Hili ni kosa la jinai kabisa.

Shirika kama Atcl mahesabu yake yanakaguliwa na nani na ikulu matumizi yake yanakaguliwa na nani haikaguliwi ndio maana rais anajichotea pesa na kutembea nazo mikoani akizigawa ovyo apendavyo.

Halafu ujue AG hana jukumu la kukagua mahesabu ya serikali ila ni CAG.
 
Mbona unatoa povu tu sijaona fact hapo kwaiyo vitimbi inavyofanya kenya kutaka kuaminisha dunia Tz kuna corona huvioni?
Mimi ningependa kusema hivi, jmbo la kwanza ni mimi ni mkenya na mara nyingi huwa nashindwa kueleza tofauti hii yaletwa na nini haswa, samehea kiswahili changu.
Anyway kuna mambo kadhaa ambayo nilifanya uchunguzi wangu na kuona ndio yaweza kuwa shida halisi. Awali nilijiuliza mbona iwe hivi wakati TZ lina idadi kubwa zaidi ya watu ,TZ ina eneo kubwa la ardhi tena lenye rotuba na madini kibao? and so I came up with the following issues which if you tanzanians mkiyatilia maanani basi mnaweza kutu pita tena kwa mbali;

1. UVIVU
Kuna muda fulani nilikuwa tanzania kwa muda wa mwezi mmoja hivi na nilizuru sehemu za arusha, manyara, ngorongoro na serengeti. Jambo nlilojionea pale lilinishangaza, watu wengi hawana msukumo wa kufanya kazi, jambo hili lina wadhuru sana kiuchumi. inastahili muwe mnaamka saa kumi asubuhi na kuchapa kazi ya aina yoyote kwa udi na uvumba. kenya twa fanya hivyo,,, twaamka mapema na twa fanya kazi kweli.

2. HASIRA ZA KIPUZI KUFWATIWA MAAMUZI YASIYO FAA
Kuna kipindi kenya ilizozana na uganda kuhusu migingo, tz wakashika ngombe za kenya na kuzipiga mnada halafu pia tz waka choma vifaranga zetu. tz ikaikataza kenya airways kupaa katika anga ya tz among others.
Chunguzeni kwa makini vile kenya huwa ina handle such issues. WE SIMPLY DONT FIGHT BACK, actually what we do ni kutafuta mazungumzo ya ki diplomasia ili kile kidogo tunapata kutoka tz au ug kiuchumi na tuendelee kukipata. Mna stahili kufata mfano huo kwa sababu TZ mnapenda sana kulipza kisasi mkiddani ndio njia bora.

3.KUTOPENDA WAGENI

Leo hii ukija kenya utakuta wa chaga kibao, utakuta wasomali kibao, utakuta wahindi kibao, utakuta wa sudanese kibao... hawa wote tunaishi nao kwa upendo hutojua hata kama si wakenya. kipindi kile nilikuwa TZ nilijionea ubaguzi openly na sio wakufichwa ...niliambiwa kabisa peupe. ilifika wakati hadi nikaletewa askari . ilhali wakati huo mimi nilikuwa tz kihalali kabisaa.
Cha ukweli hapa hampendi wageni, kuna vile wageni wanawakera kimpango sijawahi elewa ni kwa nini na jambo hili pia lina wagharimu kiuchumi.
Acheni wageni waje hata na waishi huko , wafanye biashara na hii kwa njia moja au nyingine itawainulia uchumi.

USHINDANI MBAYA

Mashindano ya aina yoyote ilre ni mazuri lakini do not put hard feelings ndani yake, shida nyingine hii hapa, mna machungu sana na kenya kwa kuwa ipo juu. machungu haya huwa yanafanya kubaki nyuma maana mtu hujisahau na kuanza kufikiria ya mwenzake sana. although hili sikulipa uzito sana.

ni kitambo niandike kiswahili kinachokaa sanifu hivi... I have really tried.
 
Matumizi ya pesa za umma lazima yaidhinishwe na bunge sasa hii ya mtu mmoja kunyakua mamlaka ya bunge inatoka wapi na sisi walipa kodi tunajua kazitumiaje? Hili ni kosa la jinai kabisa.

Shirika kama Atcl mahesabu yake yanakaguliwa na nani na ikulu matumizi yake yanakaguliwa na nani haikaguliwi ndio maana rais anajichotea pesa na kutembea nazo mikoani akizigawa ovyo apendavyo.

Halafu ujue AG hana jukumu la kukagua mahesabu ya serikali ila ni CAG.

Kazi mnayo. Ndio maana nasema Dola mtaisikia redioni
 
Back
Top Bottom