Mpaka sasa Umejifunza nini kuhusu Maisha?

Mfilisiti

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2020
Posts
396
Reaction score
1,958
Wakuu poleni na Majukumu, moja kwa moja kwenye mada .
Binafsi Mpaka sasa nimejifunza haya hapa👇👇
1: Kama hutapambana kufanya kazi kwa bidi kutimiza ndoto zako mwenyewe, kuna mtu atakuajiri na kukupa kusudi.

2: Maisha hayangojei uwe sawa, amka kila siku na uendelee kusonga mbele.

3: Wathamini sana Watu wanaokusema na kukufuatilia Maisha yako

Maana si kazi rahisi Mtu kuacha Matatizo yake na Kuyabeba yako.

4: Kaka jitaidi kuwa Smart, piga pasi na kaperfume kwa mbali.

Kuna wanawake Shida yao ni Mwanaume Smart tu.😀😀

5: Brother Unampenda? Mwambie Akatae yaishe, kuliko kumtumia hizo HEY,HI,Umekula??,Karibu Chai, n.k(be straight to the point)

6: Kuna mpaka ‘’Mabadiliko ya tabia ya Nchi’’ halafu wewe bado unaamini huyo mpenzi wako hawezi badilika??? really😀😀

7: Umri wa Miaka 30 ni Miaka mingi sana Kukaa Ofisini huku ukisubiri kuambiwa ni kipi chakufanya.

8: Maisha ni bora 100% wakati hakuna mtu anajua chochote kukuhusu wewe.

9: Ugali dagaa ni chakula kitamu sana endapo usipozingatia harufu ya pilau kwa jirani yako.

10: Kadri Umri unavyoenda ndio nagundua kwa nini baba alikua hataki kufungulia redio kwa sauti kubwa, jamani KELELE na MADENI haviendani kabisa😀😀

11: Ukifatilia sana Maisha ya Watu Utapishana na Maisha yako.

12: Kila mtu anayo hekima, hadi pale tu atakapo fungua mdomo wake.

Binafsi nimechelewa sana kujua ukweli kuhusu Maisha, hasa ukitokea kwenye familia inayoamini kwamba ''education is better than Money''
Yaani hata kama kuna fursa ya Kuuza mchicha mtaani basi ukiifanya dharau na kejeli utakazokutana nazo sio za nchi hii.
Je? wewe mpaka sasa umejifunza nini kuhusu maisha????
 
Maisha yako ni jukumu lako mwenyewe 100%..

Watu hawabadiliki bali wanaamua kujidhihirisha jinsi walivyo.

Usitarajie lolote kwa mtu yeyote maana matarajio mengi yanaumiza.

Namna nzuri ya kushinda ni kuacha kushindana, kama mtu anakushinda kwa mdomo wewe mshinde kwa kunyamaza.
 
Nimejifunza zamani watu walikua wanaombana moto ila siku hizi wanapelekeana
FB_IMG_1668433228265.jpg
 
Kuishi na watu kwa wema popote pale na yeyote yule,kwa umri wangu 30+ nimeshuhudia watu waliokuwa hohehahe sasa wana vitu na waliokuwa smart leo ni makapuku.

Shida ya maisha ya kibongo watu wanaishi kwa visasi utakachofanya leo kikamkwaza atasubiri akijua ipo siku itakuwa na kwako so kwa muktadha huo ni kuishi kwa akili tu
 
Wakuu poleni na Majukumu, moja kwa moja kwenye mada .
Binafsi Mpaka sasa nimejifunza haya hapa👇👇
1: Kama hutapambana kufanya kazi kwa bidi kutimiza ndoto zako mwenyewe, kuna mtu atakuajiri na kukupa kusudi.

2: Maisha hayangojei uwe sawa, amka kila siku na uendelee kusonga mbele.

3: Wathamini sana Watu wanaokusema na kukufuatilia Maisha yako

Maana si kazi rahisi Mtu kuacha Matatizo yake na Kuyabeba yako.

4: Kaka jitaidi kuwa Smart, piga pasi na kaperfume kwa mbali.

Kuna wanawake Shida yao ni Mwanaume Smart tu.😀😀

5: Brother Unampenda? Mwambie Akatae yaishe, kuliko kumtumia hizo HEY,HI,Umekula??,Karibu Chai, n.k(be straight to the point)

6: Kuna mpaka ‘’Mabadiliko ya tabia ya Nchi’’ halafu wewe bado unaamini huyo mpenzi wako hawezi badilika??? really😀😀

7: Umri wa Miaka 30 ni Miaka mingi sana Kukaa Ofisini huku ukisubiri kuambiwa ni kipi chakufanya.

8: Maisha ni bora 100% wakati hakuna mtu anajua chochote kukuhusu wewe.

Binafsi nimechelewa sana kujua ukweli kuhusu Maisha, hasa ukitokea kwenye familia inayoamini kwamba ''education is better than Money''
Yaani hata kama kuna fursa ya Kuuza mchicha mtaani basi ukiifanya dharau na kejeli utakazokutana nazo sio za nchi hii.
Je? wewe mpaka sasa umejifunza nini kuhusu maisha????
Duniani hamna haki,mwanaume kupambana,Wadada wa kuletewa na kuongozwa,siasa ni zaidi ya uhalifu,Mtanzania uaminifu sifuri,mvivu wa kufikiri na hata kwenye kazi.mwenye nafasi anaitumia kwa manufaa yake binafsi.
 
Back
Top Bottom