Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Nataka nitangaze kuwa naunga mkono msimamo wa Chama cha CHADEMA wa NO REFORMS NO ELECTION na pia nauunga mkono uongozi wa sasa wa CHADEMA wa Mwenyekiti Lissu na Makamu wake (bara) John Heche.
Uongozi huu umeleta energy mpya, matumaini mapya na imani mpya kwa wananch, hata hivyo kuna mambo kadha wa kadha ya msingi sana uongozi huu mpya haujafanya na pengine inaonekana hauna interest ya kufanya. Nitaeleza.
1. Mpaka Sasa Uongozi huu umeshindwa kuweka pressure ya kutosha ili Kijana wa Chama Deusdedit Soka apatikane akiwa Hai au mfu.
Kwenye hili suala, Lissu naye amegeuka bubu, Lissu wa kipindi cha kuutafuta uenyekiti wa CHADEMA alikuwa akimzungumzia Soka. Ila Lissu Mwenyekiti inaonekana hana Interest hata kidogo na hatma ya hawa vijana. Siyo tu kwamba hamzungumzii kabisa kijana Deusdedith Soka na wenzie lakini haonyeshi msuli wa chama na ushawishi wa nafasi yake kuweka pressure ili kijana huyo ambaye alikuwa kada wa chama, tena kada mpambanaji aweze kupatikana akiwa hai au mfu. Hii inapunguza mori wa vijana waliodhani kuwa wakipata mwenyekiti mpya hasa Lissu, hili suala la upatikanaji wa Deusdedith Soka ama akiwa hai au mfu litapata msukumo mkubwa zaidi. Kumbuka moja ya sababu za kumuunga mkono Lissu kwenye uenyekiti ni imani kuwa Mbowe amekuwa soft kwenye ishu ya Deusdedith Soka. Tunashangaa Lissu amekuwa SOFTER TEN TIMES.
2. Lissu mpaka sasa ameshindwa kutoa Shukrani Rasmi kwa Diaspora.
Ili kufanikisha azma yake ya kugombea uenyekiti, Lissu aliungwa mkono na watu wengi nje na ndani ya nchi. Watu walijitolea muda wao, Pesa zao, organisation n.k LAKINI mpaka leo hii ameshindwa kwenda Clubhouse alipokuwa anapiga kambi kipindi siyo mwenyekiti lakini leo hii anashindwa kwenda hata huko kutoa shukrani kwa watu waliompambania kindakindaki. Ikumbukwe Diaspora wamekuwa wakifinance harakati nyingi tu za Chadema na hata Lissu mwenyewe. Sasa hapa Ishu siyo suala la kwenda au kutokwenda clubhouse ili kuongea na Base yake hii ya kisiasa. Ishu hapa inaonyesha kukosekana kwa GRATITUDE kwa ndugu Lissu, otherwise hebu niambie, unapata wapi muda wa kwenda Makerere Ugnda kumzungumzia Nyerere lakini huna Muda wa kuingia Clubhouse na kuongea na base yako hii?. Hii pengine inamaanisha kuwa Lissu anaichukulia hii base for granted, na inaonyesha kuwa pengine hana gratitude. Mbona zamani alikuwa akija clubhiuse mara kwa mara kutoa elimu na kuongea na base yake leo mbona anakacha?. Au anadhani kuwa labda Diaspora wanafaa kuwa ATM tu wa kutoa pesa lakini hana time nao baada ya kushika hstamu za chama?. Diaspora wana interests zao kwenye NO REFORMS NO ELECTION hasa ya URAIA pacha wanataka wasikie hilo linakuwa featured vipi.
3. Mpaka Sasa Lissu hajaeleza ule mchango wa Milioni zaidi ya 120 alizochangiwa kununua gari ziko wapi!
Kwa hivi sasa baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti ndugu Lissu tunaona anatembelea gari jipya, zuri, siyo lile la matundu ya Risasi. At the same time kuna pesa zaidi ya milioni 120 alizochangiwa na wananchi kununua gari, yeye aliliita gari la kazi. Hata hivyo Lissu amemute, yuko kimya, haelezi nini hatma ya hizo pesa, maana kwa sasa ana gari zuri. Je kwa nini hayuko transparent?, Je hizo pesa anakusudia kuzifanyia nini?. Je ipo haja hizo pesa aziingize katika chama ili zisaidie operesheni ya no reforms no election?. Kwa kiongizi makini lazima awe transparent na accountable kwa pesa zitokanazo na wananchi. Je Lissu atanunua lini hilo gari ambalo ameshindwa kulinunua kwa zaidi ya miezi Sita iliyopita?
4. Lissu na Heche hawajaeleza wamechangia sh ngapi kwenye TONE TONE.
Uongozi ni kuonyesha njia, ukiwa kiongozi inabidi uongozi kwa mfano. Yes umezindua operesheni ya Tone Tone, Je wewe umechanga?. Kama umechanga umechanga sh ngapi?. Au mchango wako ni siri ndugu mwenyekiti?, au mchango wako ni siri ndugu makamu mwenyekiti?.Umma unataka hamasa, wanachadema wanajua umuhimu wa kuchangia chama lakini Kiongozi akionyesha mfano inaleta hamasa zaidi. Mwananchi asiye na chama au asiye mwanachadrma hawezi kuwa na mzuka wa kuchangia kama haoni kama kiongozi wa chama na makamu wake wamechangia. SHOW US MR CHAIRMAN and MR VICE/DEPUTY CHAIRMAN how much you have put in TONETONE!