Mpaka sasa uongozi wa Lissu na Heche umeshindwa kufanya mambo ya msingi yafuatayo

Ndugu Kalamu, the best way ya kuwafanya viongozi wetu wawe makini, wasijisahau ni KUWAHOLD TO ACCOUNT. Hawa ukiwapa blank checque wanajisahau.

Tukiachilia mbali hilo, Je issue ya Deusdedith Soka huoni kuwa inahitaji extra push?
Inanisikitisha sana kutofautiana na wewe katika hili.
Ndiyo, inawezekanakabisa kwamba mada hii umeiandika kwa nia njema; lakini kwa bahati mbaya sana imekaa kama ni ya kuwa vunja moyo hawa viongozi!
Sote tunajuwa jinsi gani muda ulivyo mfinyu sana kufanya mambo muhimu kabla ya Oktoba, leo hii tunatafuta ajenda zinazotafuta kuwaondoa viongozi hawa kwenye kujipanga kufanya ajenda kuu zaidi ambayo itajumuisha hata haya unayosema viongozi wameyasahau?
Leo hii unataka Tundu Lissu aitishe maandamano kuwashinikiza serikali kuhusu vijana walio potea, kweli?
 
Sijui kama ni njaa, lakini kuna watu ambao ni vigumu kuwaweka kwenye kundi la wenye njaa kutokana na heshima waliyo jijengea kwa misimamo waliyo ishikilia kwa muda mrefu humu JF.
We elewa ndugu. Njaa haina baunsa.
 

Mimi naamini kuwa hii mada itawasaidia wawe vigilant. Na pia itawasaidia wajue kuwa umma anytime unaweza kwa bahati mbaya kuwa swayed in a wrong direction kupitia weaknesses zao. Kwa hivyo wajitahidi kuziba mashimo ili agenda kubwa ya NO REFORMS NO ELECTION iweze kwenda mbele!
 
Mimi siamini hivyo.
Historia ya nchi hii inajulikkana ni kiasi gani wananchi wake wamekuwa watiifu kwa chama ambacho kimekuwa mstari wa mbele kupigania maslahi yao, CCM. Ni wananchi hawa hawa wanao hitaji ushawishi mkubwa kuonyesha jinsi chama walicho kiamini kwa miaka yote kilivyo kwisha badilika na kuwa na maslahi tofauti kabisa na matarajio yao.
CCM ilichukua muda na ushawishi mkubwa kuwafikisha hapo wananchi. Usitegemee chama kingine kiibuke mara moja na kuwabadili wananchi, pamoja na matatizo mengi wanayo yashuhudia chini ya CCM.

kuna tatizo gani kuwapa fursa viongozi hawa wajipange kuipeleka ajenda kuu hii kwa wananchi; na badala yake tunatafuta njia za kuwachanganya kwa mada kama hii uliyo leta hapa leo?
 

Ndugu yangu, Deusdedith Soka na wenzie hawana muda ambao akina Lissu wanao.
Situation yao ni urgent!
 
We elewa ndugu. Njaa haina baunsa.
Watu hupoteza maisha kwa kulinda wanacho kisimamia kama binaadam. Akina Mwalimu Nyerere waliambiwa wachague kushiba kwa mshahara, au wakasimamie mapambano ya kupata uhuru.

Haya ya "njaa" unayo yasisitiza wewe ni ya akina Samia wanao amini kuwa kila mTanzania anayo bei ya kununua ubinaadam wake. Hakuna tusi kubwa zaidi ya hilo kwa mtu anaye jitambua.
 
Sasa wewe unataka akina Lissu wakawatoe kwenye 'situation' hiyo kwa njia zipi hasa?
Soka was CHADEMAs fresh blood, he can't dissapear in the darkness and the party gets tired to demand of his wherebouts from the government!.

You asked me of what ought to be done, Here is what I think should be done!.

Amplify the voice, invoke the party's machinery to put pressure on the government to bring Soka, alive or dead, and keep on demanding accountability for those whom the former chairman had identified as culpits of kidnappings in the country. Entice party members to unceasingly observe vigil for the kidnapped as a peaceful means of protest. Most importantly, keep discussion about Soka alive in the society.

Call on demonstrations!. Can't the new chairman put CHADEMA members on the streets to demand the release of their cadre?. Why not?
 
Ninashangaa mnapotoa excuses kwa uongozi wa sasa. Wengine hawataki kabisa kuona wakikosolewa. Natofautiana na wewe kwa sababu:
1. Uongozi wa sasa sio mgeni. Karibu wote walikuwa viongozi wa juu wakati wa Mbowe kwa hiyo shughuli za kuwashawishi wananchi walianza zamani. Hwakuibuka Januari.
2.Viongozi wa sasa walifikia uamuzi wa kupambana na Mbowe baada ya kuamini kuwa hana hoja mpya. Kwa sababu hiyo walitakiwa kujipanga namna watakavyojitofautisha na Mbowe mara walipoamua kumng'oa. Kusema kuwa wanahitaji muda ili wajipange inaweza kuonekana kama walikurupuka.
3. Ni wao ndio waliahidi kuwa watakuwa watu wa mchakamchaka lakini kinachosikika ni vikao vya kujipanga kwa ajili ya mpambano. Kuna matunda ya chini kama hayo ya wanachama waliopotea na waliouawa. Mpaka sasa njia wanazotumia zinaonekana ni ineffective. Wamemleta mjane wa mgombea wao lakini hawakutoa tamko lolote la namna watakavyomsaidia. Wanashindwa nini kuanzisha mfuko wa kuhudumia wahanga wa haya ambao maisha yao kwa kweli magumu? Ukiangalia uongozi ulivyosheheni wanasheria kwa nini mpaka leo hawasemi ile ahadi yao ya kuwafikisha wabaya wao mahakamani imefika wapi?
Wakati wa kampeni walimlaumu Mbowe kwa kutokuwa transparent katika matumizi ya pesa kiasi cha watu kuwa Mbowe anafaidika sana na mali ya chama. Kwa nini wasionyeshe tufauti yao kwa kuweka wazi hesabu za michango na matumizi yao? Kuna dhambi gani kumtaka Mwenyekiti aelezee kiasi alichochangiwa kwa ajili ya gari na ana mpango gani na michango hiyo? Hamuoni kuwa ukimya wake ndio unawapa ajenda CCM ambao walimchangia kwa mbwembwe? Hata kama alichangiwa yeye binafsi. Hauwezi kuendelea kuomba uchangiwe lakini unakuwa mkali unapoulizwa kuhusu matumizi ya hiyo michango!

Amandla...
 
Wanaweza pia kutumia social media zao kuhakikisha kuwa mtu akiingia tu anakutana na kilio chao kuhusu wakina Soka. Wanaweza kuweka mita inayoonyesha siku ambazo wamepotea au kuuawa bila maelezo ya maana. Wanaweza kuanzisha mifuko ya kushughulikia kesi zao na kuwahudumia wahanga wa hayo matumikio. Lakini ukienda sasa kwenye social media zao zimetawaliwa na picha za viongozi!
Aidha, wanaweza kuanzisha taratibu ya kuwa na dakika kadhaa za kuwakumbuka kila wanapofanya mikutano au wanapofanyiwa interviews. Ili mradi kuhakikisha kuwa jamii haiwasahau.

Amandla...
 
Pascal Mayalla alimuomba Mhe. Tundu Antipas Lissu awe anasoma Jamii Forums nina imani atasoma na kutafanyia kazi.

#NO REFORMS NO ELECTION
 
Hata wewe unaweza toa pakuanzia jinsi ya kufanya ili kuizalisha pressure waliotekwa na kupotezwa ni wengi
 
Hata wewe unaweza toa pakuanzia jinsi ya kufanya ili kuizalisha pressure waliotekwa na kupotezwa ni wengi
Deusdedith Soka alikuwa ni kiongozi wa CHADEMA, Mwenyekiti wa BAVICHA Temeke. Mwenyekiti hapaswi kupiga kimya kwa upoteaji wake!.
Kama Mwenyekiti anaweza kwenda Makerere university "kumchana" Nyerere, lazima muda wa kutosha anao wa kumpania kijana wa chama chake Deusdedith Soka!
 

Umeliweka vizuri sana.
 

..Samia Suluhu ndiye Amiri Jeshi Mkuu na ameshindwa kutoa maamuzi ili Soka na wenzake waachiwe.
 
Really?

Inaelekea hata hujaielewa kabisa dhana nzima ya NO REFORMS, NO ELECTION...

Ungekuwa unaielewa, usingeshindwa kuhusianisha maswala ya utekaji, mauaji, kupotea kwa watu nk ambayo msingi wake ni siasa za uchaguzi na madaraka na inajibu hata hoja yako hii...

Hili sio la Tundu Lissu, hili swali lielekeze kwa Rais Samia na serikali yake. Wananchi wake waliotekwa wako wapi..?
Mmmh, mbona una haraka sana?

Na mbona ni kama vile mnasubiri na kutafuta weak point ya kuukamata na uongozi mpya wa CHADEMA nyie...?

By the way, si ndo tu wana mwezi mmoja na nusu tangia washike madaraka? Unataka kila kitu kifanyike ndani ya muda huu mfupi...?

Team Freeman Mbowe na CCM, kama hamwezi kushiriki kwa moyo mweupe kwenye shughuli za chama, kaeni pembeni na acheni kuu - distract uongozi mpya...!!
Zina uhusiano gani na uenyekiti wake?

Kampeni ya mchango wa gari ulikuwa mpango mahususi wa wapenzi na mashabiki wa Tundu Lissu wenyewe kuamua kumchangia ili apate gari jipya. Umekosea kuliingiza hapa na kulihusianisha na uongozi wake..

Na kwa akili na ufahamu wako unadhani Tundu Lissu anaweza kuzitumia fedha hizi kinyume na malengo yake..?

Humjui Tundu Lissu bila shaka....

Kwa mambo ya fedha, Tundu Lissu yuko very clean, hilo ondoa shaka. Hana tabia ya ujanja ujanja wa ku - divert pesa isiyo yake, hana tabia ya na wizi au kutumia pesa isiyokuwa yake...

For instance, fedha ya mchango wa gari lake ina uhusiano gani na uenyekiti wake CHADEMA?

Mara ya mwisho alitoa updates nadhani ilikuwa mwishoni mwa mwezi November au mwanzoni/katikati ya mwezi desemba 2024 na jumla ya fedha ilikuwa kama 120+ milioni. Na azimio likawa fedha haitoshi kununua gari nzuri, imara inayokidhi mahitaji ya kuizungukia nchi. Ikaamuliwa michango iendelee ili kupata gari linalotakiwa..

Haina shaka kuwa, utapata updates soon...
Timu Freeman Mbowe haina shaka yoyote kuwa bado mna maruweruwe hamjapona vizuri...?

Kiongozi kuonesha njia ni kutangaza kiasi cha pesa ulichonanacho...?

You are after petty issues badala ya ku - focus kwenye mambo ya msingi...

Yaani kazi yenu nI kuketi huko mnakoketi na kutafuta udhaifu tu ili kupata la kusema...

Bado hamjapata bado...

NO REFORMS NO ELECTION iko fire na itajibu..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…