Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

MPAKA wa Namanga upande wa Tanzania umesitisha shughuli zote za kibiashara na nchi jirani ya Kenya kwa muda kutokana na nchi hiyo kutoamini vyeti vya ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya corona vya madereva wa malori wa Tanzania vinavyoonyesha kuwa hawajaambukizwa.

boda.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe, ameiambia Nipashe jana kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa Kenya kukiuka makubaliano ya pande hizo mbili, waliyotiliana saini Mei, mwaka huu kwa kuzuia madereva wa Tanzania, kukataa vyeti ili wawaruhusu kuingia Kenya.

“Nadhani wenzetu wana ajenda ya siri kutuhujumu kiuchumi, tumeshakubaliana dereva anapopimwa upande wa Tanzania aruhusiwe upande wa Kenya kwa cheti, sasa wamekiuka makubaliano, wakifika upande ule wanataka wawapime tena sijui wana maana ipi nashindwa kuwaelewa kabisa, tumeamua kuchukua hatua na haturudi nyuma,” alisema.

Katika makubaliano hayo waliamua katika lori itaruhusiwa dereva na wasaidizi wawili kuingia katika nchi husika wote wakiwa wamepimwa kama wana maambukizo ya corona.
Hata hivyo, alisema upande wa Kenya wamebadilika juzi (Jumatatu) kwa kuzuia na kutaka kuwapima tena.

“Pamoja na juhudi za mimi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, kuwasiliana na viongozi wenzetu wa Kenya, lakini zimegonga mwamba na ndipo tukaamua kuzuia vyeti vyote na magari ya mizigo kutoka Kenya pamoja bidhaa zote zinazoingia kutoka nchini humo hadi hapo tutakapokaa tena na kufikia muafaka maana sote tunategemeana, Kenya wanatuhitaji kama soko na sisi wanatuhitaji pia ili kuuza bidhaa,” alisema Mwaisumbe.

Alisema mwezi Mei makubaliano ya kuruhusu kuaminiana pande mbili yalikaliwa kikao na mawaziri wa mambo ya nje za nchi, makatibu wakuu, wataalamu na viongozi wengine wa mikoa na wilaya wa kutoka nchi mbili katika mpaka wa Namanga, kufuatia mazungumzo ya Rais John Magufuli na Rais Uhuru Kenyata ambao waliwaagiza viongozi wanaohusika kukaa na kufanya vikao na makubaliano, huku wakichukua tahadhari za ugonjwa huo na kuona namna ya kuendelea na biashara kwa nchi hizo.

Alisema kama hali ya kutoaminiana itaendelea, itawalazimu kutoa uamuzi wa kuigeuza Namanga kuwa bandari kavu na majirani Wakenya watashusha mizigo au bidhaa upande wake na Tanzania kuichukua na pia hata Tanzania itapeleka wa Tanzania ili Kenya waifuate.

“Nchi yetu ni huru inayojitegemea haihitaji kubembeleza nchi nyingine kufanya biashara kwa sababu sisi tunategemeana, haiwezekani mambo ambayo yameagizwa na marais viongozi wa chini hawatekelezi…linaashiria dharau na ajenda ambayo wanadhani ni siri iliyofichika kumbe sisi tunaifahamu, hatutaweza kuivumilia hata kidogo,” alisema.

Alisema, nia ya Rais Magufuli ni kuwasaidia watu wa hali ya chini kwa kuwa uamuzi huo unapofanyika wanao umia ni watu wa chini.

“Nataka nikuhakikishie ndugu kupima kipimo cha Covid-19 sio lelemama kinaumiza sana, sasa haiwezekani siku mbili mtu amechokonolewa pua, halafu anatoka upande wa Tanzania anaenda upande wa Kenya anafanyiwa kitu kile kile, sasa hali hii kwa kweli sio sahihi, tunataka hiyo agenda yao ya siri ijitokeze hadharani tushughulike nayo kuliko kutumia ugonjwa wa Covid-19, sisi hatutakuwa tayari,” alisema Mwaisumbe.

I've said several times KNY has always been having ILL MOTIVES with TZN. There is no such a thing as "Oooh you know hii mipaka iliwekwa na Wakoloni" !!! "Oohh sisi sote ni ndungu". The are just after one way benefiting !! They are just after US (KNYNS) and not WE !!!
 
Kuna wakati lazima upigane kutafuta Amani, Kenya anachokifanya ni kujidekeza tu nakujiliza liza Sasa Huyo dawa yake ni kuchukua maamuzi magumu walau ya Mwezi mzima ivi ili atie akili, Waswahili wanasema mtoto akililia wembe, kama tunakaa nao mezani tunapanga then wanaenda huko na kugeuka basi wanahitaji adhabu

Mkuu hii ni wrong approach - kuwa wote tukose. Tukubali kwanza nchi hizi mbili zina mbinu tofauti za kukabiliana na corona. Tusiwalazimishe kutumia za kwetu kwani hata wao walikubaliana na za kwetu. Kwani kuna ugumu na ubaya gani kama madereva wetu ambao tumewapima na kukuta -ve watapimwa tena???

Kumbuka hatuwezi kuwalazimisha kukubali majibu ya vipimo vyetu huku sisi tukiutangazia ulimwengu kuwa hatuna tena corona na hata tahadhari zetu bado ni za kiwango cha chini. Hakuna asiyejua kuwa hatupimi tena corona Tanzania!! Si kwa wageni wala wenyeji.

Jambo hili halihitaji sayansi ya rocket kulifahamu- sisi hatuwapimi madereva wao tena kwa sababu hatufanyi vipimo kabisa!! Na ndio yalikuwa makubaliano. Wametambua hatuthibitishi vipimo vyao - ndio sababu ya kukataa taarifa tunazoita “vipimo”.
 
Gud, hili ni kwa majirani zetu ambao wao hawana mgogoro; sasa vipi kwetu balozi wa Marekani anasema hali ya ugonjwa bado mbaya, halafu sisi tunasema wamebaki wanne, wakenya wamuamini nani hapa?!

Kwanini msiwaache wakapima wagonjwa wetu wao wenyewe wajiridhishe, km kweli wamebaki wanne pressure ya nini!.
 
MPAKA wa Namanga upande wa Tanzania umesitisha shughuli zote za kibiashara na nchi jirani ya Kenya kwa muda kutokana na nchi hiyo kutoamini vyeti vya ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya corona vya madereva wa malori wa Tanzania vinavyoonyesha kuwa hawajaambukizwa.

boda.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe, ameiambia Nipashe jana kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa Kenya kukiuka makubaliano ya pande hizo mbili, waliyotiliana saini Mei, mwaka huu kwa kuzuia madereva wa Tanzania, kukataa vyeti ili wawaruhusu kuingia Kenya.

“Nadhani wenzetu wana ajenda ya siri kutuhujumu kiuchumi, tumeshakubaliana dereva anapopimwa upande wa Tanzania aruhusiwe upande wa Kenya kwa cheti, sasa wamekiuka makubaliano, wakifika upande ule wanataka wawapime tena sijui wana maana ipi nashindwa kuwaelewa kabisa, tumeamua kuchukua hatua na haturudi nyuma,” alisema.

Katika makubaliano hayo waliamua katika lori itaruhusiwa dereva na wasaidizi wawili kuingia katika nchi husika wote wakiwa wamepimwa kama wana maambukizo ya corona.
Hata hivyo, alisema upande wa Kenya wamebadilika juzi (Jumatatu) kwa kuzuia na kutaka kuwapima tena.

“Pamoja na juhudi za mimi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, kuwasiliana na viongozi wenzetu wa Kenya, lakini zimegonga mwamba na ndipo tukaamua kuzuia vyeti vyote na magari ya mizigo kutoka Kenya pamoja bidhaa zote zinazoingia kutoka nchini humo hadi hapo tutakapokaa tena na kufikia muafaka maana sote tunategemeana, Kenya wanatuhitaji kama soko na sisi wanatuhitaji pia ili kuuza bidhaa,” alisema Mwaisumbe.

Alisema mwezi Mei makubaliano ya kuruhusu kuaminiana pande mbili yalikaliwa kikao na mawaziri wa mambo ya nje za nchi, makatibu wakuu, wataalamu na viongozi wengine wa mikoa na wilaya wa kutoka nchi mbili katika mpaka wa Namanga, kufuatia mazungumzo ya Rais John Magufuli na Rais Uhuru Kenyata ambao waliwaagiza viongozi wanaohusika kukaa na kufanya vikao na makubaliano, huku wakichukua tahadhari za ugonjwa huo na kuona namna ya kuendelea na biashara kwa nchi hizo.

Alisema kama hali ya kutoaminiana itaendelea, itawalazimu kutoa uamuzi wa kuigeuza Namanga kuwa bandari kavu na majirani Wakenya watashusha mizigo au bidhaa upande wake na Tanzania kuichukua na pia hata Tanzania itapeleka wa Tanzania ili Kenya waifuate.

“Nchi yetu ni huru inayojitegemea haihitaji kubembeleza nchi nyingine kufanya biashara kwa sababu sisi tunategemeana, haiwezekani mambo ambayo yameagizwa na marais viongozi wa chini hawatekelezi…linaashiria dharau na ajenda ambayo wanadhani ni siri iliyofichika kumbe sisi tunaifahamu, hatutaweza kuivumilia hata kidogo,” alisema.

Alisema, nia ya Rais Magufuli ni kuwasaidia watu wa hali ya chini kwa kuwa uamuzi huo unapofanyika wanao umia ni watu wa chini.

“Nataka nikuhakikishie ndugu kupima kipimo cha Covid-19 sio lelemama kinaumiza sana, sasa haiwezekani siku mbili mtu amechokonolewa pua, halafu anatoka upande wa Tanzania anaenda upande wa Kenya anafanyiwa kitu kile kile, sasa hali hii kwa kweli sio sahihi, tunataka hiyo agenda yao ya siri ijitokeze hadharani tushughulike nayo kuliko kutumia ugonjwa wa Covid-19, sisi hatutakuwa tayari,” alisema Mwaisumbe.

Kuna tofauti ya kuwa na cheti chenye matokeo ya upimwaji na kupimwa ukapewa matokeo.

Nini kinashindikana bongo? Yote halali yetu.
 
Kwenye hili la corona wako sahihi tupunguze matumiz ya bangi za kolomijr ktk kukabiliana na jambo hili

Wako sahihi kitu gani, sisi ndo tungetakiwa kuwaogopa maana maabukizi kwao ni mengi na vifo vinaongezeka,
Sasa wao wanatuogipa nini wakati sisi tunaanza kusahau huo ugonjwa?
Wao mdo watazidi kutuambukiza maana wengi wanaingia bila kupimwa vipimo vikubwa.
 
Safi sana. Nilikua napata hasira nikijaribu kuamini eti Kenya itaruhusu Watanzania waingie ingie kisa wana vyeti, na walivyo makajanja watafoji vyeti kariokoo na kuingia na corona.

Nchi inayothamini uhai na afya ya watu wake lazima iwe makini, hata kama italazimu kufungiana mipaka kabisa. Miaka ya 1977 EAC ilivunjwa na kutupwa kule, mipaka ikafungwa na kila mtu akaishi kwake, na wala hakuna aliyekufa.
Mwambieni uhuruto asipige simu tena Dodoma
 
Tanzania tunafanya mambo kiajabu sana, na hii yote inasababishwa na kufuata mawazo ya mtu mmoja, haiwezekani mseme vipimo vyenu vilikuwa vibovu baada ya kuvichunguza, halafu baada ya muda mnaanza kulazimisha idadi ya wagonjwa wa Corona imepungua, mtu mwenye akili atajiuliza imepungua kwa vipimo gani mlivyowapimia?

Hao wakenya ni haki yao kugoma, kwasababu kwanza tulishajifunga wenyewe kwa kukiri vipimo vyetu vilikuwa vibovu, sasa kwanini waamini hivyo vyeti vinavyopelekwa na madereva wetu? waacheni watumie vipimo vyao kuwapima wajiridhishe.

Halafu kwa akili za viongozi wetu watakurupuka nao kuwazuia wakenya, sijui watawazuia kwasababu gani wakati wakenya hawakuwahi kukiri kama vipimo vyao ni vibovu hivyo tusiwaamini madereva wao.
Jamani Maabara mpya yenye uwezo ilishafunguliwa kule Mabibo na bora zaidi kuliko ile iliyokuwa NIMRI.Hope inaleta sense.
 
Gud, hili ni kwa majirani zetu ambao wao hawana mgogoro; sasa vipi kwetu balozi wa Marekani anasema hali ya ugonjwa bado mbaya, halafu sisi tunasema wamebaki wanne, wakenya wamuamini nani hapa?!

Kwanini msiwaache wakapima wagonjwa wetu wao wenyewe wajiridhishe, km kweli wamebaki wanne pressure ya nini!.

Ni upumbavu kwa mtu kushabikia tabia za hovyo, yaani sisi tuamini za kwao alafu wao wasituamini, sasa wao wana u special gani wa nchi yao,
Uhuru anashindwa kuiongoza kenya kwa sasa, wamebaki kuhujumiana yeye na Ruto,
Na asipokuwa makini kufika 2022 kutawaka moto huko kwao
 
Kabisa kiongozi unasapoti kazi ya kupima madereva wetu tuwaachie wakenya?! Mbona Uganda wanataja takwimu za madereva wetu hatuwabugudhi,hujiulizi?
 
Jamani Maabara mpya yenye uwezo ilishafunguliwa kule Mabibo na bora zaidi kuliko ile iliyokuwa NIMRI.Hope inaleta sense.
Kwahiyo uwepo wa maabara mpya ndio umepunguza idadi ya wagonjwa wa COVID-19 tz!.
 
Kenya wana cheza na siasa juu ya corona, governor wengi wa Kenya wana penda sana pesa wana mchezea Uhuru pasipo kujua, iko hivi, kila governor anajitahidi kupima na kutafuta wagonjwa wa corona na hata kutoa idadi kubwa ya corona ili waimbie serikali mimi nina wagonjwa wengi nipatieni pesa za Ku control corona,akipewa tumbo lake lina chake hii ndio fursa unaona Kenya hawako nyuma kila pande kutoa data.

Kibera wakazi huko walikuwa wana pimwa hata kama huna corona una pesa 1K unaambiwa useme uko na corona wanaingizwa kwenye gari wana pelekwa mahali jioni wana muona mtu mwenye corona karudi mitaani ,wakazi wakaandamana.

Issue hii ya mpakani ni same tu shida iko wapi madereva wa Tz wakipimwa Tz na kuonyesha certificate na madereva wa Kenya wakafanya hivyo? hofu iko wapi kama kungekuwa na corona Tz serious basi Arusha na mpakani namanga tungesikia visa vingi watu kufariki ambacho hakipo, wao wana taka records kuombea pesa nothing else, ndio maana nilisema hatua za Shigela kwangu ni hatua bora kabisa haya mambo ya kujadili muda mtefu ni kupoteza muda. Mbaya zaidi juzi kulikuwa na mgomo wa madereva wa Kenya juu ya serikali ya uganda kuwazuia kuingia hadi wapime corona utaona hao madereva wa kenya walivyo pia na corona.
 
Hamkujifunza kujifukiza?? kibongobongo tunaita NYUNGU, Kikwenu sijui mnaita "steaming??" inasaidiaga ujue?

Hakuna Mwafrika asiyejua kujifukiza, watu tunajifukiza na kuendelea kupukutika tu, kirusi kikishaingia kwenye damu hata ujifukize kivipi hamna chochote kitakusaidia.
 
Ni upumbavu kwa mtu kushabikia tabia za hovyo, yaani sisi tuamini za kwao alafu wao wasituamini, sasa wao wana u special gani wa nchi yao,
Uhuru anashindwa kuiongoza kenya kwa sasa, wamebaki kuhujumiana yeye na Ruto,
Na asipokuwa makini kufika 2022 kutawaka moto huko kwao
No; ni upumbavu kuweka imani yako kwa wengine zaidi ya unavyojiamini wewe.

Ni sawa na kutembea uchi barabarani usubiri kuvishwa nguo na wapita njia!.
 
Wako sahihi kitu gani, sisi ndo tungetakiwa kuwaogopa maana maabukizi kwao ni mengi na vifo vinaongezeka,
Sasa wao wanatuogipa nini wakati sisi tunaanza kusahau huo ugonjwa?
Wao mdo watazidi kutuambukiza maana wengi wanaingia bila kupimwa vipimo vikubwa.
Umejuaje kwao wengi kuliko sis tumerelac ebu acheni uzuzu wa kushangilia kila jambo
 
Tatizo lipo Tanzania! Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu. Ukute madereva wote kutoka Tanzania wanapewa tu vyeti hata Corona hawapimwi tena kwa sababu Tanzania inaamini kuwa Corona ilishaisha!
Tatizo ni wewe usiyeelewa msingi wa msimamo wa Tanzania, na uchovu wako wa kifikra na uzwazwa wako wa kudhani kuwa Tanzania ya sasa bado ni kichwa cha mwendawazimu. Jitambue kijana na hakuna kiongozi wa Tanzania aliyetangaza kuwa corona haipo Tanzania km unavyojiyakinisha.

Corona ipo na tutaendelea kuishi nayo kwa muda kama ambavyo tunavyoishi na magonjwa mbalimbali, mengine yanayoua watu kwa wingi kuliko Corona.

Kwa sababu hiyo ndiyo maana viongozi wetu na watalaamu wa afya wanazidi kutuhimiza kuchukua tahadhari binafsi katika kujikinga na maambukizo ya virusi hivyo ambavyo havina chanjo wala dawa za kimagharibi.
 
Mnasema kwenu wagonjwa wamebaki wanne, balozi wa Marekani anatoa taarifa yake anaonesha hali bado mbaya, nani atawaamini nyie?

Hamuwezi kuchakachua hivyo vipimo kuwalinda madereva wenu?

A second thought also is a thought, huwezi kumdharau mtu simply bcoz kabadilisha msimamo wake, kama una akili timamu jiulize why?

There is nothing clear over there, unless you are myopic.
Acha ubwege wewe balozi wa marekani ndo nani, kama rais kasema imepungua basi imepungua na wote tunaona hali ilivyo sasa , si kama ilivyokuwa mwanzo, cha muhimu tuendelee kuishi nayo kwa tahadhari, hao wazungu kazi yao ni kusemea mtatizo ya waafrika tu yao kimya, mbona hatumsikii kutoa tamko juu ya mauaji ya kibaguzi kwa George Floyd?
 
Tanzania bana.....korona hakuna bado tunaogopa kupimwa...tunagawa vyeti kwa madereva wetu bila hata kuwapima afu tunataka wakenya watukubalie? Nchi ya ajabu sana hii.
 
Back
Top Bottom