Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

Mwanzoni ni kama ilikuwa hivyo. Madereva wa Tanzania wakaja juu kwamba karibu 6 katika 10 wanaopimwa wanaambiwa wana Corona. Wakasema hawaamii vipimo vya Kenya, wanaonewa nk, ndio ilaleta mgogoro.

Nadhani unaweza kuelewa kwa nini Kenya wanashituka ikiwa katika madereva 10 wa Tanzania waliokuwa wanawapima walikuta 6 wana Corona, kwa wastani. Leo Tanzania ikiwapima hao madereva wanaonekana karibu wote hawana Corona!
 
Sasa kwa nini Kenya walikubali in the first place, wangeonyesha msimamo kuwa haawaamini hizo certificate za vipimo kutoka Tz, sio wakubali halafu wabadilike tena.
Ni Siasa. Next Election Laila Odinga lazima atachukua nchi!
 

Kama una akiri jiulize, walizuia magari nasi tukazuia kama wao, kila mtu ana haki.ya.kujilinda na nchi yake,
Sasa Uhuru alipiga simu ya kumaliza tatizo ili iweje?
Kama anaona Tanzania kuna corona alipiga simu ya nini, atangaze tu kuwa hakuna kuruhusu m tz kuingia basi nasi tutafanya hivyo na maisha yataendelea.
Hawa wakenya wana dharau sana.
 
Hawa Wakenya wanaimani zaidi na ubalozi wa Marekani TZ kuliko taarifa kutoka kwa maabara zetu! Huwezi kumlazimisha mtu kuamini wakati general infos ni shida kutolewa
 
Kwa utakatifu gani viongozi wetu walionao wa kuomba na kusikilizwa kuliko Pope Italy, Allahtoya Iran, na chi nyingine zote za Africa hazimjui Mungu?
Kwani wewe unatumia kipimo gani cha kufahamu utakatifu wa mtu?

Kibali cha kile ulichokiomba Kwa Mungu kikijibiwa ndio kipimo dada angu, sasa wewe ukishajibiwa shida yako unaanza kulia Kwa nini Mungu amekupa, Kwa nini eti asiawape wenye majina maarufu na vyeo vya kidini?

Mungu hahangaiki na hivyo vyeo vya kidini dada,
 
Safi sana WAKENYA be blessed.......
 
Hivi Mnadhani corona ni kama kisukari etii? Hata hao waliofanya makubaliano ya kijinga kama hayo naona hawakufikiria vizuri labda kama waliweka mikakati ya kumfatilia dereva toka kupimwa hadi anavuka mpakani mana unaweza kumpima mtu akawa safi akaupata njiani akielekea kuvuka na sababu watu wengi hawaonyeshi dalili yeyote .
 
Sasa kwa nini Kenya walikubali in the first place, wangeonyesha msimamo kuwa haawaamini hizo certificate za vipimo kutoka Tz, sio wakubali halafu wabadilike tena.
Waliamini kwa kuwa walijua Tanzania hawatafanya mzaha katika suala la huu ugonjwa. Twende Arusha nitakupeleka sehemu unapata cheti bila kupima, dau lako tu. Ukitaka hata vya watu 10 utapata.

Na by the way, Tanzania unaweza kupewa cheti kwa kupimwa joto tu!
 
Kuna Kitu Wakenya wanatutafuta nacho Sisi Watanzania na nadhani wamesahau kuwa Tanzania ni ' a Sleeping Giant ' hasa kwa Ukanda Wetu huu.
 

kama umepata dawa ya kutibu nitaenda, ila kama hakuna na sijasikia dalili yoyote siwezi kwenda, maana hiyo 120000 inatosha kununua tangawizi na vitunguu pamoja na limao, pia nitaingia sauna kwa muda mrefu sana.
Kumbuka kupima corona sio kama kupima mkojo, kuna maumivu watu wanapata, sasa usifikili kuchokonolewa watu wansikia raha.
 
H
Waliamini kwa kuwa walijua Tanzania hawatafanya mzaha katika suala la huu ugonjwa. Twende Arusha nitakupeleka sehemu unapata cheti bila kupima, dau lako tu. Ukitaka hata vya watu 10 utapata.

Hiyo ni mamlaka ya serikari au ni vichochoroni kwenu? Na kama unajua hilo kwa nini usitoe taarifa kwa vyombo husika?
 
Hii imani ndiyo Ina tufanye tusitangaze idadi ya maambukizi?
 
H

Hiyo ni mamlaka ya serikari au ni vichochoroni kwenu? Na kama unajua hilo kwa nini usitoe taarifa kwa vyombo husika?
Hahahaha! You are not serious my brother. Serikali hii inayosema corona imeisha ndio nikaiambie kuna watu wenye corona wanapewa vyeti bila kupima?

Hapo mie ndio nitawekwa ndani.
 
Sisi CORONA tulishaifanyia kigodoro haipo..
Kenyans nao wafanye tu hivyo hivyo itaondoka..mbona ize!

Everyday is Saturday......................... 😎
 
Wewe mwenye akili unaishi wapi
Mkuu atakuambia wewe ni mjinga mmojawapo. Amesema nchi hii ina wajinga wengi kuliko werevu, ikimaanisha wapo weruvu pia katika nchi hii japo ni wachache na bila shaka yeye ni mmojawapo. Sasa inakuwaje unamuuliza swali kama vile amesema nchi hii wote ni wajinga? Unaona basi ilivyorahisi kujionyesha uko upande gani?
 

Sawa naomba jibu la maana
Marekani wanaongoza kwa wingi wa wagonjwa na vifo wamepata zawadi gani? au wamesaidiaje kumaliza huo ugonjwa?

Je waliopimwa hawataambukizwa wakikutana na ugonjwa?

Hakuna haja kutumia pesa nyingi kwa jambo ambalo halina faida, ni bola utunze hiyo peaa imtibu mgonjwa ambae ameonyesha kuumwa, kuliko kumpima mtu hana kesho anapata ugonjwa unampima na kumtibu tena,
Kipimo cha kwanza kinakuwa ni hasara,
Nchi yetu haina uwezo wa kuchezea pes kiasi hicho.
 
Kwani ubaya uko wapi, kama hawana kweli si wapimwe then majibu yatakuwa sawa tu.
 
Hahahaha! You are not serious my brother. Serikali hii inayosema corona imeisha ndio nikaiambie kuna watu wenye corona wanapewa vyeti bila kupima?

Hapo mie ndio nitawekwa ndani.
Mkuu naomba unijibu maswali machache haya, Ni kiongozi gani mwenye mamlaka ya kutangaza kuhusu corona aliyesema corona imeisha Tanzania? Toka itangazwe kuhusu kuruhusu maisha kuendelea lakini kwa tahadhari ni ndugu au majirani zako wangapi wamekufa na corona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…