Pre GE2025 Mpaka yanatumika magari kutangaza birthday ya Rais Samia lakini bado kiki imebuma. Safari hii watanzania wamenuna kwelikweli!

Pre GE2025 Mpaka yanatumika magari kutangaza birthday ya Rais Samia lakini bado kiki imebuma. Safari hii watanzania wamenuna kwelikweli!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi huyu mama Abdul ana tatizo gani wajameni, bibi mwenye wajukuu anataka sherehe ya birthday kama mjukuu wake wa miaka 16?

Au Kizimkazi kwenye makuzi hakufanyiwa sherehe huko sasa analipizia? Mimi yangu ya mwisho nilifanya mwaka 1975 nikiwa shule ya msingi ilala boma
 
Uchaguzi utawajua watanzania na ccm yao mtabaki kusema tumeibiwa tumeibiwa
Kabisa kama vile kuwaengua wapinzani kwa 96% kweli watanzania na CCM yao hata ikibidi kuwaengua wapinzani wako tayari, au siyo?
 
..Ni miundombinu yetu Watanzania, sio mali ya kiongozi fulani.
Eeh; ndio maana bora kusoma nyuzi za kule International news, kule kuna wachangiaji wanakupa burudani; utasikia "kobazi" mara Yahudi, kafiri hivo yaani, ilimradi msomaji huboreki. Sio huku mambo ya uchawa tu.
 
Kaulize masheikh! Halijafanikiwa jambo la watu ambao kiongozi wao mkuu ni mwanamke,ndivyo ilivyo.
Embu tutolee huo upupu wako hapa, hao wanaume waliopita wamefanya nini cha tofauti na alichofanya Samia? Wote ni upupu, na kwa maeneo mengine ni worse... hizo chuki zako za kijinsia baki nazo mwenyewe
 
Ukweli wa Mwenyezi Mungu wa kiislamu siyo upupu wala chuki za kijinsia,kuwa na heshima kwa dini kijana. Kama hujui nimekwambia kaulize masheikh wapo. Halafu alichofanya Samia na walichofanya wanaume ni kuna mjadala wake tofauti ujue.
 
Sasa barabara zimefungwa hakuna raia mjini wanatangaza kwa nani ?

Halafu kuchora picha ya mtu juu bendera ya taifa ni uhuni, kesho na Lissu akiweka picha yake itakuwa sawa ?
Kweli kabisaaaa kaka
 
Back
Top Bottom