Aiseee halafu huu ushindani upo hata kwa mabasi ya Dar - Mbeya kama Sauli, Al Saedy na Imani Plus siku hiyo tunatoka Mbeya kuja Dar nilipanda Sauli yaani ilikuwa ni mashindano tu na hayo mabasi mawili
Kwanza nasikia mwenye Imani Plus alishamfukuza dereva wake eti kwanini alipitwa na Sauli kwahiyo siku hiyo aliendesha basi lake yeye mwenyewe kutoka Mbeya hadi Dar ili awe wa kwanza kufika Ubungo
Ila aibu yake akaishia kuwa wa tatu maana ilitangulia Al Saedy ikafuata Sauli halafu ndiyo hiyo Imani Plus aise sijui alijisikiaje maana kuanzia Kibaha yeye ndiyo alishika nafasi ya kwanza akawa anahakikisha hakuna basi inayompita ila alikuja kupitwa kizembe pale Mbezi
Lakini mwisho wa siku nikawaelewa tu kuwa yote hiyo ni katika kujitangazia jina na kugombea soko na kwa sasa basi inayosifika kwa kuwahi kufika kwa safari za Dar - Mbeya ni Sauli na ndiyo inashika chati kwa kuwa na wateja wengi kwa sasa