Mpanda: Tundu Lissu ayalipua Maridhiano, Kingai, Byakanwa na Wambura Watajwa

Watu wa pwani, waswahili, si watu wa kuaminika. Mbowe anatakiwa kuwa makini na Samia
 
Lissu yeye huwa anapasuka palepale hataki kuzunguka
 
Wananchi tunahitaji sera na sio majungu na lawama kila uchao.

Tunataka taifa la kisasa na sio taifa la visasi.
 
Mungu Ibariki CHADEMA[emoji419][emoji375]
 
jamaa namkubali sana ijapokuwa wengi huwa hawamwelewi lakini naamini iko siku watafunguliwa na kuanza kumwelewa.
 
Lisu bila kumtaja taja Magufuli ni mweupe tu.
Asipotajwa na binadamu wenzake walioshuhudia fikra zake mbaya, mipango yake ovu na matndo yake ya kinyama, kwa hakika hata mawe yatamtaja. Lissu kataja uongozi wa awamu ya tano kwa ujumla kwamba ulihusishwa na mambo mabaya sana dhidi ya raia lakini wako watu wanaona ametajwa mtu mmoja! Wenye shida hiyo ni wale washirika wa karibu wa uovu huo. Shida yao hao washirika wa uovu ni kutaka uovu huo usahaulike; watu wasikumbushwe! Hapana. Sehemu kubwa ya kizazi chetu hatukuwepo wakati wa vita vya pili vya dunia. Watu wastaarabu wameturithisha historia hiyo muhimu ikiwa ni pamoja na majina ya watu waovu waliohusika na maafa hayo. Vivyo hivyo watu wema wa nchi hii hawana budi kukumbusha uovu kila mara na kuweka katika historia.
 
Mbowe alishasema maridhiano hayawazuii kusema wala kuendelea na mipango yao

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Sahihi mno!!!

Kuna vitu Lissu akiongea anatumia maneno na style sahihi yenye kufikisha ujumbe 100%. Hiyo ni moja ya strength zake muhimu.
 
Yuko sahihi
Wanakosea wanapoangalia yaliyotokea kwenye awamu ya tano tu, huo ni ubinafsi uliopitiliza kwa kuwa wao ndio wahanga.

Kwanini tusirudi nyuma tukaangalia yaliyowapata kina Dr Ulimboka, Mwangosi?

Au hata nyuma zaidi tukaangalia familia za kina Kaselabantu zilivyoathiriwa na ukatili wa tawala za kipindi kile na namna zinavyoweza kufidiwa?

Kama mmeamua kuridhiana shurti mridhiane kiukweli.
 
Kama Lisu bado ana siasa za namna hii anafeli pakubwa sana,hizi siasa za lawama zimepitwa na wakati ,aseme atafanya nini tofauti na CCM ikiwa atakamata dola,aache porojo
Fact
 
Wewe yaangazie hayo sasa kwani Tanzania ni Lissu peke yake? Yeye anafanyap pale anapoweza
 
Hakuna makundi kama ndio malengo yenu mtasubiri sana.

Anachosema Lissu ni kukazia kwenye maridhiano.

Ni kumshtua yule mnayeridhiani kwenye hila anazofanya ndani ya maridhiano.

Ni sawa na kumwambia mtu kuwa mbona umekiri umenisamehe lakini bado unapeleka kesi mahakamani?? Sasa mtu ukimwambia hivyo ni kosa gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…