DOKEZO Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu Ushauri wangu nin,Kwanza Mpe Eviction Note kutoka kwa mwanasheria wak0 na uksiema kabisa kakiuka masharti ya mkataba kwa kutumia nyumba kinyume na mlivyokubaliana.Kwenye Notes Usigusie issue ya Vinywaji feki wala nini bali weka Clear kwamba nyumba ulimpangishia kwa makazi na yeye anatumia kwa biashara.

Baada ya Kumpa Eviction note akikutafuta Mwambie tu aondoke.Wala Usihangaike kutaka sound maana muda sio mrefu Hicho kiwanda kitakuwa ni chako na wewe ndio utakuwa mtuhumiwa namba moja
 
nenda tbs
 
Yaani kwa maoni ya humu nimegundua akili za Wabongo zilivyo,
Yaani zimejaa Uoga,Rushwa,Ujinga,ujuaji,
akili ndogo,Ubunifu zero,Mamlaka za hovyo yaani hii nchi ukiwa na shida utakufa unajiona ni shaghala baghala tu..

Na ndio maana watu wanatekwa na kuuawa mchana kweupe na watu wanaofahamika kabisa na raia hawana msaada wowote,

Kuwapigania Raia wa namna hii ni ngumu sana bora CCM iendelee kutuburuza tu,

Yaani hili ni tatizo dogo tu ila inaonesha wazi hadi mifumo inayohitajika kutoa msaada nao ni wahusika namba moja tutafika kweli?
😁😁
 
IKiwa imebaki miezi 3 ya kodi yake kwisha,

Mwandie mkataba mpya wa kuongeza kodi mara mbili ya mwanzo na anatakiwa kulipa ndani ya miaka 2 kwa pamoja,

Lkn pia shirikiana na viongozi wa selikali ya mtaa uwaeleze juu ya hofu yako kwa maana chochote itakusaidia zaid siku za mbele
 
tatizo mkuu hatakiwi kukurupuka sijui kuripot kwa mjumbe au serikali ya mtaa au polisi tatizo watengeneza vitu feki washafika kote huko kuna watu wapo kwenye malipo yao hao wanakuwa ma infoma wao huko kwenye mamlaka sio ww ujipeleke kichwa kichwa eti naripot wanakuchora tu hivo vinywaji vina mpaka stika original ya TRA unafikiri wanazipata wapi..
 
Watataifisha nyumba kwani iko chini ya Jina lao? Wewe umepangisha, yanayoendelea hapo huna udhibiti nayo, tena akijua umemshtaki unaweza shitakiwa kwa kusababisha au kuvunja mkataba kabla ya muda mliokubaliana.
Kwani wanavyotaifisha gari iliyokutwa imebeba magendo au madawa ya kulevya hua inakuaje mkuu?
 
Ukifika mahakamani huna nyumba kwa hio fanya km umeitoa Sadaka km unataka kuufuatilia kiundani huo msala au waachie Polisi wafanye kazi yao ya kukusanya Posho, usijifanye unajua zaidi kuwazidi wao halafu huyo msiri wako hakutakii mema kakuset hio nyumba ikipigwa mnada atainunua yeye ndio imekula kwako
 
wengi watakuja hapa na kukuuliza kama anakulipa kodi au hakulipi, na wewe unaathirika nini? kwa uzoefu, kitakachotokea, akama anachofanya ni kosa la jinai, atakamatwa, na mitambo yake itataifishwa, na nyumba yako itataifishwa, wewe utahangaika sana kwenda mahakamani au kwa DPP kujieleza kwamba wasitaifishe nyumba yako iliyokuwa inatumika kutengenezea vinywaji kimakosa, kwamba isiunganishwe kwenye vitendea kazi vya kutaifisha. utapata shida sana. ila itakusumbua kwasababu hoja itakuwa, ulikuwa unajua au ulikuwa hujui? kama ulikuwa unajua nyumba yako inatumika kufanyia uhalifu na ukaacha hivyohivyo bila kureport au kustopisha, itaonekana uliridhia, na icho kinaweza kuwa kielelezo cha kutaifishwa na DPP. dpp ataiomba mahakama itaifishe, na akitoa maelezo ya kueleweka wewe ukawa hauna, nyumba yako itataifishwa na itauzwa pesa itaenda serikalini. chukua hatua, utanishukuru, ama la labda kama anafanya kazi kihalali ana vibali kila kitu.
 
Sawa,ila kwa maelezo yake polisi hao hao wanakujaga kudaka hapo 😄
Anyway kikubwa aripoti,hata kikinuka atajitetea mbona nlitoa taarifa

Ova
Mzee mwenye nyumba wajibu wake ni kuripoti polisi kuwa nyumba yake ana wasiwasi inatumika kwa uhakifu na mpangaji wake. Achukue RB au maandishi yoyote kuthibitisha katoa taarifa. Hapo sasa aanze taratibu za kumuondoa huyo mpangaji kwa msaada wa mjumbe,seriakli za mtaa na polisi. Polisi wakiamua kumuachia mbele kwa mbele sio tatizo lake tena.
 
Kweli kabisa

Ova
 
Umeelezea vizuri sana. Na wengi humu wanaongea kama ulivyosema,kirahisirahisi tu.
 
Mpangaji wako ashukuru kakukuta wew.
Angekua na Mzee NGONGOPOJO Mda mrefu angakua hana miguu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…