Mpango, Majaliwa na Polepole ni watu walioamua kuacha kuendelea kufanya kazi na utawala huu. Je nini kinaendelea?

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Makamu wa Rais Muheshimiwa Philip Mpango alidai kuwa ametosha kuwa Makamu wa Rais na hakutaka kuendelea kuwa Makamu kwa muhula wa Urais ujao ambao Rais Samia bado anautetea. Mpango ametaka kustaafu kwa hiari cheo icho ambacho amedumu nacho kwa Muhula mmoja wa Urais.

Hatujakaa sawa Waziri Mkuu nae amedai kuacha kugombea ubunge katika jimbo lake la Namungo, na ameshangaza wengi kwa uamuzi huo... Majaliwa aliteuliwa na Magufuli kuwa waziri mkuu, ambapo pia Rais Samia alimuamini na kumbakiza kuwa waziri mkuu. Lakini baada ya kudumu kwa muhula mmoja akifanya kazi na Samia ameamua kujitoa na kuachia jimbo la namungo na kustaafu uwaziri huo.

Vilevile bado hatujakaa sawa hii leo balozi Tanzania Nchini Cuba, Muheshimiwa Humphrey Polepole nae ameomba kuachia ngazi ya ubalozi na utawala na kuamua kuwa mwananchi wa kawaida kwa madai ya kwamba Chama chake cha siasa ambacho ndicho kinachoshikilia dola kimeshindwa kufuata matakwa, kanuni na sheria za chama.

Kwa huu mfululizo wa matukio unaona ni nini kilichofanya hawa wajiuzuru huu uongozi ambao kila mwanasiasa anaulilia angalau ateuliwe.
 
Wewe ukiacha kufanya kazi na kampuni yako,haukubaliani na bosi wako/umechoka kufanya kazi.........na uliajiriwa ukaikuta kampuni ipo hai.....nini kitaendelea?
 
Back
Top Bottom