Mpango mauaji ya Wayne Derek Lotter ulivyosukwa na kutekelezwa jijini Dar

Mpango mauaji ya Wayne Derek Lotter ulivyosukwa na kutekelezwa jijini Dar

Kuna watu walisomea na kubobea kufanya uchunguzi.

Huezi fanya mauaji watu wasikukamate. Lazima utaacha trace ambayo ndo itasababisha wewe kukamatwa.

Labda uue mbuzi wa jirani yako.
kuna watu wanafanya uhalifu,hata FBI,wanachemka,mgoogle,Curl gursian,The friday night bank robber...ni kuwa smart tu kupangilia mambo,na uwe peke yako tu.
 
Kuna watu walisomea na kubobea kufanya uchunguzi.

Huezi fanya mauaji watu wasikukamate. Lazima utaacha trace ambayo ndo itasababisha wewe kukamatwa.

Labda uue mbuzi wa jirani yako.

Trace moja tu ikipatikana ambayo mara nyingi ni simu, utawapata wote, na baada ta hapo ni mwendo wa Kipondo tu mtaeleza mpaka mlipoenda uwani
 
View attachment 2444122
Agosti 16, 2017 jiji la Dar es Salaam na dunia kwa ujumla lilipokea taarifa ya kusikitisha ya kifo cha Wayne Lotter, Mkurugenzi wa Taasisi ya Protected Area Management System (PAMS), inayojishughulisha na harakati za kupambana na ujangili chini ya mwamvuli wa utetezi na uhifadhi wa wanyama pori.

Lotter ambaye anatambulika Tanzania kama Mwanaharakati wa Tembo alikutwa na umauti baada ya kupigwa risasi karibu na eneo la makazi yake la Baobab Village, Masaki, Dar es Salaam alikokuwa anaishi. Siku ya tukio, Lotter na Mkurugenzi mwenza wa PAMS ambaye hakutajwa jina walikuwa wakitoka jijini Arusha katika harakati zao za kazi.

Walipofika karibu na eneo hilo walikutana na majambazi ambao waliwavamia na baadaye walimpiga risasi Lotter. Tukio hilo kama yalivyo matukio mengine ya uhalifu liliingiza Jeshi la Polisi katika uchunguzi ili kubaini wahusika wa tukio ambapo takribani watuhumiwa 22 walikamatwa kabla ya kuchujwa kwa sababu mbalimbali na kubaki 11 waliokwenda hadi mwisho walipohukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyoketi kusikiliza shauri hilo chini ya Jaji Leyla Mgonya.

Washtakiwa hao ni Rahma Mwinyi, Nduimana Ogiste, Godfrey Salamba, Chambie Ally, Allan Mafue, Ismail Mohamed, Leonard Makoi, Ayoub Kiholi, Abuu Mkingie, Habonimana Nyandwi na Michael Kwavava. Ni katika hukumu hiyo ndipo maelezo ya wahusika wa mauaji hayo yanapobainisha mpango mzima ulivyofanyika mpaka kutekeleza mauaji ya mwanaharakati huyo.

Mpango ulianzia jijini Arusha kwa mshtakiwa wa nane, Leonard Makoi ambaye katika ushaihidi ndiye anaonekana kuratibu mpango mzima kuanzia mwanzo. Makoi kwenye maelezo ya onyo alieleza kushiriki kutafuta watu wa kutekeleza mpango huo kuanzia mwanzoni.

Alikaririwa akisema: “Ni kwamba, mwaka 2017 mwezi wa saba tarehe sikumbuki, alinipigia simu mzee mmoja anayeitwa Machips, jina kamili silifahamu (akimaanisha mshtakiwa wa saba, Ismail Mohamed). Akaniambia kuna biashara anataka aongee na mimi.

“Majira ya saa saba usiku nilienda tukakutana na Mzee Machips, akaniambia kuna kazi ya Dar es Salaam. Nilipomuuliza ni kazi gani akaniambia kuna Mzungu anayehusika na meno ya tembo anatakiwa auwawe. “Akaniambia kama kuna watu wanaweza kufanya hiyo kazi niongee nao, tukubaliane ili kazi ifanyike. Baada ya kuniambia hivyo nilimweleza kwamba kuna kijana anaitwa Karama anaweza akafanikisha hiyo kazi,” alieleza katika sehemu ya maelezo yake.

Kwa mujibu wa maelezo yake walikubaliana na Karama ambaye baada ya makubaliano alimpigia akimtaka amtumie fedha kwa ajili ya maandalizi ya kazi hiyo.

“Baadaye Karama alinipigia simu akaniambia nimtumie pesa Sh milioni tatu kwa ajili ya kununua bunduki ya kufanyia kazi. Niliwasiliana na Mzee Machips akanipa hiyo pesa nikaituma kwa njia ya basi la Kilimanjaro Express. “Mwezi wa nane tarehe sikumbuki mwaka 2017. Ile kazi ilikuwa imekaribia na Mzee Machipsi alinipa pesa Sh milioni 58, nikaenda nazo Dar es Salaam kwa ajili ya kuwalipa akina Karama na wenzake akiwemo Gody na Mrundi ambae simfahamu kwa jina. “Ile kazi ilifanyika yule Mzungu akauwawa. Baada ya kazi kesho yake nilimpigia Karama akaja maeneo ya Ubungo katika hoteli ya Blue Pearl, nikamkabidhi kibegi kikiwa na Sh milioni 52 na kiasi kilichobaki, Sh milioni 6 nikabaki nacho, nikarudi Arusha,” alieleza.

Karama ambaye hakuwa mmoja washtakiwa mahakamani aliendelea kutajwa katika maelezo ya washtakiwa wengine kwamba ndiye aliyeratibu mpango huo kwa asilimia kubwa ikiwa ni pamoja kutafuta silaha, kuwahifadhi na kufanya nao vikao vya kuratibu mpango huo nyumbani kwake.

Katika maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu, Nduimana Ogiste, raia wa Burundi, alieleza namna alivyowasiliana na Karama ambaye alimtaarifu kuhusu mpango wa mauaji uliopangwa kufanyika Dar es Salaam na kuthibitisha kuwa alitumiwa shilingi milioni tatu kwa ajili ya kununua silaha.

Yeye alikiri pia kupokelewa na Karama alipowasili Stendi ya mabasi Ubungo kutoka Burundi na kupelekwa kuishi nyumbani kwake (Karama) Temeke.

Alikiri pia kushiriki vikao mbalimali vilivyofanyika kwa Karama kwa lengo la kupanga na kutekeleza mauaji ya Lotter.

Agosti 16, 2017 Lotter na Mkurugenzi mwenza wa PAMS walikuwa wakisafiri kutoka Arusha kuelekea Dar es Salaam kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) bila kujua kuwa walikuwa katika mpango wa kuuawa kwani nyuma yao kulikuwa na mtu anayetoa taarifa za safari yao na mbele yao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kulikuwa na watu wanaowasubiri kutekeleza uharamia juu yao.

Kati yao walikuwa ni watu wanaowafahamu, yaani madereva wao wanaowatumia katika safari zao mara zote yaani Chambie Ally na Daudi Kwavava.

Chambie yeye alishiriki mpango huo kutokea Arusha ambapo alitoa taarifa ya kuondoka kwa Lotter Kiwanja cha Ndege wa Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) kuelekea Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA) na Kwavava alishiriki mpango huo kwa kwenda kuwapokea na kuhakikisha anarahisisha mazingira ya kutekeleza mauaji hayo.

Saa chache kabla ya kwenda JNIA kuwapokea Lotter na mwenzake, Kwavava kwa mujibu wa ushahidi inaelezwa kwamba alipitia dukani kwa mshtakiwa wa sita, Allan Mafue ambaye anatajwa kuwa alifadhili mpango huo wa mauaji na ndiye aliyemlipa Ogiste ujira wake wa Sh milioni 20 kutokana na kazi aliyofanya katika mpango huo.

Kwavava alienda kuonana na Mafue kwa ajili ya maelekezo ya mwisho ya utekelezaji wa mpango wao. Tukio hilo pia lilithibitishwa na Ogiste ambaye kwenye maelezo yake alieleza kuwa alimshuhudia Kwavava akiingia dukani kwa Mafue ambako alikaa kwa dakika thelathini kwa ajili ya kukamilisha mpango huo.

“Walikaa kama dakika thelathini au zaidi, baadaye walitoka na yule mzee aliondoka. Karama aliniambia, tuingie ndani ya gari. Tulipoingia alisema kazi ipo. Na yule mzee aliyekuwa naye (akimaanisha Kwavava) ndiye dereva atakayemchukua Mzungu uwanja wa ndege. Wameshaongea naye walipoingia ndani kwa Mafue, tuliondoka kwenda uwanja wa ndege.” Ushahidi ulionesha kwamba walipofika JNIA, Kwavava aliwapokea Lotter na mwenzake na safari ya kuelekea Masaki ilianza bila Lotter kujua kwamba nyuma yao Karama na Ogiste walikuwa wakiwafuatilia kwa kutumia gari aina ya Toyota IST kwa lengo la kuwaua.

Katikati yao dereva wa bodaboda, Ayoub Kiholi alikuwa akihakikisha usalama wa wauaji kwa kujiweka tayari kuwaokoa dhidi ya askari polisi na kuhakikisha hawavurugi mpango wao.

Awali katika maelezo yake, Kwavava alisema kuwa Agosti 16, 2017 akiwa amewabeba abiria wake kutoka JNIA, walifika katika makutano ya barabara ya Haile Sellassie ambako gari aina ya Toyota IST yenye paa jeusi iliwazuia kwa mbele na wakashuka watu wawili wenye silaha kuelekea kwenye gari yake.

Alisema mmoja wao alifyatua risasi na kumpiga Lotter karibu na kidevu huku akimwacha mwenzake ambaye ndiye aliyekuwa karibu zaidi.

Kwavava alitoa maelezo hayo kana kwamba alikuwa hajui chochote kuhusu mpango huo mpaka pale uchunguzi wa wa polisi ulipokuja kumbaini kwamba alishiriki na kumtia nguvuni.

Washtakiwa wengine kama Rahma wanaingia katika kesi hii kwa kushiriki njama za mauaji ambapo ushahidi ulionesha alishiriki kuwahifadhi na kuwaandalia chakula wahalifu walioshiriki mpango huo nyumbani kwa kaka yake Karama ambaye alikuwa akiishi naye huko Temeke Pia Rahma, kwa mujibu wa ushahidi alishiriki kuficha silaha zilizotumika kutekeleza mpango huo kwa kwenda kuzizika katika makaburi ya Ngazija Upanga, Dar es Salaam baada ya kusikia kuwa kaka yake alichukuliwa na watu wasiojulikana na yeye kuhisi kuwa amekamatwa na polisi.

Ingawa haikujitokeza waziwazi sababu ya kumuua Lotter, lakini inaaminika ni kutokana na harakati za kupambana na majangili.
Maelezo haya ya onyo yalimpasa Jaji kutumia weledi wake kutanzua hizi mbinu za polisi kutunga kesi kupitia maelezo aina hii.

Nikikumbuka ya kina Adamoo ninadisqualify 90% ya maelezo ya washtakiwa wakiwa vituo vya polisi

Huyo Mchina ilishindikana nini kutumia Interpol kumkamata?

Karama kwa nini hakuwepo mahakamani? Hakuna maelezo kama alikwepa viunzi vya polisi au kafa
 
Kuna umuhimu kweli wa kuua MTU ili upate pesa?
Sidhani, hata ujangili unaweza kufanyika bila kupoteza uhai wa MTU.
 
Mzungu atakuwa kaondoka na wengi kama kweli hawa watu 11 watanyongwa. Ni jambo la ajabu sana ukifikiria roho ya Mzungu mmoja Kaburu ni sawa na roho za Waafrika 11 Wazawa au tuseme 12 pamoja na Karama. Hukumu ya ajabu sana hii.
Hapo muuaji ni mmoja au wawili Tu. Wengine wanashtakiwa kwa kusaidia mauaji kufanyika. Iweje wapewe adhabu ya kunyongwa? Hebu wasomi tusaidieni Sisi tulio mbumbumbu wa sheria.
 
Hilo dau vijana wengi tu wangeingia tamaa ya kumuua mzungu.

Uchunguzi wetu upo shallow mno,hiyo 58M ilianzia kwa Machips tu au kuna chain zaidi ya hapo?

Machips ana athirikaje na harakati za Lotter hadi afadhili mauaji yake?
 
Lazima kuna mtu mzito ambaye ndo mpango wake huu ambaye ndo alitoa pesa na kumuajiri Karama kama.mtu wa kuratibu mpango
 
Kuna watu walisomea na kubobea kufanya uchunguzi.

Huezi fanya mauaji watu wasikukamate. Lazima utaacha trace ambayo ndo itasababisha wewe kukamatwa.

Labda uue mbuzi wa jirani yako.
Labda wafanye wenyewe ndo hawatajikamata ila watu wengine lazima tu utadakwa kwenye maelezo.

Pia kwenye hii kesi wamedakwa sababu uharifu ulihusisha watu wengi sana.
 
Hao watu waliosome na kubobea kufanya uchunguzi hawawezi kutumiwa na majambazi ili kuondoa traces zote?
Kwa teknolojianya kibongo mi naona ni rahisi sana, na majambazi wengi tu wanaua na kudunda mtaani.
Utahonga watu wote kweli?
 
Rahma na dereva bodaboda wameonewa,kupika chakula watu wanaoukuja nyumbani kwa kakaake sidhan kama wamehusika na mauaji,hata kama alificha silaha ni ktk hali ya kawaida ya kujihami,anahitaji mwanasheria mzuri,kuna watu wanastahili kunyongwa ila siyo rahma na dereva wa bodaboda,halafu hajasema hizo milion 58 zilitoks kwanani na zilienda kwa lengo gani ikiwa huyo mrundi alipewa milioni 20 na myu mwingine
Usije jaribu ficha silaha ya uharifu afu useme hujahusika
 
Mzungu atakuwa kaondoka na wengi kama kweli hawa watu 11 watanyongwa. Ni jambo la ajabu sana ukifikiria roho ya Mzungu mmoja Kaburu ni sawa na roho za Waafrika 11 Wazawa au tuseme 12 pamoja na Karama. Hukumu ya ajabu sana hii.
Acha ubaguzi
 
Yap cheni ni ndefu ila hata hawa watu pia inaonekana wanajihusisha na biashara haramu
Haiwezekani ushirikishwe tu kwenye mauaji kama haujiusishi na mambo hizo
Huwezi husishwa kwenye dili la ujambazi au uharifu kama sio mharifu wa kuaminika
 
Kuna watu walisomea na kubobea kufanya uchunguzi.

Huezi fanya mauaji watu wasikukamate. Lazima utaacha trace ambayo ndo itasababisha wewe kukamatwa.

Labda uue mbuzi wa jirani yako.
Tatizo simu na mipango yenye kushirikisha watu wengi ....simu zinawakamatisha wengi ....ndiyo maana watu wahuni wamefuta kumbukumbu za simu baadhi kwenye siku za kufa kwa JPM hapo katikati kabla na baada ya kifo kumbukumbu zimepotezwa
 
Kwahiyo Mwenendo wa Upelelezi na kesi mahakamani mawakili walishindwa kubaini aliyemtuma Machips?
Waliomtuma hawajatajwa na watuhumiwa. Na sababu ni usalama wao na familia zao. Na pia watumaji huwa hawataki husika moja kwa moja
 
swala la ujangiri ni mtambuka,mdogo wake Rost pamoja na yule mbunge wa Shy walihusishwa na ujangiri mambo yalizimwa kiaina,mambo haya huwa kuna wakubwa nyuma yake,na utawala huu ndo utawala wa ujangiri wa kuvuna pembe za ndovu.
SA1000 siyo binadamu ni jini
 
Back
Top Bottom