SoC04 Mpango wa miaka 25 wa kubadilisha Tanzania kutoka nchi maskini zaidi hadi nchi iliyoendelea kwa kuchukua mifano kutoka Korea Kusini

SoC04 Mpango wa miaka 25 wa kubadilisha Tanzania kutoka nchi maskini zaidi hadi nchi iliyoendelea kwa kuchukua mifano kutoka Korea Kusini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Professor Aaron Jackson

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2024
Posts
224
Reaction score
241
Umoja wa Mataifa unaiweka Tanzania katika kundi la Nchi maskini Zaidi (LDC). Hata hivyo, ikizingatiwa rasilimali nyingi na uwezo mkubwa wa nchi yetu, hadhi hii inaonekana kutofaa. Miaka ya 1950, Korea Kusini ilikuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani ikitegemea sana kilimo na haikuwa na misingi thabiti ya viwanda. Licha ya changamoto hizi, Korea Kusini iliweza kujijenga kutoka chini na kuibuka kama taifa lenye mafanikio. Kama Korea Kusini iliweza, Kwanini Sisi Tushindwe? Sisi pia tunaweza.

Je, Tanzania ifanye nini ili kutoka katika kundi la nchi duni mpaka kuwa nchi iliyoendelea?
Kwanza kabisa ni uwekezaji katika elimu na rasilimali watu. Kundi la wafanyakazi waliosoma vizuri na wenye ujuzi ni muhimu kwa ukuaji wa viwanda. Tanzania inapaswa kurekebisha mfumo wake wa elimu ufundishwe kwa kiingereza kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu, ili kuongeza ushindani wetu kimataifa. Nikiwa kama mmoja wa wanafunzi wanaotafuta Ufadhili wa kusoma shahada ya uzamili nje, nimegundua kuwa wanafunzi wengi wa kutoka Tanzania tunakosa fursa hizo sababu ya kufeli mitihani ya kiingereza kama IELTS, ukilinganisha na wenzetu Kenya ambao Kingereza kinatumika kama lugha ya kufundishia. Aidha serikali inatakiwa kubuni ufadhili wake “Tanzanian Government Scholarship” ambao utaruhusu wanafunzi wa nchi za nje kuja kusoma nchini. Na wakifika hapa ni lazima wasome Kiswahili(for beginners) kama sehemu ya masomo yao.Hii itasaida sana kuitangaza sio tu elimu yetu bali hata Kiswahili ulimwenguni. Wakati Kiswahili kinapaswa kudumishwa kama lugha ya taifa, kiingereza kinapaswa kuwa lugha ya kufundishia.

Elimu ya sekondari inatakiwa kuhusishwa karibu na viwanda. Wanafunzi wanapaswa kushiriki katika mafunzo ya vitendo wakiwa bado shuleni ili kuhakikisha wanakuwa na ajira mara tu wanapohitimu. Somo la ujasiriamali ni lazima lifundishwe kuanzia sekondari tena kwa vitendo. Hii itasaidia sana hata kwa wale watakaofeli kuwa na ujuzi wa kujiajiri. Mfumo wa Elimu unapaswa kuwa wa ushindani, kipaumbele kikiwa ni ubora juu ya wingi hasa katika udahili wa vyuo vikuu. Ubora utavipa vyuo vyetu hadhi kimataifa (Kwenye QS university world rankings).

Elimu na Vitendo.jpg

Chanzo: Remix AI

Pili, serikali ya Tanzania inapaswa kutiliza mkazo uanzishwaji wa mazingira rafiki ya biashara yanayochochea ukuaji wa soko la ndani na kuvutia wawekezaji wa kigeni. Mazingira rafiki yanajumuisha urahisi wa kufanya biashara, uwepo wa umeme, upatikanaji wa mikopo, taratibu bora za biashara pamoja na kodi nafuu. Billionea Dangote alisema "Tanzania inabidi kutengeza sera nzuri Ili kuvutia wawekezaji wengi Zaidi". Pia utafiti unaonyesha kuwa makampuni makubwa kama Nike yanashindwa kuwekeza kwenye Nchi za kimaskini kama Tanzania Kwa sababu ya kodi kandamizi. Kwa kuiga mfano wa Korea Kusini, taifa ambalo linang’ara katika kuwezesha kuanzishwa kwa biashara kwa kiwango cha kimataifa, Tanzania inaweza kufaidika sana kwa kuboresha mazingira yake ya biashara ili kuvutia wawekezaji mbalimbali.

View: https://youtu.be/AAOs8EXq-qw?si=7-I-upNndk2ClNub
Tatu, ni muhimu serikali ya Tanzania kuendeleza teknolojia na kukuza ubunifu. Tanzania ina vijana wabunifu wengi Ila wameshindwa kushikwa mkono. Ubunifu na teknolojia vina jukumu muhimu katika kuinua nchi kutoka hadhi ya maendeleo duni hadi kuwa nchi iliyoendelea. Tanzania inapaswa kukumbatia mfumo thabiti wa Utafiti na Maendeleo (R&D), hasa katika teknolojia za viwanda. Ili kukuza ubunifu kwa ufanisi, ni muhimu kutambua kwamba ubunifu wenye mafanikio huimarika kupitia juhudi za pamoja kati ya vyuo vikuu, serikali na sekta binafsi. Aidha, teknolojia inajitokeza kama kipengele muhimu kitakachoweiwezesha Tanzania kupanda juu kwenye mnyororo wa thamani na kuongeza tija. Yote hayo yatawezekana kama Tanzania ikiwa na wizara maalumu ya sayansi, ubunifu na Teknolojia. Wizara hii itajikita kuwapa vipaumbele vijana wabunifu, kuongoza tafiti na kuendana na kasi ya Teknolojia ya Dunia (Robotics, Industrial 4.0 & artificial intelligence ).

View: https://youtube.com/watch?v=t3U5mcUfnso&si=I2g_OirBB7rP5UEA

View: https://youtu.be/3tJ7HLY-oe0?si=EN3wI9gky2IrpvN9
Serikali inapaswa kuunda sera ya kuhimiza viwanda vinavyolenga mauzo ya nje (export-oriented industrialization). Sera hii inatakiwa kulenga kuboresha ufanisi na ubora wa bidhaa za ndani Ili ziweze kushindana kimataifa. Kwa mkakati huu, kampuni za ndani zitabuni teknolojia mpya. Sambamba na hili, serikali inapaswa kuhakikisha kwamba kampuni zinapata ruzuku na uwekezaji ili kukuza masoko yao hasa masoko ya nje kupitia maonyesho ya biashara ya kimataifa na programu za uuzaji nje (export promotion programs).Kwa kuzingatia mauzo ya nje, kutakuwa na mtiririko wa mtaji wa kigeni, ambao utasaidia kuziba pengo la uhaba wa akiba za ndani. Kwa mfano, Korea Kusini ilikuwa kupitia sera za Seoul zilizolenga kuuza nje.

Export oriented Industralization.jpg

Chanzo: Remix AI
Mwisho serikali ingejitahidi sana kukuza sekta ya Sanaa hasa katika upande wa Sanaa ya kuigiza. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la umaarufu wa tamthilia za Korea Kusini nchini Tanzania. Tamthilia za ndani zimeonekana kukosa ubora hasa katika Teknolojia na maudhui huku nyingi zikiwa na hadithi za kufanana. Ili Tanzania iweze kukuza sanaa yake, inatakiwa kwanza ijikite kwenye maudhui ya kipekee na utamaduni. Mfano Korea Kusini inaingiza utamaduni wake katika tamthilia zake, jambo linalovutia watazamaji wa kimataifa. Tanzania pia ingejikita kukuza ubora wa watayarishaji wetu pamoja na Teknolojia ya uzalishaji kwa kushirikiana na Nchi zilizoendelea.

Mfano hatua aliyofanya Rais Samia kuwakutanisha watayarishaji wetu na wa Korea Kusini tarehe 01/06/2024 ni mwanzo mzuri. Ila tunatamani isiishie hapo. Tungependa kuona hapo mbeleni hata kazi za pamoja ( Korea Kusini na Tanzania) zikitoka. Pia ni kujenga miundombinu ya filamu. Mfano nchini Korea Kusini kuna maeneo maalumu (filming locations) ambayo hutumiwa na wazalishaji wa filamu za ndani na nje. Sanaa inawez pia kutumika kukuza utalii wetu. Mwisho serikali ingetengeneza mifumo mizuri kwajili ya kusambaza filamu na tamthilia na kuimarisha ushirikiano na wadau wa kimataifa kama NETFLIX. Mauzo yatakayo tokana na Sanaa yanawez kuongeza pato la taifa.

View: https://youtu.be/WUIuLpqrVSo?si=2DDAwfqcipyxVobE

View: https://youtu.be/Qt8mVDwFpnQ?si=qlz_0lIqs-KJjGGy

IMG-20240706-WA0305.jpg

20240601_125227.jpg

Angalizo:

Tanzania inaweza kufikia malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi kwa kujifunza kutoka kwa Korea Kusini, lakini kwa kutekeleza mikakati hiyo kwa njia inayoendana na misingi ya demokrasia na haki za binadamu na sio Njia za kibabe kama alizotumia Raisi Park Chung-hee. Pia ni muhimu kujua kuwa maendeleo yanaleta faida kubwa lakini yanakuja na changamoto mfano; madeni, uharibifu wa mazingira kama vile ukataji miti na uchafuzi (pollution).Hivyo basi, ni muhimu kwa Tanzania kuzingatia utawala bora wakati wa hatua za maendeleo ili kupunguza hatari hizi.
Tanzania tuitakayo si Ile yenye hadhi ya Nchi duni,Bali Nchi iliyoendelea. Kwa pamoja tunaweza kufika huko💪

Tanzania We Want.jpg

Tanzania Tuitakayo 2050.​
 
Upvote 336
Tanzania ni mwanachama wa WTO ilijiunga mwaka 1995, kuzuia bidhaa yaani protectionism ni kinyume na sheria za WTO, nchi ifanyaje kukabiliana na kikwazo hiko...

Asante kwa mchango wako mzuri katika hii point ya export-oriented industrialization. Kuna kitu nilitaka kukiweka sawa katika hii point niliotoa nikilenga maswali uliyoniuliza.

1. Kuzuia bidhaa za kigeni nchini ni kinyume na sheria za WTO, Tanzania ifanye nini kukabiliana na kikwazo hiki?

Ni kweli kwamba Tanzania ni mwanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) na hivyo inahitajika kufuata sheria za biashara huria, ambazo zinaweka vikwazo dhidi ya sera za ulinzi wa ndani (protectionism). Hata hivyo, kuna njia ambazo Tanzania inaweza kuchukua ili kuendeleza viwanda vya ndani bila kuvunja sheria za WTO. Moja ya njia ni kupitia sera za kipaumbele (incentives) badala ya vizuizi (restrictions). Serikali inaweza kutoa ruzuku kwa viwanda vya ndani, kutoa mikopo yenye riba nafuu, na kuanzisha maeneo maalum ya kiuchumi (special economic zones) ambayo yatatoa motisha kwa wazalishaji wa ndani. Hii itasaidia kuongeza ushindani wa bidhaa za ndani bila kuingilia moja kwa moja biashara ya kimataifa.

2. Itakuwaje nchi zingine zikiweka vikwazo dhidi ya bidhaa za Tanzania kama Tanzania imekataza bidhaa zao?

Hili ni suala muhimu linalohusisha diplomasia ya biashara. Ili kuepuka hali ambapo nchi nyingine zinaweza kujibu kwa hatua za ulinzi (retaliation), ni muhimu kwa Tanzania kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara na nchi zingine, kushiriki kikamilifu katika majadiliano ya kibiashara ya kimataifa, na kufuata kanuni za WTO. Pia, Tanzania inaweza kuzingatia mikataba ya biashara ya kikanda (regional trade agreements) ambayo inaweza kusaidia kuongeza fursa za mauzo ya nje bila kugongana na sheria za WTO.

3. Jinsi ya kufanikisha export-oriented economy kwa mazingira hayo?

Tanzania inaweza kufanikisha uchumi unaolenga mauzo ya nje kwa kuboresha ubora na ufanisi wa bidhaa zake ili ziweze kushindana kimataifa. Hii inajumuisha kuboresha miundombinu, kama vile barabara na bandari, na kuongeza uwekezaji katika teknolojia na elimu. Kwa kuongeza, serikali inaweza kusaidia makampuni ya ndani kupata masoko ya nje kupitia maonyesho ya biashara ya kimataifa na programu za uuzaji nje (export promotion programs). Kwa njia hii, makampuni ya ndani yataweza kupanua wigo wao wa mauzo bila kutegemea sera za ulinzi.

4. Jinsi ya kukabiliana na hatari za exportation kama vile mabadiliko ya thamani ya sarafu?

Hatari za kiuchumi, kama vile mabadiliko ya thamani ya sarafu, zinaweza kupunguzwa kupitia sera za fedha na bajeti zilizo imara. Tanzania inaweza kuanzisha mifumo ya kudhibiti viwango vya ubadilishaji wa fedha (currency hedging mechanisms) ili kulinda kampuni zake dhidi ya kushuka kwa thamani ya sarafu. Kwa mfano wa Japan na Plaza Accord, ni muhimu kuwa na sera zinazosaidia kupunguza utegemezi kwa soko moja la nje. Kupitia ushirikiano wa kikanda na kuboresha bidhaa na huduma ili ziweze kuingia kwenye masoko mbalimbali, Tanzania inaweza kupunguza hatari za mabadiliko ya bei za bidhaa zake katika soko la kimataifa.

Kwa kumalizia, Tanzania inapaswa kuzingatia sera za kuboresha ubora wa bidhaa zake, kuongeza uzalishaji na teknolojia, na kujenga miundombinu bora ili kushindana katika soko la kimataifa bila kuhitaji sera za ulinzi wa ndani. Hii itaiwezesha kufikia uchumi unaolenga mauzo ya nje huku ikiheshimu sheria za WTO.
Hope that made sense and cleared all doubts about that point of Export oriented industrialization.
PLEASE DON'T FORGET TO VOTE FOR ME 🙏😊
 
Tanzania inapaswa kukumbatia mfumo thabiti wa Utafiti na Maendeleo (R&D), hasa katika teknolojia za viwanda. R&D inatumika kama kichecheo cha msingi kwa ukuaji wa kiuchumi na maendeleo ya viwanda, hasa kwa mataifa yanayoendelea. Ili kukuza ubunifu kwa ufanisi, ni muhimu kutambua kwamba ubunifu wenye mafanikio huimarika kupitia juhudi za pamoja kati ya vyuo vikuu, serikali na sekta binafsi.
Najiuliza, ikiwa nchi ikifanya hivi itaendelea si inapaswa pia kampuni iwe ikifanya hivyo inaendelea? Kampuni zil8zopo bongo tunaomba mifano hai ya jinsi rnd imeinua kampuni zenu.

Mfano rnd ya ukwaju kuwa barafu ya taifa...... sasa mtupe vitu zaidi.

Ahsante mleta mada
 
Ahsante na wewe pia kwa kuchangia kwenye hii point ya R&D. PLEASE DON'T FORGET TO VOTE FOR ME 🙏😊
 
Baadhi ya majibu yako Yana mkanganyiko na mada kuu. Swali linguine.

Umesema tuige Korea kusini Ila kumbuka raisi Park Chung Hee alikuwa dikteta.

Kufanikisha hayo malengo ya rapid economic growth, Kwanza.
1. Alikamata wafanya biashara wote wakubwa Kwa Madai ya kujipatia pesa chafu, hata kama hakuna ushahidi na wakawekwa jela.

2. Wakalazimishwa kusaini mkataba unaosema "nipo tayari kutoa Mali zangu Kwa ajili ya maendeleo ya taifa pale itakapohitajika" ndipo unaruhusiwa kutoka jela.

3-Mkataba huu ukawaweka wafanyabiashara kitanzini Kwa maana utatengeneza bidhaa kulingana na matakwa ya serikali kupitia mpango WA miaka mitano, na kampuni ikiwa inafanya vibaya kwenye mauzo ya nje.yafuatayo yatakukuta

Serikali haikupi tena mikopo ya bei na nafuu na unalazimishwa kukabidhi kiwanda Kwa serikali na inampa kampuni nyingine inayofanya vizuri kwenye mauzo ya nje. Na hicho ndio chanzo cha kuibuka makampuni makubwa kama Samsung, LG, Hyundai, Kia.

Hapo hatujazungumzia ukandamizaji WA upinzani na kubadilisha katiba iliyomfanya raisi WA maisha asiyepingwa na yoyote.

Je TZ ipite njia hiyo? Na Kwa namna gani serikali italazimisha wafanyabiashara kufuta development plan za nchi?
Maswali yako yanaonyesha unaufahamu wa kina wa historia ya Korea Kusini na changamoto zinazoweza kutokea katika kuiga mifano ya maendeleo ya kiuchumi kutoka nchi nyingine. Ni muhimu kuelewa kwamba kila nchi ina njia yake ya kipekee ya kufikia maendeleo, na kile kilichofanya kazi kwa Korea Kusini kinaweza kuwa na changamoto tofauti kwa Tanzania. Hapa kuna majibu na mapendekezo kuhusu maswali na hoja zako:

1. Je, Tanzania ipite njia kama ile ya Korea Kusini chini ya utawala wa dikteta Park Chung Hee?

Tanzania haihitaji kufuata njia ya utawala wa kimabavu ili kufikia maendeleo ya haraka ya kiuchumi. Badala yake, inaweza kujifunza baadhi ya mikakati ya kiuchumi ya Korea Kusini na kuziendekeza kwa njia inayoheshimu utawala bora na haki za binadamu. Njia za kimabavu hazilingani na misingi ya demokrasia na haki za binadamu ambazo ni muhimu kwa maendeleo endelevu na ya haki.

2. Kwa namna gani serikali italazimisha wafanyabiashara kufuata mipango ya maendeleo ya nchi?

Hii inaweza kufanywa kupitia sera bora na motisha (incentives) badala ya kulazimisha. Serikali inaweza kuweka mazingira bora ya kibiashara yanayovutia uwekezaji na kuruhusu ubunifu. Hapa kuna njia kadhaa ambazo zinaweza kusaidia:

Motisha za kifedha: Serikali inaweza kutoa ruzuku, mikopo yenye riba nafuu, na faida za kodi kwa kampuni zinazofuata mipango ya maendeleo ya kitaifa.

Uwekezaji katika miundombinu: Kuwekeza katika miundombinu kama barabara, reli, na bandari kutasaidia kampuni kupata masoko ya ndani na nje kwa urahisi zaidi.

Kujenga mazingira wezeshi ya kibiashara: Kupunguza urasimu na kuimarisha utawala wa sheria ili kurahisisha kufanya biashara nchini. Hii itavutia wawekezaji wa ndani na nje.

Mafunzo na elimu: Kutoa mafunzo na elimu kwa wafanyakazi ili wawe na ujuzi unaohitajika katika sekta mbalimbali, na hivyo kuboresha uzalishaji na ushindani wa kimataifa.

Ubunifu na teknolojia: Kuhimiza ubunifu na matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji ili kuboresha ubora wa bidhaa na huduma.

3. Njia za kuhakikisha kampuni zinafuata mipango ya maendeleo bila kutumia nguvu?

Badala ya kutumia nguvu, serikali inaweza kutumia njia zifuatazo:

Ushirikiano na sekta binafsi: Kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi katika kubuni na kutekeleza mipango ya maendeleo. Ushirikiano huu unaweza kujumuisha majadiliano ya wazi na ushirikiano katika miradi mikubwa ya kitaifa.

Kuweka malengo ya pamoja: Kutengeneza malengo ya kitaifa ya maendeleo ambayo yanakubalika na sekta binafsi. Hii inaweza kujumuisha malengo ya muda mfupi na mrefu ambayo kampuni zinaweza kuyatimiza.

Mfumo wa tathmini na motisha: Kuanzisha mfumo wa tathmini na motisha kwa kampuni zinazofanya vizuri katika kufuata mipango ya maendeleo. Hii inaweza kujumuisha tuzo za kitaifa na kimataifa, ruzuku za ziada, au faida za kodi.

Kwa muhtasari, Tanzania inaweza kufikia malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi kwa kujifunza kutoka kwa nchi kama Korea Kusini, lakini kwa kutekeleza mikakati hiyo kwa njia inayoendana na misingi ya demokrasia, haki za binadamu, na utawala bora. Njia za kibabe hazifai na zinaweza kusababisha matatizo makubwa ya kijamii na kiuchumi. Serikali inapaswa kuweka mazingira wezeshi yanayovutia uwekezaji na ubunifu, na kufanya kazi kwa karibu na sekta binafsi ili kufikia malengo ya kitaifa ya maendeleo.
I hope that made sense..
PLEASE DON'T FORGET TO VOTE FOR ME 🙏😊
 
Kuna fursa ya kutumia soko la AGOA imefunguliwa miaka mingi sana, lkn tumeshindwa kuitumia.

Sababu kubwa ni teknolojia duni
inayotumika inayopelekea kumzalisha mazo yenye viwango dunia vya ubora, mfano sumu kuvu kwenye mahindi, vimelea vya magonjwa kwenye mauaji, matunda na nyama. Na hata ngozi na kwato za ng'ombe zinakuwa duni. Mazao yetu yakipelkwa yanakataliwa huko.

Jambo la pili ni ukosefu wa mwendelezo wa ku-supply hayo mazao hata kama atapatikana mnunuzi wa hayo mazao. Mfano itokee kampuni Inataka maharage ya Mbeya, tuna uwezo wa kuzalisha maharage ya Mbeya kwa mwaka miezi yote 12 wakati kilimo chetu kinategemea mvua?
 
Ni kwel kabisa ulichosema. PLEASE DON'T FORGET TO VOTE FOR ME 😊🙏
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Umoja wa Mataifa unaiweka Tanzania katika kundi la Nchi maskini Zaidi (LDC). Hata hivyo, ikizingatiwa rasilimali nyingi na uwezo mkubwa wa nchi yetu, hadhi hii inaonekana kutofaa. Miaka ya 1950, Korea Kusini ilikuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani ikitegemea sana kilimo na haikuwa na misingi thabiti ya viwanda. Licha ya changamoto hizi, Korea Kusini iliweza kujijenga kutoka chini na kuibuka kama taifa lenye mafanikio. Kama Korea Kusini iliweza, Kwanini Sisi Tushindwe? Sisi pia tunaweza.

Je Tanzania ifanye nini ili kutoka katika kundi la nchi duni mpaka kuwa nchi iliyoendelea?
Kwanza kabisa ni uwekezaji katika elimu na rasilimali watu. Kundi la wafanyakazi waliosoma vizuri na wenye ujuzi ni muhimu kwa ukuaji wa viwanda. Tanzania inapaswa kurekebisha mfumo wake wa elimu ufundishwe kwa kiingereza kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu, ili kuongeza ushindani wetu kimataifa. Nikiwa kama mmoja wa wanafunzi wanaotafuta Ufadhili wa kusoma shahada ya uzamili nje, nimegundua kuwa wanafunzi wengi wa kutoka Tanzania tunakosa fursa hizo sababu ya kufeli mitihani ya kiingereza kama IELTS, ukilinganisha na wenzetu Kenya ambao Kingereza kinatumika kama lugha ya kufundishia. Aidha serikali inatakiwa kubuni ufadhili wake “Tanzanian Government Scholarship” ambao utaruhusu wanafunzi wa nchi za nje kuja kusoma nchini. Na wakifika hapa ni lazima wasome Kiswahili(for beginners) kama sehemu ya masomo yao.Hii itasaida sana kuitangaza sio tu elimu yetu bali hata Kiswahili ulimwenguni. Wakati Kiswahili kinapaswa kudumishwa kama lugha ya taifa, kiingereza kinapaswa kuwa lugha ya kufundishia.

Elimu ya sekondari inatakiwa kuhusishwa karibu na viwanda. Wanafunzi wanapaswa kushiriki katika mafunzo ya vitendo wakiwa bado shuleni ili kuhakikisha wanakuwa na ajira mara tu wanapohitimu. Somo la ujasiriamali ni lazima lifundishwe kuanzia sekondari tena kwa vitendo. Hii itasaidia sana hata kwa wale watakaofeli kuwa na ujuzi wa kujiajiri. Mfumo wa Elimu unapaswa kuwa wa ushindani, kipaumbele kikiwa ni ubora juu ya wingi hasa katika udahili wa vyuo vikuu. Ubora utavipa vyuo vyetu hadhi kimataifa (Kwenye QS university world rankings).

View attachment 3013700
Chanzo: Remix AI

Pili, serikali ya Tanzania inapaswa kutiliza mkazo uanzishwaji wa mazingira rafiki ya biashara yanayochochea ukuaji wa soko la ndani na kuvutia wawekezaji wa kigeni. Mazingira rafiki yanajumuisha urahisi wa kufanya biashara, uwepo wa umeme, upatikanaji wa mikopo, taratibu bora za biashara pamoja na utekelezaji mzuri wa mikataba na mifumo ya kutatua madeni. Billionea Dangote alisema "Tanzania inabidi kutengeza sera nzuri Ili kuvutia wawekezaji wengi Zaidi". Kwa kuiga mfano wa Korea Kusini, taifa ambalo linang’ara katika kuwezesha kuanzishwa kwa biashara na utekelezaji wa mikataba kwa kiwango cha kimataifa, Tanzania inaweza kufaidika sana kwa kuboresha mazingira yake ya biashara na kuimarisha ubunifu ili kuvutia makundi mbalimbali ya wawekezaji.

View: https://youtu.be/AAOs8EXq-qw?si=7-I-upNndk2ClNub

Tatu, ni muhimu serikali ya Tanzania kuendeleza teknolojia na kukuza ubunifu. Tanzania ina vijana wabunifu wengi Ila wameshindwa kushikwa mkono. Ubunifu na teknolojia vina jukumu muhimu katika kuinua nchi kutoka hadhi ya maendeleo duni hadi kuwa nchi iliyoendelea. Tanzania inapaswa kukumbatia mfumo thabiti wa Utafiti na Maendeleo (R&D), hasa katika teknolojia za viwanda. Ili kukuza ubunifu kwa ufanisi, ni muhimu kutambua kwamba ubunifu wenye mafanikio huimarika kupitia juhudi za pamoja kati ya vyuo vikuu, serikali na sekta binafsi. Aidha, teknolojia inajitokeza kama kipengele muhimu kitakachoweiwezesha Tanzania kupanda juu kwenye mnyororo wa thamani na kuongeza tija. Kwa kuiga uwekezaji mkubwa wa Korea Kusini katika utafiti na Maendeleo ambao umefungua njia kwa uongozi wake katika viwanda, Tanzania inaweza pia kutumia nguvu ya ubunifu na teknolojia ili kusukuma mbele safari yake ya maendeleo.

View: https://youtube.com/watch?v=t3U5mcUfnso&si=I2g_OirBB7rP5UEA

View: https://youtu.be/3tJ7HLY-oe0?si=EN3wI9gky2IrpvN9

Serikali inapaswa kuunda sera ya kuhimiza viwanda vinavyolenga mauzo ya nje (export-oriented industrialization). Sera hii inatakiwa kulenga kuboresha ufanisi na ubora wa bidhaa za ndani Ili ziweze kushindana kimataifa. Kwa mkakati huu, kampuni za ndani zitabuni teknolojia mpya. Sambamba na hili, serikali inapaswa kuhakikisha kwamba kampuni zinapata ruzuku na uwekezaji ili kukuza masoko yao hasa masoko ya nje kupitia maonyesho ya biashara ya kimataifa na programu za uuzaji nje (export promotion programs).Kwa kuzingatia mauzo ya nje, kutakuwa na mtiririko wa mtaji wa kigeni, ambao utasaidia kuziba pengo la uhaba wa akiba za ndani. Kwa mfano, Korea Kusini ilikuwa kupitia sera za Seoul zilizolenga kuuza nje.

View attachment 3009644
Chanzo: Remix AI
Mwisho serikali ingejitahidi sana kukuza sekta ya Sanaa hasa katika upande wa Sanaa ya kuigiza. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la umaarufu wa tamthilia za Korea Kusini nchini Tanzania. Tamthilia za ndani zimeonekana kukosa ubora hasa katika Teknolojia na maudhui huku nyingi zikiwa na hadithi za kufanana. Ili Tanzania iweze kukuza sanaa yake, Kwanza ni kuboresha ubora wa uzalishaji kama vile Korea Kusini. Pili Tanzania inatakiwa ijikite kwenye maudhui ya kipekee na utamaduni. Mfano Korea Kusini inaingiza utamaduni wake katika tamthilia zake, jambo linalovutia watazamaji wa kimataifa. Tanzania inaweza kukuza tamthilia zinazohusisha hadithi za kipekee za kitanzania, tamaduni ambazo zinaweza kuvutia watazamaji wa ndani na nje. Pia ni kujenga miundombinu ya filamu. Mfano nchini Korea Kusini kuna maeneo maalumu (filming locations) ambayo hutumiwa na wazalishaji wa filamu za ndani na nje. Sanaa inawez pia kutumika kukuza utalii wetu. Mwisho serikali ingetengeneza mifumo mizuri kwajili ya kusambaza filamu na tamthilia na kuimarisha ushirikiano na wadau wa kimataifa kama NETFLIX. Mauzo yatakayo tokana na Sanaa yanawez kuongeza pato la taifa.

View: https://youtu.be/WUIuLpqrVSo?si=2DDAwfqcipyxVobE

View: https://youtu.be/j17pTr9c-sk?si=fwMntYDMLUn_S1Z1

Angalizo:
Tanzania inaweza kufikia malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi kwa kujifunza kutoka kwa Korea Kusini, lakini kwa kutekeleza mikakati hiyo kwa njia inayoendana na misingi ya demokrasia, haki za binadamu, na utawala bora na sio Njia za kibabe kama alizotumia Raisi Park Chung-hee. Pia ni muhimu kujua kuwa maendeleo yanaleta faida kubwa lakini yanakuja na changamoto mfano; madeni, uharibifu wa mazingira kama vile ukataji miti na uchafuzi (pollution).Hivyo basi, ni muhimu kwa Tanzania kuzingatia utawala bora wakati wa hatua za maendeleo ili kupunguza hatari hizi.
Tanzania tuitakayo si Ile yenye hadhi ya Nchi duni,Bali Nchi iliyoendelea. Kwa pamoja tunaweza kufika huko💪

View attachment 3009665
Tanzania Tuitakayo 2050.​

Safi sana, habari making

Well deserved
 
Back
Top Bottom