SoC04 Mpango wa miaka 25 wa kubadilisha Tanzania kutoka nchi maskini zaidi hadi nchi iliyoendelea kwa kuchukua mifano kutoka Korea Kusini

SoC04 Mpango wa miaka 25 wa kubadilisha Tanzania kutoka nchi maskini zaidi hadi nchi iliyoendelea kwa kuchukua mifano kutoka Korea Kusini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Professor Aaron Jackson

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2024
Posts
224
Reaction score
241
Umoja wa Mataifa unaiweka Tanzania katika kundi la Nchi maskini Zaidi (LDC). Hata hivyo, ikizingatiwa rasilimali nyingi na uwezo mkubwa wa nchi yetu, hadhi hii inaonekana kutofaa. Miaka ya 1950, Korea Kusini ilikuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani ikitegemea sana kilimo na haikuwa na misingi thabiti ya viwanda. Licha ya changamoto hizi, Korea Kusini iliweza kujijenga kutoka chini na kuibuka kama taifa lenye mafanikio. Kama Korea Kusini iliweza, Kwanini Sisi Tushindwe? Sisi pia tunaweza.

Je, Tanzania ifanye nini ili kutoka katika kundi la nchi duni mpaka kuwa nchi iliyoendelea?
Kwanza kabisa ni uwekezaji katika elimu na rasilimali watu. Kundi la wafanyakazi waliosoma vizuri na wenye ujuzi ni muhimu kwa ukuaji wa viwanda. Tanzania inapaswa kurekebisha mfumo wake wa elimu ufundishwe kwa kiingereza kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu, ili kuongeza ushindani wetu kimataifa. Nikiwa kama mmoja wa wanafunzi wanaotafuta Ufadhili wa kusoma shahada ya uzamili nje, nimegundua kuwa wanafunzi wengi wa kutoka Tanzania tunakosa fursa hizo sababu ya kufeli mitihani ya kiingereza kama IELTS, ukilinganisha na wenzetu Kenya ambao Kingereza kinatumika kama lugha ya kufundishia. Aidha serikali inatakiwa kubuni ufadhili wake “Tanzanian Government Scholarship” ambao utaruhusu wanafunzi wa nchi za nje kuja kusoma nchini. Na wakifika hapa ni lazima wasome Kiswahili(for beginners) kama sehemu ya masomo yao.Hii itasaida sana kuitangaza sio tu elimu yetu bali hata Kiswahili ulimwenguni. Wakati Kiswahili kinapaswa kudumishwa kama lugha ya taifa, kiingereza kinapaswa kuwa lugha ya kufundishia.

Elimu ya sekondari inatakiwa kuhusishwa karibu na viwanda. Wanafunzi wanapaswa kushiriki katika mafunzo ya vitendo wakiwa bado shuleni ili kuhakikisha wanakuwa na ajira mara tu wanapohitimu. Somo la ujasiriamali ni lazima lifundishwe kuanzia sekondari tena kwa vitendo. Hii itasaidia sana hata kwa wale watakaofeli kuwa na ujuzi wa kujiajiri. Mfumo wa Elimu unapaswa kuwa wa ushindani, kipaumbele kikiwa ni ubora juu ya wingi hasa katika udahili wa vyuo vikuu. Ubora utavipa vyuo vyetu hadhi kimataifa (Kwenye QS university world rankings).

Elimu na Vitendo.jpg

Chanzo: Remix AI

Pili, serikali ya Tanzania inapaswa kutiliza mkazo uanzishwaji wa mazingira rafiki ya biashara yanayochochea ukuaji wa soko la ndani na kuvutia wawekezaji wa kigeni. Mazingira rafiki yanajumuisha urahisi wa kufanya biashara, uwepo wa umeme, upatikanaji wa mikopo, taratibu bora za biashara pamoja na kodi nafuu. Billionea Dangote alisema "Tanzania inabidi kutengeza sera nzuri Ili kuvutia wawekezaji wengi Zaidi". Pia utafiti unaonyesha kuwa makampuni makubwa kama Nike yanashindwa kuwekeza kwenye Nchi za kimaskini kama Tanzania Kwa sababu ya kodi kandamizi. Kwa kuiga mfano wa Korea Kusini, taifa ambalo linang’ara katika kuwezesha kuanzishwa kwa biashara kwa kiwango cha kimataifa, Tanzania inaweza kufaidika sana kwa kuboresha mazingira yake ya biashara ili kuvutia wawekezaji mbalimbali.

View: https://youtu.be/AAOs8EXq-qw?si=7-I-upNndk2ClNub
Tatu, ni muhimu serikali ya Tanzania kuendeleza teknolojia na kukuza ubunifu. Tanzania ina vijana wabunifu wengi Ila wameshindwa kushikwa mkono. Ubunifu na teknolojia vina jukumu muhimu katika kuinua nchi kutoka hadhi ya maendeleo duni hadi kuwa nchi iliyoendelea. Tanzania inapaswa kukumbatia mfumo thabiti wa Utafiti na Maendeleo (R&D), hasa katika teknolojia za viwanda. Ili kukuza ubunifu kwa ufanisi, ni muhimu kutambua kwamba ubunifu wenye mafanikio huimarika kupitia juhudi za pamoja kati ya vyuo vikuu, serikali na sekta binafsi. Aidha, teknolojia inajitokeza kama kipengele muhimu kitakachoweiwezesha Tanzania kupanda juu kwenye mnyororo wa thamani na kuongeza tija. Yote hayo yatawezekana kama Tanzania ikiwa na wizara maalumu ya sayansi, ubunifu na Teknolojia. Wizara hii itajikita kuwapa vipaumbele vijana wabunifu, kuongoza tafiti na kuendana na kasi ya Teknolojia ya Dunia (Robotics, Industrial 4.0 & artificial intelligence ).

View: https://youtube.com/watch?v=t3U5mcUfnso&si=I2g_OirBB7rP5UEA

View: https://youtu.be/3tJ7HLY-oe0?si=EN3wI9gky2IrpvN9
Serikali inapaswa kuunda sera ya kuhimiza viwanda vinavyolenga mauzo ya nje (export-oriented industrialization). Sera hii inatakiwa kulenga kuboresha ufanisi na ubora wa bidhaa za ndani Ili ziweze kushindana kimataifa. Kwa mkakati huu, kampuni za ndani zitabuni teknolojia mpya. Sambamba na hili, serikali inapaswa kuhakikisha kwamba kampuni zinapata ruzuku na uwekezaji ili kukuza masoko yao hasa masoko ya nje kupitia maonyesho ya biashara ya kimataifa na programu za uuzaji nje (export promotion programs).Kwa kuzingatia mauzo ya nje, kutakuwa na mtiririko wa mtaji wa kigeni, ambao utasaidia kuziba pengo la uhaba wa akiba za ndani. Kwa mfano, Korea Kusini ilikuwa kupitia sera za Seoul zilizolenga kuuza nje.

Export oriented Industralization.jpg

Chanzo: Remix AI
Mwisho serikali ingejitahidi sana kukuza sekta ya Sanaa hasa katika upande wa Sanaa ya kuigiza. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la umaarufu wa tamthilia za Korea Kusini nchini Tanzania. Tamthilia za ndani zimeonekana kukosa ubora hasa katika Teknolojia na maudhui huku nyingi zikiwa na hadithi za kufanana. Ili Tanzania iweze kukuza sanaa yake, inatakiwa kwanza ijikite kwenye maudhui ya kipekee na utamaduni. Mfano Korea Kusini inaingiza utamaduni wake katika tamthilia zake, jambo linalovutia watazamaji wa kimataifa. Tanzania pia ingejikita kukuza ubora wa watayarishaji wetu pamoja na Teknolojia ya uzalishaji kwa kushirikiana na Nchi zilizoendelea.

Mfano hatua aliyofanya Rais Samia kuwakutanisha watayarishaji wetu na wa Korea Kusini tarehe 01/06/2024 ni mwanzo mzuri. Ila tunatamani isiishie hapo. Tungependa kuona hapo mbeleni hata kazi za pamoja ( Korea Kusini na Tanzania) zikitoka. Pia ni kujenga miundombinu ya filamu. Mfano nchini Korea Kusini kuna maeneo maalumu (filming locations) ambayo hutumiwa na wazalishaji wa filamu za ndani na nje. Sanaa inawez pia kutumika kukuza utalii wetu. Mwisho serikali ingetengeneza mifumo mizuri kwajili ya kusambaza filamu na tamthilia na kuimarisha ushirikiano na wadau wa kimataifa kama NETFLIX. Mauzo yatakayo tokana na Sanaa yanawez kuongeza pato la taifa.

View: https://youtu.be/WUIuLpqrVSo?si=2DDAwfqcipyxVobE

View: https://youtu.be/Qt8mVDwFpnQ?si=qlz_0lIqs-KJjGGy

IMG-20240706-WA0305.jpg

20240601_125227.jpg

Angalizo:

Tanzania inaweza kufikia malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi kwa kujifunza kutoka kwa Korea Kusini, lakini kwa kutekeleza mikakati hiyo kwa njia inayoendana na misingi ya demokrasia na haki za binadamu na sio Njia za kibabe kama alizotumia Raisi Park Chung-hee. Pia ni muhimu kujua kuwa maendeleo yanaleta faida kubwa lakini yanakuja na changamoto mfano; madeni, uharibifu wa mazingira kama vile ukataji miti na uchafuzi (pollution).Hivyo basi, ni muhimu kwa Tanzania kuzingatia utawala bora wakati wa hatua za maendeleo ili kupunguza hatari hizi.
Tanzania tuitakayo si Ile yenye hadhi ya Nchi duni,Bali Nchi iliyoendelea. Kwa pamoja tunaweza kufika huko💪

Tanzania We Want.jpg

Tanzania Tuitakayo 2050.​
 
Upvote 336
Umoja wa Mataifa unaiweka Tanzania katika kundi la Nchi maskini Zaidi (LDC). Hata hivyo, ikizingatiwa rasilimali nyingi na uwezo mkubwa wa nchi yetu, hadhi hii inaonekana kutofaa. Miaka ya 1950, Korea Kusini ilikuwa moja ya nchi maskini zaidi duniani ikitegemea sana kilimo na haikuwa na misingi thabiti ya viwanda. Licha ya changamoto hizi, Korea Kusini iliweza kujijenga kutoka chini na kuibuka kama taifa lenye mafanikio. Kama Korea Kusini iliweza, Kwanini Sisi Tushindwe? Sisi pia tunaweza.

Je Tanzania ifanye nini ili kutoka katika kundi la nchi duni mpaka kuwa nchi iliyoendelea?
Kwanza kabisa ni uwekezaji katika elimu na rasilimali watu. Kundi la wafanyakazi waliosoma vizuri na wenye ujuzi ni muhimu kwa ukuaji wa viwanda. Tanzania inapaswa kurekebisha mfumo wake wa elimu ufundishwe kwa kiingereza kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu, ili kuongeza ushindani wetu kimataifa. Nikiwa kama mmoja wa wanafunzi wanaotafuta Ufadhili wa kusoma shahada ya uzamili nje, nimegundua kuwa wanafunzi wengi wa kutoka Tanzania tunakosa fursa hizo sababu ya kufeli mitihani ya kiingereza kama IELTS, ukilinganisha na wenzetu Kenya ambao Kingereza kinatumika kama lugha ya kufundishia. Aidha serikali inatakiwa kubuni ufadhili wake “Tanzanian Government Scholarship” ambao utaruhusu wanafunzi wa nchi za nje kuja kusoma nchini. Na wakifika hapa ni lazima wasome Kiswahili(for beginners) kama sehemu ya masomo yao.Hii itasaida sana kuitangaza sio tu elimu yetu bali hata Kiswahili ulimwenguni. Wakati Kiswahili kinapaswa kudumishwa kama lugha ya taifa, kiingereza kinapaswa kuwa lugha ya kufundishia.

Elimu ya sekondari inatakiwa kuhusishwa karibu na viwanda. Wanafunzi wanapaswa kushiriki katika mafunzo ya vitendo wakiwa bado shuleni ili kuhakikisha wanakuwa na ajira mara tu wanapohitimu. Somo la ujasiriamali ni lazima lifundishwe kuanzia sekondari tena kwa vitendo. Hii itasaidia sana hata kwa wale watakaofeli kuwa na ujuzi wa kujiajiri. Mfumo wa Elimu unapaswa kuwa wa ushindani, kipaumbele kikiwa ni ubora juu ya wingi hasa katika udahili wa vyuo vikuu. Ubora utavipa vyuo vyetu hadhi kimataifa (Kwenye QS university world rankings).

View attachment 3013700
Chanzo: Remix AI

Pili, serikali ya Tanzania inapaswa kutiliza mkazo uanzishwaji wa mazingira rafiki ya biashara yanayochochea ukuaji wa soko la ndani na kuvutia wawekezaji wa kigeni. Mazingira rafiki yanajumuisha urahisi wa kufanya biashara, uwepo wa umeme, upatikanaji wa mikopo, taratibu bora za biashara pamoja na utekelezaji mzuri wa mikataba na mifumo ya kutatua madeni. Billionea Dangote alisema "Tanzania inabidi kutengeza sera nzuri Ili kuvutia wawekezaji wengi Zaidi". Kwa kuiga mfano wa Korea Kusini, taifa ambalo linang’ara katika kuwezesha kuanzishwa kwa biashara na utekelezaji wa mikataba kwa kiwango cha kimataifa, Tanzania inaweza kufaidika sana kwa kuboresha mazingira yake ya biashara na kuimarisha ubunifu ili kuvutia makundi mbalimbali ya wawekezaji.

View: https://youtu.be/AAOs8EXq-qw?si=7-I-upNndk2ClNub

Tatu, ni muhimu serikali ya Tanzania kuendeleza teknolojia na kukuza ubunifu. Tanzania ina vijana wabunifu wengi Ila wameshindwa kushikwa mkono. Ubunifu na teknolojia vina jukumu muhimu katika kuinua nchi kutoka hadhi ya maendeleo duni hadi kuwa nchi iliyoendelea. Tanzania inapaswa kukumbatia mfumo thabiti wa Utafiti na Maendeleo (R&D), hasa katika teknolojia za viwanda. Ili kukuza ubunifu kwa ufanisi, ni muhimu kutambua kwamba ubunifu wenye mafanikio huimarika kupitia juhudi za pamoja kati ya vyuo vikuu, serikali na sekta binafsi. Aidha, teknolojia inajitokeza kama kipengele muhimu kitakachoweiwezesha Tanzania kupanda juu kwenye mnyororo wa thamani na kuongeza tija. Kwa kuiga uwekezaji mkubwa wa Korea Kusini katika utafiti na Maendeleo ambao umefungua njia kwa uongozi wake katika viwanda, Tanzania inaweza pia kutumia nguvu ya ubunifu na teknolojia ili kusukuma mbele safari yake ya maendeleo.

View: https://youtube.com/watch?v=t3U5mcUfnso&si=I2g_OirBB7rP5UEA

View: https://youtu.be/3tJ7HLY-oe0?si=EN3wI9gky2IrpvN9

Serikali inapaswa kuunda sera ya kuhimiza viwanda vinavyolenga mauzo ya nje (export-oriented industrialization). Sera hii inatakiwa kulenga kuboresha ufanisi na ubora wa bidhaa za ndani Ili ziweze kushindana kimataifa. Kwa mkakati huu, kampuni za ndani zitabuni teknolojia mpya. Sambamba na hili, serikali inapaswa kuhakikisha kwamba kampuni zinapata ruzuku na uwekezaji ili kukuza masoko yao hasa masoko ya nje kupitia maonyesho ya biashara ya kimataifa na programu za uuzaji nje (export promotion programs).Kwa kuzingatia mauzo ya nje, kutakuwa na mtiririko wa mtaji wa kigeni, ambao utasaidia kuziba pengo la uhaba wa akiba za ndani. Kwa mfano, Korea Kusini ilikuwa kupitia sera za Seoul zilizolenga kuuza nje.

View attachment 3009644
Chanzo: Remix AI
Mwisho serikali ingejitahidi sana kukuza sekta ya Sanaa hasa katika upande wa Sanaa ya kuigiza. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la umaarufu wa tamthilia za Korea Kusini nchini Tanzania. Tamthilia za ndani zimeonekana kukosa ubora hasa katika Teknolojia na maudhui huku nyingi zikiwa na hadithi za kufanana. Ili Tanzania iweze kukuza sanaa yake, Kwanza ni kuboresha ubora wa uzalishaji kama vile Korea Kusini. Pili Tanzania inatakiwa ijikite kwenye maudhui ya kipekee na utamaduni. Mfano Korea Kusini inaingiza utamaduni wake katika tamthilia zake, jambo linalovutia watazamaji wa kimataifa. Tanzania pia ingejikita kukuza ubora wa watayarishaji wetu kwa kushirikiana na Nchi zilizoendelea. Mfano hatua aliyofanya Rais Samia kuwakutanisha watayarishaji wetu na wa Korea Kusini tarehe 01/06/2024 ni mwanzo mzuri. Ila tunatamani isiishie hapo. Tungependa kuona hapo mbeleni hata kazi za pamoja ( Korea Kusini na Tanzania) zikitoka. Pia ni kujenga miundombinu ya filamu. Mfano nchini Korea Kusini kuna maeneo maalumu (filming locations) ambayo hutumiwa na wazalishaji wa filamu za ndani na nje. Sanaa inawez pia kutumika kukuza utalii wetu. Mwisho serikali ingetengeneza mifumo mizuri kwajili ya kusambaza filamu na tamthilia na kuimarisha ushirikiano na wadau wa kimataifa kama NETFLIX. Mauzo yatakayo tokana na Sanaa yanawez kuongeza pato la taifa.

View: https://youtu.be/WUIuLpqrVSo?si=2DDAwfqcipyxVobE

View: https://youtu.be/j17pTr9c-sk?si=fwMntYDMLUn_S1Z1

Angalizo:
Tanzania inaweza kufikia malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi kwa kujifunza kutoka kwa Korea Kusini, lakini kwa kutekeleza mikakati hiyo kwa njia inayoendana na misingi ya demokrasia, haki za binadamu, na utawala bora na sio Njia za kibabe kama alizotumia Raisi Park Chung-hee. Pia ni muhimu kujua kuwa maendeleo yanaleta faida kubwa lakini yanakuja na changamoto mfano; madeni, uharibifu wa mazingira kama vile ukataji miti na uchafuzi (pollution).Hivyo basi, ni muhimu kwa Tanzania kuzingatia utawala bora wakati wa hatua za maendeleo ili kupunguza hatari hizi.
Tanzania tuitakayo si Ile yenye hadhi ya Nchi duni,Bali Nchi iliyoendelea. Kwa pamoja tunaweza kufika huko💪

View attachment 3009665
Tanzania Tuitakayo 2050.​

Daaah! Tukiwa na madhari kama hii Tz itapendeza haswa! Uoto + mji wa kisasa! Ubunifu mzuri saana
 
Hatuwezi fikia Korea bila kwanza kupanda roho ya uaminifu,bidii na nidhamu ya kazi, kuondoa ubinafsi hizi sifa mtu mweusi hana.Zinasababishwa na uwezo mdogo wa kufikiri.
 
Tuna nguvu kazi tele iddle tumeshindwa tu hata kuiexport nje nchi zenye kuhitaji wafanyakazi ili tupate pesa za kigeni vizingiti na vikwazo kibao vimewekwa kuwazuia vijana wasitoke nje ya nchi wakalete pesa nje
 
Mbunifu haihitaji kushikwa mkono na serikali kama amebuni technology inayotatua changamoto kwa jamii jamii husika kupitia marketing ya huo ubunifu wake ni rahisi kujisaidia mwenyewe akatimiza ndoto zake kwa kuzidi kuongeza wigo wa soko la ubunifu wake.
 
Hata mimi huwa sijui namna ya ku vote, naombwa kura ili sijui namna ya ku submit vote
Ooh ahsante sana kwa kuonyesha Nia ya kutaka kunipigia kura🙏 Ubarikiwe sana 🙏.. kunipigia kura ni rahis Sana unaenda hapo kwenye chapisho langu hapo linapoishia utaona sehem imeandikwa 231 votes unabofya hapo mpak panakuwa pekundu kura itaongezeka utakuwa umeshanipigia kura tayar 🙏.. ndo hivyo
 
Hapa kuna orodha ya vitabu ambavyo nilivisoma wakat naandaa hili chapisho.
  1. "Park Chung-hee: From Poverty to Power"by Hyung-A Kim
    • Hiki ni wasifu wa Park Chung-hee kinachoeleza jinsi alivyoiongoza Korea Kusini kutoka kwenye umasikini hadi kuwa taifa lenye nguvu kiuchumi.
  2. "The Park Chung Hee Era: The Transformation of South Korea"kilichohaririwa na Byung-Kook Kim na Ezra F. Vogel
    • Mkusanyiko wa insha zinazojadili mabadiliko ya kijamii na kiuchumi yaliyotokea wakati wa utawala wa Park Chung-hee.
  3. "South Korea's Rise: Economic Development, Power and Foreign Relations"by Uk Heo na Terence Roehrig
    • Kitabu hiki kinaeleza kuhusu ukuaji wa kiuchumi wa Korea Kusini, nguvu za kijeshi, na uhusiano wa kigeni, ikiwa ni pamoja na jukumu la Park Chung-hee katika mchakato huo.
  4. "Korea: The Impossible Country"by Daniel Tudor
    • Hiki kitabu kinaangazia jinsi Korea Kusini ilivyoinuka kutoka kwenye umaskini hadi kuwa taifa lenye maendeleo, na kinamzungumzia kwa kina Park Chung-hee na sera zake.
hello can you sen me those books
alphajozee27@gmail.com or whtasap 0746414742
 
Back
Top Bottom