DOKEZO Responded Mpango wa Serikali kuendeleza upya maeneo ya Sinza unahitaji uwazi na uwajibikaji

DOKEZO Responded Mpango wa Serikali kuendeleza upya maeneo ya Sinza unahitaji uwazi na uwajibikaji

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Natoa wito kwa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuuangalia kwa karibu mpango wa uendelezaji upya wa eneo la Sinza, Dar es Salaam, unaoratibiwa na Manispaa ya Ubungo, kutokana na kuwepo kwa viashiria vya shinikizo na ukosefu wa uwazi.

Kwa muda sasa, wananchi wa Sinza tumekuwa tukisikia tetesi kuwa Serikali inapanga kuendeleza upya maeneo yetu kupitia mpango wa ubia kati ya wananchi na wawekezaji. Hata hivyo, mchakato huu umeibua hofu na maswali mengi kutokana na namna unavyotekelezwa.

Kufuatia kuenea kwa taarifa hizo, wananchi tuliitishwa kwenye mikutano ambao umefanyika Jumapili April 19, 2026 ukiongozwa na watendaji kutoka Manispaa ya Ubungo. Katika mikutano hiyo, ilielezwa kuwa lengo la mpango huu ni kuboresha mandhari ya Sinza kwa kujenga majengo ya ghorofa, kuimarisha miundombinu ya barabara na maji taka, pamoja na kupanga makazi kwa utaratibu bora zaidi.

Ni kweli kuwa Sinza imekuwa kwa kasi na inakabiliwa na changamoto za miundombinu duni. Hata hivyo, changamoto hizo haziwezi kuwa sababu ya kuendesha mchakato unaotia shaka, hasa pale ambapo wananchi wanahisi kushinikizwa kufanya maamuzi makubwa kuhusu mali zao.
Ubungo barua.jpg
Mfano, wametueleza kuwa uliofanyika ni mkutano wa pili baina ya mamlaka na wananchi lakini jambo la kushangaza wananchi wengi wamesema hawajawahi kushiriki mkutano wa kwanza ambao ulijadili na kupokea maoni yao, baada ya sintofahamu hiyo ilibidi watendaji wakubali kwamba ni mkutano wa kwanza. Jambo hilo limeonesha uwepo wa changamoto ya ushirikishwaji unaozingatia misingi ya utawala bora.

Jambo hili limepelekea baadhi wananchi ambao wameshiriki mkutano kukataa kusaini kutokana na kuhisi uwepo wa hila au taarifa zao kutumiwa vibaya.

Aidha, kuna taarifa zilizopo mtaani juu ya kuwepo kwa shinikizo la chini kwa chini kwa baadhi ya wamiliki wa viwanja, kuwa wasipoviuza au kuingia ubia, mali zao zinaweza kuchukuliwa. Hali hii inatajwa kuwa tayari imesababisha baadhi ya wananchi kuuza maeneo yao kwa bei ya chini isiyoendana na thamani halisi ya soko.

Pia soma ~ Sinza kujengwa upya. Wamiliki waibua maswali

Ingawa mamlaka zinaeleza kuwa mchakato huu ni shirikishi, uhalisia unaonekana kuwa tofauti. Kuna dalili kwamba tayari wawekezaji wamepatikana na kinachoendelea sasa ni kutafuta namna ya kurasimisha uwepo wao kupitia makubaliano yanayowahusisha wananchi.

Vilevile, kauli kwamba taasisi kama Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) na Manispaa ya Ubungo ndizo zitakazosimamia upatikanaji wa wawekezaji na utekelezaji wa mpango huu, zinapaswa kuambatana na uwazi wa hali ya juu ili kuondoa shaka iliyopo kwa wananchi.

Ni muhimu pia kutambua kuwa mchakato huu unaendelea wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la ununuzi wa ardhi katika maeneo ya kimkakati kama Mwenge na Sinza na watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha. Hali hii inazidisha hofu kwamba huenda kuna maslahi binafsi yanayosukuma mchakato huu.

Kwa msingi huo, wito wangu ni kuwa TAKUKURU inapaswa kuchunguza kwa kina iwapo kuna viashiria vya rushwa au matumizi mabaya ya madaraka katika upangaji na utekelezaji wa mpango huu.

Vilevile, mamlaka husika zinapaswa kuhakikisha kuwa maslahi ya wananchi yanatangulizwa mbele ya maslahi binafsi; mchakato unakuwa wa uwazi na unaoshirikisha wananchi kikamilifu, Sheria, taratibu, na haki za wamiliki wa ardhi zinazingatiwa kikamilifu.

Maendeleo ya miji ni muhimu, lakini lazima yaende sambamba na haki, uwazi, na ridhaa ya wananchi. Bila hivyo, hata mipango mizuri inaweza kupoteza uhalali wake mbele ya jamii.

Jambo lingine ni kuwa nyaraka nyingi zinazoletwa kwa Wananchi kueleza mkakati huo zimeandikwa kwa Kingereza jambo ambalo ni changamoto kwa baadhi ya watu.

Ufafanuzi wa Serikali ~ Serikali: Mpango wa uendelezaji upya wa eneo la Sinza haulengi kuwaondoa wananchi, unalenga kuboresha matumizi ya ardhi
 
Sema serikali huwa inapenda kununua migogoro na magomvi bila sababu:
Wao watengeneze miundo mbinu, wasimamie sheria na miongozo ya mipangomiji kwa ufasaha, watengeneze open spaces, wahakikishe ulinzi na usalama wa kutosha, n.k.Naturally watu watajijenga wenyewe, watakaouza watauza kwa utashi wao, n.k
 
Waende pia kinondoni shamba,msisiri huko,mwananyamala kisiwani kote watu wahamishwe ile misquatter
Haifai

Ova
 
Hebu fikiria, KATA NZIMA WANAITAKA. JAMANI !
HAKUNA DIWANI WALA MBUNGE ALIEKUJA KUONANA NA WANANCHI.
 
Kwanini
Sema serikali huwa inapenda kununua migogoro na magomvi bila sababu:
Wao watengeneze miundo mbinu, wasimamie sheria na miongozo ya mipangomiji kwa ufasaha, watengeneze open spaces, wahakikishe ulinzi na usalama wa kutosha, n.k.Naturally watu watajijenga wenyewe, watakaouza watauza kwa utashi wao, n.k
Kwanini wasifanye huo mradi maeneo ya Uswahilini huko kama Mazense, Magomeni, Mburahati na Kigogo.
 
Back
Top Bottom