Mpango wowote wa TRA kukamata wasiodai risiti hautofanikiwa hadi pale Wamachinga watakapoondolewa

Nahsindwaga kuelewa kwa nini serikali inakujaga na mikakati mufilisi kiasi hiki, dawa ya mkwepa kodi haswa kwa wafanya biashara kwanzA ni kujua kwa nini wanakwepa kodi!?

Jibu ni simple tu, wanakwepa kodi kwa kuwa ni kubwa plus hawaoni mantiki ya hizo kodi wanazotoa Kwan bado hakujawa na namna ambavyo wanaweza kuhakikisha kodi zao zinafanya kazi stahiki.

Nadhani. Kodi ishushwe mpaka asilimia 10% , iendeshwe kampeni ya kulipa kodi ,watu wahamasishwe kulipa kodi kww namna iwezekanavyo.plus kuonekane namna Gani hiyo kodi inasaidia jamii husika kwanzA..na sio hizi za asilimia 70 kulipana mishahara na 30 ndio miradi ya maendeleo.
 
Magufuli aliapa kuwafanya matajiri waishi kama Mashetani, nina uhakika wa asilimia zote kwamba hawezi kufanikiwa. Na watakao ishi kama mashetani ni hawa hawa raia maskini wanaopenda kuitwa wanyonge.
 
Hapa kuna haja kwa Serikali kuangalia upya suala la vitambulisho vya machinga interms mtaji/aina ya biashara.
Lakini pia TRA wanaweza kubuni app ya risiti ili kila machinga mwenye biashara atoe risiti ya kielectronic.
Waache kupepesa macho
Wamwambie magufuli laivu kuwa matamko yake yanaharibu mifumo ya kukuza uchumi wa nchi, period

Huwezi kuruhusu watu wafanye biashara kiholelea kwa malipo ya tsh 20000 kwa mwaka wakati huo huo unategemea kukusanya kodi kubwa isiyo na uhalisia.
 
Wakina humphrey polepole wanajitamba mitaani kutumia kodi za wananchi kujinunulia mavi8
 
Rais wetu alikuwa na nia nzuri sana na wafanyabiashara wadogo na moja ya lengo lake kuu ni wakue kibiashara shida kubwa ni kwamba wafanya biashara wakubwa wamekuwa wajanja sana wanaingiza mzigo kwa makontena halafu hawaingizi dukani hapana bali huwapa machinga moja kwa moja hapa lipo jambo ambalo serekali inatakiwa kufanya
 
Kweli tupu mkuu
 
Tatizo hujawahi kufanya biashara mkuu, machinga halipi kodi ya pango, VAT, Halmshauri, sijui fire, umeme, maji, ulinzi n.k, lakini anatakiwa kuuza sawa bei sawa na mfanyabiashara, is that fair?
 
Kodi yao wanaicgukuliaga bandarini
 
Watu wakipigwa faini wataacha kununua vitu barabarani na badala yake kuingia madukani na kununua humo. Huu msako ukifanywa kwa weledi utawaondoa Wamachinga wote wanauza vitu vya madukani barabarani na hivyo kuongeza pata la Taifa.
 
Tatizo hujawahi kufanya biashara mkuu, machinga halipi kodi ya pango, VAT, Halmshauri, sijui fire, umeme, maji, ulinzi n.k, lakini anatakiwa kuuza sawa bei sawa na mfanyabiashara, is that fair?
🈶🈶🈶🚳🚳🚳
 
Pale Akiba karibu na CBE Dar es salaam Machinga wanauza mpaka Pombe( bia na Konyagi,KVANT n.k) Bila Risiti yoyote na hii ipo kwa sasa nchi nzima.
Duh, Wapiga Kura hawa kwa kujiongeza?.
 
Ni vyema sasa kukawa na mwongozo wa nini machinga auze. Vitu kama vyakula, matunda na mbogamboa wapewe ruhusa kuuza, pia bidhaa za ufundi wa mikono kama nguo za kushona wenyewe, ususi, mama ntilie waachiwe machinga.

Mitumba (itozwe kodi), pasi, dawa na bidhaa zilizotoka viwandani ziuzwe madukani pekee na ndio tudaiane risiti. Haiyumkiniki bidhaa ya dukani auze machinga hii si sawa kwani ndio inatumika kama mianya ya kukwepa kodi. Sio fair pia kwa wafanyabiashara waaminifu wanaolipa kodi kushindana kuuza bidhaa na wamachinga
 
Tatizo hujawahi kufanya biashara mkuu, machinga halipi kodi ya pango, VAT, Halmshauri, sijui fire, umeme, maji, ulinzi n.k, lakini anatakiwa kuuza sawa bei sawa na mfanyabiashara, is that fair?
Hata maofisa wengi wa TRA , Waziri wa fedha , Rais na wanaccm wenzake wa juu hawajawahi kufanya biashara yoyote , wachache wamewahi kupata tenda za bwelele zile wanazoingiziana hela kwenye akaunti zao , lakini kama kweli hawa wangewahi hata kuuza Mapera ya kuzunguka mitaani wangetuheshimu sana sisi wafanyabiashara
 
Kama kweli wapo seriously hakuna haja ya kukamata wanunuzi, wakamate wamachinga bidhaa walizonazo Zina receipt? Mbona zinatoka madukani bila receipt na zinasambazwa mabarabarani tunanunua.
 
Issue ya kodi ni kitu kidogo tu.. Serikali yetu sijui ina fail wapi

Weka kodi ndogo ambayo hata mtu wa kawaida au machinga akiaangalia anajua anaweza kulipa kodi na faida anapata..

Toa mashine za lisit bure kbsa... Kutoa machine bure kina wapa watu nguvu ya kwenda kuchukua machine.. Ambapo hata machinga tu anaweza kwenda kuchukua..

Punguza mlolongo wa upatikanaji wa machine.. Machine ziweze kutolewa hata na afsa mtendaji..
 
Wapiga kura wa Rais hawatakiwi kulipa kodi ya biashara, ukitaka nawe hamia huko.
Kama ambavyo Naye halipi kodi,like father like son.Walipa kodi nchi hii hawaongezeki Bali kodi ndiyo hu9ngezeka kila uchao.
Kwa nini TRA haifanyi ubunifu?Kwa kuwa Watanzania wengi wanapenda Betting, waweke Bahati nasibu kupitia EFD receipts za kupata Prizes toka TRA kwa maana ya wauzaji/wanunuzi?Lazima morali ya kudai receipts itaongezeka na Machinga watakufa kifo cha mende kwa sababu watu wataenda kununua kwa wauzaji kwenye kutoa EFD receipts.Suala ni kufanya kila kitu kwa mazoea.
 
Machine za EFD ziwe za TRA na anayemilikishwa awajibike asipoitumia/kuipoteza.Kuwe na bonus ya ukusanyaji wa kodi kwa wanaofanya vizuri.
It's a matter of creativity.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…