Mpango wowote wa TRA kukamata wasiodai risiti hautofanikiwa hadi pale Wamachinga watakapoondolewa

Watu wakipigwa faini wataacha kununua vitu barabarani na badala yake kuingia madukani na kununua humo. Huu msako ukifanywa kwa weledi utawaondoa Wamachinga wote wanauza vitu vya madukani barabarani na hivyo kuongeza pata la Taifa.
Ni sawa lakini pawepo na specific name ya nani ni machinga na nani ni mfanyabiashara.
Kwa kuwa naweza kuwa machinga lakini nina stoo kubwa ya kutunzia bidhaa.
Urashimishaji wa biashara zinazofanywa na machinga ni jambo muhimu ili kuweka usawa/mzani ya ulipaji kodi kwa ufasaha.
 
Watu wengi wataumia. Na biashara zitakufa.
 
MATCHING GUY - mtu anayetembeza vitu mitaani na siyo anayepanga vitu barabarani
 
Kwasisi wakazi wa barabara zote wamejenga vibanda wamachinga mbele ya maduka na walikatazwa wasibuguziwe wapange bidhaa hata mlangoni kwa ofisi ya mkuu wa wilaya kisa wana kale kakaratasi ka 20,000 na watu wengi wananunua bidhaa kwao.. lakini hizi bidhaa zinatoka madukani wanapewa chinga anauza naye kwa bei itakayomlipa aliyoambiwabna tajiri anarejesha... walipotoa vitambulisho vya machinga hapo ndio biashara iliishia hapo
 
Ni mtego wa fursa, hawa watakamatwa kwa wingi na kukubaliana kulipa faini hivyo serikali itaingiza mabilioni kufidia tulizoziponda wakati wa uchaguzi.
Shida ya hizi sheria utumika Kama fursa za kujipatia kipato kwa baadhi ya walinda sheria.Imehisiwa pia kuna michezo ufanyika ya kuwakamua wafanyabiashara wanatumwa watu wakanunue vitu kisha ugoma kuchukua risiti then uenda uza cd kwa maafisa kwamba wameuziwa bila risiti then mfanyabiashara ukamatwa uyamaliza kwa nusu ya pesa ya faini.
 
Watu wakipigwa faini wataacha kununua vitu barabarani na badala yake kuingia madukani na kununua humo. Huu msako ukifanywa kwa weledi utawaondoa Wamachinga wote wanauza vitu vya madukani barabarani na hivyo kuongeza pata la Taifa.

Madhara ya huu ushauri wako unayajua? Jiandae kupigwa ngeta kwa vijana kukosa kipato.
 
Nafikiri watakachofanya ni kukaa karibu na maduka au wauzaji wa bidhaa (say petrol station), kwa hivyo anayekukamata anakuwa na uhakika kabisa sehemu uliponunua bidhaa...
 
Wewe una akili kama mimi.
Excellent marverlous.
 
Watu wakipigwa faini wataacha kununua vitu barabarani na badala yake kuingia madukani na kununua humo. Huu msako ukifanywa kwa weledi utawaondoa Wamachinga wote wanauza vitu vya madukani barabarani na hivyo kuongeza pata la Taifa.
Wakishaondolewa barabarani unadhani nini kitatokea kama si uhalifu na ujambazi
 
Tunakoenda tutakuwa tunaagiza bidhaa zinatukuta majumbani!
Na biashara hii ndiyo inayokuja juu kwa sasa agiza tunakuletea mpaka mlangoni japo hapa tunawashtua wakuda huenda wakuda nao wakaanza kuagiza bidhaa ili ukimfikishia tu akudai risiti au umwonyeshe godown lipo wapi
 
Nimewaza sana hilo la kutoka Petrol Station. Ndipo watakapopigia sana.
 
Kuna siku nilikuwa naenda Sumbawanga from Mbeya. Sasa kufika Tunduma nikaona abiria wengi tuu wananunua sukari from Zambia ambazo wamachinga wanauza openly hapo Tunduma. Tulipofika huko mbele wakaingia TRA na kutaka eti kukamata abiria walionunua sukari, which was 2 to 3 kgs kwa walio wengi. Bwana wee watu wakachachamaa kwamba how come hawaendi kuwakamata wauzaji pale Tunduma? Wengine wakasema wamenunua Mbeya kwenye maduka, yaani ilikuwa balaa, mwishowe ilibidi waondoke tuu.
 
Hiyo kuwafokea na kuchimba biti wanawaiga mabosi wao mawaziri...
 
Mwanzo 47
18]Na mwaka ule ulipokwisha wakamjia mwaka wa pili, wakamwambia, Hatumfichi bwana wetu ya kwamba fedha zetu zimekwisha, na makundi ya wanyama ni mali ya bwana wetu, hakikusalia kitu mbele ya bwana wetu, ila miili yetu na nchi zetu.
[19]Kwa nini tufe mbele ya macho yako, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu kwa chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumwa wa Farao; kisha utupe mbegu, tuishi wala tusife, wala nchi yetu isipotee.
[20]Basi Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri; maana Wamisri waliuza kila mtu shamba lake; kwa sababu njaa ilikuwa imewazidi sana, nchi ikawa mali yake Farao
 
Na biashara hii ndiyo inayokuja juu kwa sasa agiza tunakuletea mpaka mlangoni japo hapa tunawashtua wakuda huenda wakuda nao wakaanza kuagiza bidhaa ili ukimfikishia tu akudai risiti au umwonyeshe godown lipo wapi
Unaagiza kwa mtu mnayefahamiana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…