sanalii
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,639
- 5,767
Ni suala nililolisikia muda ila nimethibitisha baada ya mpapai kurefuka tu bila kuzaa nikaufunga gunzi ukazaa mapapai mawili, kutokana na mvua gunzi lilianguka, ukaacha kuzaa, ukafungwa gunzi tena sasa hivi una mapapai mengi tu.
Je, hili suala laweza thibitika kisayansi?
Je, hili suala laweza thibitika kisayansi?
Wakuu hiyo imesibitishwa kisayansi.. Ipo hivi kuna mipapai dume (male plant) hii haizai matunda, na kuna mipapai jike (female plant) na yenye jinsia zote mbili (hermaphrodite) hii ndio inayozaa matunda isipokua dume tu! Sasa kuna mimea inaweza kubadili jinsia yake (sex labile plant) moja wapo ni mipapai na inabadilika pale mazingira yatakapokua magumu kwa yenyewe kuishi sasa ili uendeleze kizazi chake ni lazima ubadilike kutoka dume kuwa jike ile uweze kuacha kizazi chake
Kufunga bunzi/gunzi ni watu wameaminishwa tu ila unaweza kufunga chochote kile ata ukipigilia misumari ilimradi mmea upate shuruba (stress) hapo mmea utahisi kuwa upo kwenye mazingira magumu na unaweza kufa muda wowote . Hapo mmea utachukua hatua ya kubadili jinsia na kuzaa matunda haraka sana kabra haujafa ili uache kizazi chake.. [emoji3][emoji3][emoji3] kama binadamu tu akinusurika na ajari utasikia sina hata mtoto.
Siku moja tu ya uumbaji ila mimea ina physiology nyingi na zakustaajabisha![emoji1544]
Sent from my iPhone using JamiiForums