Mpasuko mkubwa CHADEMA Mbeya mjini, Msigwa avunja uongozi huku walioondolewa wakimpinga. Ni mparaganyiko mkuu

Mpasuko mkubwa CHADEMA Mbeya mjini, Msigwa avunja uongozi huku walioondolewa wakimpinga. Ni mparaganyiko mkuu

Mpasuko mkubwa umeukumba uongozi wa Chadema Mbeya mjini na hii ni dalili kuwa hawako kwenye good terms. Sijui lini watafika mbali

View attachment 2102008
Kama Ccm imewafukuza kina Bashiru, Polepole nk tena uongozi wa kitaifa. Na maisha yanaenda, itakuwa hawa wa Cdm, tena wa ngazi ya mkoa ?!

Fikiria tena propaganda nyingine. Siyo hiyo ya mbeya
 
Puuzeni uzushi huu, hauna kweli ndani yake, chama hakina mpasuko
hahaaaa ipendacho roho hula nyma mbichi yaani mpasuko uko wazi hivyo mpaka anafukuzana wewe unasema hakuna mpasuko? kweliiii CHADEMA kila siku mkiambiwa hamna sera za kushika dola mnakataa una mmeanza kufukuzana hovyo
 
Kilichokuwa Chama kikuu cha Upinzani Tanzani, CHADEMA kimeendelea kuwa na wakati mgumu baada ya viongozi katika kanda muhimu za Kaskazini na pamoja le ya Nyanda za Nyasa (nyanda za juu kusini) kutofautiana vikali na kushambualiana hadharani.

Huko Arusha mjini kumewaka vibaya, lakini huko Nyasa viongozi wa Jimbo La Mbyea Mjini na viongozi wa Mkoa wa Rukwa, wameamua kuvunja ukimya na kufichua matendo maovu ya mwenyekiti wa Kanda yao Mchungaji Peter Msigwa.

Msigwa na baadhi ya viongozi wenzake wa Kanda, wanalalamikiwa kwa kuwa Wababe, na kushughulikia mtu yeyote anayeonekana kuwa kinyuma na mipango yao ya kukusanya michango mara kwa mara.Viongozi wa CHADEMA katika mikoa na majimbo wanaeleza kwamba MSIGWA anatuvuja pesa, na kuwa mbabe kila anaposhtukiwa.

SAUTI KUTOKA KWA KIONGOZI WA CHADEMA MKOA WA RUKWA INAELEZA ZAIDI PICHA YA MPASUKO HUO (sikiliza video hizo mbili nilizokuwekea)

 
Erythrocyte kubali kataa, hii ni effect ya baba mwenye nyumba kuwa mahabusu kwa muda Mrefu. Nyumba inakosa uongozi na kila mtoto anakuwa ni decision taker. Hapa kuna tatizo maana baba msaidizi naye anag’ang’ania ubeleji! Asingekuwa mbinafsi asharudi nchini kujaza vacuum iliyoachwa na baba. Nyie mnafurahia kwenda Mahakamani na kula mandazi! Ona sasa
Acha uongo
 
Hujui kitu wewe kapuku , Tulia .
hahaaaaa yaani bado unaamini hakuna mgogoro huko? yaani chadema wote tabia zenu ziko sawa mbowe anawachangisha hela anakula mnashabikia msigwa anawachangisha anakula wamemshitukia anakuwa mkali anafukuza wat hovyo halafu mnataka kuchukuwa nchi mnaweza kuiongoza kama mnashindwa kujiongoza ndani ya chama?
 
Niko mahakamani , lakini hakuna Tatizo kubwa Mbeya Mjini
msigwa kala hela huko kama vile anavyokulaga mbowe lakini msigwa wamemshtukia wamekuja juu anaanza kuwafukuza uanachama hukooooooo
 
Back
Top Bottom