Mpasuko mkubwa kwenye Baraza la Mawaziri kisa kuuzwa kwa Bandari

Mpasuko mkubwa kwenye Baraza la Mawaziri kisa kuuzwa kwa Bandari

Kuna viashiria si shwari tena Baraza la Mawaziri;

1) Waziri Mkuu kumwakilisha Rais nchini Urusi taifa tajiri kuliko yote duniani kwa maliasili ni dhahiri Makamu wa Rais ananyanyapaliwa. Wakati wa Magufuli Makamu wa Rais ndiye aliyekuwa ana mwakilisha Rais nje ya nchi na wala siyo Waziri Mkuu.

2) Makamu wa Rais na wengi wa Mawaziri Watanganyika wamejizuia kuutetea wizi wa maliasili za nchi yao na kuonyesha kuna mifarakano na sintofahamu ndani ya Baraza la Mawaziri.

3) Agizo la Rais la kumwelekeza Waziri wa uchukuzi aingie mkataba wa kimataifa haukuonyesha ulitokana na vikao vya baraza la mawaziri. Hii ni ushahidi tosha uamuzi wa kuuza nchi haukuwa wa baraza la mawaziri.

4) Hakuna jitihada zozote zile zilizofanywa na serikali kuambatanisha muhtasari wa Baraza la Mawaziri kulithibitishia bunge uamuzi wa kuuza bandari zetu ulitokana na maamuzi ya vikao vya Baraza la Mawaziri kabla ya Rais kumwagiza Waziri wa Uchukuzi kusaini mkataba wa kuuza nchi yetu pendwa.

Tungependa kukumbusha tu hakuna uwajibikaji wa pamoja kwenye maamuzi yasiyo shirikishi.

5) Kwa vile mkataba wa kuuza nchi ulifanywa bila ya kuzingatia mpango wa miaka 5 ya uendelezaji wa bandari zetu hii ni ushahidi tosha msukumo wa kuuza bandari zetu haukutoka kwa Mamlaka ya bandari zetu. Na ndiyo maana Mtendaji Mkuu wa bandari zetu alitupiwa virago vyake kwa sababu alipinga huu wizi wa mali ya umma.

6) Kuna viashiria uamuzi wa kuuza bandari zetu ulikuwa wa kukurupuka kwa sababu ulifanyika baada ya kupokea mkopo wa benki ya dunia wa dola 420 milioni na hata hizo hela hatujajua kama zingetatua matatizo yetu ya ufanisi, uthibiti wa mapato nk, wao wakaamua kumtajirisha mwekezaji.

7) Wanaoupigia upatu huu wizi wa mali ya umma hawamo kwenye Baraza la Mawaziri ila wanaona huu ni mwanya wa kujenga hoja ya kufikiriwa kujaza nafasi ya mawaziri waliopo ambao wanaonekana hawaafiki nchi yao kuuzwa.

8) Ukimwondoa Waziri wa uchukuzi hakuna Mzanzibara hata mmoja ambaye aliandamana na genge la makada wa CCM ambao walikuwa wanapigia upatu wizi wa mali ya umma. Ni dhahiri hata Wazanzibara hawaafiki na hili.

9) Pamoja na Kikwete kujitokeza hadharani na kudai anamuunga mkono Rais lakini hajawahi kuuteteta huu wizi wa mali ya umma.

10) Makamu wa Rais hajawahi hata mara moja kutetea nchi kuuzwa na hii inaashiria mpasuko mkubwa ndani ya Baraza la Mawaziri na tunabashiri wakati wa Uchaguzi wa 2025 jina lake litakatwa na hatarudi kwenye nafasi yake ya Umakamu wa Urais. Tutafafanua zaidi kwenye hili.
Kumbe na wewe ni “askofu”?
 
Hakuna wajinga Tanzania kama wanaopinga bandari kukodishwa hivi kusanya 1000 kwa zaidi yanusu karne nakukusanya m10 kwa mwaka mmoja kipi bora tukumbuke serekali inashindwa kutekeleza mambo kwakuwa na bajeti isiyokamilika kilamwaka lakiñi tukikodisha bandari bajeti inajaa mpaka inamwagika shida ninitena nyie mazuzu
 
MFALME WA WAGAGAGIGIKO ALIVYO TEMBEA UCHI

Hii hapa[emoji1370]
Hapo zamani za kale katika nchi ya Wagagagigikoko alikuwepo jamaa mmoja MASKINI lakini mwelevu sana aitwaye ABDUL. Siku moja aliketi chini na kutafakari kwa kina jinsi ya kuondokana na lindi la Umasikini. Mara, WAZO Pevu likamjia. Akajisemea moyoni, "nitakwenda Msituni na kujenga Kibanda kidogo. Ndani yake nitaweka Kiti kimoja na Viatu Pea MOJA". Kwa vile MFALME pamoja na RAIA wa nchi ya Wagagagigikoko walikuwa wamebobea kwa unafiki,uwongo, kupenda kusifiwa na kujipendekeza kwa MFALME, Abdul akajisemea mwenyewe, "nitatumia udhaifu wao kupata fedha. Baada ya kumaliza ujenzi wa kibanda akaenda mjini na kuanza kusambaza uzushi ya kwamba alikwenda Polini, huko akakutana na MALAIKA aliyempa SIRI nyingi za MAISHA. Hata hivyo MALAIKA amesema kwamba MTU yeyote anayetaka kukutana na MALAIKA huyo sharti asiwe na DHAMBI. Kwamba MTU yeyote akiwa na DHAMBI hataweza kumwona MALAIKA, Bali ataona kiti na viatu tu. Watu wa Mji ule wakafurika kwenda kwenye msitu ule ili waweze kupata MAFUNUO ya MALAIKA. Kila alieingia KIBANDANI hakumwona MALAIKA Bali ni kiti kimoja Pamoja na viatu chini ya kiti kile... Hata hivyo kwa sababu ya HOFU ya kuonekana MDHAMBI, kila MTU alipotoka mlangoni Aliwamulia walio Nje UZURI wa MALAIKA na MAFUNUO aliyopewa...HABARI za MUUJIZA huo FEKI ukawafikia MAWAZIRI hatimaye hata MFALME wa nchi ile ya Wagagagigikoko. Mawaziri wake wakamweleza juu ya Muujiza wa MALAIKA na Sharti la kumwona kwamba LAZIMA awe MTAKATIFU.Kwa madaha na MBWEMBWE Mfalme akapanda gari LA kukokotwa na FARASI na kufika hadi kwenye BANDA lile.Akavua viatu na kuingia ndani. Akachungulia kila kona bila kuona alama ya MALAIKA. Kutokana na AIBU ya kuonekana ni MDHAMBI mfalme akajitojeza nje na kuwatangazia RAIA wake UZURI wa MALAIKA yule FEKI na jinsi alivyopewa SIRI kubwa. Wakati Mfalme akiongea kwa Tambo kila aliyeingia mle kibandani akawa anajisemea moyoni nadhani Mimi peke yangu ni MDHAMBI maana sikumwona MALAIKA. Baada ya Ujanja wa kwanza kufanikiwa ABDUL alimuendea mfalme wa Wagagagigikoko na UWONGO wa kupigia PESA.. Akamwambia anaweza kumshonea suti ya thamani sana ambayo wenye dhambi watakuwa hawaioni na wasio na dhambi tu ndio watakuwa wanaiona. Na kitambaa cha SUTI hiyo ni ZAWADI toka kwa MALAIKA..Mfalme akampa kazi Abdul ya kutengeneza suti ya aina hiyo kwa ajili yake. Kwa siku kadhaa Abdul alijifungia katika chumba akawa bize anashona suti ya mfalme. Baada ya siku tatu, mfalme akamtuma msaidizi wake akaangalie kazi inavyoendelea, yule msaidizi akaingia chumba alichokuwa akishonea Abduli lakini hakuona kitu japo alimuona Abdul akifanya vitendo kama vile yuko bize anashona nguo. Msaidizi akamwambia Abdul, ‘Nimetumwa na mfalme niulizie umefikia wapi?” Abdul akamjibu, “Kwani wewe huioni jinsi suti ilivyoanza kupendeza, ila bado namalizia nguo nyingine nataka kuanzia nguo za ndani ziwe ni hizi za kitambaa ambacho hakionekani kwa wenye dhambi”. Hakika yule msaidizi alikuwa haoni kitu lakini ili aonekane hana dhambi akaanza kusifu jinsi nguo zilivyoshonwa kwa ufundi. Akatoka na kurudi kumueleza mfalme kuwa Abdul kamshonea nguo nzuri sana si za dunia hii kwa jinsi zilivyo nzuri. Mfalme alifurahi sana, kesho yake akamtuma msaidizi mwingine, nae kama yule wa jana akarudi kwa mfalme na ripoti nzuri sana ya maendeleo ya koti, pia akaleta taarifa nzuri kuwa kesho yake Abdul angemaliza kazi na angeleta nguo ili mfalme azivae. Kesho yake mapema Abdul akaingia katika kasri la mfalme akiwa kama kashika lundo la nguo, ambazo mwenyewe alisema wasio na dhambi tu ndio wataziona. Wasaidizi wa mfalme wote hawakuwa wanaona kitu lakini walianza kupiga makofi wakisifu jinsi nguo zilivyokuwa nzuri, hamna aliyekuwa anataka kuonekana ana dhambi. Hatimaye Abdul akamkabidhi mfalme nguo, na kupewa KITITA CHA PESA.. Mfalme naye hakuwa anaona kitu lakini ili asiambiwe ana dhambi akajidai eti nae anaziona akaanza kumsifu Abdul kwa umahiri wake wa kuchanganya rangi na hata ufundi mkubwa wa kushona. Abdul akamuomba mfalme azivae zile nguo, wakaingia faragha mfalme akavua nguo zake na akaanza kuvaa nguo asizoziona kwa msaada wa Abdul. Kwa vile alivua nguo zote na kuvalishwa mpya zisizoonekana, rohoni mwake alikuwa anajiona yuko uchi lakini akaona akitangaza haoni kitu wananchi wangemshangaa kuwa mfalme ana dhambi, hivyo akaendelea kusifia na kujiangalia kwenye kioo akisifu nguo zilivyompendeza. Kisha akalazimika kutoka nje ili wananchi waone nguo mpya za mfalme. Wote walikuwa wanamwona mfalme yuko uchi lakini wakawa wanaogopa kuonekana wana dhambi hivyo kila mtu akawa anashangilia na kusifu uzuri wa nguo za mfalme. Lakini ghafla mtoto moja mdogo kwa sauti kubwa akamuuliza baba yake, “Baba mbona mfalme yuko uchi?”. Minong’ono ikaanza mwishowe watu wakaanza kumuunga mkono mtoto, mfalme aibu ikamshika kwani alijua sasa watu wote wanamuona uchi, akatimka na kujificha kwenye kasri lake na hadithi yangu imeishia hapo.
 
Hakuna wajinga Tanzania kama wanaopinga bandari kukodishwa hivi kusanya 1000 kwa zaidi yanusu karne nakukusanya m10 kwa mwaka mmoja kipi bora tukumbuke serekali inashindwa kutekeleza mambo kwakuwa na bajeti isiyokamilika kilamwaka lakiñi tukikodisha bandari bajeti inajaa mpaka inamwagika shida ninitena nyie mazuzu
Kwa kuipanga upya TPA tunao uwezo wa kuzalisha mapato ya teillioni 600 kwa bandari zetu sasa huyo mwekezaji wa trilioni 22 baada ya miaka 10 si ni mporaji tu?

Kuhusu mapato ni sisi wenyewe tunajikwaza kwa kuamini tuna mjomba huko ughaibuni.

Huko ni maumivu tu angalia kesi zaidi ya 20 wanadai zaidi ya trilioni na hawajawekeza hata sumni.
 
Napata ukakasi kusikia tukijipanga miaka 60 + badotunasema tukijipanga ingekuwa vizuri tungeambiwa ukomo wakujipanga tumechoka nano hilo
 
Hakuna wajinga Tanzania kama wanaopinga bandari kukodishwa hivi kusanya 1000 kwa zaidi yanusu karne nakukusanya m10 kwa mwaka mmoja kipi bora tukumbuke serekali inashindwa kutekeleza mambo kwakuwa na bajeti isiyokamilika kilamwaka lakiñi tukikodisha bandari bajeti inajaa mpaka inamwagika shida ninitena nyie mazuzu
Umeuliza swali mahali ambako sipo, hawa ni waajiriwa tu wa mafisadi pale TPA, hawana shughuli yoyote wanayoifanya mahali pale.
 
Kuna viashiria si shwari tena Baraza la Mawaziri;
....9) Pamoja na Kikwete kujitokeza hadharani na kudai anamuunga mkono Rais lakini hajawahi kuuteteta huu wizi wa mali ya umma.....
Point ipo hapa.
Je umepanga kumtetea kijana wa Msoga dhidi ya mwangwi unaovuma dhidi yake?
 
Hao mbwa wakizanzibar wakae waendelee kunya wao ni wa muda tu, time will tell.
Hii haikubaliki na siyo sawa hata kidogo. Usiwatukane raia wengine, tena kwa ubaguzi wa wanapotoka (ethnicity), ni mbaya sana.
Tujenge hoja zenye mantiki na kuheshimiana.
 
Rubbish.

Mnashusha hadhi ya jukwaa la siasa, Samia ndio Mwenyekiti wa Ccm na Amiri Jeshi mkuu.

Kama una akili ndogo si lazima kuanzisha thread.
Hii ndio ile PhD lissu anaiitaga professorial rubbish
 
Back
Top Bottom