Eeenh...Heee, mkuu 'Mystery,' inaeleweka sana na kukubalika kuja hapa JF na 'Heading' kubwa kama hiyo uliyotumia hapo juu.
Nasema inaeleweka, kwa sababu wengi wetu ndiko matumaini yetu makuu yanakolenga; kwamba hatimae mtafaruku utatokea na ipatikane njia ya kulegeza kama sio kubomoa kabisa chanzo cha huzuni inayoikumba taifa letu.
Haya matumaini siyo ya kweli mkuu wangu.
Kwanza wewe mwenyewe fikiria hiyo "Katiba?", makaratasi ya chama ambacho anakimiliki mwenyewe, umnyime usingizi, kwa sababu zipi hasa!
Unategemea katiba ya chama, huku ukijisahaulisha "KATIBA KUU", ambayo kila mmoja wetu angepashwa kuiangalia kama msahafu wa nchi yetu..., tunaona inakanyagwa na hakuna wa kusema lolote?
Sasa unataka kuaminisha wakuu hapa JF, kwamba 'kikatiba' ka CCM, chama ambacho ni kama mali yake itamfanya asite kuitupilia mbali na kufanya atakavyo yeye?
Ni nani mwenye ubavu ndani ya chama kile, aliyebaki na kusimama kuitetea hiyo katiba takataka. Membe anasemea pembeni, na hana njia yoyote tena ya kumrudisha ndani wakati huu.
Hizi ni kelele zake za mwisho, na baada ya hapo hutamsikia tena.