UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,753
- 12,932
Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane.
Naongea na wewe ambaye kila siku ni kukopa kwa matatizo yako halafu kulipa mpaka yafanyike matanga! Mbwembwe kibao wakati wa kukopa lakini kulipa deni ni shuruti!
Mara ooh "niazime elfu 30 hapo niweke mafuta kwenye gari nitakurudishia ndugu yangu"
Mara ooh "Niazime elfu 10 hapo niweke luku nitakurudishia kesho kutwa"
Mara ooh " Niazime elfu 50 hapo nimpeleke shemeji yako anaumwa halafu ndani ya wiki nitakurudishia"
Mara ooh "Jana nimepiga deshi mkuu tafadhari niazime buku 5 hapo halafu jioni mimi nitakurudishia"
Mara ooh "Sista/bro niazime laki moja hapo Dogo karudishwa shule,nitakurudishia mwisho wa mwezi"
Kwanini ukope kama unajua kulipa mpaka usumbue?,tafadhali nakuomba MPE HELA YAKE hiyo ni halali yake na ulikopa mwenyewe,hivyo inakupasa ulipe.
Naongea na wewe ambaye kutwa kukopa Supu na chakula kwa huyo mama hapo jirani na kulipa mpaka usemwe, kwahiyo furaha yako ni kuona huyo mama anafirisika? Kwanini unakopa chakula cha watu na hulipi?,tafadhali hebu kuwa muungwana MPE HELA YAKE,hiyo ni halali yake.
Naongea na wewe ambaye kutwa kukopa vyakula kwenye maduka ya watu halafu kulipa inakuwa changamoto, kwanini ukope mchele,maharage na mafuta kama unajua kulipa ni matatizo? Yaani kujinunulisha vimahitaji vyako kwa muda kadhaa kwenye hilo duka ndo uanze sasa na kukopa? Unategemea huyo mwenye duka ataendesha duka lake kwa mikopo mpaka lini? Ukishaanza kudaiwa unabadili kabisa na njia ili usisumbuliwe, hebu acha dharau nakuomba MPE HELA YAKE,hiyo ni halali yake,kama unashindwa kulipa kwa wakati acha kukopa.
Naongea na wewe ambaye mnafanya biashara na mtu halafu unaishia kudhurumu, kwanini udhurumu kama ulijua biashara huiwezi? Yaani mtu akupe zaidi ya milioni mfanye biashara halafu unaingia mitini, kwanini udhurumu kama ulijua huiwezi biashara? Hiyo ni pesa yake aliitafuta kwa jasho lake, tafadhali kuwa mstaarabu MPE HELA YAKE.
Naongea na wewe ambaye kila uchwao unaenda kukopa magengeni mboga mboga na viungo lakini kulipa mpaka ushikiwe mtutu wa bunduki,kwanini ufirisi kigenge cha watu kisa ujuaji na jinga wako? Unataka huyo mwenye genge afunge ili aishi vipi? Kwanini unakosa ustaarabu? Hebu MPE HELA YAKE huo ndio mtaji wake,acha dharau!
Naongea na wewe ambaye ulikopa pesa ili ufanye harusi lakini kulipa imekuwa matanga,mjomba au baba yako mkubwa alikukopesha pesa pale ulipopungukiwa ili ufanyie harusi lakini kulipa hutaki,ukipigiwa unashindwa kupokea simu na unazima kabisa, wakati unashauriwa ufanye sherehe ya gharama ya wastani wewe ukanga'ng'ania ufahari ili upate heshima ukweni wakati huna kitu,LIPA HELA ZA WATU, acha dharau zako za kijinga, suti yenyewe ulikopa na hela za watu bado hujamaliza,kwanini ukope kama ulijua utashindwa kulipa? Hiyo shera aliyovaa mkeo mlikopa kwa kuaminiwa lakini kulipa imekuwa tatizo, nakuomba ULIPE HELA ZA WATU.
Naongea na wewe hapo ambaye kila siku unahama Grocery au Bar kwasababu ya mikopo, kwanini ukope kama unajua kulipa huwezi? Yaani watu hadi wanashindwa kununua vinywaji kwasababu hutaki kulipa!,ukishaambiwa ulipe wewe unamuona mwenye chake mbaya hadi unamletea fitina na unaamua kuhama kabisa,acha dharau hizi za kijinga, MPE HELA YAKE, hiyo ni halali yake, ukiwa unashindwa kunywa na kulipa acha kukopa maana utawaona watu wabaya kila siku kumbe ni wewe ndiye mwenye tatizo!.
Naongea na wewe ambaye kila kijora kipya hutaki kikupite, tena bora ungekuwa unanunua kwa cash ila kibaya ni unakopa na kulipa inakuwa shida! Kwani aliyekwambia kila kijora kipya mpaka uwe nacho nani? Huwezi kununua acha kukopa, MPE HELA YAKE mwenye vijora vyake, hiyo ni haki yake!
Naongea na wewe ambaye ushakopa bodaboda wa watu mpaka imekuwa taabu kuwalipa,ukishadaiwa unawaona bodaboda wahuni, hivi unataka wao waishije? Yaani unakopeshwa kwa ajili ya kuwapeleka wanao shule na kuwarejesha kama mlivyokubaliana,lakini kila inapofika mwisho wa mwezi bodaboda anapodai hela yake unaanza kumpiga chenga,acha huu uhuni,MPE HELA YAKE,hii ni halali yake,au unadhani pikipiki inatumia maji na damu yako? Acha dharau!
Unapokopa hela ya rafiki au ndugu yako hakikisha unalipa,acheni uhuni!,wakati unakuja kukopa mnakuwaga wapole kana kwamba mnaumwa,ila mkishapewa hata mkipigiwa simu hamshiki! Hivi mnamatatizo gani. LIPENI HELA ZA WATU!
NAJUA WAKOPAJI MNAUPITA HUU UZI KAMA MNAAGA MAITI VILE!
ACHENI UHUNI, LIPENI HELA ZA WATU.