Mpenzi kajilisha nyama ya kitimoto kinyume na Imani

Usimwambie,mezea maana atakuwa hana dhambi
 
Kausha tu nguruwe kwetu ni haramu hata akigusa nguo unabid ukikate hicho kipande cha nguo


Ukitaka uhasama mwambie
 
Acha mkuu usimwambie Ila siku nyingine chukua tahadhari
 
Hilo Tendo siyo kama kula ngurwe mkuu kwa iman zao duh👏
Unajua nini kuhusu Dini na imani ya kiislamu?
Unajua maana ya Haramu? Au unadhani kwamba uislamu ukisema haramu ni kwamba Inapishana?

Haramu kwenye uislamu vina uzito sawa hakuna haramu ndogo mkuu elewa hivyo.
 
Hebu ngoja kwanza, yaani unahifadhi wese la mdudu!!!

Halafu hilo wese limekarangiza wali, huo wali si utakuwa na ile shombo ya mdudu aisee
 
Kausha..✌️😂😂

Ila mkuu ukidate na mtu wa iman tofauti jitahidi vitu kama hivyo ukaloe huko huko mbali. Wengine wana mashetani hata vyombo tu ni havifai yeye kutumia.
huyu hana mashetani ndio maana hajapandisha na nyama inamfaa mtoto wa shekhe
 
Mkuu siku shauri useme chochote jambo usilo lijuwa ni kama usiku wa giza, usimwamshe alie lala maana utalala wewe. Kosa limesha tendeka ukimwambia sasahivi mtaishia kuleta ugomvi kati yenu ni heri libaki kimya kama lilivyo. Kosa jingine kama hilo ndio mmeona ni kosa tu ndoa mnayo au mna mega tunda kisirisiri kama vile mko sawa? Kama kweli uko na mko serious kuhusu kula kwake kitimoto mwende mkatubu dhambi ya kula tunda gizani na kwa siri kabla halija halalishwa ndio mwongeze na hilo na kiti moto.
 
Kimwingiacho mtu sio haramu bali kimtokacho ndio haramu.wee potezea usimwambie na kama utamwambia kama ana imani ya dini huyo utamkosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ipo wapi? Hiyo nyama ya Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…