Mpenzi wako alikwambia au alifanya nini ukasema kimoyomoyo huyu hawezi kuwa mke/mume wangu

Mpenzi wako alikwambia au alifanya nini ukasema kimoyomoyo huyu hawezi kuwa mke/mume wangu

1.Jion moja nilikuwa natembea na huyu dem tunaelekea gheto tukiwa tumekaribia kama mita 50 tu hv namuona anaingia kwenye vichaka anachuchumaa na kukojoa i was so dissapointed sikutegemea sista du kama yeye akojoe vichakan kirahisi rahis tu mahali pasipo na maji na hata tishu haikuwepo
2. Mwingine alikuja mji ninaoishi alikuwa na ishu zake binafsi so nikawa naishi nae kwa muda ule alokuwa mji ule , tatizo likawa kila muda anazungumzia jinsi maisha ya nyumban kwao yalivyo ya shida huku akionesha ni mtu anaetafuta sababu ya kuondoka home muda wowote ule , nikasema mi mwenyewe bado nina matatizo yangu kibao nibebe yako ya nini ?
3. Huyu alifanyiwa opereshen ya uzaz so kuna kipindi tukawa hatuwezi kuamshiana popo , siku ananitext ananiambia kama nimezidiwa sana atanipa nyuma ilihali hata sikumwambia kuwa nimezidiwa, nikaona hapa sipo ndo mambo zake itakuwa huyu
 
Niliamua kumtoa out huko sehemu za starehe tule tunywe na kulala hoteli kubwa .
Tukiwa pale akaingia bwana mmoja ana kakitambi ka kiasi hakijafika kwangu si demu anadai simpendi mwanamume mwenye tumbo tumbo Kama huyo baba .

Anaongea huo ujinga wake ilihali na Mimi namiliki tumbo kubwa kuliko hata huyo bwana ,Basi nikajua hapa sipendwi ,ikawa njia ya kukaacha ka sharifa
Asa mtu asiseme ya moyoni😅😅😅😅
 
Habari za weekend!

Kuna baadhi ya maneno watu wetu wa karibu wakiongea huwa yanatuumiza sana, sometimes inapelekea kupoteza interest ya kujenga maisha na huyo mtu.

Kuna mwanamke flani nilikuwa naye kwenye mahusiano takribani miaka 2, kuna siku bhana akaniuliza "hivi baby hata nikiolewa na mtu mwingine si tutakuwa tunakutana kisirisiri tunafanya mambo yetu?"

Kwa harakaharaka nikamjibu nikamjibu "ndio", ila ile kitu haikukaa vizuri kichwani mwangu, nilimwona kama mtu mwenye roho ya usaliti, kama anaweza kumfanyia mume wake hivyo si anaweza hata kunifanyia mimi.

Siku nyingine huyohuyo mwanamke akanambia maneno haya "Mimi sijali kuhusu matatizo yako, wewe ni mwanaume, wewe ndio inabidi ujali kuhusu matatizo yangu", baada ya hapo nikiwa simchukulii serious kabisa, wala sikutegemea mahusiano yetu yafike stage za kuoana.

Mwingine bhana alikuwa akiniomba hela afanye biashara, kuna siku alinieleza vizuri kabisa kuhusu hio biashara nikaipenda, nikamuahidi ntampa hela aanze, ilikuwa ni 1.5M.

Hio hela nilimpa kama baada ya wiki moja hivi, siku zilizofata nikawa nafatilia maendeleo yake na amefikia wapi, akawa tu ananiambia anasubiri vibali na issue zingine, mimi ilifika kipindi nikapotezea, kuna siku sasa mama ake akanipigia, ndio akaniambia kila kitu, ile hela bhana aliitumia kununua nguo, viatu, vipodozi, kabati la nguo na vikorokoro vingine,

Halafu ukizingatia sio mtu ambaye alikuwa hana nguo au anavaa vibaya, lahasha, hii kitu ilinifanya nipoteze interest kabisa na huyu mwanamke, nikawa namuona sio wife material kabisa, nilivoongea nae akasema sijui mambo hayakukaa sawa sijui kuna hela alizulumiwa, sababu kibao alitoa, nilimshangaa sana, hadi leo nikikumbuka nabaki nacheka tu.
Kwenda kulala kwa ex wake akisingizia eti kafiwa anakwenda kulala matanga huko na kumfariji
 
Back
Top Bottom