Mpenzi wangu alinifumania, ananichanganya!

Mpenzi wangu alinifumania, ananichanganya!

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Alinifumania lile fumanizi ambalo halina kupinga! Yaani, fumanizi la 100 percentage...

Zikapita siku mbili hanitafuti, nami nikawa kimya na mawazo sijui naanzia wapi kujitetea. Nikaona isiwe tabu, nikaenda kulanduka na Serengeti lager kama 5 hivi, kisha nikampigia simu!

Nikajua hata atakuja juu, lakini mtoto wa watu ndo kwanza akawa mpole kama maji ya kwenye mtungi! Baada ya salamu, nikamuuliza, 'Umenisamehe?' Akacheka kidogo halafu akakaa kimya.

Nikamuuliza tena, 'Au ndo umeniacha tayari?'

Akavuta pumzi akajibu, 'Nimekuacha na sijakuacha pia!' Hapo hapo akakata simu!

Nikapiga tena, akaniuliza, 'Nini?' Nikamwambia, 'Nakupenda.'

Akajibu, 'Nakupenda na sikupendi pia.'

Nipo matatani, ananichanganya sana, sielewi hapa majibu yake mawili mawili yananitia sonona na mtanziko wa mawazo! Kwa ambaye amekutana na swahibu kama hili ulifanyaje kuyaweka mambo sawa? Kijana wenu penzi bado nalitaka maana mtoto miuno kama feni bovu!
 
IMG_20240602_120311_170.jpg

Chai Cc ephen_
 
Ulikosea sana. Ulipaswa kukataa kata kata. Ungesema sio wewe, yule alikuwa ni mzimu anayefanana na wewe. Yaani ungekataa tena ukiwa serious kabisa.

Nakwambia huyo mwanamke wako angeamini maneno yako.

Mwanamke akikufumania hata kama amekukuta uko juu ya kifua kataa kabisaa, sema sio wewe.

Utanishukuru baadaye.
 
Back
Top Bottom