asante mkuu ila baada ya tukio hilo upendo wangu kwake umeisha kabisa najiuliza kama nikimuoa alafu kaenda kukojoa ukweni (kwetu) sijui nitaelewekaje huko nyumbani
Vipi kuhusu wanaume nao baadhi wanatatizo kama hili au linawahusu wanawake tu
Siri ya watu wawili hiyo nunua mpira weka ktk godoro kwa hatua za awali .
Pili msimamie usiku kuamka aende kukojoa.
Tatu afanye mazoezi.
Nne afuate ratiba za kutokunywa maji usiku
Tano kama hali inaendelea Mtafutie dawa anza na ndevu za mahindi chemsha na maji kisha anywe maji yake kwa muda wasiku kwa uwezo wa mungu atapona.Usisahau mrejesho
usimuache kisa anakojoa kitandani kama unampenda endelea nae ataacha tu kwani umesema upo nae mwezi kakojoa mara 1 hiyo ni bahati mbaya tu hata wewe inaweza kukutokea pia.,af kukojoa kitandani mara moja kwa mwezi sio mbaya[/QUOTE
Hofu yangu nikimuoa halafu akakojoa ukweni sitakuwa aibu yangu kwamba nimeoa kikojozi
asante mkuu
Wanaukumbi kwanza nawasalimu nyinyi nyote mtakaosoma post yangu hii.Nirudi kwenye mada, ninaye mpenzi ambaye tumedumu naye karibu mwezi mmoja na nusu yeye anakaa kwake amepanga nyumba na mimi ninakaa kwangu sasa katika huo muda wa mahusiano kuna muda hua naenda kulala kwake kama mara nne hivi vivyo hivyo naye huwa anakuja kulala kwangu.
Sasa sababu ya kuleta post hii hapa jamvini ili nipate ushauri, ni kwamba kuna siku alilala kwangu wakati wa usiku wa manane nikajihisi nimelalia maji nilivyoshituka kumshitua mpenzi wangu kwamba haya maji yametoka wapi akasema ni yeye amekojoa kwa bahati mbaya. Nilivyombana ni kwanini akojoe kitandani badala ya chooni akasema mkojo ulikuwa umembana sasa akasema ngoja alale kidogo ndoto ikamjia anakojoa nje kumbe ni kitandani.
Nilivyomuuliza kama hali hiyo ilishajitokeza huko nyuma akasema kama miaka mitatu iliyopita tukio hilo lilijitokeza ombi langu kwenu wadau huyu ni mpenzi niliyekuwa nina mpango wa kumchumbia hivi karibuni lakini kwa tabia hii nimevunjika moyo kabisa, nilikuwa naomba ushauri katika jambo hili kama kweli linaweza kujitokeza kwa mtu kukojoa kitandani kwa bahati mbaya au hilo ni tatizo la kudumu.
hayo maji muda wa siku saba
asante mkuu ila baada ya tukio hilo upendo wangu kwake umeisha kabisa najiuliza kama nikimuoa alafu kaenda kukojoa ukweni (kwetu) sijui nitaelewekaje huko nyumbani
Vipi kuhusu wanaume nao baadhi wanatatizo kama hili au linawahusu wanawake tu
Sijui kama ww ni mwanamke au mwanaume ila nikutie moyo.
Hiyo ni sehemu ya ukamilifu wa binadamu ndugu. Kama unampenda na anatimiza vigezo vyako usirudi nyuma maana Mungu ametuumba na mapungufu yetu pia unaweza kuwa na afya njema leo kesho ukawa na udhaifu wa kimwili.
Ongea naye vizuri kwa upendo utafute kujua chimbuko la tatizo kama ni la kiafya fanya jitihada umsaidie kama ni la kibinadamu unaweza kumsaidia kumuamsha kila baada ya masaa kadhaa kwenda kujisaidia ili kupunguza uwezekano wa yeye kuwa na hiyo hali.
Mimi nimeshuhudia mengi katika maisha yangu hususani kwa mama yangu ambaye mpk kesho bado anasumbuliwa na ugonjwa ambao unamdhalilisha kweli na haina tiba toka nimezaliwa 30+ now.
Pamoja na kwamba historia inaonyesha kwamba Baba hakufurahi mwanzoni lakini badae amekubaliana na hali ile kiasi cha kuhudumia mama bila matatizo.
Ndugu uwe mke au mume tafakari sana usimuache kwa hilo ila kama kuna lingine.
Barikiwa
nimecheka kwakweli nyie ndio huwa mnaota mnakula kate kumbe unatafuna godoro la dodomaHa ha haaa hata mm nilishawahi kukojoa kitandan nikiwa secondary.. acha kabisa hizi ndoto ni balaa unaota umefika chooni kabisa ndio unakojoa ndio unakojoa kweli..ila tangu hapo haijawah tokea.
Mkuu hiyo hali ni ya kawaida na mara nyingi hutokea mtu akilala mchovu. Ila sio ugonjwa wala nini
private issues kama hizi unazileta huku?
are you mentally deranged?
mnakera sasa wana MMU...!
anyway,hilo ni tatizo la kawaida tu na linatibika,kama unampenda utamtibu
lakini kama unataka kutumia kisa hichi ili kumuacha it's your choice
NB:ungepitia Jf doctors kwanza kabla ya kuja huku..!
private issues kama hizi unazileta huku?
are you mentally deranged?
mnakera sasa wana MMU...!
anyway,hilo ni tatizo la kawaida tu na linatibika,kama unampenda utamtibu
lakini kama unataka kutumia kisa hichi ili kumuacha it's your choice
NB:ungepitia Jf doctors kwanza kabla ya kuja huku..!