Mpenzi wangu amejisaidia haja ndogo kitandani, kumuuliza akasema ni bahati mbaya

Mpenzi wangu amejisaidia haja ndogo kitandani, kumuuliza akasema ni bahati mbaya

Mhhh.....
Siku 45 ulizo fahamiana na mpenzi wako hazija tosha kumjua hata kufikia hatua ya kuleta yanayo wahusu hapa jamvini.
Kama kweli unampenda, jiongeze muda ili muweze fahamiana uzuri. Pia kwa issue ya kukojoa bed, sioni kama ni jambo kubwa sana aiseee.....
Bado unayo nafasi ya kumfaham na pengine utakutana na makubwa zaidi ya kukojoa kwa bed.
Kwa hili la kukojoa bed, nakushauri mkamuone tabibu kama kweli unampenda mdada.
 
asante mkuu ila baada ya tukio hilo upendo wangu kwake umeisha kabisa najiuliza kama nikimuoa alafu kaenda kukojoa ukweni (kwetu) sijui nitaelewekaje huko nyumbani
Vipi kuhusu wanaume nao baadhi wanatatizo kama hili au linawahusu wanawake tu

Kaka wanaume wapo sana,kuna ndugu yangu alikuwa anakojoa mpaka amepata mke akawa anakojoa,sijajua kama kaacha au ni wife wake anamfichia aibu,anawatoto wawili sasa.
 
USHAURI WANGU KWENU WANAWAKE/
WASICHANA
Leo Nina jambo kwenu nyie dada zangu....
Ukitaka kuolewa olewa na mume ambaye
atakuwa rafiki kwako siyo kisa unampenda hadi
anakufunga akili kama MAHARAGE ya kwenye
MAKOPO , jaribuni hata kuzingatia umri usiolewe
na mwanaume atakaye kuwa BABA kwako! yaani
Unaolewa na mwanaume ana masharti kama
ubalozi wa MAREKANI ?? Ukitaka kumuomba au
kumshauri kitu unakuwa na HOFU kama unasubiri
MAJIBU ya UKIMWI bhana!? Ukimuelekeza jambo
utasikia kakufundisha nani? Ushaanza umalaya
eeeh basi unayweeeea kama KONOKONO kwenye
gamba atiwapo chumvi au amuonapo ADUI ?
yaani inafikia kipindi Ndoa unaiona chungu kama
umeolewa na Al-shabab?? Yaani mwanaume
mbabe utazani nyapala wa gereza la ISANGA ???
Mwanaume mjuaji kila kitu kama MAFUTA YA
KUPIKIA.. Yaani tangu amekuoa ye Ni amri tu
kama hakimu wa mahakama ya MWANZO !
Ila kinacho waponza Ni tamaa tu ukishaona
mwanaume anavijisent baaasi ushashoboka kama
mbwa koko aliyeona mfupa kwa muuza supu
Kwamba hata apigweje baadae atarudi tena
kudowea mabaki!! Na ndo maana ndoa
zinawashinda hata mwaka hammalizi.. Msione
vyaelea vimeundwa! Mnawasaliti wapenzi wenu
wanaowapenda kwa dhati kisa magari na mijengo
ukitaka kufaidi life ya raha chuma mwenyewe
mnapenda mtelemko kama MKOKOTENI kwenye
MTEREMKO mnaishia kunyanyasika tu mtakufa
ulimi nje kama MBWA anapoza MWILI kivulini.....
AMKA SASA TATIZO LENU MNAPENDA VIMTU
AMBAVYO HAVINA MBELE WALA NYUMA KISHA
MKIPIGWA CHINI MNAKUJA NA HOJA ETI
WANAUME WA SIKU HIZI.......AMKA SASA
 
ninachokiona hapa unatafuta sababu ya kummwaga....uamuzi ni wako...bado najiuliza mwezi mmoja na nusu tuuu....kweli kweli mwezi mmoja na nusu....mshafanya zinaa mbaya mnoo...kimahesabu ndani ya wiki mbili toka mkutane mshaanza uasherati.....mtoto wa kiki mpaka kufikia ankuja kulala kwako, tena anajiheshimu itamchukua muda......anywy hayanihusu....ila kaka kuwa makini na huo mpango wako wa kumuoa......kujikojolea sio issue.......watu wanajinyea kbs.....
 
Siri ya watu wawili hiyo nunua mpira weka ktk godoro kwa hatua za awali .
Pili msimamie usiku kuamka aende kukojoa.
Tatu afanye mazoezi.
Nne afuate ratiba za kutokunywa maji usiku
Tano kama hali inaendelea Mtafutie dawa anza na ndevu za mahindi chemsha na maji kisha anywe maji yake kwa muda wasiku kwa uwezo wa mungu atapona.Usisahau mrejesho

asante mkuu
 
Kukojoa mara moja unaona ni ishu? Nilidhani anakojoa kila siku mara mbilimbili
 
usimuache kisa anakojoa kitandani kama unampenda endelea nae ataacha tu kwani umesema upo nae mwezi kakojoa mara 1 hiyo ni bahati mbaya tu hata wewe inaweza kukutokea pia.,af kukojoa kitandani mara moja kwa mwezi sio mbaya[/QUOTE
Hofu yangu nikimuoa halafu akakojoa ukweni sitakuwa aibu yangu kwamba nimeoa kikojozi
 
Siyo mgonjwa aisee, ni usingizi mzito kama wa watoto wadogo... Wengine wanakojoa kila uchwao na wameoa na kuolewa sasa wewe mara moja tu umeshakuja huku.... Pia wakati mnatoa mambo ya aibu kama haya yanayowahusu wapenzi wenu msifikiri ni mambulula sana kiasi cha kukosa kupita humu.... Ukiniuliza mimi na uzee wangu bado hujawa mme bora kwa mjukuu wangu.
 
Wanaukumbi kwanza nawasalimu nyinyi nyote mtakaosoma post yangu hii.Nirudi kwenye mada, ninaye mpenzi ambaye tumedumu naye karibu mwezi mmoja na nusu yeye anakaa kwake amepanga nyumba na mimi ninakaa kwangu sasa katika huo muda wa mahusiano kuna muda hua naenda kulala kwake kama mara nne hivi vivyo hivyo naye huwa anakuja kulala kwangu.

Sasa sababu ya kuleta post hii hapa jamvini ili nipate ushauri, ni kwamba kuna siku alilala kwangu wakati wa usiku wa manane nikajihisi nimelalia maji nilivyoshituka kumshitua mpenzi wangu kwamba haya maji yametoka wapi akasema ni yeye amekojoa kwa bahati mbaya. Nilivyombana ni kwanini akojoe kitandani badala ya chooni akasema mkojo ulikuwa umembana sasa akasema ngoja alale kidogo ndoto ikamjia anakojoa nje kumbe ni kitandani.

Nilivyomuuliza kama hali hiyo ilishajitokeza huko nyuma akasema kama miaka mitatu iliyopita tukio hilo lilijitokeza ombi langu kwenu wadau huyu ni mpenzi niliyekuwa nina mpango wa kumchumbia hivi karibuni lakini kwa tabia hii nimevunjika moyo kabisa, nilikuwa naomba ushauri katika jambo hili kama kweli linaweza kujitokeza kwa mtu kukojoa kitandani kwa bahati mbaya au hilo ni tatizo la kudumu.

Sijui kama ww ni mwanamke au mwanaume ila nikutie moyo.

Hiyo ni sehemu ya ukamilifu wa binadamu ndugu. Kama unampenda na anatimiza vigezo vyako usirudi nyuma maana Mungu ametuumba na mapungufu yetu pia unaweza kuwa na afya njema leo kesho ukawa na udhaifu wa kimwili.

Ongea naye vizuri kwa upendo utafute kujua chimbuko la tatizo kama ni la kiafya fanya jitihada umsaidie kama ni la kibinadamu unaweza kumsaidia kumuamsha kila baada ya masaa kadhaa kwenda kujisaidia ili kupunguza uwezekano wa yeye kuwa na hiyo hali.

Mimi nimeshuhudia mengi katika maisha yangu hususani kwa mama yangu ambaye mpk kesho bado anasumbuliwa na ugonjwa ambao unamdhalilisha kweli na haina tiba toka nimezaliwa 30+ now.

Pamoja na kwamba historia inaonyesha kwamba Baba hakufurahi mwanzoni lakini badae amekubaliana na hali ile kiasi cha kuhudumia mama bila matatizo.

Ndugu uwe mke au mume tafakari sana usimuache kwa hilo ila kama kuna lingine.

Barikiwa
 
asante mkuu ila baada ya tukio hilo upendo wangu kwake umeisha kabisa najiuliza kama nikimuoa alafu kaenda kukojoa ukweni (kwetu) sijui nitaelewekaje huko nyumbani
Vipi kuhusu wanaume nao baadhi wanatatizo kama hili au linawahusu wanawake tu

Komaa nae tu kaka, huweiz pata malaika asie na dosari
 
Sijui kama ww ni mwanamke au mwanaume ila nikutie moyo.

Hiyo ni sehemu ya ukamilifu wa binadamu ndugu. Kama unampenda na anatimiza vigezo vyako usirudi nyuma maana Mungu ametuumba na mapungufu yetu pia unaweza kuwa na afya njema leo kesho ukawa na udhaifu wa kimwili.

Ongea naye vizuri kwa upendo utafute kujua chimbuko la tatizo kama ni la kiafya fanya jitihada umsaidie kama ni la kibinadamu unaweza kumsaidia kumuamsha kila baada ya masaa kadhaa kwenda kujisaidia ili kupunguza uwezekano wa yeye kuwa na hiyo hali.

Mimi nimeshuhudia mengi katika maisha yangu hususani kwa mama yangu ambaye mpk kesho bado anasumbuliwa na ugonjwa ambao unamdhalilisha kweli na haina tiba toka nimezaliwa 30+ now.

Pamoja na kwamba historia inaonyesha kwamba Baba hakufurahi mwanzoni lakini badae amekubaliana na hali ile kiasi cha kuhudumia mama bila matatizo.

Ndugu uwe mke au mume tafakari sana usimuache kwa hilo ila kama kuna lingine.

Barikiwa

miye ni mwanaume, asante kaka kwa ushauri wako nitafanyia kazi ushauri wako na pole kwa matatizo yanayomsumbua mwenza wako ila issue ya mwenza wangu imenisononesha sana mkuu
 
Ha ha haaa hata mm nilishawahi kukojoa kitandan nikiwa secondary.. acha kabisa hizi ndoto ni balaa unaota umefika chooni kabisa ndio unakojoa ndio unakojoa kweli..ila tangu hapo haijawah tokea.
Mkuu hiyo hali ni ya kawaida na mara nyingi hutokea mtu akilala mchovu. Ila sio ugonjwa wala nini
nimecheka kwakweli nyie ndio huwa mnaota mnakula kate kumbe unatafuna godoro la dodoma
 
private issues kama hizi unazileta huku?
are you mentally deranged?
mnakera sasa wana MMU...!
anyway,hilo ni tatizo la kawaida tu na linatibika,kama unampenda utamtibu
lakini kama unataka kutumia kisa hichi ili kumuacha it's your choice

NB:ungepitia Jf doctors kwanza kabla ya kuja huku..!

sorry mkuu kwa kukukwaza,ila lengo la kuleta jukwaa hili lilikuwa kupata experience ya watu wengine kama hili tatizo ni la kawaida na nifanyeje nashukuru wadau wengi wamenishauri kwa busara
 
private issues kama hizi unazileta huku?
are you mentally deranged?
mnakera sasa wana MMU...!
anyway,hilo ni tatizo la kawaida tu na linatibika,kama unampenda utamtibu
lakini kama unataka kutumia kisa hichi ili kumuacha it's your choice

NB:ungepitia Jf doctors kwanza kabla ya kuja huku..!

sorry mkuu kwa kukukwaza,ila lengo la kuleta jukwaa hili lilikuwa kupata experience ya watu wengine kama hili tatizo ni la kawaida na nifanyeje nashukuru wadau wengi wamenishauri kwa busara,sorry mkuu sikukusudia kukukwaza
 
Back
Top Bottom