AXIOM APEX VERBOSE
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 13,769
- 23,676
Good mimi nitakushauri ila ushauri wangu sio sheriaNaomba ushauri wa kweli, hata kama utakuwa mchungu. Sitafuti watu wa kunifariji tu; natafuta mitazamo tofauti ili nifanye uamuzi sahihi kuhusu maisha yangu na mustakabali wa mtoto wangu.
Binafsi nimewahi pia kutokuelewana na manzi fulani hivi issue ikawa km hivyo ilichukua km wiki tuna sort out mpaka yakaisha, mimi nilitumia tu ujanja wa kuzaliwa sio kingine inabidi akili yako iwe inachaji kumzidi yeye akikuzidi akili humuwezi, mwanamke anapenda mwanaume kiongozi anaemwongoza.
Lakini hua wanasema kitu kimoja niliwahi elekezwa km mwanaume ukiwa jeshini unafundishwa unapoenda kwenye uwanja wa vita usitumie vile tu ulivyofundishwa inabidi ujiongeze kwa kutumia ujanja wa porini ili uweze ku-survive.
Sasa suala km hilo limekukuta inabidi ujiongezee na ujanja wako wa kuweza kum-convince yeye asahau yaliyotokea. Issue ni kwamba unam-convince vipi? Hapo ni wewe na akili yako ndio maana Bible ikasema ishini nao kwa akili.
Kuna mbinu nyingi za kufanya suala hilo liishe na mbinu moja wapo ni kumkutanisha yeye na huyo manzi uliemnyonya mate kwenye camera, mzungumze wote kwa pamoja ili muyamalize wote kwa pamoja. Hii ni mbinu ngumu ila inawezekana kabisa ukiamua.
Narudia tena lazima utumie ujanja wa porini hata km utaonekana wewe ni mporipori haupo kimjini potelea pote ilimradi ya kwako yanakuendea na hicho ndicho huyo manzi alikua anakitaka kumthibitishia kwamba ni yeye pekee ndie unaempenda (kitu ambacho sio kweli) ila km mwanaume lazima uwe mjanja kumuhakikishia hata kwa kumdanganya kwa kutumia uongo wenye faida na manufaa kwako na kwake ili mjenge familia na kulea mtoto pamoja.
Kitu kingine huyo anachohitaji ni mapumziko yaan apate short break awe mbali na wewe kwa hio kuondoka haina maana kwamba mmeachana au hakupendi ila ameenda kupumzika.
Kikubwa unachotakiwa kufanya usipanic sana yaan manzi umeweza kumgonga ukaweza kumtia mimba ukaweza kulea mimba mpaka mtoto amezaliwa unapanic nini mwanaume?
Angalia wapi pa kuanzia ikiwezekana mfuate alipo zungumza nae ana kwa ana tumia akili zako zote ulizotumia kumtongoza lazima akae kwenye mfumo na atafungasha mabegi na kurudi.
Nitakufundisha tactic moja ya muhimu sana inaitwa counter-pressing hii inakuaje? Huyo manzi yeye si anagoma na ameondoka? Anataka umfanyie kitu kinaitwa counter-pressing.
Basi ngoja nitumie mfano rahisi sana umewahi bonyeza switch ukaona bulb haiwaki?, hivi ukibonyeza mara moja ukaona bulb haiwaki unaacha au unabonyeza tena switch ili uone ni umeme umezima au umekatika, luku imeisha au kuna hitilafu ya umeme au bulb imeungua au waya umeliwa na panya au circuit breaker imejizima kuzuia moto usiwake kwa hio umeme haufiki kwenye bulb?
Sasa hio ndio ninaiita counter-pressing itabidi uanze kubonyeza switch mara ya kwanza kisha uone bulb inawaka ukiona haiwaki angalia switch nyingi kuhakiki km bulb nyingine zinawaka, ukiona zinawaka basi tatizo litakua ni upande huo wa bulb yako kuanzia kwenye switch, waya, circuit breaker hadi kwenye bulb yenyewe.
Swali; unaanzia wapi?
Unaanzia kwenye switch, waya, circuit breaker au kwenye bulb (mpenzi wako mama watoto)?
Utafanya counter-pressing kwa sababu wewe hautaki kupoteza huu mchezo unaoitwa mapenzi kwa hio press the button look at the problem first kuanzia kwenye switch mpaka kwenye bulb (huyu ni mkeo).
Baada ya hapo angalia ulikosea wapi shida ni nini kwanini bulb haiwaki fungua circuit breaker angalia labda imejizima kuzuia moto usiwake kwa sababu kulikua na short circuit.
Natumia umeme kukuelewesha ili ujue ni nini kimetokea, hapo wewe unashindwa kuelewana na yeye sababu wewe ukiwa km switch haupati muunganiko na yeye akiwa km bulb sababu umeme haufiki kwake yeye.
Kwa hio unachotakiwa kufanya ni kubonye switch zaidi ya mara 3 kabla ya kuangalia km tatizo ni switch mbovu imeungua inabidi ubadirishe uweke switch mpya au la uone kwamba waya una shida umeliwa na panya kwa hio hakuna mawasiliano kati ya switch na bulb au la bulb imeungua kwa hio haifai tena kwa matumizi.
Sasa basi kwa sababu switch (wewe) ni nzima na bulb (yeye) ni nzima, km ukipress km ulivyofanya ila bulb ikawa haiwaki rudi uangalie je waya na circuit breaker haina shida, sasa hapa ndio hapo kwenye kusuluhisha tatizo nilipokwambia muite yeye muweke chini muite hio manzi uliyoipiga mate na wewe mkae chini mzungumze maana kilichotokea sio kwamba bulb mbovu ila circuit breaker imejizima, kwa hio unachotakiwa kufanya ni kuipandisha circuit breaker isome ON sio OFF.
Akili, hao viumbe wanataka uishi nao kwa akili. Jumlisha na ujanja wako wa kuzaliwa.
Nimeeleza kwa kadri nivyoweza kukuelewesha km haujaelewa au unaona mbinu hii ni ngumu basi kuna data utakua haujaziweka wazi ume-play victim ikiwa ya kwamba wewe ndio mwenye makosa ya wazi.
Km wewe ndio mwenye makosa ya wazi hata ukitumia hio counter-pressing haitosaidi.
Elewa neno makosa sio kosa ni makosa mengi yanaongozana leo hilo kesho lile na kuendelea yanafuatana pamoja na huchoki kukosea kila siku unakosea wewe tu mpaka mtu anachoka anasema eeh imetosha sasa ngoja niondoke zangu huyoo anapaa anakuacha mwenyewe. Kwanini? Kwa sababu wewe hauchoki kumkosea.
Ila km ni kosa hilo tu tumia hio counter-pressing umemaliza kesi. Press hio button Buddha.
NB: Counter-pressing is the immediate, coordinated attempt to win the ball back seconds after losing it.